Nilimuuliza tina kwa nini inakuwa hivi, Tina alianza kulia kisha akatoa simu yake na kunionesha zile picha ambazo nilipiga na yule rafiki yake na sakina... (nilipoziona zile picha nikagundua kumbe ule ulikuwa ni mpango wa sakina ili aniweke mbali na tina)
... Nikajaribu kuongea na tina lakini alionekana kutokunielewa, Tina alianza kuongea huku analia... huna tena cha kunificha kama kunisaliti umenisaliti vya kutosha ulikuwa unanidanganya unafanya kazi ya kuosha magari kumbe una mapenzi ya siri na mwanamke ambaye amekuzidi hadi umri na anakutunza kwa kila kitu, sasa inatosha naomba uniache na maisha yangu kama kunitumia umenitumia sana, na kunichezea umenichezea sana,david ni nini ulikuwa hupati kwangu mbona nilikupenda sana na kukuvumilia wakati wote, nilikubali kuwa na wewe hata wakati huna kitu na niliwakataa wanaume wengi kwa ajili yako lakini kumbe wewe hukujali hisia zangu, sawa wewe endelea na huyo mke wako kizee, lakini mimi na wewe kwa sasa ndio tunaishia hapa sitaki tena kukuona kwenye maisha yangu...
(tina aliongea maneno kwa uchungu na maumivu nilijaribu kumuelewesha kwamba mipango yote imepangwa na sakina ili kutugombanisha,lakini tina hakunielewa)
...mahusiano na wewe yamekufa sahau kila kitu kuhusu mimi, sahau kama ulishawahi kuwa na mahusiano na tina,na kuanzia sasa mimi nina mtu wangu ambaye tayari tumeshapanga kufunga ndoa.
Niliposikia neno (ndoa) kwa hasira nilimpiga kofi tina, Lakini wakati nampiga kofi, Mtoto wa sakina alifika na kusema unampiga mchumba wangu, Tukaanza kupigana ngumi mimi na mtoto wa sakina, Kwakuwa pale ilikuwa ni hoteli ya kifahari na tunaleta fujo, Walikuja polisi haraka na kutukamata mimi na mtoto wa sakina kisha tukapelekwa kituo cha polisi.
Kwakuwa mwenzangu yeye kwao wanapesa alikaa muda mchache pale kituo cha polisi akawa ametoka, Mimi nililala kituo cha polisi siku tatu bila kuelewa kinachoendelea, Mule nilipokuwa nimefungiwa palikuwa ni pachafu sana na ndoo ya kukojolea ipo kwa pembeni kiukweli mazingira ya jela sio rafiki,
Siku ya nne sakina alikuja pale kituo cha polisi na kuanza kuniambia maneno ya kejeri... sasa baby wangu nilikwambia ukaonane na tina lakini wewe ukaenda kuleta fujo kwenye sehemu ya starehe za watu, umeona sasa kilichokukuta, mwenzio tina anakwenda kufunga ndoa, haya mimi na wewe ndoa yetu lini.
Nilichukia na kumtukana sakina, Nikamwambia mwanamke mpumbavu sana wewe, najuta kuwa na wewe katika maisha yangu laiti kama ningelikuwa na bunduki ningekuua kabla jua halijazama. Sakina alicheka na kuniambia umeongeza kosa lingine la kunitukana na kunitishia maisha kwa sasa naamini harusi ya tina utaisikia ukiwa gerezani,
Nikamwambia sawa lakini siku moja dunia itashindwa kuvumilia maovu yako na siku hiyo utatengwa na ulimwengu na utaaibika kwa kila ulichokifanya,
Sakina akasema hiyo siku niliivuka bila alibu na ilishapita lakini kwa sasa mambo yangu naamini yatakuwa sawa.
Inamaana lengo la sakina kunikutanisha na tina alitaka nigombane na tina, harafu ampigie mwanae aje kunifumania ili nilete fujo nikamatwe harafu wao washerehekee harusi bila usumbufu wangu, ndio maana mwanae alikuja kule hotelini.
Niliendelea kukaa mahabusu zaidi ya wiki, Dada yangu Zai akawa amepata taarifa kwamba nimekamatwa nipo kituo cha polisi, Alikuja kuniona na kufanya mazungumzo kama kuna uwezekano wa kulipa, Polisi wakasema hadi mwenye kesi aamue kama atakubali kulipwa sawa,
Dada akajaribu kuongea na sakina lakini sakina alikataa akasema tumlipe milioni mbili sababu nilienda kuleta fujo kwenye hoteli yake ya kifahari, Lakini wakati huo sakina alikuwa kwenye maandalizi ya harusi ya mtoto wake Sadiki.
Siku moja kabla ya harusi sakina alikuja kituo cha polisi mida ya asubuh na kuniambia.. nimepata taarifa kwamba kuna nyumba ulinunua kwa siri, sasa niuzie ile nyumba ili uwe huru vinginevyo hii kesi naipeleka mahakamani, na ukifikishwa mahakamani kiasi cha kulipa kitaongezeka na ukishindwa kulipa unaweza ukafungwa miaka mitano jela, sababu kwenye hoteli yangu ulisababisha uharibifu na kunipotezea wateja.
Nilimwambia kama haya ndio malipo ya kila nilichofanya katika maisha yako sawa, lakini mpango wa kukuuzia nyumba hilo sahau.
Mwanamama sakina akaniambia sawa lakini nakualika kesho kwenye harusi ya mwanangu Sadiki. Aliondoka lakini nikaanza kuwaza kama sakina ameshajuwa kama nina nyumba basi atafanya kila mbinu kuichukuwa nyumba yangu harafu mimi nitaanza upya,!
Siku hiyohiyo mida ya mchana yule mzee ambaye ni mume wa sakina, alikuja pale kituo cha polisi, Polisi walionekana kumuheshimu sana kuliko watu wa kawaida, Mzee aliomba nitolewe kwenye chumba cha mahabusu, Nipelekwe kwenye chumba cha mahojiano, Kweli nikatolewa kisha nikapelekwa kwenye chumba mahojiano,
Nilikaa na mzee huku tumetazamana uso kwa uso, Mzee aliniuliza unataka nini kwenye maisha yangu sababu kila ninachokukataza wewe ndio unachokifanya, nimekukataza kwa mke wangu lakini hukusikia bado unaendelea kuwa karibu na mke wangu, nimekukataza usiwe na ukaribu na mchumba wa kijana wangu lakini hujanielewa hadi umeamua kwenda kumpiga mwanangu na kuleta uharibifu kwenye hoteli ya mke wangu,
Mzee aliongea mengi hadi akaanza kunisimulia jinsi alivyokutana na sakina...
Na Nukuu... nilikuwa katika ujenzi wa jengo la mahakama na katika ujenzi mimi ndio nilikuwa msimamizi mkuu, na wakati huo nilikuwa bado sijaanza kufanya kazi kwenye ikulu ya raisi, lakini katika ujenzi kuna mgahawa nilikuwa napenda sana kwenda kupata chakula ila nilianza kuvutiwa na tabia za sakina sababu alionekana ni msichana mwenye heshima na kujiheshimu, Nilikuwa napenda nikifika kwenye ule mgahawa nihudumiwe na sakina, sababu alikuwa akinitengea chakula na kunikaribisha kwa heshima na upendo, siku zinavyozidi kwenda nikajikuta nimeanza kuzoeana na sakina hatimaye nikamwambia ukweli kwamba nampenda na ninataka nimuoe, lakini kutokana na kwamba nilikuwa namzidi umri ilikuwa ni vigumu kukubali lakini sikuchoka wala sikukata tamaa,
Nikaendelea kumtongoza sakina bila kuchoka huku nampatia pesa ya matumizi, lakini sikuwahi muambia kama nina mwanamke kule nilipotoka, hatimaye sakina akanikubali nikaanza mahusiano na kumuhudumia kila kitu, lakini nikaona sakina bado hajanikubali vizuri, nikahisi huwenda sakina ana mahusiano na mwanaume mwingine, nikachunguza na kugundua kumbe kweli sakina ana mahusiano na mmoja wa wafanyakazi wangu pale kwenye ujenzi,
Nilimwambia yule mfanyakazi aachane na sakina, lakini hakunielewa ilibidi nifanye mpango wa kumpatia kesi, Nakumbuka nilimsingizia ameiba cement mifuko saba, nikaona haitoshi ikabidi nimfukuze na kazi, ila wakati namfukuza kazi kuna pesa yake ya malipo alikuwa anadai lakini mimi sikujali nilimfukuza na kumdhurumu, lakini nilipomfukuza kazi nikawa namuona pale mtaani mara mojamoja mwisho akaondoka yale maeneo, lakini baada ya kuondoka zilipita siku chache sakina akaniambia ana mimba yangu hivyo sikutaka kumtelekeza, ikabidi nimpangishie nyumba, sababu alikuwa analala kwa boss wake, tulipomaliza kazi ya ujenzi niliondoka na sakina hadi huku mjini,
Nilipofika mjini kwakuwa nilikuwa na mke mwingine ambaye ni mke wangu wa ndoa ikabidi sakina nimpangishie nyumba sehemu nyingine bila mke wangu kujuwa, nimeendelea kuishi na sakina mwishowe mke wangu akajuwa kwamba nina mwanamke mwingine, ikawa ugomvi kati ya mke wangu na sakina, maana mke wangu mkubwa alikuwa hatari niongeze mke wa pili, kwakuwa mke wangu ameshagundua kuwa nina mwanamke mwingine ikabidi mambo yote yawe wazi, nikaamuwa kufunga ndoa na sakina,
Maisha yakaendelea lakini sakina alionekana ni mwanamke anayependa sana kwenda kwa waganga, Nakumbuka kuna siku nilimkuta anafukia madude ya ajabu mlangoni huku akiwa uchi kama alivyozaliwa...
STORY NDANI YA STORY.
Itaendelea...βπ»
~Daudi~.