.............
Weka kwanza Like hapa.......
Usiku huu ulikuwa mrefu sana maana niliwaza kupindukia, kichwa changu kilikuwa na maswali ambayo yalinifanya nikose usingizi. Kila nilipowaza wapi nimekosa sikuona? Suala la kujiua mimi mwenyewe hapo ndipo palikuwa na kikwazo kabisa, hapa ndipo palikuwa pakinichanganya kichwa na kunifanya niwaze mara mbili mbili. Nakumbuka nilikaa kwenye kioo kwa zaidi ya masaa mawili yaani kutoka saa 9 hadi saa 11 alfajiri bado nilikuwa naona sura yangu kwa nyuma, hii ikazidi kunichanganya sana.
Nikiwa mahala hapa pua yangu ilinusa harufu mpya, harufu hii ilikuwa ya ubani ambao ulikuwa unachomwa. Nikataka kujua ni wapi harufu ilikuwa inatoka, taratibu nilijinyanyua katika kitanda kisha nikapiga hatua hadi kwenye mlango na kushika kitasa kisha nikafungua. Hatua yangu ya kwanza ilisimamishwa na sauti ya Sofia ambaye alikuwa mbele yangu.
“Vipi unaenda wapi? Si umetaka vita kaa hapo tukukaange kenge wewe” alisema huku akinitazama usoni.
“Nakuheshimu usitake uniharibie siku, sijui unanisikia?”
“Sasa unataka kufanyaje labda? Unadhani kuna mtu ambaye anaogopa mikwara yako? Mama na kaka wale pale sebureni wanakukaanga mbona utakiona cha moto, humu ndani atoki mtu. Si unataka tuwe masikini sasa utajua hujui” Sofia aliniambia kwa dharau huku akiwa ni mtu ambaye anamaanisha kile alichokuwa anakisema.
Nikatupa macho sebureni, nilimuona mume wangu akiwa uchi wa mnyama huku katikati ya kichwa chake akiwa amewekewa chungu. Ndani ya chungu hichi kulikuwa na moto ambao uliendelea kuchoma ubani.
“Umeona hii ni picha yako, naenda kuweka pale katika ubani. Usipokufa labda sio mimi” Sogia aliniambia kisha alipiga hatua kuelekea sebureni, alipofika aliweka picha yangu katika chungu kisha alitamka maneno kama 40 ya kiarabu lakini ilikuwa ni haraka haraka. Niliweza kusikia jina langu likitajwa ‘Zamda’ ila huko mbeleni sikujua alikuwa amezungumza maneno gani?
Wasiwasi na woga vikazidi kunipanda, mapigo ya moyo yalienda kasi maana mimi ndio naenda kupoteza maisha na sio kama ambavyo nilikuwa nimepanga. Machozi yakaanza kunindoka ila sijui nilipata wapi nguvu nikamtazama Sofia na Mama yake kisha nikasema
“Hakuna ambaye yupo juu ya Mungu, hakuna kabisa. Nitashinda hii vita na lazima mfirisike” maneno yangu haya yalinipa imani kubwa sana maana wanasema imani inaponya nami niliimani hivyo
Nkarudi tena ndani na kujitazama katika kioo kilianza kuhisi kama uso wangu ulikuwa na magamba hivi yaani mtu wa nyuma yangu ndio alikuwa anaonekana hivyo. Yalikuwa ni magamba meupe kama ya nyoka, huyu wa mbele yangu ambaye ni mimi mwenyewe original sikuwa hivyo ‘Mh! Nitakuwa nimekosea wapi sasa? Kuna nini kinaendelea au nirudi tena kwa mganga? Hapana kwakuwa alinipa siku nne acha nione usiku wa leo itakuwaje” Nilisema kwa sauti ya chini hivi kisha nilirudi tena kitandani.
Maswali na mawazo mengi hayakuacha kunisumbua, moyoni nikajiambia kwamba natakiwa kujipa siku moja mbele yaani usiku wa siku hii mpya basi niamke halafu niangalie nini kitatokea. Niliona wazo hili kidogo ni nzuri kwakuwa nilidhani labda jana ilikuwa ni mawenge tu. Kuhusu kile ambacho kilikuwa kinaendelea sebureni sikutaka kukiwaza sana maana kingenipa mawazo na mwisho ningekufa kwa woga wakati nilitakiwa kupambania uhai wa mtu wangu wa muhimu yaani Debora. Basi asubuhi ilipotia nanga kama kawaida, nilijiamsha na kubeba nguo zangu kisha huyo niliondoka kuelekea kwa Debora.
Sikutaka kuoga pale nyumbani, kula wala kupiga mswaki maana nilikuwa na wasiwasi mno, kina Sofia walibaki kuniangalia tu jinsi ambavyo nilikuwa naondoka zangu. Walijaribu kunisemesha lakini hakuna hata mmoja ambaye nilidiliki kumjibu, sikutaka kufanya nao mazungumzo kwakuwa tayari nilishaona dalili mbaya hivyo hasira zilikuwa zikiniendesha mno. Nao waliishia kunipa msonyo wa umbea ‘Mfyuuuuuuuuuuuuu marehemu huyo, ona anavyonuka sasa’ alisema Sofia lakini sikujali wala nini? nilitoka pasi kujibu dharau zake.
Nakumbuka nilifika kwa Debora kama saa tatu hivi asubuhi, nilijiandalia chai yangu kama ilivyokuwa kawaida kisha nikakaa katika sofa pale sebureni na kuanza kupangilia mambo yangu. Nikiwa mahala hapa, kiganja changu cha mkono wa kulia kilianza kuniwasha mno. Nilijikuta najikuna, nikajikuna. Sikujua ni kwaninni ulikuwa ukiniwasha kiasi kile, kwangu nikachukulia kawaida kama ambavyo mtu anayekaribia kupata pesa inavyokuwa. Kwahiyo, nikaimani kwamba huenda kungekuwa na pesa huko mbeleni.
Kiganja kiliniwasha kama masaa mawili hivi hali ambayo haikuwa kawaida kabisa, ni kama nilikuwa naoneshwa ishara ya jambo fulani katika maisha yangu lakini sikuwa nafahamu lolote lile ambalo lilikuwa likiendelea. Nikaendelea na mambo yangu hadi ilipofika mchana ambapo nilipika na kula kisha jioni ilipoingia niliona ndio muda wa kujirudisha nyumbani.
Nikiwa njiani nikiendelea kutembea nilikuwa ni mtu wa mawazo sana hali ambayo ilinifanya nigongane na Mzee mmoja hivi, alikuwa amevaa kanzu pamoja na kibarakashia pamoja na mkongojo ambao ulikuwa ukimpa nguvu. Hakuna na muonekano wa Mzee wa mjini maana kazu lake lilikuwa na viraka kupilitiza hata viatu ‘yeboyebo’ alizokavaa ni zile za miaka ya 2000. Kama ungebahatika kukutana na Mzee huyu basi ungetambua alikuwa amezaliwa katika nyakati za vita ya kwanza ya dunia maana alikuwa Mzee na umri wake haukupungua miaka 100. Meno katika mdomo wake ungeyatafuta kwa shida ingawaje alikuwa na fizi ambazo zimekomaa.
Baada ya kugongana mwenzangu alikosa nguvu na kudondoka chini huku Mkongojo wake ukienda mbali kidogo. Haraka nilirudi katika hali yangu ya kawaida na kumsaidia huyu Mzee kisha nikaokota Mkongojo na kumpatia.
“Samahani babu! Samahani” nilisema huku nikimtazama usoni na kuanza kumvuta mavumbi.
“Usijali! Asante” Mzee alisema na kuanza kuondoka.
Nilijiona mkosefu sana, kwanini nimekuwa napoteza umakini hadi sitazami mbele. Nilijichukia kwakweli lakini ningefanyaje kama nilikuwa ni mtu mwenye msongo wa mawazo. Baada ya kuona Mzee anatembea vizuri, nilianza kuondoka na mimi lakini nilipopiga hatua kama nne hivi. Niligeuka na kumtazama yule Mzee, nilishangaa kwanini naye alikuwa akinitazama. Utazamaji wake haukuwa wa kawaida mno, ni kama kuna kitu ambacho alikiona katika mwili wangu.
“Babu kuna chochote kile umesahau au kimepotea?” nilisema huku nikiwa naendelea kumtazama. Mzee alipiga hatua hadi karibu yangu, akashika kiganja changu cha mkono wa kulia na kunusu. Akasema
“Umetoka kuosha maiti?” lilikuwa ni swlai ambalo sikulitarajia wala kujua kwanini huyu Mzee alikuwa ameniuliza hili swali.
Nikabaki namshangaa pasi kujibu hadi pale ambapo aliniuliza kwa mara ya pili huku muundo wa swali ukiwa ni uleule.
“Umetoka kuosha maiti?”
“Hapana, kwanini?”
“Unanuka kama mfu! Unanuka sana au itakuwa unakaribia kufa. Unaishi wapi binti?” Mzee aliniuliza
“Hapo shangani, hapo tu” nilijibu lakini kwa kutetemeka mno.
Mzee kanitazama kwa muda kidogo huku akiruhusu kimya kichukue nafasi, nami nilikuwa ni mtu ambaye nimechanganikiwa sana. Kuambiwa kwamba nanuka kama mfu alikuwa suala la mchezo kwakweli, lilikuwa ni suala ambalo lilinichanganya sana lakini yule Mzee alisema.
“Umeshawekwa katika kikaangao, ukikanyaga ardhi ya nyumba yako tu. Basi unapoteza uhai”
“Unamaanisha nini?”
“Usiende nyumbani kwako kama unataka uwe hai”
“Babu mbona sielewi”
“Kuna kitu uliambia ufanye ila umekosea masharti. Nitakuelekeza namna ya kufanya naomba unifuate” Aliongea yule Mzee.
“Unataka kunipeleka wapi?”
“Duniani ili uishi kwa amani vinginevyo utakufa. Sasa chaguo ni lako” Mzee alijibu kisha akaanza kupiga hatua kadhaa
Kufikia hapa nikawa nimezidi kuchanganikiwa mno maana sikujua inakuwaje, nikamtazama yule Mzee ambaye aliniambia nimfuate. Akili ikaniambia nisimfuate huenda ametumwa ni mamlki kwanza nimekutana naye njiani kwanini nijifanye kuwamini? Nilijikuta napiga hatua za kinyume nyuma lakini miguu kama ilikataa hivi, ilitaka nimfuate yule Mzee ambaye alishaanza kuniacha kitambo kidogo.
Sasa nikatamani kumfuata lakini swali lilikuwa mbele yangu kama namfuata ananipeleka wapi? Huyu mzee ni nani? Je kama aniniua huko ninakoenda itakuwaje? Lakini mwisho niliona hata ninachojiuliza hakina maana kwa sababu kama watu ambao nawaamini na kuwapenda wanataka kuniua, kwanini nisimwamini huyu aliyenipa taadhari ya kifo huku akiwa anafahamu maisha yangu pasi hata kumwambia.
Nilijikuta napiga hatua na kumkimbilia yule Mzee hadi nilipofika na niliongozane naye pasi kujua tunakwenda wapi? Yeye akiwa mbele mimi niko nyuma yake, alianza kuniongelesha.
“Ulipoenda kwa mganga alikuambia kitu gani?”
“Nitangulize mguu wa kulia wakati naingia ndani kwangu”
“Nawe ulifanya hivyo?”
“Ndio, nilifanya hivyo”
“Sio kweli”
“Kweli Mzee wangu, na umejuaje kama mimi nilienda kwa mganga?”
“Unapambana na mtu hatari sana, licha ya kuwa na uchawi wa mganga lakini pia Mama yake ni mchawi” Mzee aliniambia
Majibu yake yakazidi kunipa maswali mno yaani amejuaje maana hakukuwa na utofauti wowote baina yake na Mganga, hakukuwa na utofauti kabisa. Kwanza sikuwahi kumuona katika maisha yangu yote zaidi ya hii siku tena kwa bahati mbaya tu, sikuwahi hata kusikia ama kujua kama kulikuwa na Mganga katika maeneo haya ya karibu ama hapa Mtwara mjini hali ambayo ilinifanya nitake kujua mengi kutoka kwa huyu Mzee. Nikamuuliza
“Kwahiyo unamjua hadi Mama yake?”
“Wachawi huwa wanajulika”
“Umejuaje?”
“Ukiona nyani ameishi miaka mingi?”
“Amekwepa mishale mingi”
“Ndio sababu, ebu nipe kiganja chako” Mzee alisema huku akisimama.
Ilibidi na mimi nisimame kisha nikampatia kiganja changu cha mkono wa kulia, alishika akakitazama kwa sekunde kama 13 hivi kisha alitoa nyusi moja katika eneo la jicho lake na kuweka kwenye kiganja changu kisha akasema
“Fumba macho, hesabu hadi tatu halafu fumbua na utazame katika kiganja chako” nilifanya kama alivyoniambia kwa kufumba macho kisha nilihesabu hadi tatu kisha nikafumbua macho lakini nilichokakiona katika kiganja ilikuwa ni tukio la kuingia nyumbani kwangu kwa mara ya kwanza wakati natokea kwa mganga.
“Kumbe ilikuwa mguu wa kushoto?” nilisema kwa kutahamaki
“Ndio sababu umeshindwa kufanikisha kile ambacho umetumwa, una bahati umekutana na mimi. Tuendelee na safari” Mzee aliniambia na tukaanza safari nyingine
Tukiwa tunatembea nilikuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana, nilitaka kumfahamu huyu Mzee ni nani? Kwanini nikutane naye na ajue mambo yangu tena kwa mara ya kwanza tu. Nikajikuta namuuliza maswali ya wewe ni nani? Umenijuaje na mambo mengine mengi lakini hata hakudiliki kunijibu hadi tulipofika nyumbani kwake maeneo ya Magomeni kwenye majira ya saa mbili usiku.
Kiza kilitupokea mara baada ya kuingia katika nyumba hii ambayo ilikuwa imejitenga na mji kabisa utadhani alikuwa akiishi mtu ambaye hakuwa na mawasiliano mazuri na watu. Baada ya kuingia ndani aliwasha kibatari chake ambacho kilikuwa juu ya ndoa pale sebureni sijui ndio ukumbini mnaita wenyewe. Mwanga ukatanda na kufanikiwa kukifukuza kiza chote. Mbele yangu nikakutana na matunguli mengi ambayo yalikuwa yakining’inia katika fito pamoja na mengine ambayo yalikuwa kwenye pembe mbalimbali.
Nikatazama mlangoni, niliona pembe kubwa ya Nyati ikiwa mahala pale ikining’inia juu ya mlango huku kwa chini kukiwa na ndumba ambayo sikujua ilikuwa inafanya kazi gani ila nilihisi huenda ilikuwa ya ulinzi wake binafsi. Kwa muda mfupi tu ambao nilikaa katika nyumba hii nilijipa jibu kwamba huenda huyu Mzee alikuwa ni mganga na si vinginevyo na amepanga kunisaidia.
“Kaa chini” Mzee alisema huku akitandika mkeka ambao ulikuwa umechoka haswa.
“Mh! Lakini hujaniambia wewe ni nani?”
“Usalama wa maisha yako na mtu ambaye unataka apone ni muhimu sana kuliko kunifahamu mimi ni nani?”
“Kwanini usiniambie wewe ni nani?”
“Haha! Nitakuambia ngoja kwanza nikufanyie dawa hizi hapa” Mzee alisema.
Basi kilichofuata ilikuwa ni mimi kukubali kukaa chini, nilimuona Mzee akija na ungo ambayo ilikuwa na matunguli mbalimbali pamoja wembe mpya. Aliweka chini ungo kisha akashika wembe na kuanza kuniweka chale katika unyayo na kiganja cha mkono wa kulia. Alipaka dawa ambayo alitoka katika tunguli katika kila sehemu ambayo alikuwa ameweka chela, sikufahamu ilikuwa ni dawa gani ila baada ya kupaka nilitokwa na vitu vyeusi katika miguu hasa unyayo. Nilishangaa ni nini hivi maana vilikuwa vikitembea kuelekea katika ndumba ambayo ilikuwa katika pembe.
“Leo asubuhi mkono umekuwasha sana?” aliniuliza Mzee
“Ndio”
“Unajua kwanini?”
“Hapana”
“Hujakamilisha ulichotumwa na unajua kwanini?”
“Nilikosea masharti”
“Hilo moja lakini lingine unalijua?”
“Hapana” Nilijibu na Mzee alikaa kimya huku akiangalia vidudu ambavyo viliendelea kutoka ndani ya mwili wangu huku vikitoa harufu mno mithili ya mzoga hivi.
“Umewaambia maadui zako kwamba kuna nini unakifanya? Unapowinda hupaswi kupiga kelele, kaa kimya hadi pale utakapopata nyama ndio ushangilie” Mzee aliniambia
Nikakumbuka jinsi ambavyo nilikuwa narumbana na Sofia kuhusu kumuua, hapa nikaona kabisa kweli nilikuwa nimekosea maana nilifanya mambo kitoto sana. Nikajiapiza kwamba sitasema lolote lile kuanzia hivi sasa. Basi, niliendelea kuvitazama vile vitu hadi vilivyotoka vyote ndani ya mwili wangu, nikajiona mwepesi kupita maelezo. Mzee alinipa kioo akasema
“Tazama hivi sasa kuna sura ya nani?” macho yangu yakatua katika kioo kile, safari hii nilimuona Mama Mkwe akiwa nyuma yangu.
“Mama mkwe”
“Huyo ndio unapaswa kwenda kuchoma kivuli chake patakapo pambazuka” alikaa kimya na kunitazama kisha akaendelea.
“Kesho saa sita kamili mchana yaani usizidishe wala kupunguza ndio unatakuwa kufanya hili ambalo nimekuambia”
“Kuna kingine tofauti na hicho?”
“Kingine ni kwamba hakikisha mguu wa kulia unakuwa wa kwanza kutanguliza kisha unachoma kivuli chake mara tatu. Umenisikia”
“Ndio Mzee!”
“Sawa unaweza kulala sasa” aliniambia, nami nililala mahala pale huku nikisubiri kupambazuke ili niwahi nyumbani kufanya kile ambacho nilikuwa nimeambiwa. Nisikudanganye usiku huu ulikuwa ndio miongoni mwa usiku mtamu katika maisha yangu kwani sikuwahi kuota ndoto mbaya wala kuwa mzito kama ilivuokuwa hapo kabla….Weka Like yako hapo chini
Nunua kwa pesa uliyokuwa nayo, usiache kulipia kiwango chochote maana ndio uwezo wako. Njoo WhatsApp, namba ni 0717255498..