Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘04

1st Aug, 2025 Views 41



Maria akiwa bado anafikiria Liya alimwambia
" Usijisimamishe Kama mshumaa Kama umeimaliza kuongea na simu njoo ubebe vitu.
" Liya unajua sielewi boss Bryan ananiitia Nini
" Sasa si uende ukajue unachoitiwa.
" Hapana namjua vizuri Sana atanifokea na kuniambia maneno mabaya alafu atanifukuza kazi, Bora nijiachishe mwenyewe.
" Basi sawa utatafuta kazi nyingine. Waliendelea kuhamisha vitu Maria akahamia nyumbani kwakina Liya . Malia aliondoka huku akiangalia nyumba yao
Nilipenda Sana nyumba yetu, kumbukumbu zangu zote za tangia utoto naziacha hapa .
" Imeshatoka hata ukilalamika huwezi kuirudisha kwahiyo kubaliaba na ukweli.
" Sawa ,nitafanya kazi Kama punda nipate nyumba yangu nzuri.
" Hicho ulichokiongea ndio Cha maana Tena ufanye zaidi ya punda . Wakitaniana na kucheka .

Kesho yake Bryan alimuita zakia akamuuliza
" Hivi ukifanya nilichokuagiza Jana?
" Kila unachoniagiza huwa nafanya boss.
" Kama huwa unafanya mbona sikumuons Maria?
" Nikimpigia simu nikamwambia akasema anakuja .
" Nope namba zake za simu. Zakia alitaka namba za simu Bryan akaziandika kwenye simu yake na kupiga simu ilianza kuita , zakia alikuwa bado kasimama
" Unasubiri Nini ondoka. Zakia alitoka haraka na kufunga mlango. simu ya maria iliendelea kuita hatimae ilipokelewa
" Halow
" Mmmh naongea na Maria?
" Ndio.
" Jana ulipigiwa simu na zakia akamwambia nakuita na haukuja ulikuwa inamaana gani Ni dharau au? Moja kwa moja Maria alijua Ni Bryan.
" Lakini nilikuwa Nina matatizo ndio maana sikuweza kufika kazini kwa muda wote huo.
" Ukimwambia Nani kuwa una matatizo au unamfikiria hii Ni kazi ya baba yako?
" Huko unampenda Ni mbali Sana Bryan.....
" Subiri uneniita Nani?
" Nimekuita jina lako Bryan.
" Mimi Ni boss wako, haraka nahitaji ufike hapa kazini. Aliongea Bryan kwa ukali.
" Siwezi kuja nimeacha kazi.
" Nilijua kwanza nawezaje kukuomba urudi kazini wewe Ni Nani mpaka nikubembeleze kwanza wanawake wote hamna akili.
" Punguza jazba na uache kutukana wanawake maana hata mama yako Ni mwanamke je nae Ni mjinga? Hilo jibu lilimchefua Bryan.
" Unasemaje wewe binti unaenuka umaskini , unawezaje kumtukana mama yangu , unajua alipo?
" Sijatukana wewe ndio ulietukana.
" Sitakuacha kwa hili Maria utajutia kwa kauli uliyoitamka ya kumtaja mama yangu hii Vita uliyoianzisha Ni Vita Kali Sana . Maria alipoona Bryan anaongea kwa hasira na hataki kumuelewa alikata simu.
" Mungu wangu mkisi gani asubuhi yote hii?
" Nini Tena ?
" Nimeshaingia kwenye Vita na Bryan. Sijui haya maisha yangu yataacha lini kuwa sehemu ya maigizo .
" Achana nae atakupatia wapi.alijibu Liya

Siku hiyo wafanyakazi walipata tabu Sana maana boss alikuwa na hasira Sana kila wakati alikuwa anafoka tu na wafanyakazi Saba aliwafukuza kazi kwa hiyo siku . Jordan kijana alielewa na Bryan baada ya wazazi wake kufariki alifika hotelini na kukuta Hali si shwari, alijaribu kuuliza akaambiwa kila kilichotokea
" Wafanyakazi waliofukuzwa kazi wako wapi?
" Wapo chumba Cha kubadilisha nguo.
" Kawaite. Yule mfanyakazi alienda kuwaita wakaja kukutana na Jordan.
" Hakuna aliefukuzwa kazi hapa kila mmoja arudi kwenye kitengo chake akaendelea na kazi. Wale wafanyakazi walimshukuru na kurudi kuendelea na kazi. Jordan alienda mpaka ofisini kwa Bryan akafungua mlango bila kubisha hodi
" Wewe Ni Nani unaingia bila kupiga hodi? Aliuliza Bryan huku akiwa anaangalia nje kupitia dirishani.
" Kwani una shida gani?
" Oooh kumbe Ni wewe?
" Ndio nilimuona ulivyokuwa unawafukiza kazi wafanyakazi wako Tena bila sababu ya msingi unafikiri Ni busara kufanya hivyo?
" Kuwe na sababu kusiwe na sababu ndio nimeamua .
" Lakini watu hatuendi hivyo kumbuka hii Ni biashara na hauwezi kwenda bila .....
" Jordan sitaki kusikiliza ngonjera zako na Wala sipendi kuingiliwa kwenye Mambo yangu , hii Ni Mali yangu najua jinsi ya kuiendesha.
" Lakini haupo sahihi.... Kabla hajamaliza kuongea Bryan aliondoka kwa hasira
" hivi huyu Ni mtu wa aina gani asietaka kurekebishwa anajiona yupo sahihi kwa kila anachokifanya. Jordan alichukua simu yake na kumpigia baba yake alimueleza kila kitu alichokikuta pale hotelini .
" Ndio hivyo baba Bryan hataki kumsikiliza mtu yoyote .
" Hebu mfyate nyumbani kwake nikimaliza kazi zangu nitakuja .
" Sawa baba. Jordan alitoka pale ofisini kwa Bryan na kuelekea nyumbani kwake . Alipofika aliwaulizia wafanyakazi wake .
Bryan yupo wapi?
" Yupo chumbani kwake amesema hataki kuonana na mtu. Jordan alipandisha ngazi
" Tafadhali mkuu naomba usiende kibarua changu kitaota nyasi. Jordan alimuangalia bila kumjibu Kisha akaendelea kupanda ngazi alipofika kwenye mlango wa chumba Cha Bryan alikuta mlango uko wazi aliingia na kukuta Bryan anakunywa pombe huku alivuta sigara, vipisi vya sigara vilikuwa vimetapakaa chini na chumba kulikuwa kina harufu ya Moshi wa sigara. Jordan alienda kufungua madirisha ili hewa Safi iingie alafu akamsogelea karibu
" Bryan Leo umepatwa na nini? Bryan alivuta sigara na kumpulizia Moshi mzito usoni , Jordan akaanza kukohowa
" umeamua kunifuata mpaka huku ?kuribu tuungane pamoja chukua grass nitatumia chupa. Aliongea Bryan kwa sauti ya kilevi huku akimpa Jordan grass aliyokuwa anatumia . Jordan alitoa chupa za pombe na boksi la sigara akatoka nalo nje ya chumba huku aliita wafanyakazi akampokee. Bryan alilalamika Huku akitaka kunyanyuka
" Mbona unanifanyia hivyo nipe pombe yangu. Baada ya Jordan kupokelewa alirudi akamshika na kumrudishia kitandani.
" Niache bwana
" Umelewa Sana unatakiwa kutulia .
Baada ya Jordan kumbembeleza Sana Bryan alitulia na kulala .baay ya masaa mawili baba yake Jordan alifika nyumbani kwa Bryan akaulizia wafanyakazi
" Bryan na Jordan wako wapi?
" Wapo chumbani kwa boss. Alienda chumbani na kumkuta Bryan kalala na Jordan alikuwa kibarazani akisoma jarida. Baba take alimuona na kumfuata
" oooh baba karibu.
" Asante . Vipi mbona kalala anajisikiaje?
"Amelewa Sana sidhani Kama utaweza kuongea nae.
" Sawa nitakuja kuongea nae kesho , wewe unatakiwa kubaki nae hapa kwaajili ya kumuangalia .
" Sawa . Baba yao aliondoka akawaacha . Usiku Bryan alianza kuweweseka na kuota Ile ndoto ya ajali ya wazazi wake alishituka na kupiga kelele . Jordan alisikua akatoka chumba alichokuwa amelala na kwenda kumuangalia , Bryan alikuwa alikuwa amekaa kitandani huku jasho likiwa linamtoka mithiri ya mtu aliyemwagiwa maji.
" Umepatwa na Nini?
" Ni yeye ndio amesababisha yote haya kwanini alimtaja mama yangu Tena kwa ubaya .

Itaendelea
Saa 10 : 00 jion
Whatsapp 0657171961
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘04  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-04
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest