Ilikuwa siku ya jumamosi nilikuwa nimepata dili la kutengeneza gari. Unajua katika maisha ukiwa mwanaume hutakiwi kuchagua kazi ndo nachokitambua .Ndio maana sichoki napambana
Siku hiyo nilikuwa nimejibanza kando ya barabara, chini ya kivuli cha mti, nikitengeneza gari la mteja gari dogo aina ya Probox. Vumbi lilikuwa likinijia usoni, na jasho lililokuwa linatiririka halikunifanya niache kazi yangu.
Wakati nataka nianze kulitengeneza , nikasikia honi kali ya gari barabarani, ikifuatiwa na kelele ya wasamaria:
“Eeh, yule bibi avuke bwana jamani!”
Niligeuza shingo yangu taratibu, nikamuona bibi mmoja mzee, aliyeshikilia fimbo na kuchechemea katikati ya barabara. Magari yalikuwa yanapita kwa kasi, dereva mmoja alimpigia honi hadi bibi yule akashtuka kwa hofu.
Nilishtuka.Nakutaka kwenda kumsaidia .....
Lakini kabla sijatoka kwenye mfuniko wa injini, alikuja msichana mmoja mbio kutoka upande wa pili wa barabara.
Alivaa t-shirt ya pinki na suruali nyeusi ya jeans, nywele zake alizifunga kwa ustadi . Bila kujali hatari ya magari yanayokuja wala macho ya watu, alimshika yule bibi mkono, akampitisha kwa utulivu upande wa pili wa barabara huku akimwambia:
“Usijali bibi, niko hapa. Pole na barabara hii madereva kama unavyowajua wanalewa sana na hii ni weekend yakupasa uwe makini”
Nilijiuliza huyi mwanamke ni nani tena, niliinuka ili nimtazame vizuri ndipo nikagundua kuwa yule binti alikuwa ni loveness anakaa mtaa wapili .
Ni binti ambaye wengi wao wanamzungumzia kwa aina yake wengine wakisema ana ringa ,hasalimii watu ana dharau na hata mimi nilimjuwa kwa hizo sifa ambazo watu walisema kwa kuwa katokea kwenye familia ya watu wenye hele ....
Sikuamini macho yangu. Binti wa kifahari, anayejulikana kwa maringo mtaani, ndiye aliyemshika mkono bibi mzee mwenye mavazi yaliyochakaa ? Yaani hata ukiwaona tu unajua hapa ni mbingu na ardhi ...
Na zaidi ya hapo, baada ya kumvusha barabara alimpakiza kwenye bajaji na kumlipia nauli yule bibi alimshukuru maana niliona ishara wakipeana mikono....
Lakini nilihisi kitu ndani yangu ,Nilijikuta nikimpenda ghafla kwa namna ambayo nashindwa kuwaeleza . Ila nilimpenda
Nilimkodolea macho akitokomea upande wa pili wa barabara, na moyo wangu ukasema:
“Wewe ndiye niliyekusubiri kwa muda mrefu san. Wewe ndiye kipandw cha moyo wangu kilichopotea kwa muda mrefu hatimaye nimekupata Nitaingia kwenye dunia yako, hata kama siifai n ilimradi tu niwe karibu na wewe.”
Nilijitahidi kila mara kujibanza kwenye kona anazopita lakini wala hakuonekana tena. Nilijaribu kumuuliza mama muuza vitumbua aliyekuwa akiuza karibu na mitaa ya kwao .Akasema ni siku hizi kabadilisha njia sababu hiyo ina matope sana ....
Nilianza kumvizia kwenye njia nyingine lakini mara nyingi alikuwa yupo tu ndani ya gari yaani akishuka ni ofisini akishuka ni nyumbani hivyo kwangu ilikuwa ngumu sana kuonana naye . Nilijikuta kukata tamaa sasa .....
Niliwashirikisha rafiki zangu lakini wote walikuwa walikuwa wakinicheka kasoro rafiki yangu mmoja kwa jina la Robert .Yeye alinipa wazo moja ambalo niliona nila muhimu sana. Alisema " ukitaka kumuua adui yako mjuwe kwanza yaani alikuwa anamaanish nikaombe kazi kwao
Wengi waliona ni wazo.la kijinga ila kwangu ,niliona kuwa jamaa kaongea bonge la point.Nilicheka na kusema
" Hilo ndio neno " nikaondoka hapo hapo ...
Ndipo nikafanya uamuzi.
Sikutaka kumtazama tu kila siku kutoka mbali.
Niliamua Kwenda kuomba kazi kwao kazi ya kuwa mfanyakazi wa ndani(house boy)
Nilitembea taratibu, jua kali likinipiga kichwani kama moto, lakini ndani ya moyo wangu na akili yangu nilijisemea lazima nipate kazi kwao.
Nilijua siendi sehemu ya kawaida. Nilienda kwenye jumba la kifahari, sio kutembelea bali kufanya kazi. Kazi ya ndani.
Nilijiambia, “Maiko, utavumilia. Hili si suala la kudeki sakafu tu, maana mchumia jua hulia kivuli .”
Ndio, nilikubali kuwa houseboy kwao, ilimradi tu niwe karibu na Loveness.
Nilitembea mpaka nilipofika kwenye jumba hilo la kifahari kulikuwa na geti kubwa jeusi yaani kuliona geti kuna onyesha nani wanaishi humo.Nilivuta pumzi na kugonga geti...
Halikufunguliwa nilipotaka kuligonga tena .ghafla honi ilisikika nyuma yangu niligeuka na kumuona Baba yake niliogopa sana
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
NILIOMBA KAZI KWAO ILI NIWE NAYE
BY KELVIN MLOWE( 0699286085)
EPISODE 2
Honi ile ilinistua kama radi inavopiga ghafla kipindi cha mvua . Nilipogeuka, nikakutana uso kwa uso na gari la Range Rover lenye vioo vyeusi ile ambalo mara nyingi nililiona akiliendesha Loveness .
Mlango wa dereva ukafunguka taratibu; nikatamani hiyo ardhi ifunguke nizame, lakini miguu ilikuwa kama imesilibwa na cement .hivyo ilikuwa mizito
Baba yake Loveness watu humwita Mhandisi Makani akashuka. Mtu huyu alitazama kama anaweza kukukadiria thamani yako kwa sekunde mbili tu.
Sura yake ilikuwa ngumu kama chuma kilichopakwa rangi ya fedha.Nilikuwa natetemeka ujuwe hakuna kazi ngumu kama. Kuongea na mtu aliyekuzdi kila kitu.
Makani: “Unafanya nini getini kwangu, kijana?”
“Shikamoo mzee! Naitwa Maiko… ehm… nilikuja kuomba kazi ya ndani.”
Nilijisikia mjinga si kwa sababu ya neno ‘kazi ya ndani,’ bali kwa sababu sauti yangu ilitetemeka kama simy iliyowekwa vibratiom . Hata hivyo, niliangalia chini nisionekane na woga mwingi.
Makani alinitazama juu-chini, kisha akabonyeza remote aliyoishika mkononi geti likafunguka . Ni kwa njia ya kielektroniki. Milango ikafunguka.
Nilihisi kama nimepitia lango la ulimwengu mwingine bustani iliyopambwa na maua ya mazuri ya rangi ya pink .huku chemchemi ndogo iliyokuwa ikirusha maji.
Niliona kwa mbali tu nikaogopa na kusema kweli nitapata kazi maana huko ndani kulivyo duuuh nilianza kukata tamaa . Akarudi kwenye gari na kuliendesha kisha akanambia ...
“Fuata gari.”
Nilikuwa nazidi kutazama jumba hilo la kifahari. Nikagundua kuna watu wanaishi na wengine sisi tunaishia . Yaani harufu ya humo ndani ni tofauti na ya nje ....Nilikuwa nawaza huku nikifuata gari kwa nyuma ....
Ndani ya dk moja, tulikuwa tumefika kwenye kivuli kilichojengwa kwa mbao za gharama. Ambako ndiko parking ilipo
Alifunga breki, akazima injini. kisha akashuka na kunitazama moja kwa moja machoni.
" kijana mbona hatukutangaza kuwa tunataka mfanyakazi ? Kwanini umekuja kuomba kazi hapa ukichukulia ni ngumu sana watu wenye muonekano kama wako kuingia humu
Nilijitazama juu mpaka chini sio siri nilivaa kawaida sana . Yaani hata yule tajiro kunisikiliza mimi ni kama tu kanionea huruma ...Lakini nilimjibu
" Nimejaribu sehemu nyingi ila nimekosa,nikaona sio mbaya kama nikijaribu na hapa ........
“Kwa nini unapenda kazi za ndani?
Naona wengi hupita kwenye madalali; wewe umefika moja kwa moja.”
“Natokea familia maskini, mzee. Nimezoea kazi ngumu. Najua kupika, kufua, hata kufunga waya za umeme kidogo… nita—”
Makani (aliingilia): “Unajua mechanics pia?”
Mimi: “Ndiyo, naweza… nimesomea ‘basic mechanics’ kwenye karakana ndogo mtaani.”
Kwa sekunde chache hakusema kitu, kisha akatabasamu kwa upande mmoja lile tabasamu ya mtu anayeona faida inayokuja
Makani: “Sawa. Nipe wiki moja nifikilie . Halafu nitaamua.”
Alitoa simu mfukoni, akatoa card yenye namba yake na kuniambia" hakikisha jumapili saa 2 asubuhi unanipigia ili nijuwe nakupa kazi au kazi hamna . Mimi ni mtu mwenye neno moja nikipanga muda nitafute kweli. Uwe na siku njema kijana "
Nilikubaliana naye,kisha akanisindikiza mpaka getini na kulifungua si unajua mambo ya kieletronik bhana. Ushamba huu dah sema ndo maisha huwezi kujua kila kitu katika dunia hiii. Nilitoka nje ya geti nikawa natembea mdogo mdogo kuelekea nyumbani ...
Mawazo ni mengi je mzee huyu atanipokea? Sijuwi jibu ni ndiyo au hapana? Na kama atanipokea vipi siku nikimueleza hisia zangu mwanae atanikubali? .kila nikijiuliza hayo maswali kichwani kulikuwa kuna moto ulioumiza ubongo.
Nilitembea nikaingia zangu ndani kwangu nikiwa nimechoka nikapika nikala na kwa kuwa muda ulikuwa umeenda nilijipumzisha tu ndani kwangu.Nililala na kukunja nne kama namiliki hoteli wakati hela ya kula tu ni changamoto.....
Lakini ndani ya familia ya kina loveness .Mzee makani aliitisha kikao cha familia ambacho jambo walilokuwa wanaliongelea ni kunihusu mimi kufanya kazi kwao . Mzee Makani alikuwa yeye kakubali kwa asilimia mia lakini
Mama na mtoto wenyewe hawataki ,wakidai huenda wakakaribisha mwizi ndani ya familia. Kwa sababu mwaka mmoja walimleta house girl kwa jina la Utani kama KOMWE SEMITERA ...Lakini jina lake halisi ni Lucia .
Huyu binti alikomba pesa nyingi za mzee Makani ndo maana wazazi wana wasiwasi lakini mzee aliwambia kuwa wampe nafasi awaonyeshe kazi zinafanywaje na aliniongeza sifa kuwa ni fundi umeme ,magari na hata kuendesha vyombo vya moto najua.
Aliwaonyesha faida yangu katika maisha yao kwa kuwa multi purpose( naweza kutumika kwenye mambo yao mengi sana) nawakaokoa pesa nyingi ambazo wangewalipa mafundi wengine.Hapo mzee akawa amewashika pabaya ...
Walikubali kishingo upande lakini muhimu wamekubali na mzee akawa anasubiri tu ifike siku ya ahadi .Basi wiki lilikuwa linazidi kwenda na kwangu ilikuwa furaha . huwezi amini niliweka mpaka karatasi lililoandikwa JUMATATU-JUMAPILI.
Nilifanya hivi sababu nimechoka maisha ya kuhangaika na pili nataka niwe karibu na mwanamke wa ndoto zangu .Basi siku ya jumamosi majira ya saa tano usiku nilikuwa naruka ruka maana jumapili si kesho...
Nililala na siku iliyofuata yaani jumapili yenyewe . Nilizunguka asubuh kununua mihogo walau nipate kupoza koo . Nilikutana na jamaa yangu aliyenishauri niende kule kuomba kazi .Tulipiga stori nikakumbuka niliambiwa saa mbili nimpigie ....na sasa ni dakika 50
Na kwa bahati mbaya simu ipo nyumbani nilitupa mihogo na kumuacha jamaa hapo hapo ni mbio ndefu kama nipo kwenye mashindano huku nahema .Watu walinishangaa maana sio vitu vyangu.
Lakini hilo sikujali nilikimbia na kufika chumba nilichopanga kuchukua simu saa mbili kamili nilipiga haraka haraka iliita na kupokelewa ...
"Hello "
" Hello mimi ni Maiko"
" natambua beba kila kitu uje uanze kazi
Nilikenua ..............
I
FULL 1500
0699286085.