Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

‎MTEULE WA KUZIMU ‎SEHEMU6-7 ‎

27th Jul, 2025 Views 19


‎Sehemu ya 07
‎Nesi Tina alielekea mochwari kwa haraka sana. Alipofungua mlango, alishtuka kupita kiasi. Hakuamini alichokiona, akapiga kelele:

‎"Haaaaaa!!!"

‎Alimuona Daktari Mery akiwa ameshika kipande cha nyama ya maiti na kukitumbukiza mdomoni. Sauti ile ya mshangao ikamfikia Mery, na mara moja akashituka; kisu alichokishika kikaanguka chini. Machoni mwake pakatoa mwanga mkali uliomuelekea moja kwa moja Tina, na kumfanya ahisi kuungua usoni. Akili zikamrudia haraka, akaamua kukimbia kabla hajauawa.

‎Mbio zake zilimfikisha hadi kwenye kikao alichotumwa kumuita Mery. Alifika pale akiwa anahema kwa kasi, kijasho chembamba kikimtoka. Mganga mkuu akamuuliza:

‎"Vipi? Tumekutuma kumuita Mery mbona unarudi mwenyewe?"

‎Tina alitaka kujibu, lakini sauti haikutoka kabisa — alikuwa bubu ghafla. Alijaribu kuwaeleza kile alichokiona mochwari kuhusu Mery, lakini hakuweza. Alianguka na kupoteza fahamu, huku damu zikianza kumtoka puani na masikioni. Hali ile iliwashangaza sana waliokuwepo:

‎"Jamani, huyu si tuliye mtuma muda huu tu? Kumetokea nini tena?"

‎Mara ghafla Tina alianza kukoroma. Kila mtu aliamini kuwa alikuwa anakaribia kufa.

‎Pete ya Mery ilitoa mwanga — ishara kuwa kuna ujumbe anatakiwa kuupokea. Baada ya kuusikiliza, alikimbilia haraka kwenye kikao na kuwakuta watu wakiwa wametaharuki.

‎Mganga mkuu alimuuliza:

‎"Mery, mwenzako amepatwa na nini?"

‎"Sifahamu kabisa, Dokta. Kwanini, kuna nini kimempata?"

‎"Tulimtuma akuite, alivyorejea hali ikawa hii."

‎Mery alimsogelea Tina, akamgusa kwa pete yake pasipo mtu yeyote kuona, kisha akamwita kwa sauti ya upole:

‎"Tina... Tina... Tinaa..."

‎Tina alipiga chafya na akazinduka. Damu zikakoma, lakini bado alikuwa katika hali ya kulewa. Alipelekwa wodini na kuwekewa dripu.


‎---

‎Familia ya marehemu Sixbert, kwa kuwa waliamini amefariki, waliuchukua mwili na kuupeleka nyumbani kwa ajili ya mazishi. Maskini, hawakujua kuwa ndugu yao alikuwa bado hai — walichokibeba ni mti wa mgomba, si mwili wa binadamu.

‎Vilio vilitawala nyumbani kwao. Caroline, mwanae wa pekee aliyekuwa mwaka wa kwanza chuoni, alilia sana:

‎"Baba yangu... umeniacha, nani atanisomesha?"

‎Mama Caroline alimbembeleza:

‎"Tumeumbuka mwanangu, nani atakusomesha sasa?"

‎Mzee Sixbert, akiwa bado hai lakini kifungoni katika ulimwengu mwingine, alitamani awaambie hajafa. Lakini hakuweza — alikuwa amekwishaondolewa katika dunia ya kawaida.

‎Baada ya maziko, Mery bado alimshikilia Sixbert hadi walipobaki peke yao makaburini. Akamwambia:

‎"Sahau kuhusu maisha ya dunia. Wewe sasa ni wa kuzimu. Kule kuna maisha mazuri zaidi."

‎Alimshika mkono, wakatokea moja kwa moja kwenye jumba la kifahari la Mery. Jumba hilo lingeweza kuishi watu 30 lakini Mery aliishi peke yake, kwa sababu alihofia siri zake kufichuka. Alimfungia mzee Sixbert katika chumba kimoja, kisha akarudi hospitali.

‎Alipofika hospitalini, alimkuta mgonjwa anapelekwa akiwa mahututi. Akashtuka akidhani labda ni Tina, lakini alipomsogelea akagundua si yeye.

‎Mama wa mgonjwa alianza kumlilia:

‎"Dokta, nisaidie. Sina uwezo wa kumpeleka huko anakotakiwa kufikishwa."

‎Mery alimtazama yule mgonjwa, akaamuru arejeshwe wodini. Kisha alielekea chumba cha madawa, akarudi akiwa na sindano. Sindano ile ilikuwa geresha tu; nguvu halisi zilikuwa kwenye pete yake. Alipomgusa mgonjwa kwa pete ile, hali yake ilibadilika ghafla. Akafumbua macho na kumuita mama yake:

‎"Mama..."

‎Mama yake alifurahi sana. Dokta Mery alimwambia:

‎"Huna haja ya kunishukuru. Ni jukumu letu kuokoa maisha ya binadamu."


‎---

‎Tina akiwa chumbani kwake bado hajazungumza. Alipokuwa akitafakari, mlango ukagongwa. Alipofungua, alikutana uso kwa uso na Mery. Akaanza kutetemeka.

‎Mery akamuuliza:

‎"Unaogopa nini? Si unajifanya upelelezi? Umeshaijua siri yangu. Sasa chagua: unataka kushirikiana nami katika mambo yangu, au leo iwe mwisho wa maisha yako?"

‎♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️

‎SEHEMU YA SABA

‎Baada ya Tina kufungua mlango na kumkuta Daktari Mery mbele yake, alitetemeka sana.

‎Mery akasema:

‎"Unaogopa nini? Si unajitia kimbelembele kwenye mambo yasiyokuhusu?"

‎Tina alitaka kuzungumza, lakini bado hakuweza. Mery aligundua hilo, akanyoosha kidole kwenye mdomo wake. Ghafla Tina akakohoa kidogo, akaanza kuongea kwa sauti ya chini huku akilia:

‎"Nisamehe, dokta. Sitajirudia tena."

‎Mery alitabasamu kisha akasema:

‎"Umechelewa Tina. Umeshaijua siri yangu. Sasa chagua — ushirikiane nami au ufe leo."

‎"Sijakuelewa, Dokta..."

‎"Unataka kueleweshwa? Mimi ni daktari lakini nina majukumu mengine. Na kwa jinsi ulivyo — umbo lako, sura yako — utanifaa sana. Kila mwanaume anakutamani. Nakuuliza tena: uko tayari kuwa nami?"

‎Tina alikunja uso:

‎"Nishirikiane na wewe kula nyama ya watu? Hilo halitawezekana!"

‎Mery alicheka kwa kicheko kikubwa kilichotikisa chumba. Vitu vilianza kudondoka, lakini nje hakusikika sauti. Tina alitetemeka kwa woga.

‎"Najua unachowaza — mimi si jini wala shetani. Ni binadamu kama wewe. Lakini nina nguvu za ajabu. Hebu angalia ukutani."

‎Ukutani, TV iliibuka ghafla. Ilimuonyesha Tina alivyozidiwa pale ofisini hadi Mery alipomsaidia. Kisha ikamuonesha wazazi wake kijijini wakihangaika, wakila matabo. Tina alilia.

‎Mery akasema:

‎"Ndicho kilichonifanya nisikuue. Wangepata shida sana. Nikuulize tena: unapenda kuishi au kufa?"

‎Tina akajibu:

‎"Napenda kuishi ili niwasaidie wazazi wangu."

‎"Sawa. Hebu ondoa godoro kitandani."

‎Tina alipoliondoa, alikuta noti za elfu kumi zimejipanga juu ya chaga. Akashikwa na bumbuazi.

‎"Usishangae. Hizo pesa ni zako. Tumia utakavyo. Tina, sitaki kukuua. Ukijiunga nami, hutajuta. Chochochote utakachopanga, nitakijua mapema. Siri zetu ziishie hapa."

‎Tina akatikisa kichwa kuashiria anaelewa. Mery akaondoka, akimuachia Tina maswali mengi.

‎Tina aliwaza:

‎"Kama nisingepangwa zamu siku ile... haya yasingenikuta. Lakini upande mwingine naona mvuto wa nguvu alizonazo Mery..."

‎Akaamua kuwatumia wazazi wake pesa. Alielekea kwa wakala wa Mpesa.


‎---

‎Wakati huohuo, Mery alipita karibu na nyumba moja na kusikia:

‎"Kwa jina la Yesu, mponye mtu huyu!"

‎Alisimama. Maombi yalikuwa makali. Alikaribia mlango na akaingia bila kugonga:

‎"Acheni ujinga nyinyi! Mtu anapona kwa makelele?"

‎Mmoja aliyekuwa anashika Biblia akamjibu:

‎"Dada, unahitaji adabu. Hapa si makelele, tunamuomba Bwana wa mabwana!"

‎"Nendeni mkatafute gari, tumpeleke hospitali kabla hamjamsababisha kufa!"

‎Walimpeleka mgonjwa hospitali. Baada ya uchunguzi, waligundua utumbo wake umejisokota.

‎Mery akasema:

‎"Mngeendelea na makelele, huyu mtu angekufa."

‎Alimpeleka chumba cha upasuaji. Mganga mkuu Dokta Pita alishangaa kuona faili la rufaa bado ofisini. Akaenda wodini na kumkuta mgonjwa yuko sawa kabisa.

‎"Huyu si tulishampa rufaa?"

‎Nesi akamjibu:

‎"Ndiyo, lakini tulipokutana na Dokta Mery, alituambia arudishwe — na sasa anaongea!"

‎Mama wa mgonjwa alilia kwa furaha. Alimshukuru Daktari Pita, ambaye naye akasema:

‎"Nataka kumuona huyo Mery."


‎---

‎Mery akiwa chumba cha upasuaji, harufu ya damu ikamvutia sana. Akajizuia lakini tamaa ikazidi. Alimdanganya mwenzake:

‎"Kuna dawa muhimu tumewasahau, nenda ulete haraka."

‎Alibaki peke yake...

‎ITAENDELEA...
‎FULL 1000
‎0699286085.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

‎MTEULE WA KUZIMU ‎SEHEMU6-7 ‎  >>> https://gonga94.com/semajambo/mteule-wa-kuzimu-sehemu6-7
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest