Nazungumza kwa hisia Sara naomba tukutane juu ya mlima tafadhali saa kumi jioni
Sara anaitikia sawa Omar anakata simu
Nahisi furaha mpaka natetemeka mara nikae Mara nisimame naisevu namba ya Sara Ugandan Queen
.......Jioni
Nawahi kufika juu ya kilima mapema namsubiri Sara nusu saa tangu nikae lakini Sara hajatokezea mpaka nahisi kukata tamaa
Mpaka saa kumi na mbili muda wa chakula tayari nanyunyuka nataka kuteremka kilima namuona mwanamke anakuja kavaa nikabu
nashangaa najiuliza huyu nani anakuja upande wangu anafika karibu anasimama anavua nikabu anasalimia habari Omar
nakasirika anaanza kufoka ulikuepo wapi namkamata mkono Sara nambinya kwa nguvu namsogeza karibu yangu tunatizamana machoni
Sara machozi yanaanza kumtoka namuachia haraka nasema nae kwa upole samahani Sara nilikua nishakata tamaa hutokuja mamaa
Sara analia anataka kuondoka namfata namkumbatia kwa nyuma Sara usiondoke tafadhali nisikilize nakupenda
Sara anafuta machozi anatabasamu halafu anageuka uso kauvaa wa mbuzi kana kwamba hayajamfurahisha niliyomwambia
Unasemaje wewe nilifikiria umeniita kwa jambo muhimu kumbe upuuzi huu umesahau kilicho kuleta chuo
Jicho linanitoka Sara simatakwa yangu moyo umechagua kupenda na umekuona wewe
Sara niamini nakuhitaji katika maisha uwe mama watoto wangu tukaishi Tanzania
Sara anajikaza kisabuni ndani anateketea anaguna hmm mimi sikupendi Omar anageuka anakunja mikono kifuani
Chozi la uchungu linananitoka mwanaume nauliza kwanini
Sara anageuka sikupendi tu anabidua midomo
nahisi mvurugiko wa hisia namkumbatia Sara nambusu kwenye shingo oya ee akili zishahama
Sara anashindwa kushikilia Msimamo wake anaanza kuropoka nakupenda Omar l love you l love you kwa sauti yakunong'ona iliyoregea ya puani nyororo anarudia umo kwa umo kama anapiga msuaki😁
narudi nyuma kidogo namtizama Sara anavyoweweseka
Sara anaita Omar anahisi nyuma yake sipo anageuka namtizama macho nimeyafinya anahisi aibu
nageuaka naanza kutembea naondoka taratibu Sara nanifata mbio ananikumbatia kwa nyuma ya kifua
Omar nakupenda usiondoke analia machozi natabasamu la ushindi
namtizama sara kwa upande nageuka namlaza kifuani nampiga busu la kwenye paji la uso
Tunatafuta sehemu nzuri iliyojificha tunakaa
Ardhi ya Uganda inamilima mengi ndio maana hali ya hewa yake ni baridi
Sara karibuni mtaondoka nasisi tunaanza mitihani pia tutaondoka tutakuwa hatuonani tafadhali tuwe tunawasiliana
Sawa Omar nitakukumbuka sana anatabasamu
Tutaonana disemba kipenzi changu nakuomba ujitunze kwa ajili yangu sawa
Sara anaitikia kwa kichwa halmashauri ya akili yangu haitulii kila nikimtizama Sara inanambia nisipofanya kitu nitamkosa
Namuita Sara anaitikia kama katoto mmm ananyanyua kasura kake kaupole nakatazama nahisi raha
Sara nataka nikuoe kabla sijaondoka kwenda Tanzania
Sara macho yanamtoka Lakini Omar kabla hajamaliza namziba mdomo Sara najua una wasiwasi na wazazi tutafanya siri mpaka tumalize kusoma tutawambia sawa kipenzi
Sara ni mpole sana jumlisha na upendo ninachomwambia anakubali hapindui
Siku ya pili tunaenda kufunga ndoa kwa kadhi Shahidi rafiki yangu ndoa inapitishwa kimyakimya
Kama mnavyojua mwanamke na mwaname wakikaa pamoja hisia haziachi kujileta kati ukizingatia tushahalalisha ndoa
Sara wangu nikamtoa usichana wake nilibembeleza kaka enu mpaka kijasho chembamba kikanitoka Sara anadeka nyie
Ikawa ndio kamchezo ketu tukijiskia kupalilia ndoa tunakodi chumba buheri mpaka nilipomaliza mitihani Safari imewadia usiku wake kucha nimelala na Sara namuaga
Sara analia tu ananisihi nisije kumsahau na wivu ananipa vitisho nikija kugundua una mwanamke mwengine namuua
Mchana nimeshinda nae tunapeana za mwisho mwisho
Siku Sara kalia mpaka macho yamevimba mida ya saa kumi na mbili ndio Safari Sara ananikumbatia kwa nguvu hataki kuniachia
Inabidi niseme nae namuita kwa sauti laini Sara Sara anaitikia abee nampiga busu la wakubwa anatulia
Nitarudi mke wangu niamini kama ningekuwa na nia mbaya nisingekuoa nakutaka nakuhitaji ndio maana nimekuoa
Sara anakuwa mnyonge nataka kupiga hatua nagusa kitasa cha mlango Sara ananikumbatia analia kama kafiwa Omar mume wangu aaah😭
Ananifanya mpaka namimi machozi yananitoka sigeuki nyuma natoka na begi langu
Sara anagaragara analia kama hatolia tena
Tunaondoka na basi tunarudi Tanzania tunafika mpakani tunakaguliwa hati ya kusafiria na kadi ya homa ya manjano
Tunaanza safari mkoa mmoja badala ya mwengine
Narudisha laini yangu ya Tanzania naangalia kwenye Whatsap status kipenzi changu Sara kaweka imoji ya kulia kaandika kuna mtu anakumbukwa
Namtumia kopa naandika mimi pia anajibu mbio unaendeleaje na safari
Vizuri tu kipenzi tuko bukoba Tanzania nawewe unaendeleaje
Sara anaenda mwao mimi sijiskii vizuri najihisi mchovu sana nalala tu
Pole basi pumzika tutazungumza baadae Sara wangu anaitikia sawa anakata simu
Sara anazungumza na shoga ake kaona status anamfanyia mzaha, vipi shoga naona huwezi kujishikilia nani tena huyo au Omar
Sara anaguna hmm Shara mbeya wewe awe nani mwengine ndio yeye
Tunajuana wanawake tukipenda hatuwezi kuvunga kila mtu atajua
Shara anacheka kiasi shogaa angu maana Omar alivyo ungezubaa ningejibebea mimi mrefu anakifua OG chakuzaliwa sichakufanya mazoezi
Ana sura ya kike ya mama yake mweupe ananimaliza sauti yake
Sara anakasirika anamkaripia Shara tafadhali urafiki utaisha sasa Hivi unamsifu bwana wangu mpaka nahisi wivu
Shara anajidai shoga angu mimi nawewe tusigombane kisa bwana utamu
Sara anazima data analala
Siku ya pili anafungua whatsap anaona kimya sijamtumia kitu anakuta text za Shara tu
Hee shoga angu umekuwa na hasira siku hizi ndio kukimbiwa na bwana au kuna jengine
Sara anasunya anaitupa simu kwenye kitanda akili yake kashavurugwa nayeye anamletea ishu za kajamba nani😁
Anaingia bafuni anapiga msuaki anatapika anajinadhifisha anatoka kwenda kutafuta kitafunwa na chai
Anatia mkate na chai kinywani tayari anahisi kutapika
Anarudi chumbani anajiuliza Omar hajanitumia ujumbe ana nini analia kama mtu aloonewa anachukua simu anarekodi audio
Omar mume wangu siwezi kuwa mbali nawe leo moja nahisi kama mwaka napata tabu mimi
Sara anaitwa na mama yake anajifuta machozi haraka anakwenda ukumbini anakutana na ugeni anasalimia mke wa balozi ooh Sara umekuwa sasa
Sara anatabasamu anaamuangalia kwa mshangao huyo mwanamke anajiuliza amaekuja kufanya nini huyu dingi
Mama yake Sara anamkaribisha kinywaji na kitafunwa nimekuja kukualika wewe na Sara kutakuwa na sherehe ya kumpokea mwanetu Yassir anarudi masomini Malaysia
Bi Zena anaitikia kwa bashasha Usijali bi Fatima tutakuja na Sara
Sara anakasirika ndani ya nafsi yake anasema Kwani huyu bibi kaambiwa anitaje
Bi Fatima anamtizama Sara anatabasamu mkamwana wangu asikose Yassir hatanielewa
Sara ndani ya nafsi anachukia mimi simkamwana wako nina mume wangu Omar anakumbuka Hajazungumza nae anaaga anaondoka anaingia chumbani
Anaiwasha simu anatizama whatsap Sijamtafuta kisirani kinamjaa tele anaanza kulia
Da es salaam .....
Nafika dar es Ssalam saa tatu asubuhi miguu imetuvimba kwa safari ya muda mrefu
nachukua bodaboda mpaka bandarini nanunua zawadi za nyumbani
Nakata tiketi ya boti saa sita tunaingia kwenye meli nakaa nje napanda juu
Zanzibar....
Tunafika Zanzibar saa nane kasoro nachukua bajaji mpaka nyumbani mwera
Namkuta bimkubwa kashaandaa mahanjumati mezani
Tunasalimiana na mama yangu ananibusu kwenye paji la uso namimi namkumbatia
Omar mwanangu sihaba alhamdulillah umerudi salama
Bi Jokha ndio jina la mama yangu kwao Mwera mswahili mwenye asili ya kiarabu mama yangu na baba yangu familia zao wengi wanaishi kenya
Baba yangu mzee Salim asili yake mombasa Kenya msomali
Baba yangu rubani anasafiri nchi mbalimbali kwetu pesa ipo lakini mimi ninaishi maisha yakawaida mpaka mtaani nimetungwa jina cha baba sichako jina la umaarufu
Ukiniulizia Omar huenda usinipate kitaani kwetu kuliko jina ilo au Chotara na msomali
Nimezaliwa peke yangu nadeka nyie kwa mama yangu
Ila Bi Jokha kalea watoto wa ndugu zake wengine washaolewa wengine wapo nyumbani bado wanasoma Aisha na Rauhia
Naingia chumbani kwangu natoa simu naweka chaji naingia bafuni nakoga inanijia taswira ya Sara nahisi mvurugiko wa hisia naita Sara ah
Natoka navaa nguo naingia kwenye anga za bimkubwa mezani nakula bimkubwa yupo pembeni
Mara anichambulie samaki anilishe nimewambia nadeka kwa mama yangu raha nyie
Nimeshiba mahanjumati ya kizanzibari mama asante kwa chakula nilikumbuka sana baraka za mikono yako nambusu mama yangu mikono
Naaga naingia chumbani naiwasha simu nakuta miscall 28 jumbe 12 audio 5 video call 3 zote za Sara
Naanza kusikiliza audio 1- Mume wangu mbona kimya
Kusikia naitwa hio mume wangu kwa sauti ya Sara nyororo na ya upole nahisi kusisimka na kangalikuepo karibu kangenitambua ninge kahenya mpaka maji kakaita mma😁
Audio 2- Omar nimekukumbuka mpenzi
Audio 3- unaendeleaje
Audio 4- Omar mbona hunijibu umepatwa na nini, nina wasiwasi mwenzio😒
Audio 5 anazungumza analia Omar mimi siwezi kukaa bila kusikia chochote tafadhali nijibu naumia Omar😭
Nasoma jumbe nahisi raha natabasamu tu jumbe kutoka kwa umpendae zina raha hasa akiwa analalamika amekukumbuka kwa mahaba
Omar mpenzi nakupenda natumai upo salama kipenzi chako nina hofu sijaskia chochote kutoka kwako tafadhali nitoe hofu na mashaka
Hubbi natamani nisikie sauti yako nitulie mchana na usiku umekuwa mrefu nawaza penzi lako tamu sana
Natabasamu nafsini mwangu nasema siuseme Sara wangu umemiss naniliu yangu basi
Jumbe zinaendelea ......
Mme wangu sijisikii vizuri huzuni imetanda moyoni wewe ndio faraja yangu nakupenda Omar
Omar naumwa mwenzio upendo wako kwangu tiba sindano yako inaniponya maradhi yasionekana njoo unipe dozi kutwa mara tatu
Nimechovya buyu la asali yako natamani kurudia tena na tena ladha ya ajabu nimeonja natamani unipe tena niradhi inzi nife kwenye kidonda chako kwa raha nilizoziona
Nasisimka kwa maneno ya Sara mpaka nabadilika mnara unasoma nampigia simu Sara yupo ukumbini anaona simu inatoa muangaza anaangalia jina Omar anaingia chumbani mbio anajikomelea
Anaipokea kwa pupa anatabasamu anaita Omar anasema hamezi mate nimekukumbuka mume wangu kwanini ulikuwa kimya nilikuwa nahofu kipenzi changu mimi natumai upo salama
Namnyamazisha shhhh Sara niko mbali mama punguza vionjo sina pakupunguza upwiru mimi au unataka mali yako nianze kugawa
Sara anakasirika anabadilika hapo igawe uone naikata hio
nacheka sana halafu utanitaka nikesha kuwa mkia butu utapata wapi raha unazozisifia
Sara anahema kwa hasira wivu ushamkaba hafahamu anauliza uko wapi
Namjibu kwa utulivu nipo nyumbani Sara anageuza video call anione
Ananiona nimelala kwenye kitanda anachungulia labda kama ataona kitu nacheka
Namuita Sara mamii usijali uko peke yako unaendeleaje na hali
Sara anaitikia kinyonge machozi yanamtoka mimi sijambo Omar nimekukumbuka rudi analia kwa kwikwi
Nahisi hatia nambembeleza Sara mamii usilie
Sara anazungumza kwa sauti ya kilio Omar nahisi siwezi kukaa mbali nawe
Usijali kipenzi karibuni tutakuwa pamoja vumilia kidogo tu
Sara jicho linamtoka, kidogo miezi sita Omar mimi siwezi nakufata
Macho yananitoka mwanaume siamini anacho kisema Sara
Utafanya nini wazee utawaaga vipi kusema ukweli mimi mwenyewe siwezi kukaa mbali nawe kipindi chote hicho Sara naona nitakuwa chizi
Nitawambia nimepata rafiki wa kizanzibari wazazi wake wameomba nikatembee
natabasamu vizuri mke wangu unaakili sana mashaAllah
namuita kwa sauti fulani hivi Sara ndio anaejua tukiwa zerodistance tunashuka mlima kilimanjaro
Sara anatabasamu ananiita Omar anashusha pumzi anajilaza kitandani ananitizama kwa jicho nyanya
Tunatazamana muda wa dakika nzima bila yoyote kati yetu kusema lolote kimya kinatawala
Navunja ukimya nakupenda Sara nimekumbuka tamu yangu
Sara anajifanya kama anajieka sawa ananambia njoo nikupe
Najikuta nacheka sana asante mke wangu wewe mtamu sana hunishi hamu
Sara hacheki mpaka macho yashambadilika inabidi nifanye kitu cha kumtoa kwenye dimbwi la mawazo
Habibty wangu mzuri nikutumie pesa uje eee
Sara anachangamka sawa mume nitumie anatabasamu
Nakutumia jioni sasa hivi wacha nipumzike nimechoka sana miguu imevimba anampigia picha anamtumia
Sara anamuonea huruma mume wake nije nikukande kipenzi
Njoo unikande miguu yangu mitatu yote imevimba
Sara anacheka sana nakuja nitakufanyia masaji nzuri
Asante kipenzi usiku mwema ulale uniote eee
Sara anacheka nawewe pia nisalimie mguu wako watatu
Nacheka sana tunaagana kwa mabusu Sara haikati simu mimi mpaka napitiwa na usingizi ananiangalia tu
Mekuwa wavivu wa kucomment na kulike namimi naingia uvivu hahah
Simulizi hii muendelezo nishatuma kwenye kurasa
Follow👇👇
Simulizi Za Mpemba OG
0778955701.