Mayner akiwa ndani alipata kusikia kile kilichozungumzwa na Mama Garma. Alibaki mdomo wazi ๐ฎ, asijue ni wapi alisikia kwamba anataka kwenda kwa mganga? Alijaribu kuchanganya akili yakeโฆ je, aliona ukaribu wa Rasma na mama yake? Lakini kumbukumbu kamili zilimkosa.
โMama kajuaje kama nataka kwenda kwa mganga? Au itakuwa ni mwanga? Mbona anajikinga sana hivi?โ alijiuliza, lakini majibu hayakuja ๐คทโโ๏ธ.
Akiwa katika dimbwi la mawazo ๐, alistuliwa na Garma ambaye alifungua mlango kisha akaingia ndani.
โMama anasema kwamba unataka kwenda kwa mganga ili umroge... sijui kufanyaje... ya kweli hayo?โ aliuliza.
โMganga? Kumroga Mama? Nani ambaye amesema?โ aliuliza Mayner kwa mshangao ๐ณ.
โNi yeye. Nilikuwa naongea naye hapo nje. Kasema kwamba amekusikia ukitaka kwenda kwa mganga. Kama ni kweli unataka kufanya hivyo, ebu simamisha mara moja!โ Garma aliongea kwa hasira ๐ .
โMume wangu, tangu lini umeniona mimi nikienda kwa mganga lakini?โ
โNdio nakuambia hapo. Tusije kuonana wabaya mbeleni. Mambo ya kishirikina, sijui makombe na mitishamba, humu kwangu sitaki. Ukiona unaumwa sana Qurโan ile pale, fungua zako soma ๐ฟ,โ alizungumza Garma huku akiwa na sura ya kuchukiza ๐.
Kwa namna ambavyo alikuwa akiongea, ni wazi kwamba alikuwa amechukia kupita maelezo. Na huu ndio ulikuwa ni ukweli. Kwake, hakupenda kusikia lolote kuhusiana na waganga wa kienyeji ama jadi.
Aliwachukia kuliko hata anavyoichukia njaa. Hakuna hata mmoja ambaye alikuwa akimwamini. Alikuwa na dhana kwamba kila anayekwenda kwa mganga wa kienyeji ni mchawi ๐งโโ๏ธ.
โMume wangu, sio kweli. Nilitegemea kwamba ungeniuliza hospitali wanasemaje hata kabla ya kuuliza kuhusu mimi na mganga. Hata sielewi,โ Mayner alijitetea kwa kuleta habari za hospitali ๐ฅ.
โMama kanichanganya hadi nashahau... enh, wanasemaje?โ aliuliza Garma.
โSina ugonjwa.โ
โKhe! Tena?โ
โNdio. Hadi nashangaa ni nini ambacho naumwa.โ
โUlipima vipimo vyote?โ
โNdio. Nilifanya hivyo. Ila... ila kuna dawa ambazo wamenipa. Ni hizi hapa.โ alisema, kisha aliinuka na kwenda hadi sehemu aliyoweka mkoba wake uliokuwa na dawa ๐.
Alirudi tena sehemu ya mwanzo na kumkabidhi zile dawa Garma, ambaye alipokea na kuzitazama.
โUnameza kwa siku ngapi?โ
โNi tano. Na kama sitakuwa sawa, natakiwa kwenda tena.โ
โInamaanisha huna hata fangasi au magonjwa ya ngono?โ
โNiyatolee wapi? Kila siku nalala na wewe na nimekuwa msafi kupitiliza ๐. Hata hivyo, nikifanikiwa kumaliza tu kama sijapona, basi nitarudi tena hospitali.โ alisema Mayner.
Waliingia katika kina cha maongezi kilichojawa na stori za hapa na pale. Kila mmoja alisimulia na kuzungumza lake, huku mpango wa ndoa ukiendelea kuwa kiini kikuu cha mazungumzo ๐.
Waliambiana namna ambavyo ndoa yao itakuwa ya tofauti โ kuanzia muonekano hata namna ukumbi utapambwa. Hatimaye, usingizi uliwapa salamu, nao walikubali kuitikia ๐ด. Walilala.
---
๐
Asubuhi ilipotia nanga
Garma alikuwa wa kwanza kuamka. Alienda kuoga ๐ฟ. Alipomaliza alirudi tena chumbani, akajiweka sawa hadi alipomaliza. Kisha akamwamsha Mayner.
โNataka kutoka nawahi kwa designer, utaenda kazini?โ alimuuliza.
โHapana, nahisi kama bado nina harufu,โ alisema huku akijinusa ๐คง.
Pua yake ilipokea harufu mbaya, akajikuta akipiga chafya ๐คง na kumtazama mume wake, ambaye alisema:
โZingatia dawa. Hata hivyo, nitaenda pia kuangalia ukumbi. Nahisi kama nitachelewa kurudi.โ
โMh! Ila isiwe kama jana โ ile ilikuwa ni too much. Kupigwa na baridi muda mwingine kunachosha.โ
โHahaha! ๐ Usijali baby. Lakini zingatia, usitoke. Usiende kwa mganga.โ
โBaby bwana, mbona unashindwa kunielewa? Mimi na mganga wapi na wapi bwana?โ alisema Mayner huku akiweka sura ya kuchukiza kidogo ๐.
Garma aliona bora amuage kwa busu ndogo katika paji la uso ๐ huku akisindikiza na neno โNakupenda,โ kisha aliondoka. Alifika hadi sebuleni ambako alimkuta Rasma akiendelea na usafi ๐งน.
โMwangaruka (Habari za asubuhi)โ
โMwangaruka Wawa, Mola sana (Habari za asubuhi, uko poa?)โ
โSalama,โ walisalimiana kwa Kisukuma huku wakipeana tabasamu ๐.
Rasma alimwangalia kaka yake, akagundua kama alikuwa na jambo alilotaka kuzungumza. Ilibidi amuulize:
โKuna nini, mbona kama kuna kitu hivi?โ
โNdio, nataka nikuambie kwamba usimruhusu Mayner kutoka hapa. Na endapo akifanya hivyo basi nipe taarifa.โ
โKwani haendi kazini?โ
โAnaumwa. Akipona ataanza.โ
โMh! Sawa, hakuna shida.โ
โOk,โ alisema Garma, na kuanza kupiga hatua ili kutoka nje. Lakini alikumbuka jambo na kusema:
โHalafu nimekumbuka...โ
Alirudi hadi sehemu ambayo Rasma alikuwepo, kisha akamnongโoneza โ hali iliyowafanya wote wacheke ๐คญ.
โKa fala hivi, nenda huko!โ Rasma alisema. Garma akaondoka mahala pale.
Utani ulikuwa ni sehemu ya familia hii. Licha ya kila mmoja kukuwa, Garma hakuacha kumtania ndugu yake. Muda mwingine alikuwa akimtoa na kumpeleka maeneo mbalimbali, ambako walipiga stori kama ndugu ๐ค.
Kufanya hivi, aliamini kungeimarisha udugu wao. Na hakika alifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana, kwani mapenzi ya Rasma kwa kaka yake yalikuwa makubwa mno โค๏ธ.
Baada ya kaka yake kuondoka, alibaki sebuleni huku akitafakari:
> โUsimruhusu Mayner kutoka hapa, na endapo akifanya hivyo basi nipe taarifa.โ
Ilikuwa ni kauli ya kaka yake iliyopitapita kichwani mwake. Aliwaza โ je, kaka yake alisikia nini kuhusu kile walichokipanga na Mayner?
Wakati anaendelea kuwaza ๐ค, mama yake alitokea huku akiwa na tabasamu la kasi ๐.
โUnawaza kwenda kwa mganga na huyu mwenzako enh?โ aliuliza Mama Garma.
โNani amekuambia?โ
โKhe! Kwani nani hajui kwamba huyu mwanamke ni mchawi? Unadhani sijui? Sasa wewe jifanye unapeleka peleka watu kwa waganga โ ufe huko huko, shauri yako!โ Mama Garma alisema kisha akarudi zake chumbani ๐ช.
Rasma alibaki njia panda ๐ค๏ธ, akiwa amechanganyikiwa na kukosa uelewa wa kile kilichokuwa kinaendelea. Aliwaza โ ni nani alimwambia mama na kaka yake kuhusu mganga? Mwisho aliamua kwenda kumuuliza Mayner.
Alipiga hatua hadi chumbani kwake, akagonga mlango na kujitambulisha. Mayner alimruhusu kuingia.
โAsubuhi sana... kuna nini?โ aliuliza Mayner huku akijiweka sawa.
โMama amejuaje kama tunataka kwenda kwa mganga?โ
โMh! Mwenyewe sijui kwa kweli. Usiku alikuwa akiongea na kaka yako... amemchimbia mkwara mpaka nikasema labda wewe ndio ulisema.โ
โAku! Niseme wapi? Ila sikia, twende tu. Jiandae nami naenda kujiandaa.โ alizungumza Rasma.
Mayner alifikiria kidogo kuhusu aliyosema mume wake usiku na asubuhi. Aliona bado hana uhuru wa kuondoka, hivyo alikataa ๐
โโ๏ธ.
โMimi ndio mlinzi mkuu hapa, najua kila kitu. Kaa kwa kutulia, tuondoke zetu. Utabakia kuumwa hadi lini? Ugonjwa sio wa kawaida huo!โ Rasma alimsisitiza.
โKwa jinsi ambavyo natoa harufu hivi... itakuwa ni kile chupi nilichopigwa nacho usoni?โ aliwaza Mayner, na mwisho akaona hana namna zaidi ya kukubali kwenda kwa mganga ๐.
Baada ya kukubali, Rasma aliondoka kwenda kujiandaa. Huku naye Mayner akibadilisha nguo na kwenda kuoga ๐ฟ. Dakika 50 zilitosha kwao kufanya kila kitu. Walikutana sebuleni.
โMnataka kwenda wapi?โ lilikuwa ni swali la Mama Garma, ambaye alisimama kwenye korido ๐ถโโ๏ธ.
โUshaanza maswali yako?โ aliuliza Rasma.
โNataka kujua. Na kama kwa mganga basi msiende! Litakalotokea, mtajua wenyewe.โ
โBwana, usitutishe. Ebu tuondoke, Wizo!โ Rasma alimshika mkono Mayner ๐ค na wakaondoka mahala pale, wakiwa na matumaini kwamba sehemu wanayoenda watapata msaada wa kuelewa nini kinamsumbua Mayner.
Baada ya kuondoka, Mama Garma alirudi chumbani kwake. Akachukua simu iliyokuwa kitandani ๐ฑ, akaichezea kidogo na kuweka sikioni.
โTayari wameshatoka. Ndio... jukumu ni lako. Utachagua afe nani. Kama ni wote, hakuna shida. Ila itapendeza kama huyu anayeitwa Mayner huyu akafa.โ alisema kama akimpa maelezo mtu ambaye hakujulikana ni nani, kisha akakata simu... ๐ด
ITAENDELEA... ๐ฅ
Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..