Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

MPENZI WA DADA S2 SEHEMU YA 33

27th Jul, 2025 Views 4



MTUNZI RITHA STORIES

WHATSAPP 0763 826152

FB RITHA STORIES &HADITHI ZA RITHA

SONGA NAYO...............

Nilibaki kimya kama dakika mbili huku nikitafakari jibu la kumpa, si mnajua huyu ni boss eeh yaani boss hakataliwi kama vijana wa mtaani boss anakutongoza unamkataa kwa heshima ukijibu hovyo kazi huna.
Basi kwa sauti ya upole iliyojaa utii nikamwambia " aaam Abel naomba sana unisamehe kwani s...." hakusubiri nimalize akanikatisha na kusema.

"It okay nakupitia mda maana nahisi imekuwa mapema sana kwako so take your time nitasubiri"

Nilitabasamu na kuishia kukaa kimya , basi akaniaga na kunipatia elfu 50 madai nitanunua chakula 😏, chakula ninacho na hela nikachukua nikamshukuru na kushuka .

Aliniangalia hadi naingia ndani ndo akageuza na kuondoka, nilifika ndani nikakaa kama mzigo maana kichwa tayr kishapata moto.

Mda ulienda jioni Julie akarudi kutoka kazn na kukuta tayar nimeshapika chakula, basi alioga kisha akaja tukapata chakula pamoja kisha story za hapa na pale zikandelea.

Wakati wote niliongea kama vile niko sawa wala sikutaka kuonesha lolote, na hii ni kwasababu sikutaka kumwambia kilichojili, maana kuna namna Julie huwa anakuwa kama anakaunafki flani hivi.

Basi mda ulienda wakati wa kulala ulipofika niliinuka na kumuacha akiangalia movie, nilipanda kitandani kabla sijalala nikasema niangalie sm kidogo maana mda wote nilikuwa nimeitelekeza.

Kushika nikakuta meseji nyingi tatu zilikuwa zinatoka kwa Shania,mbili za Felix na tatu za boss.

Nilianza kufungua kwa Felix zilikuwa zinasomeka , "Lolah ,I love you and niko tayari kwa lolote lakin si kukukosa please usiukatili moyo wangu." Niliishia kusoma moja tu zingine nikaziruka na kwenda kufungua za Shania.

Meseji ya kwanza alisema " We kima nakupa siku tatu tu uwe umesharudisha penzi langu laa sivyo utanitambua mpuuzi wewe"

Nyingine akasema " kwanza uko wapi?"meseji ya mwisho akasema "kwahiyo unajifanya jeuri kutokujibu meseji zangu?"

Sikutaka kujibu nikaona wananichanganya tu , bila hata kusoma meseji za boss nikaweka sm pembeni na kujifunika shuka nikalala.

Kesho yake asubuhi na mapema niliamka na kujiandaa Kisha nikaenda kazini, sasa bwana ile nimefika ofisini kwangu nilishangaa kukuta nimewekewa maziwa ,sambusa na sausage .

Na pembeni ya hivyo kulikuwa na maua,niliviangalia na kubaki nikijiuliza nani kavileta bila ya mimi kumuagiza, maana sijaongea na mtu yoyote wa ofisini au wa chakula sa hivi vitu vimetoka wapi?.πŸ€”

Taratibu nilisogea na kushika yale maua nikayaangalia nikiwa na lengo la kuona kama kuna karatasi yoyote ,lakini hakukuwa na ujumbe wowote.

Niliwaza mwisho nikakumbuka jana nilitongozwa na boss bila shaka yeye ndo atakuwa ameleta hivi vitu.

Basi nilivuta kiti nikaa na kubaki najiuliza nile au nivirudishe ?,akili ikanambia we kula vitu hivyo unakataaje msosi wewe eeeh πŸ˜€.

Bwanaee mimi ni nani nikaipinge akili yangu , bila kupoteza mda nilisogeza na kukaumua kisha nikaweka maua pembeni na kuanza kazi .

Na sikutaka kumtumia ujumbe sijui nimwambie asante au hivi no yeye si kaamua kucheza mchezo wa kizungu fresh acha niende nae vile anataka.

Haya baada ya kula nilifanya kazi zangu kwa amani kabisa , mda ulisogea ikapita kama saa moja na madakika hivi akaja mkaka ambae yuko ofisi jirani na yangu.

Nilimkaribisha kwa ukarimu kama ilivyo kawaida yangu, kijana alitabasamu na kuvuta kiti akakaa kisha akanambia.

"Mmh naona unaenjoy hapo kitumbo kimejaa ndiiii" nilishangazwa na kauli yake maana sikutegemea kama ataongea vile,kwa mshangao nikamuuliza.

"Vice unamaanisha nini?"

"Oh came on Lolah, unataka kujifanya hujui naongea nini?"

"Vice! kama ningekuwa najua basi nisinge kuuliza ila kwasababu sijui ndo maana nakuuliza"

"Mmmh , sema haya hayo ni mambo ya kike ,iko hivi nimekuja kuchukua file ulilopewa na Meneja"

Sikutaka kujichosha kumuuliza tena nikachukua file na kumpatia,sasa badala apokee na aondoke akabaki amekaa huku akinitolea mimacho.

Nilimshangaa na kumuuliza " we vp mbona umenitolea macho namna hiyo ?"

"Nakuangalia wewe binti unaekuja kutikisa vigogo kwa lugha ya mapenzi "

"Vice, sikuelewi ulikuja kuchukua file una lingine? "

"Aah nilikuja na yote, hivi Lolah unajua nyie wanawake mmebarikiwa sana ? ,yaani mtu unatoka zako nyumbani unafika ofisin unakuta umewekewa chai ya maziwa pure kabisa.

Mh viudambwi udambwi vya kutosha ,kubwa zaidi unawekewa maua ambayo pesa yake ni kodi yangu ya mwezi na bills zote, aaah kweli mlipendelewa."

"Kijana bado sijakuelewa unataka kusema nini haswa,maana naona unajikanyaga kanyaga tu"

"Aaah sina cha kusema mie,ila nikwambie kitu ndugu yangu ,chagua mwanaume huyu mmoja halafu tulia nae .

Ila hii asubuhi unaletewa chai na Mr miraba minne mchana na Mr abel sijui jioni
Chief director, dada utakufa na magonjwa ohoo shauri yako"

Alimaliza kuongea akainuka akitaka kuondoka nikamwambia " Vice! subiri umesema asubuhi na letewa chai na nani??"

" simjui ila wewe unamjua na nisamehe kama nimekosea ila nimeona nikwambie ukweli ,na siku zote anae kuambia ukweli anakupenda, so kazi kwako"

Aliondoka na kuniacha nikijiuliza maswali mengi, ina maana alieniletea chai na maua si Mr Abel !? Na kama si yeye atakuwa nani??.

Kichwa kilikuwa kizito nikashindwa kuelewa ni nani haswa, haraka niliinuka na kumfuata Vice nikamuonesha picha ya Felix kama ni yeye maana tofauti na Felix hakuna mwingine anaeweza kuja ofisini kwangu.

Nilishusha pumzi baada ya kusema ni yeye, kinyonge nilirudi ofisini kwangu na kukaa , kichwani nilijawa na mawazo kwanini Felix ameamua kufikia hatua ya kufanya vitu kama hivi.

Sasa wakati nikiwa katika dimbwi la mawazo, mlango wa ofisi yangu uligongwa nikajiweka sawa na kuruhusu anaegonga kuingia.

Mlango ulifunguliwa akaingia Mr Abel akiwa na uso uliojaa tabasamu, taratibu alipiga hatua hadi nilipo na kunisalimia.

"Hello beautiful "

"Hello boss,karibu sana "

"Asante ,vp umefika sangap maana niliacha ujumbe juu ya meza nikitaka ufike ofisini kwangu mara tu utakapofika"

Alivyosema hivyo niliangaza macho yangu pande zote za meza na kumwambia " sorry sikuona ujumbe wowote "

"Acha zako bhna ,niliuweka mwenyewe na baada yangu hakuna mtu alieingia "

"Kweli boss sijaona ujumbe wowote "

"Okay achana nalo, vp lakini uko poa?"

"Yeah niko poa"

"Vizuri, sasa nimekuja kukuchukua tukapate chai maana mda ndo huu"

"Aaam asante ila tayar nimeshapata chai "

"Lolah unajifunza uongo?"

"No boss ni kweli nimesha kunywa chai"

"Okay, next time kabla hujapata chai au chakula cha mchana nijulishe ili tupate kwa pamoja sawa" niliitikia sawa kisha akainuka na kuondoka.

Baada ya kuondoka niliangalia maua aliyoleta Felix na kujisemea (ni wewe ulietoa ujumbe aliouweka boss , Felix natamani kuwa mbali na wewe maana najua kuwa karibu na wewe kutaniletea matatizo makubwa.)

Niliongea na kuendelea na kazi, mchana ulipofika boss alinifuata tukaenda kupata chakula pamoja kisha tukarudi na kila mmoja akaendelea na kazi.

Taratibu mda ulienda jioni ilipofika nikakusanya vitu vyangu na kutaka kuondoka, mara mlango ukafunguliwa akaingia boss na kunambia.

"Nimekuwahi,aam naomba kutoka na wewe kama hutojali "

"Aaam boss nashukuru sana ila naomba iwe wakati mwingine "

"Why? ,kingine mda wa kazi umeisha unaweza kuniita kwa jina langu "

"Ooh! sawa ila ndo hivyo siwezi kuongozana na wewe leo"

"Kwanini huwezi ,kuna mahali unataka kwenda?"

"No ila nina ugeni nyumbani so lazima niwepo"

"Oooh ! Basi naomba nikurudishe hope hii itakuwa nzuri " nilitaka kukataa ila akanibana mwisho nikaamua kumkubalia ,basi tukatoka kwa kuongozana hadi chini .

Sasa bwana ile tumefika nilishangaa kukuta Felix amesimama kwa kuekegea gari la Mr Abel, nisiwe muongo moyo wangu ulishtuka sana kumuona akiwa pale.

Na sio kuwa pale tu ila namna alivyokuwa ilionesha anakitu, basi Mr Abel aliniangalia na kumgeukia Felix na kusema.

FULL S3 NI 1000 TU , UKITAKA KUMALIZIA S2 NI 800 ZOTE NI 1500.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MPENZI WA DADA S2 SEHEMU YA 33  >>> https://gonga94.com/semajambo/mpenzi-wa-dada-s2-sehemu-ya-33
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest