Juddy kwa raha zote akiwa na furaha alianza kwa kunisifia kuwa nimependeza sana kuliko mtu yeyote na naonekana mrembo ambae naweza mvutia kila atakae nitazama..
Juddy alimaliza kuwa namuomba huyu mrembo wetu wa leo salma atufungulie bango letu na kila mtu asikie ,naomba usimame salma ,alikuwa amechangamka unaweza sema mimi ni shg ake wa damu kabisa😒😒
Nilitulia kila mtu akiwa ananitazama mie nikajiona sina thamani kweli kweli,yaan kwa hapa juddy aliniweza aisee.
'"Salmaaaa jamaniiii!!!" Akarudia kwa sauti kama ananibembeleza hivi , felix akawa amefika kwenye meza yetu"
"Salma hii ni heshima yako tunaomba utusomee" nilitamani nimpige hata na chupa ya uso aisee nilikuwa na hasira zenye aibu kubwa ndani yake"
Wakati nababaika hapo mara Alex akasimama "hey Guys salma huyu hajazoea mambo kama haya sauti yake sio yenye Confidence nitasoma kwa niaba ya....."
"Hana confidence au hajui kusoma😝?, Tusomee salma bwana tunataka kuisikia hiyo hiyo sauti isiyo na confidence"
"Au kama hajui kusoma msaidie" juddy alimkatisha alex na maneno hayo ya shombo.. ,lakini alex hakumjali akasema atasoma yeye tuu"
"Inno alimkatisha Alex akamwambia embu alex kaa chini, salma inuka usome wewe.. huyu mly anataka sifa naona "
Mungu wangu🥹ivi mnajua inno hajui chochote kuhusu mimi kutokujua kusoma😢 so yeye alitaka niinuke nisome ili juddy aaibike pale mbele za watu..
nilimtazama inno moyoni nikasema ungejua hapo naona kama mavitu vitu tu sina chochote ninachoelewa mie🥹😢
Alex alikataa kukaa chini akachukua mic akasoma yale maneno yalikuwa kwa English, nilitamani hata chozi linitoke aisee , nilijikaza mnoo.
Baada ya kusoma alex akarudi , ila hakua sawa nilimuona tu sura yake haikuwa sawa hata kidogo... alikaa akawa amenishika mkono muda wote,nilimuelewa ananipa moyo ila dah💔
Yaan hata sikujua hapo mbele nini kinaendelea, mana akili yangu ilikuwa imeshahama kabisa ,baada ya muda nilimuona bruno anakuja kwenye meza yetu..
"Kumbe nyie watatu mnajuana??" Aliwauliza kina alex, alex akamjibu ndio huyu ni sister yetu, bruno akasema kumbe mnaweza kuwa mashemeji zangu huku anacheka, inno akamwambia dogo acha upuzi huku amekaza sura hatari🥵".
Nilianza kuiona taswira ya bruno ni wazi ananitaka huyu kaka ,ndio akili yangu iliwaza hivyo lakini mmh sikuvutiwa nae namuona tu kama ndugu yake Felix wote hamnazo,
bruno alicheka akasema mwenye dada hakosi shemeji bwanaaa , akawa anaweka utani mwingi humo ,huku ananitazama sana mie ,mwisho akavuta kiti akawa amekaa ,
zilipita kama dakika kadhaa hivi akawa amekuja juddy na mdada mwingine hivi, yule dada akasema shemu tunahitaj kampani naona wakaka wengi girl mmoja ,
Waliongea huku wanachukua viti wanakaa hakuna hata aliewajibu zaidi ya bruno peke yake ,ndie aliwachangamkia ,akaja na Felix akawa ameket hapo hapo..
Walikuwa wanapiga sana story mi naona kelele tu mana hata usiku ulikuwa umeenda sana
Inno akanambia kama upo bored tunaweza kuhama hapa ,nikasema hapana nipo sawa ,juddy akajibu na kwanini awe bored sasa ?? Inno alimtazama hakujibu kitu
Alex akainuka muda huo huo akanishika mkono huku ananiinua kwenye kiti.
"Felix naona tumejumuika vyema ,Bruno wacha si tukapumzike " alex aliongea huku anachukua na pochi yangu alipo taka kuondoka bruno akasema mbona shemu juddy unamuacha vipii??"
Alex hakujibu tukaondoka
"Twende ukalale kwangu nitakupeleka asubuhi kwako,ni salama kule" aliniambia wakat tunakaribia Gari yake"
Kabla sijajibu nyuma aliitwa
"Alex..." tukageuka wote kwa pamoja, alikua Juddy anakuja mbio , alex alisimama akiwa kanishika mkono na mkono wake mwingine ameshikiria pochi yangu
"Vipii!!"
"Inatosha alex inatosha ,utanitesa mpaka linii , nimebadilika alex and You know how much i lov you " yangu macho watu na vingeleza vyaoo"
"Umemaliza??? Haya kama umemaliza unaweza kuendelea na mambo yako sawa??....tuondoke salma"
Wakati tunageuka juddy akapiga magot mbele ya alex akamshika miguu🥵
"Please alex ,naweza hata kuf usinitende hivii, najua huyu mwanamke sio staili yako please inatosha sasa,"
"ushamtumia mwache aende"
Alex hakujibu kitu akampita tukaenda kwenye gari juddy akabaki chini ,sijui alikuwa analia kweli au anajiliza mi sijui
"Naapa salma Utajutia huu muda unao upoteza nakuhakikishia tajuta hii nafasi ni bora ungefanya Maisha yako mengine"
"judd akaniapiza kwa kisasi wala sikujali mie mladi sitembei na mwanaume wake"
"Naomba Nisamehe kwa siku nzima ya leo ,nilitegemea itakuwa nzuri mwisho imekuwa ngumu kotee" Alex aliniambia tukiwa tupo ndani ya gari ,"
"Mbona mi nipo sawa alex" nilimjibu huku nacheka lakini moyoni anajua tu mungu😢😢"
"Naomba basi nikkmbatie"
Sikumjibu nilifungua tu mikono yangu akanikumbatia kwa muda kidogo, nilijisikia amani kweli ,afu akanks shingoni🙈🙈dah nyiee nilijihisi kihali fulani hivi..
Alex alinitizama machoni akaniambia kwa sauti ya chini akanambia..
"Sorry salma leo nimeshindwa kukulinda naapa halitajitokeza tena ,nipe nafasi ingine" alikuwa anaongea huku ananippsa mgongoni mwenzie naskia kama nipo peponi na Vyenye ananukia sasa woooih nusu usingizi unipitiee😌" ..
Basi Alex aliendelea mie nikawa nasikilizia tu sitaki aache😌😌hapo gari imesimama hata hatujaondoka parking😌basi wakati tuko hapo Gafla nilisikia mlango wa gari umefunguliwa alafu alex akavutwa nje ,
hee nikashtuka nini tenaaaa😳😳
Nilishuka baada ya kuona alex anavutwa kwa nguvu kutolewa nje,mungu wangu nilipiga kelele huku natoka haraka kwenye gari kuenda huo upande.
Nashangaa namkuta inno anampiga ngumi ndugu yake yaan ngumi za uhakika ,alex yupo chini inno kamkalia Juu😳😳
Ni anampiga ngumi za kila sehemu kheee😳na cha Ajabu alex alikuwa ametulia tu yaan hazuii ngumi wala hajitoi ametulia et..
"We mpuzi wewe ,unamwacha huyo mly wako amamfanya salma anavyo jisikia yeye, anamgeuza komedi kufurahisha nafs yake na haufanyi kitu,"
"kwani sikukuambia mie uachane na salma sikukuambiaa eeh sikukuambia weweeee unataka umfanye kama ulivyomfanya yule bint wa paris, "
Inno alikuwa anaongea mpaka anatetemeka watu sasa wakaanza kusogea mana nahisi hawakuw wameona🥵
Nikaanza kumvuta inno kumtoa juu ya alex nikamvuta mwenzangu mpaka akamuachia ,Alex anavuja dam mdomoni, nikawa nawaza hivii huu ugomvi ni kwa ajili yangu au,kwanini inno amepanic sana hivi??
Inno akanishika mkono tuondoke,mi namtazama alex alikua amechafuka anavuja damu,roho ikawa inaniuma kwanini namuacha vile alex afu niende na Inno..
Nilimwambia inno NO. niacheee nitakwenda kwangu mwenyewe nitachukua boda...nilimkataa inno kuliko kuondoka nae bora nichukue boda nijiondokee zangu mwenyewe..
"Inno kwani alikubali sasa?. Aliniambia Noo!! Salma ni usiku huwezi kwenda peke yako ,naomba twende wote" ingia kwenye gari tuondoke...
Je itakuwaje??
Full 1000
WhatsApp 0742133100.