Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MKE ALIYECHUMA NAYE MALK | EP 14.

27th Jul, 2025 Views 3



Garma alimtazama Mayner huku akihema kwa hasira. Kauli ambayo ilikuwa imetolewa dhidi ya Mama yake ilimfanya awe tofauti. Akashika mkanda vyema na kumsogelea. Kilichofuata ni kipigo cha mbwa koko. πŸ‘ŠπŸ”₯

Kilikuwa ni kipigo ambacho kilimfanya Mayner aanze kulia 😭, chozi lake lilimdondoka hata kama alikuwa amesema ukweli. Mama Garma aliendelea kufurahia vile ambavyo Mayner alikuwa akipigwa.

β€œKaka muache! Kama mama ni mchawi, asiseme? Mama yako ndio mchawi! Tena mchawi haswa!” Rasma naye alifoka kwa hasira huku akimsogelea Garma na kutaka kumshika, lakini alisukumwa, akatupwa mbali. 😠🀬

Licha ya kutupwa, aliinuka, akajikung’uta na kuwa imara. Akamtazama kaka yake ambaye aliendelea kumpiga Mayner, akasema:
β€œKaka, unahisi kumpiga huyo ndio suluhisho?”
β€œNawe usiingilie yasiyokuhusu, utauawa!” Mama Garma alidakia.
β€œSiongei na wewe! Uchawi wako ndio umesababisha haya yote,” alimwambia Mama yake.

Kimya kilimpitia Mama Garma ambaye alimtazama mwanawe wa kiume akiendelea kufanya unyanyasaji wa kijinsia kwa Mayner. πŸ’”
β€œKosa langu kwani ni lipi? Nini ni kosa langu?” Mayner aliuliza huku akitaka kujitoa katika mikono ya Garma.
β€œNani ambaye amekuambia uende kwa mganga? Ni nani? Kwahiyo unataka umroge Mama yangu si ndio?” Garma alifoka.
β€œKama mama ndio mchawi je?” Rasma aliuliza kwa hasira.
β€œRasma kelele! Nitakubutua!” Garma alifoka huku akimtazama Mayner ambaye aliuliza:
β€œKwahiyo ndio kosa la kunipiga?”
β€œUsipigwe wewe ni nani?” Mama Garma alidakia kwa jazba mno. Alikuwa akihema kana kwamba anataka kupasuka hivi. 😀😑

β€œKelele na wewe mchawi! Kwahiyo unataka kuniua si ndio? Unataka kuniua nakuuliza! Kama kosa ni kuwa katika mahusiano na mtoto wako si ungesema tu. Ungesema unadhani kwamba ningeshindwa kumuacha? Au nashindwa kufanya hivyo?” Mayner aliyaongea maneno haya huku machozi yakimtoka. 😒

Kilikuwa ni kipindi kigumu kwake. πŸ’” Moyo wake ulipitia maumivu ya mapenzi ambayo hakujua ashike wapi? Huku mwili nao ukipitia maumivu ya kuchapwa. Uso wake ulilowana kwa machozi 😭. Alimtazama Rasma ambaye alikuwa ameshikwa na hasira huku akimtazama Mama yake, akasema:

β€œRasma, niko tayari kuyaanza maisha mapya. Haitajalisha yatakuwaje. Nina imani maisha ambayo naenda kuyaishi yatakuwa ya furaha sana kuliko hata ya kupigwa.”
β€œKwenda pegele wewe! Tazama midomo imekusimama utadhani sangara, mfyuuuuuu!” Mama Garma alisema kisha akametua midomo yake. πŸ™„

β€œMama, hichi ambacho unakifanya hii leo kitakuja kukugharimu. Utakuja kujutia kila jibu ambalo unalisema hivi sasa,” Rasma naye alisema. 😠
β€œKisa huyu mchawi ambaye anataka kumroga Mama yangu au? Kisa huyu? Hakuna laana ya mwanamke mjinga maishani,” alisema Garma.

Mayner aliweka tabasamu 😒, akamtazama Garma kwa sekunde hivi. Macho yake yalikuwa yanadondoka machozi. Aliyafuta kwa mkono wake wa kuume kisha akasema:
β€œMimi ni miongoni mwa wanawake wajinga ambao walikubali kukubadilisha, walikubali kukufanya uwe miongoni mwa wanaume ma-gentle. Kumbuka kuna muda uligoma kabisa kuanzisha kampuni huku akili yako ikiwa kwenye kuajiriwa. Nilikuambia nini? Uliposema huna hela ya mtaji na kampuni inataka kufirisika, niliuza nyumba yangu ya Pasiasi. Nyumba ambayo kila mmoja alinilaumu baada ya kuuza. Niliitoa ile nyumba nikasema basi, kwa kuwa mume wangu nakupenda, acha tuuze hii nyumba ili tukae kwa pamoja.

Mimi ni miongoni mwa wanawake wajinga, sawa. Na nimekubali kwa kila aina ya tusi ambalo Mama yako ametukana kwangu. Lakini mkumbushe kwamba kila kitu ambacho alikuwa anakula humu ndani ni mimi ndiye nilikuwa napika. Kile ambacho kilikuwa kinampeleka chooni basi kilitokana na mimi. Hata nguo zake nilikuwa nafua na kupiga pasi.

Yes, ndio mimi mjinga ambaye nilikuambia mlete Mama nyumbani kutoka Mkuyuni ambako alikuwa anateseka, mlete ili awe sehemu ya furaha yangu. Ni mimi huyo huyo ambaye uliniambia niende Mkuyuni nikamuone Mama, nikamsaidie kazi mbalimbali.

Unakumbuka kama Mama aliumwa sana, unakumbuka hilo? Alitakiwa kuongezewa damu, na sio wewe wala Rasma ambaye alikuwa na damu safi ya kumfaa Mama. Unakumbuka hilo? Ni nani ambaye alikwenda Bugando kutoa damu ya Mama? Leo hii huyo mtu amekuwa mjinga, hana akili na sio sehemu sahihi ya maisha yako.

Nina imani dunia inafunza, inafunza katika wakati sahihi ambao uliuchezea. Kila neno limtokalo kwa mwanamke ambaye analia kisa mapenzi basi tambua kwamba limebeba laana. Na hili ambalo natamka kwako, usitegemee kama litakuacha.

Naondoka hapa, ila kaa ukijua kwamba hutompata mwanamke mwenye mapenzi ya dhati kunizidi. Hutokaa kamwe. Na kila la kheri.” 😭

Aliweka hapa kituo Mayner, lakini machozi yalikuwa yanamtoka. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujilipua kama askari vitani. πŸ’£ Aliamini kwamba lazima akubali ukweli ili aishi kwa amani. Alitambua kwamba kawaida ya ukweli huwa unauma. Alimtazama Rasma kwa sekunde hivi, akasema:

β€œWifi, nenda kachukue nguo zako na zangu tuondoke.”
β€œMnataka kwenda wapi?” aliuliza Mama Garma.
β€œKaa na mtoto wako. Mtafutie mke ambaye wewe unampenda. Sisi wachawi tuache tukarogane.” 😀 Rasma alizungumza kisha aliondoka mahala pale na kuingia katika chumba chake.

Mayner naye aliondoka pia, akaenda chumbani kwake na kuchagua kila kitu. Katika mwili wake kulikuwa na nywele ambazo ziligandana katika nguo. Nywele hizi zilikuwa za kwake pamoja na Rasma, kwa kuwa zilikuwa katika mwili anaoumiliki basi kwa sasa zilihesabika kama za kwake.

Alipofika chumbani alichagua kila kitu ambacho kilikuwa kinamhusu, alichukua muhimu. Kisha alitoka zake nje, lakini alipofika tu mlangoni alikutana na Mama Garma ambaye hata hakutaka kuzungumza. Badala yake, alipeleka mkono katika mwili wa Mayner na kuchukua nywele moja.
β€œNenda mwana kwenda wewe,” alizungumza kwa dharau baada ya kuona amepata kile alichokuwa akikihitaji. πŸ˜‘

Mayner hakutaka kumsemesha, badala yake aliamua kuondoka na kufika sebuleni ambako alikutana na Rasma. Naye alikuwa tayari amejiandaa kwa safari.
β€œNaondoka,” alisema Mayner kumwambia Garma.
β€œNenda bwana! Nenda kawaagane na wachawi wenzako huko,” Garma alisema kwa dharau huku akiangalia upande wa pili.
β€œKhe! Haa, hamjaondoka tu?” Mama Garma, ambaye alikuwa katika korido ya kuingia vyumbani, alisema.
β€œTunaenda, hata usitupangie,” Mayner alijibu.
β€œToka bwana! Umekalia kujilalamisha tu. Huna hadhi ya kuishi katika hii nyumba. Lakini uwi! Kelele kibao. Na wewe Rasma, kama unaondoka hapa, nisikuone tena. Usije hata kuomba msaada wa chumvi,” Mama Garma aliongea.

Rasma alimtazama Mama yake, akameza fundo la mate ambalo alitamani kulitema 😀, kisha akasema:
β€œUkiona nimekuja hapa, labda nimekuwa maiti, lakini sio wakati nikiwa hai.”
β€œHata hiyo maiti yako hakuna mtu ambaye ataipokea,” Mama Garma alizungumza.
β€œOk, tusijuane. Kila mmoja apambane na hali yake. Tuone sisi na ninyi, nani atakuwa yupo sahihi. Mungu atajibu kila chozi ambalo limemwagika hapa,” alisema Rasma ambaye hakuonesha kustuka kutokana na kauli za Mama yake. Ndio kwanza alichukua begi kisha akamwambia Mayner waondoke mahala pale. πŸ™πŸ’”

Huu ndio ulikuwa mwisho wa Mayner kumiliki penzi la Garma πŸ’”. Penzi ambalo walishapanga kila kitu kuhusu ndoa, lakini mwisho wa siku uwepo wa Mama yake pale nyumbani unawatenganisha. Mayner anakwenda kuanza maisha mapya akiwa na Rasma, huku asijue huko aendako maisha yatakuwa ya namna gani. Kikubwa ambacho alikiangalia ni yeye kuondoka mahala pale…

Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MKE ALIYECHUMA NAYE MALK | EP 14.  >>> https://gonga94.com/semajambo/alifirisika-baada-ya-kumuacha-mke-aliyechuma-naye-malk-ep-14
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest