Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Alibeba sefu yake na kuondoka.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Katika tembea tembea za Bieber alikutana uso kwa uso na Nanah.
Nanah alimpita kama amfahamu huku akiigiza upole wake.
Bieber aliukamata mkono wake na kumrudisha pale alipo.
"Unataka nini?" Aliuliza Nanah kwa sauti ya chini na huku akiutoa mkono wake mkononi kwa Bieber.
"Nilikulipia pesa nusu ambayo hukuilipa kwa dereva tax, nahitaji pesa yangu".
Nanah alimtizama kwa hasira kisha akaondoka na kuelekea ofisini kwake.
Bieber alimfuata nyuma na kushangaa ya kuwa ameenda meza ile ile aliyotoka pale na kuongezea kitu katika nguo aliyokuwa aki I design.
Nanah alitoa fedha na kumshikisha mkono.
"Hi Mr Handsome" alisalimia Bob huku akimshika begani Bieber aliyegeuka na kumtizama.
"Naitwa Bob" alijitambulisha Bob kwa mara nyingine na kumuwekea mkono wake karibu na mdomo wake ishara ya am busu.
"Oooohhh Boss Bieber umekuja kutembelea ofisini kwetu?" Aliuliza Doy aliyeingia ndani na nduguye Kurwa kwani walitoka kidogo na kwenda kwenye kikao.
Nanah alimtizama Bieber na kumtizama Doy aliyemuita Boss.
"Ooh Bieber, upo huku? Vipi ungependa twende tukapate chai kwa pamoja?" Aliuliza Shalha akitabasamu na Bieber hakufanya hivyo kabisa.
Shalha aliacha kujichekesha baada ya kuona Bieber akimtizama kama mgeni kwake.
"Utakuwa Sekretari wangu" alimwambia hilo Nanah.
"Mimi?" Aliuliza Nanah akishangaa na Bieber aliondoka akiwaacha.
Shalha alikunja ngumi yake kwa hasira pamoja na sura yake ila alipoona watu wanamshangaa yeye alitabasamu.
Bieber!!!! Alijichekesha akiita na kumfuata kwa mara nyingine tena.
"Mimi sihitaji mazoea na mke wa mtu tafadhali behave". Alisema hilo Bieber na kumkazia macho kisha akaondoka zake.
"Sekretari wake?" Alishangaa Kurwa.
"Sasa nimeamini watu walivyosemaga ya kuwa wewe ni mchawi, yani umekuja jana tu leo unakuwa Sekretari wa Boss?" Aliuliza Doy.
"Na jana amepewa kazi ambayo miaka yote anaifanyaga Shalha" alikumbushia hilo Kurwa.
"I hate you , umeweza kuwa Sekretari wa Mr Handsome?" Aliuliza Bob na Nanah ndo hakuwa amemuelewa yoyote yule kati yao.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Bieber alirudi ofisini kwa kaka yake na kukuta kweli anahamisha vitu vyake.
"Si ihitaji hii ofisini tena"
"Embu acha utoto basi. Unajua wewe ni mtu mzima?" Aliuliza Brown akimgeukia ndugu yake.
"Nataka kuisimamia ofisi ya ma designer, so ofisi yangu iwe karibu na pale"
"Lakini kile ni kitengo cha Shalha, Bieber"
"Nimesema nataka" alijibu Bieber na Brown aliguna tu.
"Dah!!! Huku akishika kiuno chake.
Alimtizama Bieber aliyekuwa serious akimtizama.
Shalha aliingia ndani na Everline aliyekuwa ameshafika ofisini.
"Uko sawa wewe?" Aliuliza Shalha baada ya kumkuta Brown akitizamana na Bieber kama mabeberu mawili.
"Mnataka kupigana?" Aliuliza Everline.
"Ongea na mwanao, asinipeleke peleke. Mimi siyo wewe" alijibu Brown na kuondoka akimuacha Shalha , Everline na Bieber.
"Umemfanya nini kaka yako?" Aliuliza Everline.
Bieber alitaka kuondoka na Everline alimshika mkono akimzuia.
"Nimekuja hapa kwaajili yako, we unataka kwenda wapi?"
"Mama sasa hivi ni asubuhi nani muda wa kazi. Naanda ofisi yangu kuna tatizo kwani?"
"Utawaambia watu wakuandalie, mimi na wewe tunapaswa kuwa na muda mwingi sana leo" Everline alimshika mkono mwanaye na kuondoka naye pale akimkokota.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Boss tunafanyaje?" Aliuliza Sekretari wake aliokuwa na watu wanne wakihamisha vitu.
"Yani naona kazi yangu leo itakuwa ni kupanga ofisi tu".
"Acheni hapa twendeni tukamuangalizie ofisi huyo kisirani" alijibu Brown.
Ufunge hapa sawa?
Ndiyo Boss. Alijibu Sekretari na Brown alitoka na kwenda kutizama atageuza chumba kipi ofisi.
Aliingia hadi ndani ya ofisi ambayo niya ma designer na wote waliinuka wakimpa heshima.
"Za asubuhi jamani"
"Salama" walijibu wote kwa pamoja.
"Kaeni tu muendelee na kazi zenu".
Brown alipatizama pale ndani na aliona kuna nafasi kwa ile ofisini.
"Hivi kwa hiyo nafasi iliyopo hapo. Tukitoa na huu ubao hapa pamoja na shelf si inatosha kabisa kuwa ofisi.
"Ofisi? Ofisi ya nani?" Alihoji Kurwa akimuuliza mdogo wake kwa siri.
"Mmmmhh usishangae huyu Bi mkosi ndo anaandaliwa ofisi maana mganga wake Fundi bwana aloooo".
"Ndiyo pakubwa sana" alijibu Sekretari.
"Hapa tutaweza tu vioo kutenganisha ofisi yake na ofisi yama designer".
"Boss Brown una akili kwelikweli, umewaza vizuri sana ujue".
"Sasa hapa ni kazi ya mafundi kwakweli haya hayatuhusu" alisema hilo Boss Brown na alimuelekea Nanah.
"MAMBO" Alisalimia Brown na Nanah alitengenezea miwani yake vizuri kama mtu mshamba mmoja hivi na kujibu.
"POA"
"Jana uliondoka saa ngapi? Nilikusubiria sana ila sikukuona ukitoka kabisa ofisini"
"Aaammmhhh Boss Brown, sikuwa najisikia vizuri hivyo niliondoka mapema kidogo". Alijibu kwa kudanganya Nanah
"Sawa, basi kama leo hautajali nitaomba nikupeleke kwako".
"Kwangu? Hapana. Kuna wageni. Naishi na mama yangu pia" alidanganya Nanah ambaye hakutaka kabisa Brown afahamu mahala anapoishi.
"Lakini si..........
"Nashukuru ila hapana" alikazia Nanah na Brown aliona kabisa haitakuwa rahisi kumpata Nanah tena katika maisha yake.
Alitabasamu akimtizama Nanah kwa nyuma tu.
Itaendelea In Shaa Allah.