Masha akainuka kumfatulia Vicky
Vicky hatua ya kwanza aliamua kurudi pale pale Hotel, labda afatilie kwa kina labda anaweza pata hata mawasiliano ya huyo baba mtoto wake
Alienda mpaka kwa Supervises
"Mose aliacha kazi gafla sanaa ,nyumbani kwake labda umuulize lydia mana walikuwa na mahusiano "
"Sawa ahsante "
Vicky akatoka kwenda kumtafuta huyo Lydia ,
Lydia yeye ni mfuaji hapo mara zote yupo hapo
Hakuangaika sana kwa sababu anapajua anapo patikana akamkuta
Akamwelezea kila kitu, lydia alishangaa akamwambia namjua Vizuri sana Moze kweli ni muhuni lakini akubakee We Vicky wewe ulimuonaa??
Vicky akamwambia hapana lakini ni yeye ndie alikuwa humo baada ya Yule aliekodisha chumba kuondoka "
"Moze hawezi kubaka jamani nakataa!!"
ITAENDELEA.....
SEHEM YA 07
MWANDISHI ::HURU MEDIA
"Hapana Vicky hapana,, moze atafanya yote lakini kubakaa aah hapana"
"Sawa nipatie basi namba yake niongee nae mwenyewe "
"Hapatikani "
"Yupo wapi??"
"Kwakwel mie sijui moze alipo aliondoka hakuna aliemuaga hata anapo ishi hakubeba chochote kile chumba aliacha kama kilivyo "
"Ameondoka lini??"
"Wiki tatu zimepita sasa"
"Lydia , halafu unakataa kwamba hakunifanyia ujinga kwanini atoroke kipindi hicho hicho"
Lydia kimyaa , Vicky akamwambia basi sawa ila ukimuona mwambie nina mimba yake wala sihitaji malezi yake lakini nataka mwanangu akizaliwa aite baba hilo kwangu linatosha
"We Vicky wewee una mimba ya moze , hamkubakana nyie mlielewana"
"Utajua wewe iwe tulielewana au alinibaka mwambie nina mimba y..."
Kabla hajafikisha neno lake lydia alimnasa kibao cha uso
"Mpuuzi malaya wewe , kwahiyo umebeba mimba ndio imekuja mbona hukunifata wakati mnaelewana kulala"
Vicky nae mambo yashamvuruga alimuweka kibao na yeye cha uso , lydia akarudisha
Vicky akaona mambo yasiwe mengi alimvamia wakaanza kuzibuana ma ngumii na walikuwa wawili tu
Walipigana , hali ya Vicky ilikuwa bado dhaifu ,lydia akajipatia point zake alimpiga
Bahati mbaya kwa lydia , Bahati nzuri kwa Vicky siku hiyo Rahul alikuwa yupo hapo hotelini kwa mambo yake
Ndie alikuwa mtu wa kwanza kuona huo ugomvi , alikimbia mbio kwenda kuamua
Akamvuta Vicky pembeni , alikuwa ashaumia Usoni na mdomoni damu zinatoka
Lydia akamwambia nitakuumiza wewe mjinga ,chezea hao hao na hilo mimba toa bwana ndo kakukimbia hivyoo!! Mfyuuu"
Rahul akamtoa Vicky bila hata kusema neno akamchukua mpaka ndani ya Gari yake akamuweka akatoka kufata maji akamletea
"Kunywa haya maji kidogo " Rahul akampa Vicky akanywa kwa hasira kweli
"Nilikuona wakati unaingia kuna vitu nilikuwa namalizia malizia mpaka nimemaliza sikukuona kurudi ndio nikaamua kufata ile njia niliyokuona" Rahul akatoa maelezo kwa Vicky bila hata kuulizwa
Vicky akamjibu aah sawa , hakuwa hata na mood ya kuongea , Rahul akamwambia twende hospital sawa
Vicky akasema hapana niache tu niende nyumbani ,
"Hapana nitakuwa sina akili kukuacha uende njia yako wakati upo kwenye hali hii Vicky hapana "
Rahul alilazimisha sana ndio Vicky akakubali kwenda huko hospital
"Shiiit , Vicky unastahili kumbe kufaaaa aah" masha alipiga ngumi ukutani baada ya kuona Tukio zima tangu Rahul anakuja na Vicky , na sasa wanaondoka wotee
" Huu ukaribu hapana hapana lazima niukomeshee na kwanini imekuwaje??"
Alichukua simu yake haraka akarafuta namba ya Vicky akaipiga
Simu ya Vicky iliita akaitazama anapiga masha akataka kupokea lakini Rahul akaichukua ile simu akamwambia
"Sio sasa ,Unatakiwa kupumzika sawa " aliizima ile simu akaiweka pembeni
Masha simu haikupokelewa akapiga tena haipatikani
Hasiraa zilizidi akaanza kufata gari upende ilipo pita ile ya Rahul , hakuiona hata imekatishia wapiii alitembeza gari kwa hasiraaa lakini wapi alipiga na kupiga namba ya Vicky bado haikuwa hewani
Akakumbuka namba ya Rahul hakupatiwa Rahul alimwambia ukiwa na shida na mimii piga simu ya ofisini kwahiyo hakuwahi kumpatia namba yake ya mkononi
"Rahul nakuapiaaa , siku nikiolewa na Mr Alberto walai nakufukuza kazi mimi mwenyewe mfyu" akaitupa simu yake huko kwa hasiraa
Rahul alimpeleka hospital , Vicky alishangaa kuona Rahul analipia kipimo cha Ultrasound akamuuliza kwanini nipige hiyo
Rahul akamwambia wewe ni mjamzito purukushani kama zile ni hatari kwa afya yako na mtotoo"
Vicky alikuwa kama ametoneshwa alianza kuliaa bila hata kujivunga alilia mnoo
Rahul akaingia kibarua kwa kumbembeleza Vicky
"Pata vipimo kwanza utakuwa sawa, Usijali kukataliwa na mwanaume sio mwisho wa safari yako maisha bado yako upande wako na wewe ni mschana mmoja hivi ambaee sijui nikuelezee vipii ,lakini Vicky wewe ni mwanamke ambae natamani Sana mambo yabadilike uwe wewe"
"Ni we mimi kivipi ??"
"Ooh pima kwanza tutaongea"
Alipima vipimo vingi vingi hali yake ilikuwa sawa , rahul akamwambia acha kugombana na mtu yeyote yule mimi nitakuwa na wewe bega kwa bega unanielewa Vicky???
.