Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

ππˆπ“π€πŠπ”π†π€ππƒπ€πŸ˜ ⁽NΙͺα΄›α΄€α΄‹α΄œκœ°α΄œα΄€α΄›α΄€ α΄˜α΄α΄˜α΄α΄›α΄‡βΎπŸ₯° SEHEMU YA 01

27th Jul, 2025 Views 43



Naitwa Tatiana Ni binti wa miaka 25 Ni mtoto wa Pili Kati ya watoto wa mzee Ponda Kaka yangu mkubwa anaitwa Barack na wa Pili Ni Mimi . maisha yetu yalikuwa ya kawaida sana Ila ilikuwa na furaha na upendo wa hali ya juu wazazi wetu walihakikisha tunapata haki zetu Kama watoto ikiwepo kusoma pamoja na nahitaji yetu muhimu Barack alikuwa kidato Cha sita Mimi nilikuwa nimemaliza kidato Cha nne Ila bahati mbaya sikufanya vizuri matokeo yangu hayakuwa mazuri wazazi wangu walitaka kunirudisha Tena shule kwaajili ya kulisiti kutokana na kipato kidogo Cha wazazi wangu niliwaomba wasinifikirie Sana Mimi wajiwekee akiba kwaajili ya Kaka yangu Barack ambae niliamini lazima afanye vizuri kwani alikuwa anajiweza Sana kimasomo . Badala yakukaa nyumbani Kama mzigo niliamua na Mimi nitoke kwaajili ya kujitafutia rizki nilikuwa naenda kushinda saloon kwa shoga yangu Vera nikimsaidia kusuka watu pamoja na kazi mbalimbali huku na Mimi niliendekea kujifunza Mambo mengine .

Siku moja baada ya kumaliza kazi tulifunga saloon Vera akaniambia
" Shosti Leo utaenda mwenyewe Mimi naenda kulala kwa shemeji yako .
" Sawa lakini kesho si utafungua saloon?
" Naachaje shoga yangu wakati nadaiwa kikoba Tena kesho uwahi Kuna wateja wawili wakusuka Rasta .
" Poa nitawahi .
" Tena shika hii fungu naweza nikachelewa kuja wewe ukiwahi Anza kufanya kazi
" Poa. Nilipokea zile funguo na kuweka kwenye pochi kisha
nikaondoka na nikaelekea nyumbani kesho yake nilijidamka mapema na kumsaidia mama baadhi ya kazi Kisha nikajiandaa nilipomaliza nilianza safari ya kwenda saloon . Nilipofika maeneo ya saloon Kuna gari ilikuwa nyuma yangu ikanipigia honi nilipogeuka nilimuona mama mmoja aliyekuwa kwenye Ile gari alitoa mkono na kuniita nilienda nikamsalimia maana alikuwa mkubwa Sana kwangu Malika Kama mama yangu
" Shikamoo
" Marahaba binti hujambo
" Sijambo
" Samahani unaweza kupanda kwenye gari tuongee kidogo? Kidogo nilisita na kuwa na wasiwasi Yule mama aliligundua Hilo
" Usiogope Ni kitu kizuri tu nataka tuongee. Nilizunguka upande wa Pili nikapanda kwenye Lile gari na kufunga mlango nikawa namsikiliza Yule mama anachotaka kuniambia
" Naitwa mama T sijui wewe unaitwa Nani?
" Naitwa Tatiana
" Tatiana binti mrembo Kuna kitu kizuri nataka nikwambie
" Kitu gani
" Kwanza hii Ni saloon yako au umeajiliwa
" Ni saloon ya rafiki yangu
" Nimefungua barber shop kubwa mjini so nilikuwa nahitaji binti wa kazi na kwa jinsi ulivyo naona kabisa unafaa kwenye barber shop yangu pia nitakulipa mshahara mzuri .
" Kiasi gani ?
" Laki mbili na nusu kwa mwezi pia Kuna marupurupu kutoka kwa wateja endapo utachangamka . Nilifikiria pesa ninayoipata kwa Vera Ni ndogo alafu nimejishikiza tu ikabidi nimuulize mama T
" Unataka nianze kazi lini?
" Hata kesho Kama itawezekana
" Sawa Ila naomba uniachie namba yako ya simu kwaajili ya kukupa jibu maana siwezi kukurupuka . Mama T alichukua pochi yake akatoa business card na noti mbili za elfu kumi akanipati.
" Na hiyo Ni hela ya vocha . Nilishangaa hela ya vocha nyingi hivi Ila Nika zuga nikadumbukiza kwenye pochi yangu na kumshukuru .
" Asante Basi badae nitakutafuta
" Sawa usiache kufanya hivyo kazi njema . Mama T aliongea huku akiachia tabasamu nilishuka kwenye gari nikaenda kufungua saloon na kuanza kufanya usafi nilipomaliza tu kufanya usafi alikuja mteja nikaanza kumsuka huku tuliendekea kupiga story ilipofika majira ya saa nne Vera alikuja akiwa kaongozana na mteja mwingine tulisalimiana Kisha akaanza kumuhudumia tulipomaliza kuwasuka wateja wetu nilimwambia Vera kuhusu mama T Vera akaniambia
" Weeee shoga yangu bahati hiyo mama T namjua Ni mama mwenye hela zake mjini na mabiashara yakutosha sio mbabaishaji Kama umeridhia nenda . Kutokana na ushauri wa shoga yangu Vera moyo wangu ulilidhika nikampigia simu Mama T na kumueleza nipo tayari kufanya kazi ikiwezekana aniekekeze kesho niende mama T alifurahi Sana na kunieleza ilipo barber shop yake na kuniambia kesho saa mbili asubuhi niwe nimefika

Kesho yake nilijiandaa nikatoka nyumbani mapema kuwahi usafiri nikapanda daladala mpaka mjini niliposhuka kwenye daladala nilitembea mwendo mdogomdogo nikafika kwenye barber shop ya mama T mida ya saa mbili kasoro nilikuta pameshafunguliwa niliingia na kuwakuta wadada wawili waliokuwa wamevalia tishet nyeupe zenye nembo ya barber shop na skin nyeusi niliwasalimia wakanikaribisha nikajitambulisha
" Mimi Ni mgeni wa mama T
" Oooh karibu ukae atafika hapa muda sio mrefu huu ndio muda wake. Nilikaa na kuanza kushangaa mazingira ya mule ndani jinsi yalivyokuwa mazur na ya kuvutia. Baada ya dakika kumi mama T akawa amewasili mfanya kazi wake mmoja alienda kumpokea pochi yake na kumsalimia aliponiona aliachia tabasamu
" Waooo Tatiana umefika ? Nilisimama na kumsalimia aliitikia Kisha akanishika mkono tukaenda kwenye chumba kidogo kilichoonekana Kama ofisi kulikuwa na viti viwili pamoja na meza
" Karibu ukae . Nilikaa kwa nidhamu na kunyenyekea huku nikitulia kusikiliza maagizo nitakayopewa
" Tatiana ofisi ndio hii utafanya kazi hapa pamoja na wenzako Kuna wadada wawili na wavulana wawili na wewe utakuwa wa tano nitaenda kukutanisha na wenzako watakuelekeza kazi sawa .
" Sawa
" Alafu kuhusu nguo unatakiwa ubadilishe uvae Kama wenzako walivyovaa . Aliongea mama T huku akifungua droo akatoa skin nyeusi na tishet akanipatia Kisha akaniambia nimfuate nilibeba vitu vyangu akanipeleka kwenye chumba kimoja nikabadilishe nguo Kisha nikatoka alinitambulisha kwa wafanyakazi wote na kuwaambia wanielekeze jinsi ya kufanya kazi.
" Paulina muelekeze mwenzio. Paulina alinishika mkono na kunizungusha sehemu zote na jinsi ya kutumia vifaa vya kazi tulipofika chumba Cha massage alikaa kitandani na kuniambia
" Hii ndio sehemu inayotupa marupurupu ukiitumia vizuri utafaidika . Sikuelewa Paulina alikuwa anamaanisha nini Ila nilimuitikia tu bora yaishe

ππˆπ“π€πŠπ”π†π€ππƒπ€πŸ˜ ⁽NΙͺα΄›α΄€α΄‹α΄œκœ°α΄œα΄€α΄›α΄€ α΄˜α΄α΄˜α΄α΄›α΄‡βΎπŸ₯°
Na 𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 π‘Ίπ’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š

SEHEMU YA 02

Paulina alimuangalia Kisha akasema
" Sasa unatakiwa usizubae mteja anapokuja unatakiwa kuchanga mka na hivyo ulivyo lazima uwakamate .
" Sijakuelewa kuchangamka kivipi ? Paulina aliachia tabasamu
" Usijali Mambo ni taratibu utaelewa tu. Basi tukitoka na kwenda kufanya kazi nyingine .

Taratibu nilianza kuzoea kazi kazi kubwa nilivyokuwa nafanya ni kufanyia wateja scrab na kusokota dred. Wateja waliokuwa wanakuja kupata huduma pale wengi walikuwa Ni watu wakubwa wenye pesa zao Mara nyingi walikuwa wakituachia vichenchi wakati mwingine mteja alifurahishwa na huduma anakuachia hela ya soda kidogo maisha yangu yalianza kubadilika nilianza kubadilisha hata viwigi na kupaka mafuta mazuri .

Siku moja hakukuwa na wateja tulikuwa tumekaa tunapiga story huku Paulina na Martha wakiongelea kuhusu huduma walivyokuwa wanawapa wateja wao wa massage na pesa walizopata Mimi nilibaki kucheka Mara alikuja Kaka mmoja mtanashati mrefu mwenye six pack alitusalimia Martha na Paulina walimchangamkia huku waki mkaribisha kwa shangwe .
" Patrick ulikuwa wapi siku zote hizo hunone Kani Nani alinificha jamani . Nilikuwa nawaangalia walivyokuwa wanajishauwa Ila sikuwashangaa kwani Ni kawaida yao kufanya hivyo kwa baadhi ya wateja Yule Kaka hakuwatilia manani alivua miwani na kuniangalia Kisha akapiga hatua na kunisogekea pale nilipo kaa na kunipa mkono
" Habari mrembo .
" Salama
" Nimefurahi kukuona . Martha na Paulina walicheka na kugonga
" Makubwa haya inaonekana macho yameona kitu hapa . Patrick aliwageukia na kuwajibu
" Sio macho tu kuona Bali na moyo umependa.
" Weweeeeee nilijua tu chezea Patrick mutu mutukubwa . Nilibaki natoa macho sikuwa naelewa wanachoongea na Yule mtu ni Nani kwao . Patrick alijitambulisha
" Naitwa Patrick
" Tatiana .
" Waooo Tatiana jina zuri . Martha alimshika Patrick begani
" Mzee naona umeshapagawa tununulie bia tuzimue wakati ukiwa unamuangalia mrembo .
Patrick alitoa pesa na kuwapatia Kisha akarudi kwangu na kuniambia
"Nshitaji huduma ya massage nshitaji unihudumie
" Lakini Mimi siwezi sijawahi kufanya hiyo kazi
" Mmm unashindwaje Sasa mrembo acha kuniangusha .
" Tafadhali naomba umchague mmoja kati ya penina au Martha.
" Nimekuchagua wewe.
" Lakini nimekwambia siwezi . Martha alisikia tulivyokuwa tunavutana alikuja karibu yetu
" Tatiana utaweza lini hebu kajaribu hata sio kazi ngumu . Patrick akadakia
" Tena nitakuwa namuelekeza
" Sasa je huoni kama una bahati ya kupata mteja mzuri. Kwakuea ni sehemu ya kazi yangu na nilishawahi kuona wakina Martha wanavyohudumia watu sikuona shida niliongozana na Patrick mpaka chumba cha massage alivua nguozake na kujifunga taulo akajilaza kitandani nilichukua mafuta na kuanza kazi yangu Patrick hakuwa mtulivu alikuwa akinishoka mikono
" Sasa notakuhudumiaje ikiwa utakuwa unanishika mikono
" Nasikia Raha ninapoishika mikono Yako una mikono lakiini sana .
" Basi naomba uniacge nifanye kazi kwanza hayo mambo mengine badae. Nilimfanyia massage mpaka akawa anafumba macho nikajua kazi yangu inaenda vizuri nilipomaliza aliamka na kukaa kitandani na kuniambia
" Tatiana unaweza kunipatia namba Yako ya simu
" Hapana ila kama utataka ya ofisini nitakupa . Patrick alitabasamu
" Sawa najua unaniona msumbufu ila siku moja utanijua ni mtu was Sina Gani . Sikumjali niliweka vitu vizuri huku Bado akiwa ananiangalia nikamiiliza
" Kuna huduma nyingine unahitaji?
" Hapana ila natamani kuangalia Kila wakati wewe ni mrembo mna Tatiana.
" Asante . Nilimjibu Kwa nyodo na kutoka kwenye like chumba maana hakukuwa na dalili za yeye kutoka alipoona nimetoka alienda kuwaa nguo zake na kutoka penina akaniambia
" Tatiana mbona ulimuacha mteja haija msubiri mtoke wote? Nilishindwa nimpe jibu Gani penina ilibidi ninyamaze . Patrick alikaa na kupigapiga story huku jicho lake likiwa kwangu lakini sikuonyesha kumjali alikaa mpaka alipochoka akaondoka .

Nikiwa najiandaa kulala simu yangu iliita nikajisemea
" Ni nani anapiga Simu saizi tena namba mpya . Nilipokea Ile simu chaajabu nilisikia sauti ya Patrick ikabidi nimuulize kujihakikishia
" Wewe ni Patrick? Alicheka sana na kusema
" Nimefirahi kwakuitambua sauti yangu hii Ina maana kuwa nipo alilini mwako .
" Hakuna kitu kama hicho nimeotea tu.
" Sawa Tatiana unajua Mimi nipo serious nakupenda naomba ujaribu kunielewa mtoto wa mwanamke mwenzako kiukweli sijawahi kupagawa kama ulivyonipagawisha wewe mtoto nipo tayari kufanya chochote Ili utambue ni kiasi Gani nakupenda . Nilikaa kimnya mpaka akaniita
" Tatiana. Nikaitikia
" Abeee
" Nijibu basi mama . Nilishindwa kujibu kwasababu nyumba yetu haikuwa na silingbodi hivyo nikahofia wazi wangu wangesikia niliamua kukata simu na kutoka mlio nikaiweka chini ya mto Kisha nikalala

Soma mpaka mwisho kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ππˆπ“π€πŠπ”π†π€ππƒπ€πŸ˜ ⁽NΙͺα΄›α΄€α΄‹α΄œκœ°α΄œα΄€α΄›α΄€ α΄˜α΄α΄˜α΄α΄›α΄‡βΎπŸ₯° SEHEMU YA 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/nitakuganda-n--sehemu-ya-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest