*************
@Kila Mtu
💝💝💝💝💝💝💝💝💝💝💝
Nilikuja kushituka! asubuhi mwili wangu ulikuwa unaniuma sana nilipojiangalia miguuni nilikuwa na michirizi ya damu na haikuwa kitandani nilipokuwa jana n nilijikuta sebreni uku mkononi nikiwa nimeshikishwa kikaratasi machozi yalinitoka kuna tukio kama nililihisi ila nilijikaza nikaamua nikisome kile kikaratasi nikabaki nimetoa macho......
"Habari mke wangu mie nimeelekea kazini doctar kaniakikishia kuwa amekutoa mimba ile siku niliongea na simu makusudi ili uweze kula chakula nilichokuletea ili tuweze kufanikisha hili sasa utachagua kuzika au kusafirisha nilishasema siitaji mimba" maneno yalisomeka ivo kwenye kile kikaratasi
Fuuuuuh! nilishusha pumzi kwa hasira na nilipanga zaidi niweze kuelekea nyumbani maisha ya ndoa yalishanishinda kabisa niliamua nitoke nje nikaongee na mlinzi
"Mama la mama mbona ivo unalia shida nini ndugu yangu"
"Halichonifanyia mume wangu sio kitu kizuri ameninywesha dawa ya usingizi na kunitoa ile mimba nillyokuwepo nayo"
"Mmmmh Dada angu hapa hamna ndoa Fanya tu uondoke na nakuongezea hii elfu 50 itakusaidia njiani ila Mimi siamini isaya huyu ndo wakukufanyia hivi"
"Sina hata la kuongea kaka angu nimemuachia Mungu ata nisaidia " niliongea machache niliingia ndani na kujitaharisha kwa safari.
Baada ya dakika thelathini nilitoka ndani tukaagana na mlinzi ambae aliniambia kwa matatizo yangu ata akifukuzwa kazi ni sawa tu alinielekeza kituo cha basi na bei zake baada ya kunielekeza kituo cha mabasi ya mikoani hakika kumbe tulikuwa tukiishi mbezi beach sikuwai kutoka nje toka nimeolewa na isaya hii nilikuwa mara yangu ya kwanza hakika madhari ya mbezi yalikuwa mazuri mno.
Nilipanga gari na kuelekea kijijini kwetu sikujua wangelipokeaje swala hili la Mimi kurudi nyumbani lakini ilinibidi tu kurudi kurejea nyumbani mkataa kwao ni mtumwa
Baada ya masaa yasiyopungua manne niliweza kufanikiwa kufika nyumbani hakika mazingira ya nyumbani yalibadilika kidogo nadhani kwa kuwa nilikaa dar es salaam kwa muda mrefu hii nayo pia ilichangia kuona mabadiliko
Kwa mbali niliweza kumuona mama akipeta mchele alikuwa amekaa juu ya kisturi tabasamu lilichanua usoni mwangu na kujikuta nakimbia kwa furaha
"Woooh mama mko poa lakini wazima nimewakumbuka" hakunijibu alibaki amenikazia macho"mbona umekuja peke yako mwenzako yuko wapi"aliniuliza kwa mshangao
"Kwani mama kuja peke yangu kuna ubaya gani ata ivo uko nitokapo sio kwema mama angu"
"Ebu toka nitolee uchuro apa kijijini unadhani watatuonaje watajua mimi sijakufundisha maisha ya ndoa ndoa ina miezi sita tu usharudi nyumbani"alisema mama kwa hasira
"Mama kwani hapa nyumbani nimeua mpaka msikie nimekufa naona ndo mtalizika na nafsi zenu"niliongea uku machozi yakinitoka
" sawa mwanangu lakini ndoa inaitaji uvumilivu sana sawa uchungu wa mwana aujuaye mzazi niambie kilochokurudisha nyumbani ni kipi unaumwa au mumeo kakufukuza"
"Hapana mama ajanifukuza ila mambo anayonifanyia Mimi sijalizika nayo"
"Sawa ujalizika nayo ndo urudi nyumbani kwanini usitafute njia mbadala wa kuyaweka sawa mpaka ukimbilie nyumbani haya unafikiri baba ako utamueleza nini"
"Sina cha kumueleza lakini mama kila napopata mimba anaitoa kwa njia isiyofaa tena kwa kuniwekea dawa kwenye chakula napoamka asubuhi nakuta ashanitoa mimba na kingine hupenda kuniingilia kinyume na maumbile mbaya zaidi huniletea mpaka wanawake wanaojiuza hiyo haki kweli"
"Isaya huyu mwenye hofu ya Mungu ndo akufanyie mambo hayo kama kweli nadhani hatodiriki kukufata maana atajua umekuja kumdhalilisha ila hakija itakuwa una sababu zako binafsi"
Basi nilikaa pale niliendelea kupiga stori za hapa na pale na mama lakini mpaka inafika saa moja jioni baba hakuweza kurejea nikaamua kumuuliza mama
"Mama baba mbona mpaka sasa ivi hajarudi kutakuwa na shida gani"
"Ata Mimi nashangaa sio kawaida yake navyojua Saa kumi na mbili anakuwa yuko hapa " alisema mama
Gafra! gari nyeusi iliingia taratibu kuangalia ilikuwa gari ya mume wangu isaya nilijikuta naishiwa nguvu kabisa ilisimama kwa muda baada ya dakika tano mlango ulifunguliwa alishuka baba ambae mkononi alikuwa ameshika mifuko mingi iliyokuwa imetuna uso wake dhahiri ulionekana kuwa na furaha akafutatiwa na mume wangu isaya
"Karibu nyumbani ,karibu sana baba pole na majukumu ya kazi"mama alimkaribisha
" asante mama nishapoa tena nilitaka nije kabisa na mke wangu sema majukumu yalikuwa mengi ndo mana katangulia peke yake ata ivo tutarudi wrote"
"Sio mbaya ila Mimi naona mngelala tu mkaondoka kesho kuliko muda huu usiku" alisema mama
"Haina shida tutaondoka kesho ,mama zawadi zako zipo kwenye mifuko baba atakupatia maaana nilikuwepo nae toka saa kumi na moja kabla sijaja huku na akanielekeza unavyovipenda"
"Asante baba angu Mungu akubariki" alisema mama ila moyoni mwangu niliona jinsi gani isaya alivyokuwa anajikosha basi ata kumshitakia kwa baba nikashidwa nikabaki kuacha kama yalivyo,story zikaendelea za hapa na pale hatimaye usiku ukawa mkubwa tukaelekea kulala.
Kesho yake saa kumi na moja tulikuwa ndani ya gari tukirudi dar es salaam kwenye gari hakuna ambae alikuwa akimuongelesha mwenzake inaonekana dhahiri isaya alikasirika kwenda kwetu bila taarifa na sikujua kipi kitatokea tutapofika nyumbani
"nani alikupa ruksa ya kuja kijijini bila taarifa kwa akili yako ulidhani unaweza ukanichafua kwa watu"aliuliza isaya akitegemea maelezo kutoka mwangu lakini hakuambulia chochote niliendelea kukaa kimya tu
" nakuuliza tena ni nani aliyekutuma uje kunichongea kwa wazazi wako u kwa taarifa yako wazazi wako ni masikini hakuna ambaye atakusikializa mbili yule mlinzi kashakuwa marehemu kwa kukupa ruksa ya kuja huku ili kukuonyesha unyama wangu maana bado ujalizika lakini siwezi kukuacha ivi ivi nitakupa adhabu ndogo ambayo ukipona basi ufi tena"
Maneno yake yalinikosesha raha muda huo gari aliliongeza mwendo ikiwa ni saa kumi na mbili na dakika thelathini na moja gafra mkono mmoja aliingiza mfukoni alitoa shilingi mia mbili akaiweka mfuko mwengine alipomaliza zoezi ilo alikanyaga mafuta kwa nguvu zaidi mpaka gari likawa linatembea kama linataka kuama njia.
Akichukua mkanda na kujifunga uku akitabasamu nadhani utaenda kusimulia uko uwendapo nilikuchukua kwa ajiri ya mama angu nadhani hauna shukrani sasa nitakuonyesha kulichomtoa kanga manyoya 'maneno yake yaliendelea kunitisha nilitamani nishuke kwenye gari lakini sikuweza
Nilivyoona hali imezidi kuwa mbaya mwendo umekuwa mkubwa niliamua kufunga mkanda lakini ulikataa nilipoangalia kwa umakini kumbe ile mia mbili hakuweka mfuko mwengine aliweka ile sehemu ya kuchomekea mpaka dhahiri alitaka kunisababishia ajari ili nitokee dirishani ,akati naendelea kutafari gafra..... ...🤔🤔 Nyieeeee....Mambo ni ya motooo.😂 Kwani wewe auogopi Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥.
Jamani comment zenu zikiwa nyingi naleta mwendelezo fasta.