Mimi nililala zangu kitandani yeye akawa bize na simu yake😴😴😴 nikalala na kupotelea usingizini kabisa😴😴😴 nilishtuka usiku wa manane na kumkuta amelala kwenye sofa🙄sasa si angeenda chumbani kwake🥱kujitia ana care sana🥲nikachukua shuka moja na kumfunika🙆🏻♀️ nikarudi kulala... nikarudi kulala, tumbo lilikuwa linauma ila sio kivile yaani🥱 asubuhi ikafika nikamuamsha na kumwamsha aende kazini buana anabaki kizembe hapo ili iweje,akajiandaa na kuondoka kazini nikabaki mwenyewe.....nikamtafuta braza angu Mustafa tukawa tunapiga stori ananiuliza maisha yangu yanakwendaje nikamjibu hakuna baya,akanisisitiza basi nikae nitulie nimeshapata ridhiki ya ndoa 👌nikaona hapa nishageukwa😹😹😹heri nitulie tu sasa....ila kila nikisema nimpende huyu Hakim siwezi kwanza kumpenda mtu ndo inakuwaje kuwaje,yaani unahisije kuwa unampenda....!!? Kuchanganyikiwa mimi😹😹😹 mbona sihisi chochote najionea yote heri🙌🙌🙌 kila mtu analala chumba chake siwezi kulala nae mimi
Nilipika ile siku mwenyewe na alivyorudi Hakim tukala na kuongea vizuri kabisa,kwanza malumbano yanini jamani😹😹😹ila sikulala nae hiyo siku kila mtu alilala chumbani kwake🤪🤪🤪 ilipofika ijumaa akanambia kuwa alihitaji kwenda mbeya akawape pole familia ya Joel ila anaona inashindikana ataendaga tu maana hata Joel mwenyewe pia bado hana mpango wa kurudi hivyo inabidi tu weekend twende anipeleke maeneo kidogo nikafanye.marekebisho ya nywele 🥱🥱🥱nilikuwa na nywele nature🤣🤣🤣 nikasema mambo ndio kama haya sasa nikaonekane na mimi kuwa niko mjini jamani😂😂😂nikamuitikia tu kwakweli hilo sio kosa mbona🤣🤣🤣
Tulijiandaa siku ya jumamosi na kutoka pale nyumbani mpaka mjini, tulifika saloon moja chini kulikuwa saloon ya kike kisha juu ya kiume maana ilikuwa na kigorofa akanambia mimi niingie ile ya kike nitengeneze nywele akanipa na hela kabisa,nae akaingia ile ya kiume akanambia nikimaliza nimshtue kuwa tayari maana yeye ndio atamaliza kuhudumiwa hiviyo atabaki kunisubiria mimi tu huku akipiga story mbili tatu,basi tukapaki gari nje hapo.....mimi nikaingia ya kike kwenda kuitengenezwa nywele❤️🔥❤️🔥❤️🔥nilipendeza kwakweli nikasema sasa si nifungue moyo nimpende huyu kaka jamani anajali hivyo🥱🥱🥱
Nilimtumia sms Hakim kuwa ni tayari tuondoke sasa,nikatoka njw nikakuta watatu wanachora chora gari na chuma😭yaani waliikwaruza hasira ilinipata nikamkata mmoja wapo wengine wakakimbia nikampiga vibao vitatu🤦🏼♀️mtanisamehe,ghafla mkono wangu ulizuiwa nisiendelee kumpiga yule mtoto,alikuwa ni mkaka mmoja ndiye aliyenishika mkono wangu
"Mbona mnampiga mpwa wangu hivyo kuna tatizo gani?"
"Ebu niachie mkono wee vipi,muulize mwenyewe kanifanya nini..!?"😏 kale katoto kakawa kanalia tu hata alivyomuuliza hakujibu kitu
"Samahani dadangu niambie amefanya nini huyu mtoto? maana mimi ni mjomba ake"
"Kwahiyo kama ni mjomba ake? nimekuuliza?"
"Mbona hauna ustaarabu dada si nimekuuliza kwa wema kabisa"
"Kwahiyo nyinyi ndo wastaarabu kutuma watoto zenu wachore magari ya watu,haya kanichorea gari langu,tena hivi vibao havitoshi bado wale wengine"
"Sawa dadangu wamekuchorea gari lako ni kweli unapaswa upanic lakini sio kufikia kumpiga mtoto hivi,je ukimuumiza ndo gari lako litakuwa limeshakuwa jipya tena? ulishindwa nini kumtaka huyu mtoto kistaarabu kabisa akupeleke kwao kisha uwaeleze kilichotokea wafanye utaratibu wa kurekebisha gari lako?"
"Usinichekeshe weee kaka...! unavyoniona nina huo muda? tena umeniambia wewe ni anko wake?kwa unavyojiona unaweza lipia uharibifu wa hii gari? ebu nipishe bwana,tena huyu mpwa wako na bahati ningemchakaza kisawasawa ili siku ingine akiona vitu vya watu atavipitia kushoto,shenzy...!"
"Aisee sawa dadangu naomba umsamehe huyu mtoto na hao wenzie kwa ajili yangu naomba unipatie mawasiliano yako tujue tunafanyaje kuhusu gari yako,ila sijapenda kabisa kitendo cha kumpiga mtoto sio kitu kizuri, imagine angekua mtoto wako ungeweza fanya hivyo au uone anafanyiwa hivi...ebu kuwa na utu na upendo kwa watoto thamini watoto hata kama sio wako maana mtoto wa mwenzio ni wako pia"
"Nadhani weee kaka ni mhubiri eeeh..! lakini chombo cha sadaka mbona huna?🤔 kwanza kabisa fundisha hawa watoto wengi kuogopa vitu vya watu halafu ndo uje kwangu kuniletea hizo porojo zako kaka upo? by the way sina muda wa kupoteza naomba unipishe niondoe gari" (nilijishaua hapo utasema hata funguo ninazo"🥱🥱🥱
Mara Hakim akawa amefika na yeye.akaniuliza.kuna kipi kinaendelea...!?
"Nimekuta watoto wanachora gari"
"Aaaah...! Hakim vipi? Samahani dogo ameleta utundu tu 🙏🙏🙏ndio dada hapa nimekuta anamuadhibu ,naomba tuwasiliane nifanye utaratibu wa kukarabati" yule kaka alimwambia Hakim,nikashangaa kumbe anajua Hakim....!!!
"Haina shida" alijibu huku anafungua mlango wa gari na kuniambia niingie🥲🙄 nikashangaa mwenyewe mbona hata hajapanic🤣🤣🤣🤣🤣🤣lilinishuka shuuuu..... nikajikuta ni chawa promax😭😭😭
Alikuwa kimya sana hata haniongeleshi,ila sipungukiwi na kitu bhana🤣🤣🤣👌tulifika nyumbani bado yuko kimya ikabidi nimuulize
"Kwani bro kuna tatizo?"🙄
"Nani bro ako Kulthum??"
"wewe hapo🙆🏻♀️yaani tangu tumetoka kule umekuwa serious sana,na vipi kuhusu gari yaani mtu kakuharibia gari lakini hujataka maneno mengi🙄🙌kwahiyo mimi niliyekuja juu kumbe nilikosea...!?''
"Kawaida tu,kulirekebisha sio gharama hivyo,vipi kuhusu wewe mtoto uliyempiga akakufia pale? hujui vifo vipo karibu miaka hii"
"Samahani,mimi tu nilipata hasira😭 unajua siko sawa muda mwingine napata hasira kidogo kutokana na period" nilisingizia period wakati nishamaliza🥱🥱🥱
"Hujamaliza period?
"Nilimaliza jana,ila bado sipo sawa"😔
"Pole,jaribu kurekebisha tabia zako.....ipo siku zitakuja kukusababishia kitu kibaya"
"Nimekuelewa nisamehe bure....ila yule mkaka anakujua nilisikia anataja jina lako....!?"
"Achana nae tu,ila sijapenda hii tabia ya kupiga watoto....nachukia sana", nikaamua nifunge mdomo wangu🤐🤐🤔kuuliza yasonihusu🤐🤐🤐
"Sawa si unisamehe tu jamani"
"Yaani kuomba msamaha huwezi...! Kwanini?"
"Sa unataka nipige na magoti...!"🙄
"Njo ulale chumbani kwangu leo nitakupatia msamaha"
Kheee naijua hiyo🤣🤣🤣🤣🤣yaani niende kabisa chumbani kwake nina wazimu...!?🤣🤣🤣 Tuendeleee kuishi hivi hivi kama mtu na dadake👌👌👌
ITAENDELEAAA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.