Nikama unavyojua ukimaliza shule na Kama unandugu mjini basi lazima uwe na hamu ya kwenda mjini ,ndivyo ilivyokuwa kwangu ,
Naitwa Ismail nimemaliza kidato Cha 4 ila sikufanikiwa kuendelea ndipo dada yangu akawapigia simu wazazi wetu kuwa niende mjini ili nikatafute kazi , nilifurahi Sana maana sikuwahi kufika mjini ndio mala yangu ya kwanza ,
Nilianza safari saa 12 alfajili na kufika daressalam majira ya saa 12 jion , dada alinipokea kwa furaha Sana na Mimi nilifurahi Sana kuliona Jiji la dar ,
Tulifika nyumbani na shemeji alikuwa bado yupo kazini , dada alinipikia chakula tukala tena ilikuwa wali na nyama aisee nilifurahi Sana ,
Shemeji alirudi usiku Kama saa 4 hivi na tukasalimiana nayeye alionesha kufurahi ujio wangu , basi tulipiga story za Kijijini kwetu na muda ulipowadia nikaenda kulala kwenye chumba changu ,
Lakini usiku nilisikia Kama malumbano chumbani kwa dada na shemeji , nikatega sikio kusikiliza vzr , japo nilikuwa sisikii vzr ila nilisikia habari za kupika wali na nyama na ujio wangu bila taarifa ,
Na nikasikia Kofi zito ni dada amepigwa , moyo ukaanza kwenda mbio , nilihisi Kama mkojo unataka kutoka au tumbo la kuhara ,
Itaendelea.