Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

CHANZO NI BOSS 03

1st Aug, 2025 Views 36



ENDELEA....
Mwanzo nilijua Isaac anatania lakini kumbe mwenzangu alidhamilia kukataa, alishikilia msimamo wake na kugoma kabisa kufunga ndoa na mimi na nilivyofika nyumbani mama aliniuliza.
"Mbona mapema tena Olivia au kuna kitu kimetokea kazini!?"
"Nahisi kufa hapa nilipo"
"Ufe kisa!?"
Nilikaa chini nikiwa sina hamu na mama alikaa pembeni yangu na kuniuliza vizuri kipi kilichonikuta.

Mdomo ulikuwa mzito kuongea mbele ya mama kuwa boss alinitaka hivyo nilibaki nikiyauma maneno yangu mbele yake.
"Unajua sikuelewi Olivia, unazunguka na hutaki kuniambia kipi kilichokukuta"
"Nashindwa pakuanzia!"
"Anza vyovyote tu"
"Boss ananitaka"
"Anakutaka kivipi mfanyekazi pamoja au?"
"Hapana sio kufanya kazi pamoja, anataka niwe mtu wake"
"Ebhu ngoja kwanza, boss huyu huyu uliyeenda kwake kwa ajili ya kuanza kazi?"
"Ndio!"
"Kumbe ni mshenzi hivyo?, kama tungejua bora tungeendelea na taratibu za ndoa yako ila hata hivyo hakijaharibika kitu mda bado upo"
"Isaac amekataa na kasema hayupo tayari tena kwa ajili ya ndoa"
"Isaac kakataa!?"
"Ndio"
"Lete simu niongee naye, bora uolewe tu uachane na mambo ya kazi"
Mama alichukua simu yangu na kumpigia Isaac lakini simu haikupokelewa, niliamini Isaac kagoma kuipokea kwakuwa ni namba yangu ndiyo iliyokuwa ikitumika kumpigia hivyo nilimshauri mama abadilishe namba ya simu na ampigie tena.

Alifanya kama nilivyomshauri na kweli Isaac alipokea simu na ndipo mama alipomweleza kile kilichotokea kwa ufupi tu huku baadhi ya mambo akimficha.
"Kama ni hivyo nimekubali lakini sijapenda kwa kile alichokuwa amenifanyia Olivia, sijapenda kabisa"
"Msamehe sana binti yangu unajua ile kazi ilikuwa na mshahara mkubwa ndiyo maana tukashauriana na kuona ni vyema tusitishe kwanza ndoa ili mwenzako apate kazi na baada ya hapo muoane"
"Sawa mama nimekuelewa"
Kupitia Mama, Isaac alikubali hivyo maandalizi tuliyokuwa tumeyasimamisha kwa ajili ya ndoa yetu yalianza upya tena japo maswali yalikuwa mengi kwa baadhi ya ndugu.

Tabasamu lilikuwepo lakini halikuwa lile la kufaana na siku iliyofata mida ya asubuhi niliitwa na mdogo wangu na kuambiwa kuna maasikari wamekuja na wapo nje wananihitaji mimi, nilitoka kwa ajili ya kwenda kuwasikiliza na ndipo nilipopigwa na butwaa kumkuta Chris akiwa nao.
"Ndio huyu hapa, alikuja ofisini kwangu kuomba kazi lakini matokeo yake akanifanyia vulugu na kuharibu document zangu zote za mhimu tena akizimwagia maji kisa tu nimemnyima kazi, nataka anilipe fidia haraka na upesi"
"Nini!?"
"Binti tuondoke"
Asikari mmoja aliongea na kunisogelea na kunishika na mda huo ndugu zangu wote walikuwa tayari wameshatoka nje kushuhudia tukio!.
"Mbona mnamkamata mwanangu kafanya kosa gani?"
"Mtoto wako kaharibu nyaraka za kwenye ofisi ya watu makusudi hivyo tunaondoka naye mtamkuta kituoni"
"Muachieni hajafanya chochote kile"
"Binti tangulia huko"
Niligeuka na kuwatazama ndugu zangu, hakuna hata mmoja aliyekuwa na uwezo wa kuvimbisha kifua mbele ya asikari na kuwazuia ili wasiweze kuondoka na mimi.

Walinichukua na kunipeleke kituoni na baada ya kunifikisha wakaniweka selo.

Iliniuma mno kuwekwa selo pasipo kuwa na kosa lolote lile na ndugu zangu pamoja na Isaac walihangaika kunitoa lakini Chris alitumia nguvu yake ya pesa kuzuia nisitolewe nje, siku mbili zilipita nikiwa selo na ndipo siku ya tatu yake nilipokuja kutolewa na kwenda kukutanishwa na Chris.
Nilimtazama kwa hasira na kutamani kummeza ila ndiyo hivyo sikuwa na uwezo huo.
"Sina mda wa kupoteza kaa kwenye kiti!"
Niliwatazama maasikari waliokuwa wamesimama pembeni yake na kushindwa kuelewa yeye ni nani mpaka awe na uwezo wa kutoa amri mbele ya askari?, sikuwa na namna zaidi ya kutii kwa kukaa kwenye kiti.

Chris alitoa karatasi na kunipatia na kuongea.
"Na uhakika wewe ni msomi mzuri tu, soma kilichoandikwa hapo na utie saini ili uwe huru"
Niliichukua karatasi na kuanza kuisoma iliyokuwa imeandikwa kwa maneno ya kiingereza kuanzia mwanzo mpaka mwisho na kubaki kwenye tafakari nzito baada ya kumaliza kuisoma.
"Umekubaliana na matakwa yangu uwe huru au niendelee na kesi yangu!?"
Baada ya kuongea nilijikuta nikipata ujasili wa ajabu mbele yake kwa kuchukua pen iliyokuwa pembeni na kuweka sahihi.
"Safi kabisa, tuonane kesho ofisini"
Baada ya kuongea alitoka nje nje akifatiwa na baadhi ya asikari na asikari mmoja alinisogelea na kuniongelesha kwa sauti ya chini.
"Binti acha kutengeneza vita na watu wazito utaumia bure!"
"Lakini hichi anachonifanyia sio sahihi kabisa afande!"
"Kwani karatasi ilikuwa imeandikwa nini!?"
"Anataka nifanye kazi kwenye kampuni yake bila malipo mpaka pale atakapotosheka ndiyo niwe huru na kingine anataka ndoa yangu nisitishe, yeye ana nguvu gani ya kunizuia mpaka nisiolewe?"
"Fanya kama anavyotaka huna namna"
"Lakini nyie si askari!?"
Hakutaka hata kunijibu zaidi ya kuniambia nijiandae kwa ajili ya kuondoka na ile natoka tu nilikutana na Mama njiani akiwa pamoja na Isaac.
"Wamekuachia!?"
"Ndio mama ila kwa masharti"
"Masharti!?"
Isaac alishangazwa zaidi na kutamani kujua kile nilichokubaliana na Chris kuliko hata mama yangu na nilipowaambia Isaac aliongea kwa hasira.
"Ndoa inafungwa na hakuna kwenda kufanya kazi ya bure alafu tuone atakachokufanya, tuondoke"
Baada ya kuongea alinishika mkono na kuanza kunivuta..........ITAENDELEA.

Full Tsh 1000, Namba ya malipo 👇🏻👇🏻

LIPA NAMBA 67027625 - VODACOM JINA JOHN ELIAS..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CHANZO NI BOSS 03  >>> https://gonga94.com/semajambo/chanzo-ni-boss-03
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest