Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

"6~~12" SWEETHEARTπŸ’‹πŸ˜˜ 06 (Ma oxygen yoooooπŸ™Œ)

27th Jul, 2025 Views 22


Sawa nilimjibu …….alinizungusha nyumba Zote na kunipa maelekezo
Halafu nimesahau naitwa Peace ✌️ napenda amani muda wote kama jina langu wewe unaitwa nani?

Naitwa Joyce nilimjibu....

Waoh jina zuri kama wewe na hii no yangu utanicheki kama kutakuwa na tatizo kipenzi ngoja sie tuwahi masomo...
poa masomo mema...

Nilimaliza kupika nikapakua chakula kwenye ma hotpot nikapeleka mezani nikiwa naanda chakula ndio akina Peace nao wakawa wanarudi nyumbani...
Nilienda kuoga nikavaa nguo zangu nilizokuja nazo
nikawakuta wamekaa sebuleni...

Yani leo tumechelewa sana tulikuwa na discussions nyumba imependeza leo na nasikia harufu nzuri ya chakula twendeni tukale basi kabla hamjaondoka Peace aliongea
Sawa......
Akina kaka wako wapi sijamuona hata mmoja sebuleni?
itakuwa wapo wamelala hata mimi sijawaona.... nilimjibu
Tangulieni mezani ngoja nikawaite napenda chakula cha pamoja ndio kitamu...

Tulielekea mezani mimi na Happy tukakaa kuwasubiri
Vipi kazi zimekuchosha leo? hata hivyo ni leo tu kazi nyingi kesho zitapungua.... Happy aliniuliza
Sio sana japo nimechoka nimefua nguo nyingi mikono inauma sikujua kama kuna mashine ushamba huu πŸ€£πŸ˜‚
Tulijikuta tunacheka tulikatisha kucheka baada ya kuona wanakuja sebuleni …….

Walipakua chakula mimi nikawa wa mwisho tulikula pale huku stori zikienda mimi nilikuwa kimya sina hata cha kuongea yule mkaka mwingine wa pili hata na yeye hakuwa muongeaji sana aliongea mara moja moja na hacheki na wowote...

Akina kaka huyu ndio dada mpya atakuwa anafanya usafi na kuondoka anaishi mbezi.... anaitwa Joyce
Joyce hawa ni kaka zangu wa kwanza ni huyu Gavin , wa pili ni huyu Daniel wa tatu ndio mimi....

Karibu Joyce jisikie upo nyumbani Gavin aliongea kisha akainuka na kuondoka chumbani kwake.

Peace ngoja sisi tuondoke tutaonana kesho yule mama asije akatumeza tumechelewa kurudi nyumbani na hili foleni la dar sijui tutafika saa ngapi...
Happy aliongea.
Sawa, Peace alichukua hela akanishikisha mkononi tukaagana pale tukaondoka zetu .
Nikiwa kwenye gari nikahesabu zile hela nikakuta ni helfu hamsini sikuamini hata kidogo...

Happy huyu dada kakosea kunipa hela nini? nilimuuliza
kwanini unasema kakosea? Amenipa Elfu hamsini nilimjibu
Mbona hiyo ni pesa ndogo sana wewe hela yako kubwa kushika ilikuwa sh ngapi?
pesa kubwa zaidi ilikuwa elfu kumi πŸ˜‚πŸ˜‚
Ndio maana unashangaa hivyo tena ukiishi nae vizuri utakula mema ya nchi hanaga roho mbaya rafiki yangu..

Tulifika nyumbani mida ya saa mbili usiku tulimkuta baba na mama wapo sebuleni wanaangalia TV tuliwasalimia nikawa naelekea chumbani mama akanizuia..
We Joy unaenda wapi hebu njoo hapa leo siku nzima hujakuwepo nyumbani ulikuwa wapi na ndio unarudi sasa hivi saa mbili usiku? mama aliuliza mbele ya baba makusudi ili nishindwe cha kujibu....

SEHEMU YA 07~~08

Kabla sijajibu Happy alidakia tulikuwa wote mama Joy aliniambia kushinda nyumbani peke yake anajisikia vibaya kwahiyo anaomba awe na sehemu ya kupoteza muda mimi nimempeleka sehemu anajifunza jinsi ya kupika keki 🍰 nikitoka chuo nampitia tunarudi wote......

Nilishusha pumzi baada ya Happy kunijibia maana sikuwa na jibu la kujibu
Ohoo wazo zuri sana mabinti zangu sasa πŸ€” ada mmetoa wapi? Baba aliuliza.

Ni rafiki yangu tu baba kwahiyo anamfundisha bure tu Happy alijibu nikamuona mama kabinua mdomo nikajua hapa hajapenda tu ....
Sawa siku nyingine msiwe mnafanya mambo wenyewe kimya kimya muwe mnatoa taarifa baba alimalizia kuongea akainuka kuelekea chumbani na mimi nikaenda chumbani kuweka hela zangu nilizopata.......
Nikawa nimejilaza tu kitandani maana nilikuwa nishashiba tayari, usingizi ulinipitia nilikuja kuamka asubuhi baada ya Happy kunishtua nijiandae tuondoke...

Niliinuka kiuchovu maana nilichoka jana yake baada ya kufanya kazi nyingi, nilijiandaa nikatoka nje kumsubiri nikamkuta mama sebuleni nikamsalimia lakini hakuitikia, sikurudia tena kumsalimia nikanyamaza kimya...
Happy alitoka akamuaga Mama yake lakini mama hakuchangamka nikaona hapa kimenuka....
Tuliondoka aliniacha kazini kwangu yeye akaendelea na safari ya kwenda chuo....

Nilifanya usafi leo kazi hazikuwa nyingi ila nilipata muda wa kupumzika kidogo.....
ilivyofika mchana nikaenda jikoni kupika nilivyomaliza nikatoka nje nikakaa kibarazani kupunga upepo kama kawaida aliwahi kurudi kivuruge Daniel aliwahi kurudi nyumbani akanikuta nimekaa kibarazani...
Alinisalimia akaingia zake ndani baada ya muda akatoka nje akaniita...

Joyce...... nikamuitikia abeh
Wewe si unaelewa vitu vinavyohitajika nyumbani tuongozane nikupele sokoni ukanunue vitu mimi sielewi...
nikamjibu sawa haina shida twende tu ...ile nainuka tuondoke akanizuia kwanza..
Unataka uende hivyo ulivyovaa na nani? yaani kila mtu ajue wewe ni mfanyakazi πŸ™„ hebu kavae vizuri bhana..

Angejua hata hizo nguo nzuri sikuwa nazo nilienda chumba cha kubadilishia nguo πŸ‘— nikajimwagia maji kidogo na hili joto la dar jasho muda wote nikavaa gauni langu nikatoka alivyoniona akanirudisha tena..
Kavue hiyo nguo chukua hata ya Peace uvae unavaaje kishamba hivyo utanitia aibu 😌 nikataka nimuulize tunaenda sokoni au kuna sehemu nyingine tunapitia nikasema mdomo koma.....
Nikaenda kuchukua nguo ya Peace nikavaa huku naogopa ogopa nilivyotoka akatabasamu..

Waoh hapo sasa umependeza tunaweza kwenda alinifungulia mlango wa gari nikaingia na yeye akaingia tukaondoka nikiwa kwenye gari simu yangu iliita kuangalia jina ni mama anapiga simu nilikuwa naona hata aibu kutoa simu mbele ya Daniel maana ilikuwa ni blauzi na sketi nimefunga na kamba kifuniko kisianguke......

Nilipokea nikaweka sikioni kiuoga uoga bahati mbaya ikaangua betri kifuniko kila kitu kwake niliona haya nikainama kuokota hivyo hivyo kishingo upande nikaiunganisha nikaiwasha nikampigia mama simu...

itaendelea

SEHEMU YA 09~~10

Simu iliita akapokea Nilimsalimia mama akaitikia akaniuliza naendeleaje mbona nipo kimya?
Naendelea vizuri mama ila sasa hivi niko bize kidogo nimepata kazi mahali hivyo narudi nyumbani usiku...

Kazi gani hiyo ina maana baba yako ameshindwa hata akupeleke sehemu usomee fani yoyote? mama aliuliza
Ha... hapana mama hadi matokeo yatoke nimeona nisikae bure nifanye kazi nikutumie hata mia mbili una majukumu mengi usijali niko salama halafu mbona unaongea hivyo kinyonge nilimuuliza..
Naumwa homa tu nimelala nimeshindwa kwenda hata kibaruani kwangu ...
Duh pole mama nitakutumia hela ya kwenda hospital baadae nikirudi nyumbani uwe na siku njema nikakata simu.....

Hatimaye tulifika sokoni mahali panaitwa kisutu akanipa hela nikaanza kuhemea vitu, ila ikipungua ananipa nilivyoona vimetosha nikamwambia tayari
tukavipeleka kwenye gari akaniambia naomba no ya mama yako nikamtajia nikaona anaandika andika akaniambia mwambie umemtumia hela...

Nilichukua simu nikampigia mama nikamwambia nimekutumia hela kidogo hapo....
Ngoja niangalie meseji usikate simu mama aliangalia akasema wewe mzima kweli 😁 yaani kwenda Dar sasa hivi laki unaona ni hela kidogo....
Sikuamini nilimuangalia Daniel nikamjibu mama sawa kama imefika baadae niko bize nikakata simu...

Nashukuru sana kaka angu nikataka nimpigie na magoti..
Wewe usinipigie magoti hapa huoni watu wengi unataka tutrendi sasa hivi hapa haya tuondoke muda umeenda..... tuliingia kwenye gari safari ya kurudi nyumbani ikaanza kwenye gari muda wote nikawa namuangalia Daniel kwa kuibia ibia...
Tulifika nyumbani akaingiza gari ndani nikashuka muda huo tulimkuta Gavin asharudi amekaa kibarazani anakunywa wine 🍷 kwenye glasi

Mmetoka wapi sasa hivi πŸ€” Gavin aliuliza
Sokoni kununua chakula nilimjibu nikaenda kwenye buti kutoa vitu nikawa napeleka ndani hadi vikaisha nikaenda kupanga kwenye friji nikawaacha nje wanapiga stori....
Nikiwa ndani akina peace wakawa wamerudi wakanikuta jikoni napanga vitu ..
Nilivyomuona nikashtuka maana nilikuwa nimevaa nguo πŸ‘— yake...
Peace samahani nimevaa nguo yako bila ruhusa yako kaka Daniel aliniambia nivae nguo nzuri twende sokoni...
Usijali kuwa na amani hela yako hii hapa ya leo alichomoa noti ya elfu kumi na kunipa nilipokea nikamshukuru..
Nilienda kuandaa chakula tukaanza kula ili tuondoke

Chakula kitamu Gavin aliongea kila mtu akageuka kumuangalia...
nikasema asante πŸ™
mh hadi Kaka Gavin leo umesifia chakula basi ni kitamu kweli 😁 Peace akavunja ukimya.
alimaliza kula akainuka huyo akaenda zake chumbani sisi tulimaliza kula nikatoa vyombo nikaosha kabisa hao tukaaga zetu tukaondoka...

Vipi umeshazoea kazi? Happy aliniuliza
Ndio nimezoea na nimetokea kuipenda kazi yangu sijui nilikua nachelewa wapi..

Sawa ila mama hajapenda wewe kuwa karibu na mimi na hapendi ukae ukijua hilo na yule mama akiamua kitu hashindwi namfahamu vizuri sana ila usijali nipo pamoja na wewe, wewe ni ndugu yangu no matter what nitakuwa pamoja na wewe ila kufanikiwa ukiwa karibu na mama yangu ni ngumu sana....
Itaemdelea

SEHEMU YA 11~~12

Sikuelewa Happy anamaanisha nini ila nilimjibu sawa nitakuwa makini zaidi najua hanipendi....
basi tulifika home 🏑 mapema sana leo..
nilimsalimia mama kama kawaida yake hakunijibu ilo sikujali sana nikaingia zangu ndani nikachukua simu nikampigia mama ili niongee nae vizuri...

alooh mama shikamoo nilimsalimia, marahaba umeshindaje? aliniuliza.... Nimeshinda salama ndio narudi kazini sasa hivi nimechoka
pole na kazi ila nashukuru kweli umenisevu wewe hela zote umezitoa wapi? usije ukaanza tu mambo ya wanaume mwanangu...
πŸ˜‚πŸ˜‚ nilicheka kidogo mama nawe hizo pesa ni jasho langu bhana mimi nafanya kazi kidogo nitakachopata tutagawana....
mh sawa ila si unaishi vizuri hapo? mama aliuliza
Ndio mama wana upendo sana hata usijali uwe na siku njema nikakata simu...
nikasema ungejua navyopigwa vita kama niko vitani πŸ˜”
nilikaa kidogo nikapitiwa na usingizi, nililala hadi asubuhi . Niliamka nikajiandaa niende zangu kazini
Tulikunywa chai tukaondoka zetu Happy aliniacha yeye akaondoka zake kama kawaida niko mwenyewe nikaanza kufanya zangu usafi...
Nilivyoenda chumbani kwa Daniel kufanya usafi nikakuta kitandani kuna simu na kikaratasi kidogo chenye ujumbe nikachukua nikakisoma..

"Unanitia aibu na kisimu chako tumia hiyo ukipata hela utanipa by Daniel"

Nilijikuta na tabasamu πŸ˜€nikaichukua nikaweka line yangu nikaendelea na kazi zingine....

Nilivyomaliza nilipumzika nikachukua simu nikaanza kuseti vitu huku nikimsubiria Happy aje tuondoke.
Sikuamini kama na mimi natumia smartphone...
Ghafla nikajikuta nimetokea kumkubali sana Daniel baada ya kunionyesha upendo...
Happy alikuja kunichukua tukarudi nyumbani tukiwa tumekaa chumbani Happy akaniona na simu mpya akaniuliza nimetoa wapi ?
Bosi wangu Daniel kaniazima nikipata hela nitampa

Kingine mbona una furaha sana mwenzetu umekutwa na nini niambie na mimi tufurahi wote Happy aliniuliza
Nipo kawaida mbona nikuulize kitu hivi ushawahi kupenda?
mh swali gani tena hilo jamani kila binadamu ana hisia ndio nishawahi kupenda na nina mpenzi pia..
anha sawa
Vipi wewe ushawahi kupenda au umependa nini 🀣?
Nahisi hivyo nimependa ila sidhani kama nina uwezo wa kumwambia Happy..
Kwanini usiweze kumwambia ni nani kwanza huyo nidokeze kidogo...
Mh nitakwambia naona aibu kuongea kwanza msichana kumwambia mwanaume nakupenda ni vibaya Niliongea

Ni kweli ila hisia zina tabia ya kufanana ukiona mtu unamfikiria sana na kumuwaza ujue na yeye anakuwaza kwa wataalamu wanavyosema ila sina hakika ngoja tuone nitamjua tu huyo anayekuumiza kichwa 🀣🀣.
Tulijikuta tunacheka wote tukapiga stori za hapa na pale hadi muda wa kula ulipofika tukaenda kula..

Kesho naweza kuondoka naenda Canada nitakaa huko takribani miezi mitatu kuna kozi tunaenda kujifunza huko baba aliongea alichukua glasi ya maji akanywa kidogo kisha akaendelea kuongea sisi tulibaki tunamsikiliza...

Itaendeleaaaaaa
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

"6~~12" SWEETHEARTπŸ’‹πŸ˜˜ 06 (Ma oxygen yoooooπŸ™Œ)  >>> https://gonga94.com/semajambo/6-12-sweetheart-06-ma-oxygen-yooooo
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest