Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

2---3 SARA TAMU YA BABA MKWE EP 02

27th Jul, 2025 Views 93



"nelson please naomba usinifanyie hivyoπŸ₯ΉπŸ™"

"Kwani Kuna ubaya gani kama tukifanya mimi na wewe si wapenzi au"

"No siko tayar kama unanishusha fine nishushe😑 "

"Hahahahaha Sarah kwaiyo uko tayari kuliwa na wanyama lakin si kulala na mimi inamaana unanuchukia kiasi hicho "

"Nelson wewe unajua kuwa sikuchukii lakin kwa hili unalolitaka siwez kulifanya kabisa "

"Fine shuka kwenye gari yangu"

Sarah alichukua pochi na kufungua mlango nakatoka

Nelson aliwasha gari na kugeuza tayar kwa kuondoka ila gafla akasimama na kutoka akitembea haraka sana

Sarah alitabasamu maana alihisi tu kuwa ni utani πŸ™‚ (Nilijua tu utarudi kwani huwezi kufanya kitu kama hicho) aliwaza huku akimuangalia kwa tabasamu

Alimfikia Cha ajabu alimfikia na kumsukuma chini Kisha akashika gauni na kulichana

😲Ohoo anabakwa mtu hapa,, alianza kupiga kelele akimuomba amuachie ila alikuwa amedhamiria kufanya kile kitendo

"Nelson naomba uniache tafadhali naomba usinifanyie hivyo please Nelson " aliongea kwa sauti ya kilio lakin hakujibu

Alimshika mikono yake Kwa mkono mmoja na mkono mwingine akawa anafungua mkanda wa suruali yake

Machozi yalimtoka hakuamini kama Nelson anaefahamiana nae kwa miaka Saba leo anaamua kumbaka kweli😭

Alijitahidi kujitoa kwake ila alimshinda nguvu akawa amechomoa dyudyu lake na kushika nguo yake yandani akitaka kuichana ila gafla lilipita gari likiwa Kasi sana likapita na sekunde kadhaa likarudi saa hiyo alikuwa akijitahidi kuzuia kwa kubana miguu

Baada ya kuona lile gari alimuachia haraka na kutaka kuondoka ila alishuka Mtu kwenye lile gari na kumshika akaanza kumshushia kipigo Nelson hakuwa mzembe kwani nayeye alikuwa akijitetea ila yule kaka alimshinda
Nelson akawa amepigika haswa bahati yake akawa amepata upenyo na kukimbiaπŸƒ

Yule kaka alimfuata Sarah mda huo alikuwa amejukunja na kuficha mwili wake maana gauni yake ilikuwa imechanwa

Alimfikia na kumnyenyua bila kuongea kitu akampeleka kwenye gari na kumfunika na koti lake

Sarah alikuwa analia tu hakuamini Nelson ambae amekuwa rafiki yake mkubwa tena wakitambo hicho anaweza kumfanyia ukatili wa namna hiii 😭

Yule kaka aliwasha gari na kuondoka alionesha kuwa na hasira sana

Gari lilitembea kama masaa mawili ndio alisimama nje ya nyumba kubwa sasa hapo ndio akili ikamrudia nakuanza kuwaza
(hivi imekuwaje nikapanda kwenye gari la mtu nisie mfahamu tana nimekaa tu hadi nimeletwa huku)

"Kaka samahani naomba unishushe tafadhali"
Sarah alimwambia yule kijana kwa sauti ya hofu sana

"Kuwa na amani siwez kukudhuru"

Aliongea huku akiwa anamuangalia ,(huyu kaka kama sijakosea atakuwa mwarabu) aliwaza Sarah huku akimuangalia.

Geti likafunguliwa wakaingia ndani akapack na kumfungulia mlango na kutaka kumbeba

"Samahani naweza kutembea mwenyewe"

"Utatembeaje na hiyo nguo"

Aliongea na Sarah alijiangalia kweli ilikuwa haifai kutembea maana ilikuwa imechanika sana.

Akambeba na kuanza kutembea kwenda ndani sasa ile wanafika mlangoni wakakutana mwanamke kasimama mlangoni

( ohoo nimekimbia kubakwa na kuja kunyongwa maana sijui🀷)

"Samiri huu ndio mda wa kurudi nyumban ee mbona unataka kuniua kwa presha we mtoto"
Aliongea mama yule kwa kulalamika,
Mda huo Sarah anatamani kushuka ila alimshika sawa sawa

"Mama unaweza kunipisha niingie ndani?"

"Nimekuuliza swali huu ndio mda wa kurudi nyumban tena unakuja na mwanamke hii ni adabu gani😑"

"Mama please unajua siko kwenye mood ya haya mambo "

Alivyoongea hivyo yule mama aliwapisha Sarah mda huo amejifanya amelala 🀣 maana hakutaka kupigwa bisu akiwa anaona

Aliingia ndani na kupandisha ngazi akamuingiza kwenye chumba akamkalisha na kusema

Unaweza kupumzika usiku mwema

😳Hata hajaniambia pole au imekuwaje ukawa pale 😏

Alifunga mlango na kuondoka, kutokana na mazingira alijikuta akishindwa kulala kabisa tukio alilotaka kufanyiwa na Nelson lilikuwa linajirudia kichwani

Kwakua mda ukikuwa umeshaenda aliamua kukaa tu hazikupita dakk kumi akasikia azanaa kumbe kumeshakucha

Akiwa Bado anashangaa alisikia kama watu wakiswali.

(πŸ€”Mmm hii nyumba ni waislam au mbona kama nasikia watu wakiswali au namawenge)

Akaona labda itakuwa mawenge basi kausingizi kaka mpitia nakulala

Alikuja kuamka mda ukiwa umeenda sana alafu kichwa kikawa kina muuma sana

Ile anafungua macho anakutana na nguo zimewekwa pembeni mwa kitanda

Akahisi zitakuwa zake akaamka sasa kupaangalia mle ndani vizuri palikuwa pazuri utafikili nyumba ya mfalme

(hivi Tanzania Kuna majumba mazuri namna hii msijawahi kuona) aliwaza huku nikiwa amesimama dirishani akiangalia mnzari ya nje mara mlango ukagongwa haraka akarudi kitandan na kujifunika shuka

Mawazo yake akajua ni yule mkaka

"Ingia "

Ooo 🫀kumbe ni yule mama wa Jana usiku

"Habari ya asubuhi"...

"Nzuri shikamoo"

"Marahaba mwanangu hujambo"

"Sijambo"

"Sawa nilikuwa nimekuja kuangalia kama umesha amka maana ni Mda wa chai sasa"

Nyie nilihisi aibu balaa maana nimelala hadi saa nne 😁

"Samahani kwa kukusumbua" niliongea kwa sauti ya aibu

"Usijali binti yangu,aa nguo hizo hapo utaoga alafu ushuke ili upate kifungua kinywaee"

"Sawa asante sana "

Aliondoka akaingia bafuni ,sasa kimbembe kinakuja hajui Bomba linafunguliwaje ,
sasa akawaza hapa Bora akojoe tu na kubadilisha nguo ataenda kuoga nyumbani

Siakakaa bhn akajisaidia pale sasa ile amemaliza anaangaza macho ili nione kidude Cha kuflashi akashangaa maji yanatoka yenyewe bila hata kubonyeza mahari heee 🀣

Heee hii Kali kumbe mambo ni yanajipa yenyewe 🀣

Basi bhn akasogea sehemu ya kupigia mswakiaikachukua mswaki mpya na kusafisha kinywa vizuri akabadilisha nguo Kisha akutoka na kwenda seblen

Alifika nakaelekezwa dining akaenda nakukuta yule mama anamsubiri basi akamimina chai na kuchukua vitanwa na Sarah nae akafanya hivyo hivyo

(Ila kitu nilichogundua jaman Hawa watu wenye maisha ya juu huwa wanakula kidunchu sio kama sisi maisha hatuna ila tunakula kama hatutokula tena)

Sasa wakati Sarah akiendelea kunywa chai alitamani kumuuliza yule mama kuhusu yule mkaka aliemsaidia ila akaona ngoja akaushe.

Mara huyu apa akamsalimia yule mama ila hakumsalimia Sarah badala yake akasema

"Ukimaliza kunywa chai Hela hii hapa natumaini itakutosha kwa nauli yako and sahau kilichotokea usiku ,naamisha nisahau na ikibidi usahau Kila kitu kuhusu mimi"
Huyoo akaondoka

😳 Alibaki kimya kwanza hakumuelewa (jamani kwani nimekosea au kwasababu nimelala hadi saa nne lakin kama tumefika hapa asubuhi alitaka nilale nusu saa,?) Aliwaza huku kumuangalia alivyokuwa akiondoka 🚢

SARA TAMU YA BABA MKWE NO 03

Upande wa Nelson alikuwa nyumbani kwake huku akiwa amekaa chini moyoni mwake alikuwa akijilaumu sana kwa kitendo alichomfanyia Sarah
"I'm sorry Sarah najua nilikosea kuweka hasira zangu kwako ila yote ni kwasababu nakupenda San Sarah"
Alichukua sm na kumpigia Sarah ila ilikuwa hapatikani baada ya kuona haipatikani aliamua kwenda nyumbani kwao

Upande wa Sarah baada ya Samiri kuongea vile aliinuka ili kumfuata ila yule mama alimshika mkono na kumwambia akae

"Kaa hapo kunywa chai"

Kwani hata hiyo hamu ya kula alikuwa nayo😁 ila hakuwa na namna kwakuwa alikuwa ameshamimina chai asinge weza kuiacha

Alimaliza kunywa chai akakaa kusubiri yule mama amalize

"Unaitwa nani"
Aliuliza baada ya kumaliza kunywa chai

"Sarah"..

"Oooo Jina zuri,mh mnafahamiana vp na Samir
"

"Aam simfahamu ila amenisiidia tu"

"Kivp "

Alikaa kimya Kwa mda kisha akajibu

"Nilitaka kubakwa akawa amenisaidia"

"Ooo sawa pole sana,ninaweza kupata namba yako"

πŸ€”Huyu mama mbon kama simuelewi

Alimpa namba Kisha akaomba kuondoka mama yule akasema nisubiri kidogo

Akainuka na kwenda chumbani kwake Kisha akarudi na kusema..

"Utaenda na dereva wetu"

"Aaaa hapana madam nitaenda mwenyewe " yule mama hakumsikiliza alimuita dereva wao akaja

"Raphael, mpeleke huyu dada nyumbani kwao, and make sure unamfikisha salama"

"Sawa madam"

"Sarah, nenda kapumzike tutaonana siku nyingine "

πŸ™„Siku nyingine natafuta nini tena

"Sawa madam asante sana "

"Karibu "

Baada ya kuangana na madam Sarah aliongozana na dereva akamfungulia mlango akapanda na safari ikaanza

Baada ya Sarah kuondoka yule mama (Mama Samiri) alichukua sm yake na kupiga

"Hello hubby" aliongea mama yule baada ya siku kupokelewa

"Yes kipenzi habari yako"

"Namshukuru Allah Niko safi,nimekupigia kukuambia good news"

"Ooo! Nambie mke wangu""

"Jana Samiri kaja na mwanamke hapa nyumbani na alilala hapa"

"What,hii nikweli ""

"Asilimia mia"

"Ni mpenzi wake au ""

"Sijui ila nahisi atakuwa anampenda maana hakuna hata siku moja ambayo alileta mwanamke hapa nyumbani tena kaja amembeba ""

" Sasa kama hujui unawezaje kusema kuwa ni habari njema"

"Kwangu mimi naona ni habari njema,japo sijui mahusiano yao ila wanapendezana sana nafikili ni mda wa kumset akae kwenye plan yetu""

" Unamset je wakati mtu mwenyewe anamisimamo chungu mzima"""

"Hakunaga msimamo kwenye mapenzi we subiri uone sasa hivi namaliza mchezo""

""Okay fine, unarudi lini ""
***Simulizi hii imeandikwa na Ritha stories ukiikuta kwingine ujue huo ni mwizi****
"Nitarudi nikishaweka mambo sawa ngoja nimfuatilie huyu binti nijue black ground yake"""

"""Okay utanijuza ""

"Okay honey byee mwaaaa😘"

Mama yule alikata sm na kuachia kicheko ambacho wewe msomaji ungesikia basi ungejiuliza Kuna nini?

Nelson alifika nyumbani kwa kina Sarah akagonga na mlango ukafunguliwa

"kaka Nelson, karibu dada yuko wapi?";alikuwa ni Angel mdogo wake Sarah

"Aaaam nimemuacha dukani vp hajafika?""

""Atafikaje wakat umemuacha dukan?"""

"" Bibi yako wapi"" Nelson aliamua kubadilisha mada

""Kaenda kanisani ""

""Na wewe mbona hujaenda""

"Basi tu,vp utaendelea kusimama hapo au unaingia ndani""

""No nataka kukaa hapa nje""

Angel hakujibu alifunga mlango na kurudi ndani

Nelson alibaki kujiuliza inamaana Sarah hakurudi nyumbani? Na yule aliemchukua Jana itakuwa alimpeleka wapi, Mungu asije kuwa mtu mbaya akawa amemdhuru

Alivyowaza hivyo aliona Bora atoke na kwenda kumtafuta japo hakujua amtafutie wapi.

""Angel '"

""Abee'""

""Natoka mara moja Sarah akifika mwambie anipigie""

""We siuna simu kwann usimtafute mwenyewe ""
Nelson alimuangalia Angel kwa sekunde kadhaa Kisha akaondoka,🀣Iko hivi Angel hampendi Nelson balaa yaani Huwa hatamani hata kumuona nyumbani kwao😁ila ndio basi Hana huo uwezo wa kumzuia.

Sasa wakat Nelson anafika getin ndio mda huo huo Sarah ndo anaingia

Sarah alitoa macho baada ya kumkuta Nelson nyumbani kwao

Nelson alimfata Sarah na kuanza kumuomba msamaha

"Naomba usiniguse tena ukae mbali na mimi"

"Sarah please naomba unisamehe sana najua nilikukosea lakin niko chini ya miguu yako please nisamehe sana "

"Nelson naomba uondoke sitaki kukuona hapa Wala sihitaji ukaribu wowote ule na wewe kwenye maisha yangu, kwaiyo ondoka "

"Sarah naomba usinihukumu kiasi hicho please naomba ukumbuke ukaribu wangu na wewe , najua ndio nimekosea ila nishetani alinipitia tu"

"Mfyuuu eti ukaribu mara ooh shetani ,hivi ungekuwa unajari kuhusu ukaribu wangu na wewe ungeweza kunifanyia ukatili kama ule , alafu unataka kumzingizia shetani eti kakupitia kwaiyo alikupitia kwangu tu"

Nelson alipiga magoti huku akitoa na machozi 😭 ila Sarah hakutaka kumsikiliza hata kidogo,mda huo Angel yuko dirishani akichungulia😁

Sarah alitaka kuingia ndani ila alimuwahi na kumshika

"Nelson nimesema niachee 😈 kwann hunisikiii"

"Siwez kukuacha Sarah please mamaa naomba unisamehe najua nimekuumiza ila nahitaji second chance nakuahidi sitorudia tena"

"Second chance?,unaona kwa ulichofanya unahitaji second chance ee hivi kama si Mungu kumleta yule kaka saizi ningekuwa katika hali gani mm ee au ungekuwa umeshaniua"

""Mmh mbona kama umbea huu ni pambe ngoja nichukue sm ni record video ili nipate umbea wenye ushahidi""aliongea Angel na kuchukua sm ya bibi yake akaanza kuchukua video

"Hapana Sarah naomba unisamehe tafadhali "

"Mfyuuu naona nikikaa hapa nazidi kuwa na hasira na wewe"
Alitaka kuondoka Nelson akamzuia tena

"Nelson nitakuitia mwizi sasa ivi ohoo jifanye husikiii"

"Sawa Sarah kama hiyo itakufanya unisamehe sawa ita"

Aliongea kwa huruma Kama sio yeye ila ukweli hakuweza kumsamehe wala hakutaka hata urafiki nae tena

"Sikia nelson urafiki wangu na wewe umeisha Jana na Kila kitu ulichokuwa unajua kuhusu mimi sahau na ukiniona popote pale pita hiviπŸ‘‰ nadhani umenielewa"

"Hapana Sarah naomba usivunje urafiki wetu tafadhali wewe unajua kuwa tumetoka wapi"

"Sitaki kujua ni umetoka wapi,na Kam ulijua Kuna urafiki kati yetu Kwann udhamilie kufanya kitu kama kile".

" Ni shetani tu"

"Basi kamwambie huyo shetani akapitie na leo mfyuuu" Sarah alikuwa ame kasirika sana akaona Haina haja ya kupigishana kelele aliingia ndani huku Nelson akijaribu kumfuata alifunga mlango haraka na kwakubamiza kwa nguvu

Nelson alibaki anagonga lakin akufungua
Aliingia ndani akashangaa kumuona mdogo wake akiwa ameshika sm huku akiwa anamchukua video

"Unafanya nn ""

"Nalima kwani huoni,mh vp shoga yangu mbona unagombana nakibwengo wako asubuhi asubuhi ""

"Uwe na adabu mjinga wewe nani shoga yako,alafu hayo majibu yako ya kijinga Iko siku nitakuja kukuvunja""

"Majibu ya kijinga yanaendana na maswali ya kijinga""

""Bibi yako wapi""

"Kapotea""

"Angel πŸ‘ˆ""

""Kaenda kanisani 😁usije ukamalizia hasira zako kwangu😏,kaka amepiga sim akasema hakupati na nimewambia Jana hujalala nyumbani kwaiyo jiandae kujibu maswali, byee naenda kucheza""

Mtoto mingine sijui ikoje

"Baada ya kuingia chumbani kwake aliwasha sm baada yakuwasha ziliingia jumbe nyingi ambazo zilitoka kwa kaka yake na zingine kwa Hilda

Kabla hajajibu sm iliita mpigaji alikuwa ni Hilda

"Ulikuwa wapi'toka usiku hupatikani"

"Kheee dada uko Honeymoon alafu unanipigia sm usiku kulikoni show ilikuwa Kali 🀣"

""Achana na habari za show we nijibu ulikuwa wapi maana huku roho ilikuwa juu juu nikihisi utakuwa kwenye hatari""

""Hamn bhn nilikuwa na Nelson na nililala kwake""

"Kwake mkawa hampokei sm wote mh mlikuwa mnafanya nn😁😁""

""Muone umbeya tu saiz asubuhi badala umpeti peti mumeo unawaza umbea yatakushinda"""

""Haya bhn nilitaka kujua kama uko poa, ngoja niende room nikatoe chakula 😁😁"'

""Nilijua tu utakuwa unaongealea mbali 😁""

""Haya bye ""

""AaaaaaaaaaπŸ€› paaaa"alikuwa Nelson baada ya kufika nyumbani alipack gari lake na kupiga kelele kwa hasira akapiga ngumu kioo Cha gari πŸš— kikapasuka

""Sarah wewe ni wangu siwez kuruhusu mwanaume mwingine kuwa karibu na wewe I swear 😑""

Itaendelea.......full 1000
Whatsp
0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

2---3 SARA TAMU YA BABA MKWE EP 02  >>> https://gonga94.com/semajambo/2-3-sara-tamu-ya-baba-mkwe-ep-02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest