... nikamuuliza unafanya nini hapo alikimbia ndani nilimfuata hadi ndani na kumwambia ukome hiyo tabia, baada ya miaka miwili mimi na sakina tulikuwa na mtoto mmoja lakini mimba aliipata wakati ule mimi nipo kwenye usimamizi wa ujenzi, na mtoto alikuwa ni wakiume ambaye kwa sasa ndio sadiki, mimi kama baba nilimpenda sana mwanangu sadiki sababu yeye pekee ndio mtoto wa kiume, lakini kwa mke mkubwa wote ni watoto wa kike na wapo wawili jumla nina watoto watatu,
Baada ya muda mrefu kuwa nimempangishia sakina nikaona ni vyema sakina nimjengee nyumba, kweli nikafanikiwa kumjengea nyumba lakini ilikuwa ni ndogo, nilipokamilisha kumjengea nyumba sakina hakushukuru bali alisema nyumba ni ndogo na anataka nyumba kubwa kama ile iliyopo kwa mke mkubwa, kwakweli sikuelewa malengo ya sakina sababu nyumba nimemjengea na inatosha kabisa kuishi sababu yeye hakuwa na familia kubwa, siku zilivyozidi kwenda nikajikuta naanza ugomvi na sakina sababu anataka nyumba kubwa,
Lakini yule mke wangu mkubwa alianza kuugua ghafla homa ambazo hata hazieleweki nimemuuguza mwisho akafariki, baada ya kufariki mke wangu mkubwa. sakina akanishauri tuhamie wote kwenye nyumba ambayo alikuwa anaishi mke wangu mkubwa, nilimkatalia lakini akawa amelazimisha hadi tukahamia,
Mimi wakati huo nilikuwa mwanasheria lakini pia nilikuwa mhandisi (Engineer) kwahiyo nilikuwa napewa kazi za kusimamia mambo ya ujenzi ndani ya nchi kwenye miladi mbalimbali nimefanya kazi hadi nikateuliwa kuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa ikulu, baada ya kuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa jengo la ikulu hapo ndipo maisha yalizidi kubadirika, nikaanza kuwa na pesa kuliko mwanzo. nilisimamia ujenzi hadi ukakamilika kwa wakati sahihi, kutokana na ufanyaji kazi wangu kuwa mzuri na wakati huo nilikuwa mwanasheria mzuri, Mhe. Raisi alipendezwa na ufanyaji kazi wangu hivyo akaniteua kuwa mwanasheria ndani ya ikulu na kunipatia mamlaka ya kuwa msimamizi wa kila kitu pale ikulu, hapo ndipo nilifanya na wizi wa kuiba zile pesa, lakini wakati huo mpango wa kuiba pesa tulikuwa wengi lakini wengine wote niliwasingizia kesi na wengine kuwaua,
Maisha yakaendelea baada ya mimi kustaafu sakina akawa ameomba nimfungulie biashara, ndio nikawa nimemfungulia ile hoteli ya kifahari, lakini jinsi ninavyomjua sakina ni mwanamke mwenye tamaa sana ya kuwa na mali, hata wewe naamini alikuwa anakutumia ili akamilishe mambo yake na hadi kufikia sasa atakuwa tayari amekutumia vya kutosha na hana tena mpango na wewe. Mwisho Wa Ku Nukuu.
Mzee alipomaliza kuongea akaniambia kama nina ukweli kuhusu sakina niseme ili anisaidie kutoka pale kituo cha polisi, Ilibidi nimwambie ukweli wa kila kitu jinsi nilivyokutana na sakina hadi kuanza kumfanyia biashara zake pamoja na zile pesa alizokuwa analeta, Nilisema ukweli wote lakini sikumwambia kama sijawahi kulala na sakina maana niliona mzee hawezi kuniamini kwenye hilo,
Tulipomaliza kuongea mzee akaniambia nikubali sakina anipeleke mahakamani harafu yeye atanitafutia mwanasheria wa kuja kunitetea na sakina atageuziwa kesi, Lakini mzee wakati anataka kutoka akaniambia niachane na tina pamoja na sakina.
Mzee alipotoka pale kituoni alienda nyumbani kwake na kuwaambia harusi haitafanyika hadi pale kesi itakapo malizika kituoni,
Sakina baada ya kuona harusi ya mwanae inataka kuingia doa, Aliamua kuja kunitoa kituo cha polisi na kufunga kesi, Niliachiwa huru, Lakini sakina alionekana kuwa na hasira na mimi sababu aligundua kwamba nimesha sema kila kitu kwa mume wake, Hivyo uadui ukaanza,
Nilipotoka kituo cha polisi nilienda nyumbani kwangu, lakini nilikaa muda mchache Edina alikuja kunisalimia na kuniuliza mbona siku nyingi huonekani? Nikamwambia kuna matatizo yalinikuta,lakini nitakueleza nikiwa sawa. Nilikaa siku mbili ya tatu niliamka nikiwa naumwa Edina alikuja kuniona na kunikuta homa imenishika nilikuwa na akiba kidogo ya pesa nikamwambia edina achukuwe ile pesa akaninunulie dawa, Edina akaenda kuniletea dawa.
Lakini wakati naumwa Edina alikuwa akinijali sana hadi nikawa najiuliza huyu mdada mbona ananijali sana, Sababu alikuwa akiniletea chakula pamoja na kunichotea maji na kunisafishia ndani, Hadi majirani wakawa wanasema mimi na edina ni wapenzi, Lakini hadi wakati huo wala hatukuwa wapenzi,
Baada ya mwili kuwa sawa kiafya na kazi sina ilibidi nianze kuwa nachukuwa mihogo nyumbani kwao na kina Edina harafu naenda kuuza mjini, Nimepeleka mihogo hadi nikajikuta nimekuwa muuza mihogo lakini ukaribu na Edina ukazidi nikajikuta naanza kumpenda nikaanza kuwaza namna ya kumtongoza,
Lakini wakati huo kule kwa sakina mzee bado hajapanga siku ya harusi, Sakina alianza kumfosi mume wake kuhusu swala la harusi kwa mwanae sababu aliona muda unazidi kwenda, Sakina baada ya kuona mume wake anachelewesha kupanga tarehe ya harusi, Sakina alianza kudai talaka ili waachane na yule mzee yey aanze maisha yake mwenyewe,
Sakina aliamini maisha ameshayapatia sababu pesa anayo, Sakina alianza kumsumbua mume wake akitaka talaka ili waachane, Sakina alipoona mzee hatoi taraka sakina alianza kumtumia majambazi yule mzee ili wamuue,lakini hawakufanikiwa, Ugomvi wa sakina na mume wake ukawa mkubwa, Sakina alipoona mambo yanazidi kuwa magumu kuhusu kupata talaka, sakina aliamua kwenda mahakamani. Lakini wakati huo ndoa ya tina na sakidi ambaye ni mtoto wa sakina imestopishwa kwanza...
Itaendelea...βπ»
~Daudi~.