Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MWANAMKE ALIYECHUMA NAYE MALI | EP 05

27th Jul, 2025 Views 5



Mayner na mume wake walimaliza kuoga walirudi hadi chumbani ambapo walimkuta mtoto akiwa amelala. Hakuna ambaye alihisi mtoto kama amepatwa na jambo, zaidi ya kudhani kwamba alipitiwa na usingizi.

Mayner, kama mama ambaye alikuwa na hamu ya mtoto wake, alimsogelea na kumpiga busu kwenye paji la uso.
“Nakupenda Mama ❤️” alisema huku akimtazama mume wake ambaye naye alisogea karibu yake na kumpa sifa zake.
“Mmeamua mchukua nyie tu, si ndiyo?” alisema huku akiweka tabasamu 😊
“Hahaha! Una wivu, ila haipendezi kwa mtoto wa kike kuwa na sura ya Baba 😅”
“Yes, for sure. Hata hivyo mwanangu ataishi maisha ya kinyamwezi sana, atapendeza kila muda 😍”
“Hahaha! Usije mrithisha mambo yako bure, huyu anatakiwa kuwa ostadhat. Asome na kuhifadhi Qur'an 📖”
“Hahaha! Aya sawa tutaona itakuwaje 😆” alisema Garma huku akiondoka na kuelekea kwenye kabati.

Alibadilisha nguo na kwenda jikoni kuandaa chakula huku akimuacha mke wake akijiweka sawa. Alipofika jikoni alianza kupika hadi chakula kilipoiva, kisha alimpelekea mke wake huku kingine akitenga kwa ajili ya mama yake ambaye alikuwa chumbani.

Walifanikiwa kula chakula kwa pamoja bila hata kuhisi tofauti yoyote ile kwa mtoto. Lakini ilipofika muda wa kulala, Mayner aliona mtoto hana joto tena kama mwanzo. Hata tabia ya kukunja vidole hakuwa nayo.

Kibaya zaidi, hata kutikisika kwake ilikuwa ni shida, wakati mwanzo alikuwa anajinyoosha viungo vyake na kuweka tabasamu. Kuna muda alikuwa akilia pia. Ilibidi amwambie mume wake kuhusiana na ile hali, akasema:
“Baby, mtoto mbona kapona hivi? 😟”
“Mh! Kapoaje tena wakati kalala? 🤔”
“Hana hata joto, mguse uone ❄️”
“Ebu ngoja…” Garma alijiamsha na kumgusa mtoto.

Baridi mithili ya barafu ilikuwa katika mwili wa kichanga kile, hakuwa na joto hata chembe 🧊.
“Kuna nini mbona sielewi?” alijiuliza moyoni, hakutaka kusema kwa sauti kuhofia asije kumpa wasiwasi mke wake. Aliweka mkono katika eneo la moyo, lakini kimya kilifuatia — moyo haukuonesha kudunda. Alibadilisha na kuweka puani, labda kungekuwa na pumzi ambayo ilikuwa ikitolewa, lakini napo palikuwa pakavu 😢

Akili yake ilimwambia kwamba pale hakukuwa na mtoto tena, mwanaye alikuwa amefariki. Akutafuta namna nzuri ya kumwambia mke wake, alifikiria mno.
“Baby, mbona upo kimya?” Mayner aliuliza 😐
“Hapa… hapana, hapana nawaza tu kwanini mtoto yupo kimya 😔”
“Niliambiwa kwamba ni kawaida kwa mtoto kulia siku za mwanzoni hasa miezi sita ya mwanzo, lakini Fazma sioni akilia?”
“Hata mimi nashangaa… ebu ngoja” alisema na kuamka mazima.

Alichukua shati lake akavaa, kisha suruali na kuondoka ndani huku mkononi akiwa ameshika funguo. Alielekea hadi sebureni. Akatupa jicho ukutani.
“Saa sita usiku… sijui watakuwa wamefunga? ⏰” alijiuliza na kutoka nje.

Alipofika, alitizama mafuta katika gari yake. Alipoona yapo, alirudi tena ndani. Alifika hadi chumbani, kwa sauti yenye kitetemeshi alisema:
“M’bebe mtoto twende 🏥”
“Wapi?”
“Hospital.”
“Kuna nini mbona sielewi?”
“Hali si hali… hayupo sawa, yaani hali yake si ya kawaida. Twende.” alisisitiza Garma.

Mayner alibaki njia panda, hakuwa anaelewa ni nini haswa kilikuwa kinaendelea 😟
“Twende hospitali, m’bebe mtoto! Wewe vipi bwana! 😠” safari hii Garma alizungumza kwa hasira mno.
“Mh! Sawa, ila usije niambia kwamba mwanangu…” Mayner alishindwa hata kuendelea, kilio kilikuwa mbele yake 😭
“Acha kulia, m’bebe tuondoke.” alisema Garma huku akimtazama mke wake.

Mtoto alibebwa na waliondoka mahala pale hadi nje ambako walipanda katika gari na kuelekea hospitalini ambako huko vipimo vingeendelea ili kujua ni nini haswa kilimkuta mtoto.

Nyuma, mama yake alitoka chumbani kwake. Mihangaiko yote ambayo ilikuwa ikiendelea aliisikia vizuri tu kwani hakuwa amelala. Alienda hadi katika dirisha na kufungua, kisha akatazama kama nje kulikuwa na gari.
“Wameondoka… wanadhani atapona. Hapa nimemuwaisha maana ile sumu ingemchelewesha 😈” alisema huku akicheka mno.

Alirudi chumbani kwake na kuchukua simu, kisha alitafuta namba ya Ninah akampigia.
“Tayari nishafanya yangu ☠️” alisema huku akijinadi.
“Usiniambie kwamba tayari ameshakufa?”
“Khe! Nimefika pale, shika miguu juu kichwa chini, mdomoni nimemwekea nguo… unadhani hata alikuwa na uhai? Basi! 😏”
“Mamaaaaaaa! Mbona umetisha hivi?! 😱 Hapo kweli hawezi pona, uwi yaani wewe ndio utakuwa shoga yangu hapo nyumbani 😂”
“Yule mtoto hakuwa wa mwanangu. Ana kidume chake maeneo ya Mabatini. Nilishawahi kuambiwaga.”
“Basi sawa mama, acha mimi nilale 😴” alisema Ninah.

Mama Garma alikata simu, uso wake ulikuwa na tabasamu kuona kwamba amefanikisha dhamira yake. Lengo lake kubwa ni kuona anamuangamiza mtoto, baada ya hapo angefuatia mama mwenyewe 😡

Baada ya kukata simu, alitoka sebureni na kwenda chumbani ambako alichukua damu ya uzazi aliyopewa na Ninah. Aliitazama kama ni yenyewe. Aliamua kuthibitisha kwa kuzamisha kidole katika chupa, akanusa kidogo.
“Yenyewe 😈” alisema na kufunga chupa kile.

Akarudi tena sebureni, aliiweka katika meza. Akaenda jikoni ambako alichukua ndimu pamoja na chumvi, akatafuta yai viza. Alipopata, alirudi tena sebureni.
“Kama ambavyo yai hili likioza na kunuka, ndivyo huyu mbwa atakavyonuka 🥚🤢” alisema na kuvunja yai lile kisha alichanganya katika kopo ambalo lilikuwa na damu ya uzazi.

Aliweka na chumvi, akasubiri kama dakika moja hivi hivi. Damu ilianza kuchemka kama ipo jikoni 🩸🔥. Mwisho akachanganya na ndimu.
“Kwisha habari yako 😤 Mbona mwanangu anakuacha siku si nyingi” alisema huku akizunguka lile kopo ambalo aliliweka mezani.

Huyu ndiye Mama Garma, mama wa watoto wawili. Kwake alikuwa mtu wa msimamo haswa. Kile ambacho alikuwa anakitaka basi alihakikisha kwamba anakipata kwa nguvu yoyote ile. Hakuwa mtu wa kubadilisha mawazo hovyo.

Mume wake alifariki miaka 20 iliyopita. Malezi ya Garma na Rasma yalikuwa mikononi mwake. Aliwalea na kuwasomesha kwa kadri alivyoweza hadi wakawa wakubwa na kufika chuo. Yote haya alifanya bila hata msaada wa mwanaume — ni yeye na nguvu zake 💪

Hatimaye, watoto wanapata kazi na hivi sasa anaishi kwa mtoto wake wa kiume. Alikuwa anampenda Ninah kwa sababu huyu alikuwa mmoja wa watoto wa shoga zake ambaye alikuwa anaishi Mkuyuni, jijini Mwanza.

Ushoga wao uliwafanya watake kukutanisha damu zao, hivyo kama wazazi walikubaliana kila kitu. Kwa bahati mbaya, upande wa Mama Ninah hakukuwa na maisha mazuri, hivyo kwake aliona kama mtoto wake akiolewa na Garma ni kurahisisha zoezi la upataji wa baadhi ya mahitaji muhimu kutoka kwa Garma.

******************
Kina Mayner walifanikiwa kufika Hospitali ya Bugando saa saba usiku. Walipofika, walimpeleka mtoto kwa daktari. Vipimo vilifanyika kwa haraka mno ili kuthibitisha kama mtoto alikuwa na uhai ama lah.

Katika kichwa cha Garma alikuwa anafahamu majibu yatakuwaje, lakini hakutaka kumuonesha ishara yoyote mke wake.
“Ameanza lini hii hali?” aliuliza daktari 🥼
“Yaani ni ghafla… nimemkuta pale kitandani kapooza, nikamwambia mume wangu tazama mtoto kapooza 😭” Mayner alisema huku machozi yakimtoka.
“Ni taarifa ngumu kuitoa kwako. Ni taarifa ambayo kila mmoja hapa sidhani kama ataipokea katika hali nzuri... lakini mtoto wetu amefariki 🕊️” daktari alidiriki kutoa taarifa ambayo ilienda kumwambia Mayner kwamba hana mtoto tena katika uso wa dunia hii.

Mayner alikaa kimya kama dakika mbili hivi. Sio kwamba hakuwa duniani — la hasha — bali mwili na akili vilikuwa vimetengana ghafla. Kichwa chake kilishindwa kuushirikisha mdomo juu ya kile ambacho alikuwa anakisikia. Kwa shida sana alisema:
“Ina-ma… ina-ameku… amekufa… Fazma wangu? 😭” lilikuwa ni swali ambalo hata daktari ilibidi akae kimya. Alikosa la kuzungumza.

Alivuta maumivu ambayo mwanamke yule alikuwa akiyapitia katika maisha yake. Alivuta hali ya moyo wake jinsi ulivyokuwa kwa muda ule.
“Kazi ya Mungu haina makosa 🙏”
“Mungu gani ambaye anachukua kiumbe cha siku moja!? Hapana! Mama yako atanitambua! 😡” Mayner alisema na kuondoka mahala pale, lakini mwili wake uligoma. Hakuweza kupiga hatua zaidi — alidondoka chini kama mzigo.
“Puuuu!” fahamu zikimpotea…

Kwa 1000Tsh, unapata simulizi hii. WhatsApp namba 0717255498..........
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MWANAMKE ALIYECHUMA NAYE MALI | EP 05  >>> https://gonga94.com/semajambo/alifirisika-baada-ya-kumuacha-mwanamke-aliyechuma-naye-mali-ep-05
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest