.......... Tulishinda wote ofisini siku yenyewe alikuwa ananisaidia ,,kitu akiona hakipo sawa ananielekeza vizuri sana , kwa kutulia yaan mpaka nikasema Asante mungu ..
Mama yake alimpigia simu akamwambia aende haraka nyumbani lakini ,Alex alikataa kabisa kwenda kwao hata mimi nilimbembeleza asije kuniongezea chuki kwa wazazi wake lakini akanambia sintaenda kwa sababu najua wanacho niitia
Nikamuuliza ni ninii?? Akasema wamepata taarifa ya uchumba wetu na kila kinachoendelea hapa kwahiyo.sitaki kuwambia chochote waache wabaki na huyo Judy mpaka watakapo kaa sawa , basi sikuwa na haja ya kumlazimisha hata...
Usiku tulifunga mida ya sa nne , tukabaki kupiga hesabu na alex wangu baada ya wahudumu wote kuondoka, akanielekeza kutunza mtaji na faida ,inakuwaje nikaelewa vizuri , ilikuwa ni siku ya kwanza lakini nilipata ma hela mengiii sanaa ya faida , mana tulijaza tena watu wenye hadhii wa maofisini hivyo chakula happ sio cha afu mbili et?? Hamna dadaa ukija hapo uwe huna pesa za mawazo
Tuliondoka usiku wenyewe tukaenda zetu kwetu ,alex akanambia nikija hapa tuhame tutafute nyumba nzima , nikasema sawa ,alikuwa ameshanifungulia acc ya bank akasema nihakikishe kila siku faida inaingia bank baada ya kuwapa posho wafanyakazi
Yaan wanalipwa mwisho wa mwezi lakini kila siku wanapewa posho kwa ajili ya usafiri au vipi watajua wao ila kula ni pale asubuhi mchana na usiku
Kesho yake asubuhi Alex alikuwa anaingia kazini , akanambia atakaa huko wiki moja ndio atarudi Tz , nikasema nitammiss hatari Alex wangu nishamzoea mwenyewe tunalala na kuamka wotee daah
Akanambia inno ataniletea simu , ameshampa maelekezo, lakini pia kuna mtu atakuwa ananiijia kwenda kazini na kurudi kila siku ,nikasema sawa
Aliamka asubuhi akaniaga mwenyewe akasema nisije wewe seka nipe tamu yangu kabisaaa, nile nishibe namie nikampa zoteeee ,mpaka zilizokatazwa na serikali..
Aliondoka Alfajir akaniacha mie, najiandaa kwenda kwenye kazi yangu, unajua pesa bwana zinambadili mtu.yaan mimi nilibadilika kwa ile siku moja hata mtembeo wangu niliuona umebadilika kabisaa sio ule nao tembea kila siku,kuongea sijui yaan kila kitu niliona nimebadilika miee salma mie mmh
Basi nilichukua zile pesa ambazo alex aliwahi kunipa mara ya kwanza kabisa kama asante , na kuna zingine niliongezea zilikuwa kama laki 8 hivii , wakati Dereva amenifata nilikwambia kuna sehemu nipite mara moja nikamuelekeza kwenye kituo flani hivi kinalea watoto wanaoshi mazingira magumu afu wengi pale huwa walemavu
Nikatoa zile pesa zote nikawapa,sikuwa na kazi nazo lakini ni pesa ambazo nilizithamini sanaaa mana ndio sababu ya hii safari yangu , nikazitoa huku namuomba mungu sadaka hii niwe mwenye kusamehewa mana nakwenda kubadili dini na siku zote nilikuwa naomba nife nikiwa mwislamu niliomba Hata siku ya mwisho nifufuliwe nikiwa mwislamu.
Lakini kila kitu naona kinakwenda kubadilika nilimkabidhi mungu hatma yangu huku nasema Dini zote ni sawa wote wanamuabudu mungu mmoja ambae yupo juu
Hata huku ninapo kwenda pia ni salama , baada ya kutoa zile pesa nikaondoka kuelekea kazini siku hii nilichelewa kidogo kuingia mana nilipita kulee
Nilifika kazini mida ya saa tatu asubuhi, ajabu nilimkuta mama yake na Alex yupo hapo ,nilishtuka kidogo lakini nikamkaribisha kwa furaha huku nacheka kawaida
Ila yeye hakuwa anacheka tena sura ameikunja kweli, niliomba mungu asije kuniaibisha hapo mana akianza kuropoka mbeele ya wafanyakazi nitakuwa nimeisha miee
Nilimwambia mama naomba tuingie ofisini, tafadhali kweli alinielewa akainuka tukawa tumeingia ndani
Nilimsalimia vizuri tu kwa heshimaaa nikamwambia mama karibu akasema asante naomba niongee kilichonileta hapa, kwanza hongera ofisi yako nzurii!!
Nikasema Asante mama" mara zote sikutaka kulisahau neno mama hata kwa sec walau nilitaka niwe mwenye heshima kidogo bila kujua amekuja kufanya nini???
" hivi wewe una wazazii??" Lili kuwa swali la kwanza aliniuliza yule mama huku ananitazama usoni
"Ndio!!"
"Huwa unawadharau eeh" nilijifikiria kidogo afu nikamtazama nikasema hapana mama kwaniniii???
"Naskia alex sasa hivi anaishi kwako sio??" Mmh nilibaki kimya sikujibu kitu akaendelea
" hata siku moja alishawahi kuja nyumbani kwao kusalimia?? Ulishamuuliza kwanini hataki kuja kwao ?? Unataka kunitengenisha na mwanangu??"
"Hapana mama sio hivyoo!!"
"Ila nini?? Unaona raha anavyochezea pesa kwako,, sasa unaendeshaje Biashara ikiwa hata kusoma hujuii?? Au ndo mnachezea zipo pesa eeeh?? "
Nilibaki kimya napikicha vidolee tu
'Hao wazazi wako wapo sawa kweli?? Unachumbiwa vipi bila wazazi wa kiume kuwepo wala kutoa baraka zao ,hivi huo ni uchumba kweli??"
"Mama naomba unisamehe mama yangu,sikujua kama alex atafanya vile ha..."
"Haya baada ya kujua ulifanya niniii?? Hujui kama katelekeza mwanamke mjamzito nyumbani kwake et hujuii??"
Dah sasa nitajitetea ninii?? Nilibaki nimeinama yule mama aliongea maneno mengi mengine hata ya kunikashfu ,aliongea tena akanambia anamtaka alex nyumbani haraka jamni utafikiri mimi nimemfunga kamba alex nyumbani kwangu
Nilibaki kuomba msamaha mara kibao,mpaka inno akaingia nilihisi wokovu umenifikia sasa
Inno alishtuka wazi kumuona mama yake pale, akamwambia mama umekuja na huku mara ngapi nimekwambia matatizo yako na Alex malizeni nyie sio kumuingiza na salmaaa???
ITAENDELEA
KWETU morogoro.