Story………………...
Mtunzi……………..Simulizi Za Zooper
WhatsApp……....0748697173
Umri………………...18+
ILIPOISHIA........
Licha ya kazi nyingi alizoambiwa kufanya ila zote alizimaliza kwa wakati na mda huo ulikuwa mda wa yeye kupumzika, Sierra aliingia chumbani kwake na kujilaza kitandani ila mwili wote ulikuwa ukiuma kutoka na viboko alivyopigwa na mama yake mkubwa, alijikuta akitokwa na machozi na kuachia kilio cha chini chini huku akiwaza kwanini ndugu zake wanamchukia bila sababu ya msingi, akiwa ametulia mlango ulifunguliwa na Mama yake mkubwa akiwa kabeba ndoo ya maji na kumwagia pasipo kujali kama yupo kitandani........
ENDELEA.........
Sierra alikulupuka na kushuka kitandani kwa hofu.
"Umekuja kulala hapa!?"
"Kazi zote nimemaliza mama!"
"Nani kakwambia kama kazi zimeisha kwenye hii nyumba?, umeshafagia uwanja!?"
"Ndio tayari nilifagia asubuhi!"
"Kama ulifagia asubuhi sasa ni asubuhi!?"
"Hapana!"
"Toka nje haraka ukafagie uwanja alaaaa!"
Sierra alisogea mlango alipokuwa amesimama ili apite ila alisindikizwa na kofi zito lililomfanya atoe mwano na kukimbilia nje akiwapita Sienna, Maya, Layla na Imelda wakitazama tv.
"Eeee wewe kupigwa kidogo tu unapiga kelele kama unataka kuuliwa?"
"Ndio hapo sasa kanishitua sana huyu mbwa!"
"Na nyie mpunguze kumchukia mwenzenu mbona sioni kosa la Sierra hapo?"
"Nilijua tu lazima umtetee sijui ameshakuloga!"
"Achana naye anajifanya ni mama huruma sana!"
Layla alionekana kuwa na huruma kidogo na Sierra kuliko ndugu zake waliokuwa wakimchukia pasipo kuwa na sababu za msingi.
Sierra alianza kufagia uwanja licha ya kuwa uwanja ulikuwa bado msafi, dakika 10 zilimtosha kabisa kumaliza kufagia na akiwa anaenda kumwaga uchafu alikutana na kijana mmoja aliyekuwa akiishi nyumba ya jirani.
"Mrembo Sierra mambo!"
"Poa!"
Sierra aliweka tabasamu kama vile hamna kilichompa.
"Vipi lile ombi langu sasa Sierra!?"
"Bado nafikiria!"
"Mmmmh huu mwaka wa pili unafikiria tu au kisa sina pesa?, mimi nakupenda kutoka moyoni na ukinikubalia tu nitakufanya uwe bonge la mrembo kila mtu akikuona anasema kweli huyu ndiyo Sierra!"
"Mmmmh lakini....
Sierra alisita kuongea baada ya kukutwa na Mama yake mkubwa.
"Kumbe ndiyo tabia yako hii leo utaenda kunieleza!"
Alishikwa sikio na kuanza kuvutwa na kijana baada ya kuona Sierra anavutwa sikio alimsogelea na kumzuia.
"Tulikuwa tunaongea maongezi ya kawaida tu hamna kibaya tulichokifanya!"
"Wewe kama nani unizuie!?"
"Rafiki wa Sierra!"
"Toka mbele yangu kabra sijakubadilikia sasa ivi!"
Kijana aitwae Logan alisogea pembeni.
"Twende ukanieleze vizuri ndani!"
"Sijafanya chochote mama mkubwa!"
logan alimhurumia Sierra alivyokuwa akivutwa na kuingizwa ndani na baada ya hapo alianza kusikia kelele za Sierra kuchapwa viboko kitu kilichomnyima uvumilivu na kuamua kuingia ndani kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa kike.
"Toka ndani ya nyumba yangu haraka!"
"Sitoki mpaka uache kumpiga Sierra"
Mama Sienna alinyenyua fimbo juu na kutaka kumpiga Sierra ila Logan aliidaka na kuivuta kwa nguvu hali iliyomfanya Mama Sienna au Mama mkubwa wa Sierra ayumbe na kuanguka chini.
"Naona umeamua kuingilia kesi isiyokuhusu kwa ajili tu ya kumtetea malaya wako sasa subiri nikufunze adabu"
Alinyenyuka na kujaribu kumpiga Logan ambaye naye hakutaka kukubali zaidi ya kuanza kupigana naye.
Wakati huo mabinti zake walibaki kwenye mshangao kuona mama yao akipigana na Logan na Sienna aliongea.
"Logan hana ubavu wa kumpiga mama nyie subirini mtaona tu!"
"Ivi unaakili wewe!?, yaani badala ukawaachanishe wewe unafurahia kuona wanapigana alafu ndiyo mkubwa hapa kuliko sisi wote!?"
Layla aliongea lakini Sienna hakuyumbishwa na maneno yake zaidi ya kuendelea kutazama mapigano yalivyokuwa yakiendelea.
Logan alimpiga ngumi ya kwenye kifua Mama Sienna na kumfanya apate mshituko na kuanguka pale pale chini akikishika kifua chake.
"Umemfanya nini Mama mkubwa!?"
Sierra aliongea na kumshangaza Logan!.
"Alikuwa anakupiga angekuuwa huyu!"
Sierra hakutaka kuhangaika zaidi ya kuinama chini kuangalia hali ya Mama yake mkubwa kitu kilichomwacha mdomo wazi Logan.
"Mama mkubwa, Mama mkubwa!"
"Kifua, Kifua, kifua!"
Aliongea kwa kulalamika akiendelea kukishika kifua chake.
"Mama!"
Sienna, Maya, Layla na Imelda nao waliita na kusogea alipokuwa kalala mama yao.
"Mwache usimshike wewe ndiyo sababu!"
Maya aliongea kwa hasira akimzuia Sierra asiendelee kumshika mama yao.
"Kifua, kifua!"
Logan baada ya kuona mambo yameharibika alimsogelea Sierra na kumshika mkono akimtaka wakimbie wote.
"Tuondoke hapa sio pakukaa tena!"
Sierra alitikisa kichwa akikataa kuwa hawezi kuondoka.
"Tuondoke Sierra lasivyo atakuuwa huyu akiamka!"
"Siwezi kwenda mbali na familia yangu!"
"Tumia akili Sierra hii sio familia yako!, familia gani inayokutesa karibu kila siku tuondoke!"
Sierra aligoma na kuusukuma mkono wa Logan na kusogea walipokuwa ndugu zake na Logan baada ya kuona Sierra hataki kuondoka alitoka nje kwa hasira.
"Namsaidia alafu hataki kusaidiwa sawa!"
aliongea na kuondoka tena akiwa na mpango wa kwenda mbali baada ya kusababisha matatizo kwa Mama Sienna.
Huku ndani Mama Sienna alizimia na karibu kila mtu alichanganyikiwa kivyake na kuongea kila neno lililokuwa likija kwenye kinywa chake, lawama zote ziliangukia kwa Sierra aliyeonekana ndiyo sababu ya yote.
"Mama yetu akifa ujiandae kufa na wewe!"
Sienna aliongea kwa uchungu.
"Mimi sihusiki ni Logan!"
"Paaaaaah!"
Maya aliyekuwa karibu yake alimpiga kibao Sierra kilichomfanya akae kimya.
"Funga domo lako kabisa!"
Maya baada ya kuongea aliwambia wasaidizane kumbeba mama yao ili wamuwahishe hospital na Sierra alivyotaka kuwasaidia jicho aliloangaliwa na Sienna lilimfanya asogee pembeni.
"Sierra hana kosa lolote lile mnamuonea tu!"
Layla aliongea.
"Kaa kimya na wewe!"
Sauti kali ya Maya ilimfanya Layla akae kimya.
Walimchukua mama yao na kuondoka naye huku ndani ya nyumba akibaki Sierra aliyekuwa kwenye wakati mgumu na machozi hayakukauka kwenye macho yake, alipiga magoti chini na kumuomba mungu amponye Mama yake mkubwa huko alipo na asikutwe na jambo baya lolote lile.
************************
Tuje kwenye kasili la kifalme, Msafara ulikuwa tayari umeshafika kwenye kubwa kasili la kifalme lililotawaliwa na walinzi pamoja na uzuri wa kipekee, Prince Hayden aliteremka kwenye gari lake na kutembea haraka kuelekea ndani ya kasili la kifalme ila kuna sauti ya juu iliyosikika nyuma yake.
"Simama hapo hapo!"
Prince Hayden alisimama baada ya kuisikia sauti ya Mfalme na kugeuka nyuma kumtazama.
"Kitu gani kilichokwondoa ukweni pasipo kututarifu na wapi ulipokuwa umeenda pasipo kuwa na walinzi!?"
"Kuna kitu mhimu kilichoniondoa na ndicho hicho hicho kilichonifanya nikakitafte pasipo kuwa na walinzi!"
"Ni kitu gani hicho!?"..........ITAENDELEA.
Je? Prince Hayden atawaambia ukweli wote kuhusu Sierra na Mfalme Leo atachakua uamzi gani kama ataambiwa?, sehemu ya nne sio ya kukosa.
Full Tsh 1000, Namba za Malipo 👇👇👇👇
0613083801 HALOPESA JINA JOHN
0748697173 M-PESA JINA JOHN..