... yaan hata wewe ungemuona subira ungebaki mdomo wazi kwa jinsi alivyobadilika na hivi mdogo wangu anamshape ule mkubwaa sio kama mimi ni simple simple tu
Sasa alikuwa amevaa ki skert kifupii cha suti, kipo juu ya magoti afu juu amevaa ki Blauz cha Shifoni , kiatu chake kirefuu usoni hiyo make up jamani hee
Kawa kama wa kwenye video ,wale wadadaaa , afu na Inno amevaaa suti za kufanana na Skert ya Subira wamependeza jamani sio poaa
Nikashangaa subira ana bonge qa simu , ameshika mkononi hee ,
"Umependeza weweee!!!"
"Shoga tutaongea baadae tulia ""
Akapita subira mi nawatizama tu nasema hapa inno hapa mmh usikute kashajipata hahah haya bwana nimependa naomba iwe hivyo kweli nitafurahi hatarii
Basi nikashangaa mama yangu nae yupo kapendeza mwenyewe , pale akaja kunipa hongera nikasema Asante mama yangu akarudi kuketi
Watu wote sasa walikuwa wamekaa wametulia , Mc akasema tunaenda kufungua Rasm ofisi yetu baada ya kutambulisha wafanya kazi
Basi wakitwa hapo team ya wafanya kazi wote mpaka zakia na shoga zake , wapishi mpaka watu wa Kusambaza chakula nje ya ofisi
Zakia alikuwa ananitazamaa najua tu huyu hapo anakabwa hatari mana nimemfanyia surprise nami ndo naenda kuwa boss wake , wale wadada wa mtaani kwetu wanatoa machoo mie hapo nikasema safiii
Basi tulikwenda pale nikakata utepe rasmi kufungua ofisi yangu nikapigiwa makofi watu wakaendelea kuparty hapo kunywa na kulaaa , mimi na alex hapo tupo tunapita kila meza kuongea na watu ile kuwakaribisha kupiga story mbili tatu
Tulifika meza ambayo alikuwa amekaa felix na bruno afu kulikuwa na wakaka kama watatu jumla wakawa wa tano
Tuliwasalimia vizuri kila mtu alikua anatoa neno lake wengine wananisifia huku wanamwambia alex umeokota dodo ,Hongera hapo kama zoteee
Felix yeye alisimama akasogea karibu na sikio langu akanambia ulivyo pendeza utafikiri unajua kusoma!!
Alinambia kwa sauti ndogo sanaaa lakini ilinishtua moyo nikaona aibu afu yeye alikuwa anacheka akasema kwa sauti hongera bwanaaaa
Mi nae nilicheka nikasema sawa usijali, bruno akamwambia Alex uwe unatutambulisha mapema jamani mi nilikua naandaa mashambulizi hapa.makali baada ya lile la mwanzo kufel , Salma ni mrembo sana kila mtu anatamani awe nae Hongera Alex
"Awe na nanii?? Nani anataka kuona mwanamke hajui kusoma si unaleta ujinga kwenye ukoo dogo vipi weww" Felix alimjibu bruno huku ananitazama kwa dharau mnooo mkononi kashika grass ya pombe kali afu akainywa yotee kwa pamoja
Alex alitabasam akanishika mkono afu akamjibu bruno tukaondoka zetu , mpaka kwa kina inno wakati huo mama alikuwa ashaenda nyumbani tayari
Nilimwambia njoo tupige story zetu ,tukaondoka pale tukamuacha inno na kaka yake
"Weee umependeza shoga angu"
Wee dada wewe heheh nimejitazama kwenye kiooo zaidi ya lisaaa shoga angu yaan sijiamini kama ni mimi ujueee!! Ila nawewe umewaka jamanii nilitaka kusema ni Aunt Ezekiel nini huyu sio salma wangu"
"Hahaha acha bassss!!!! Unasimu kubwa??"
"Kaka inno kaniletea jana tu yaan we dada heheh mi siamini kila kitu kimekuwa gafla hivi "
"Aaaah au ndo teyari amejiwekaaa"
"Mmmh sio bwana, mbona hajawahi hata kunitongoza ,sasa hivi ananisimamia yeye shule amesema anataka kuni support mpaka nitakapo fika mwisho wa elimu yangu alimwambia hivyo mama piaa, afu ananionea tu huruma"'
"Mmmmh hayaa ila akikutongoza hata usimkataee mwenzangu ndo tunatoka hivyo kwenye unasikini"
" hahaha we mwehu kweli, ila mwenyewe nampenda inno dada ,Natamani anitongoze lakini mmh hana hata muda"
"Mpe mudaaa"
Tukapiga story zetu za ujinga ujinga mwingiii tunachekaaa, simu yangu ikaita namba ngeni
Nikapokea ile haloo yakafata matusiii , baadae nilijua ni juddy nikaikata ile simu akapiga tena , subira akanambia embu asituharibie siku nipe hiyo simu
Akaipokea
"Weeee ukiachwa achikaa bwanaaa embu tuache tupo kwenye raha zetuu" subira aliongea huku anacheka yaan kam anafanya utani
"Yaaan siku ya leo naaapa salma utailipa salmaaa naapaa nitakukomeshaaa, mimi mjini nimekuja kabla yako!!" Judy alikuwa anaongea huku analia , nikasema taarifa kashazipataa hukooo tukio la leoo
Subira akamjibu kumbe we umekuja polee sie wenzio tulitangulia enzi tupo kwenye kiuno cha baba kwahiyo Born town kitamboooo mnooo bye"
Akaikata ile simu akasema achana nae huyu yaan we hakuna kuachana na alex , Sisi ni ving'ang'aniziii
Hahaha tulicheka kama mazurii, Alex alituita akauliza jamani hamjamaliza tu tukasema sie teyari akasema mje basi huku
Tukaenda kujumuika wote tukawa wanne sasa mimi na Alex wangu inno yupo na Subira mi nawatizamaaa nacheka mwenyewe tu
Sikumwambia hata alex kama juddy umenipigia simu, ila nilikuja kugundua Juddy anaipiga sanaaa simu ya Alex afu alex ana mute ,mi namkata jicho la chini chini tu
Siku yetu ilikuwa nzuri sana ,hiyo siku, tuliondoka sa 5 usiku baada ya watu wote kutawanyika , nilipanga ratiba fresh kesho ndio tunaanza kazi
Nikiwa njiani kuna sms iliingia , tulirudi Nyumbani hapo tushakuwa wachumba sasa nikajiachia penzini sina shaka ..
Kesho yake niliamka Alfajir et nawahi kazini , alex akanambia kuna wafanyakazi kibao we uwe unaingia sa moja tu , baada ya huo muda tulienda na alex akanielekeza jinsi ya kusimamia wafanyakazi kupiga hesabu yaan alinielekeza kila kituu ,kwa ukaribu nikasikiliza na kumuelewa vizuri
Hakujali sijui kusoma wala nini lakini alinipa majukumu makubwa niyabebe akanambia jiamini mpenzi wangu lazima uwe bora hata kama wengine watakudhihaki nikasema sawa .....
Polen kwa changamoto mmesubir mnooo
Changamoto ya page yetu ilifungiwa hivyo tumepambana sana imetumika zaid ya pesa ya kitanzania elfu 81 hiv ili tu kufanikisha hili jambo
Kwahyo tunaomba kidogo kamchango kahiari tu atakayejisikia tunashukuru sana
Ahsanteni
KWETU morogoro.