Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

Niliolewa na mwana ume mwingine nikiwa kwenye ndoa *6-10* *

27th Jul, 2025 Views 41

________________________________________*

*SEHEMU YA SITA*

Kuna tabia kwenye maisha yangu nilijiapiza sitakaa nifanye.
1. Kutoa mimba. 2. Kwenda kwa waganga na 3.Kuchepuka. ni Tabia ambazo nimeshuhudia madhara ya moja kwa moja kwa wanaofanya hivyo. Hivyo nilijiapiza kamwe sitathubutu maishani mwangu kuchepuka. Haijalishi nitapitia changamoto gani.
Nimeishi ndoa ya mateso sana. Lakini nachepukaje?mume kahama chumba. Kamjengea mdogo wangu nyumba na ni mke wake. Wanaishi maisha ya starehe sana. Sasa si aniache tu wakishi na mdogo wangu?mbona ananiganda?nawaza.
Lulu wangu, mbona umehama kabisa kimawazo?Machozi yanaana kunichuruzika.
Filex nisikilize, hakuna kitu naogopa kama kuchepuka. Naogopa sana. Sijwahi na sitamani kufanya hivyo kabisa. Niliendelea kulia.
Lulu mama yangu, huna sababu ya kulia. Hutakiwi kabisa kulia. Unatakiwa kufanya maamuzi. Tena magumu sana. Kama unasema mumeo kaoa, tena mdogo wako, alafu kahama chumba na sasa una muda hata haki yako yandoa hupati. Na anajigamba kabisa kwamba Mdogo wako ni mtamu kukuzidi, huoni kama hakuhitaji tena na umekuwa mzigo kwake?
Filex alinihoji.
Nilitulia nikiwa natafakari. Nilikuwa nawaza mambo mengi sana.
Kabla sijasema lolote na wala sikuwa na la kusema, Filex alinitazama na kuniambia kwa sauti ya pole pole sana.
Nakununulia simu kesho. Utanielekeza unataka kuipataje.
Kisha nakuachia maamuzi peke yako.
Na utaniambia unataka nini. Kam utaweza kuwa na mimk kimapenzi nitafurahia sana. Ka pia huwezi usifosi. Ila jua nakupenda sana. Tangu ile siku nimekuona sijawahi kupoteza sura yako machoni,moyoni na akilini mwangu. Nakupenda Lulu.
Maliza kinywaji chako nikurudishe . Filex alisema.
Mhhhhh... nilivuta pumzi ndefu kuongiza ndani na kutoa nje.
Acha presure mama. Una bahati kipendwa na mimi.
I am so much selective mamii. Mpaka nimetupa ndoano yangu kwako najua sijakosea. Hapa nasubiri aiza nipoteze chambo changu ama niibuke kidedea na samaki wangu.
Filex aliongea akatabasamu.
Alinifanya nami nitabasamu.
Katika maisha kama una changamoto ya mapenzi ama ndoa ni hatari sana ukiruhusu mwanaume kuwa karibu na wewe. Ni hatari sana. Na kama unafikiri huauko tayari kuacha ndoa ama mume wako ni bora ukae ndani ulie mpaka uzoeee. Lakini kuna wanaume wana ushawishi mkubwa sana.
Tulipanda kwenye gari na kurejea pale aliponishusha. Tayari ilikuwa ni jioni sana. Naniliondoka nyumbani mapema sana.
Mungu wangu. Nitakuwa mgeni wa nani?Naomba tuu Mungu nisimkute mume wangu nyumbani.
Nilifanya manunuzi haraka haraka kisha nikakimbia nyumbani.
Nafika nyumbani nje ya geti naona gari ya mume wangu. Mapigo ya moyo yalianza kudunda kwa kasi sana. Nilianza kuogopa. Sio kawaida yangu kuchelewa nyumbani. Leo ndiyo mara ya kwanza.
Wewe mbwa malaya mshenzi mkubwa... masaa manne ulikuwa wapi?
Nilishtukia tu kofi moja rwaachu, sijakaa sawa kibao kingine,mara mtama mara katoa mkanda kwenye suruali kaanza kunichapa nao. Najizuia lakini simuwezi. Bakoli ya mkanda ndiyo ananichapa nayo naameno ya kejeli.
Alinivutia chumbani kwangu na kuniambia haya vua nguo zoote, alafu nikukague, nikikikuta una harufu ya manii utanitambua. Leo ndio nitakuuua.
Nilinza kuvua nguo zangu na kuziweka kitandani.
Aliniambia vua zoote. Nikavua zote. Akanikagua akaniambia bahati yako.
Enhe, ulikuwa wapi?sema mwenyewe.
Nakuuliza soko gani la masaa manne?
Huku ananipiga.
Nilikuwa nawaza, je nimwambie ukweli ama ninyamaze?
Nakuambia wewe mwanamke sema ukweli. Maana sishindwi kukufuatilia nikajua ulipo. Sishindwi. Bora usem mwenywe. Nikijua kwa jitihada zangu nakukata hiyo shingo mmbwa koko wewe.
Alitoka nje akabamiza mlango paaaaa.
Nillimsikia akisema Omi fungua geti
Omi alifungua geti na akaondoka zake.

*SEHEMU YA SABA*

Omi kashamfungulia geti. Bila shaka huyu anaenda kwa mke mdogo. Unajua kuna nyakati mtu unakuwa na mawazo na tafakari ambayo kiuhalisia majibu na maamuzi unayoweza kuyafanya yanaweza kushangaza kila atakayeshuhudia.
Hivi nina kasoro gari?
Nimekosea wapi?
Na hata kama nimekosea ina maana nastahili haya? Bila shaka hata kama nimekosea basi haya hayapaswi kuwa malipo yangu.
Nilijitazama. Ndani ya maumivu makali na hasira nilitabasamu.
Niliona tabasamu halitoshi. Nikaachia cheko.
Wanakuambia hiviii, muogope anaye tabasamu ndani ya maumivu ama anayecheka ndani ya msiba.
Nicheka kabisa.
Huyu sitamuuliza lolote. Ila si kaha chumba, atanitambua.
Moyoni nimepanga mikakati mizito hasa.
Nilimeza dawa.
Ni kweli nilikuwa nimeumia sana. Lakini nilisema nivumilie.
Kwanza naenda wapi?
Pili kwa niondoke? Tatu huyu naye lazima aumie hasa. Hivyo tatu yangu ni kuunda kisasi. Nataka nimuumize mara kumi zaidi ya nilivyoumia.
Hakurudi usiku huo.
Nilitulia.
Kesho yake saa saba mchana alituma gari yake ya kwendea machimboni. Hakuaga. Alituma tu gari. Moyoni nikasema huyu hajaenda popote anataka tuu kunipima imani. Nami sikutoa kabisa mguu hiii siku. Niliamua kutulia kabisa nyumbani.
Mida ya saa kumi jioni alirudi. Hakunisalimia.alinipita sebuleni akaelekea chumbani. Akakaa kama dakika kumi kisha Kaniita.
Nilimfuata.
Jana ulikuwa wapi?Alihoji.
Nilimwambia nilikuwa sokoni.
Ahaaa.. kwa hivyo unaniona mimi ni kiazi eee. Umeanza umalaya wako alafu unasema ulikuwa sokoni!. Sasa ni hiviii.
Juanzia leo, mguu hutatoa hapa ndani. Yani ukitaka nifanye kituko duniani ni wewe kutoa mguu hapa. Umesikia?
Alifoka.
Nikiachia tabasamu kisha kwa ujasiri nikamjibu hivi.
"Endapo sitakuwa na cha kufanya sitatoka. Lakini nikipata cha kufanya nitatoka"

Unasemaje? Alifoka.
"Bila shaka umesikia"
Mume akishangaa mimi kumjibu hivyo. Alishangaa sana.
Unatoa wapi ujasiri wa kunijibu hivyo?Alihoji.
Mh... niliguna kwanza.
Sikia, mimi ni binadamu kabisa. Nina hisia pia. Umenifanyia ubaya mkubwa sana na nimenyamaza. Sasa naona unataka kuanzisha tena jambo lingine. Ni hivii hapa nitakaa. Ila nikowa na shuhuli nitatoka.
Alisimama ili atake kunipiga.
Moyoni nikajiambia, akilogwa kunigusa tutauana.

*SEHEMU YA NANE*

Hivi nikisema tupigane kwani sitamuweza? Hivi huyu nyang’au ananishinda nini ?
Nilianza kupata hasira za hali ya juu. Nilikuwa natetemeka kabisa na nilikuwa nina hasira na sura imebadilika.
Ha ha ha ha, unanitetemekea mimi kwa hasira? Ni kama unataka kufanyaje? Mume aliongea. Nilimtizama nikamwambia , leo nataka uniguse alafu nione itakuwaje, nataka unipige nione itakuwaje. Nilimjibu.
Alicheka, ha ha ha.
Sikusema kitu chochote Nilikuwa bado namtazama ili atakaporusha tu mkono wake nimpiga ngumi moja kubwa ya shingoni, kama kufa na afe.
Tayari moyo wangu ulikuwa umeshaingiwa na chuki kubwa sana juu yake, sikuwa najali lolote tena, licha ya kujiona mimi si kitu kabisa katika ulimwengu huu.
Akili yangu ilikuwa imevurugika sana.
Kweli wanaouana kati ya mume na mke sasa naweza kuona kabisa sio kosa la siku moja wala masaa kadhaa, bali ni kukusanya visasi, hasira na vinyongo moyoni.
Nikiwa nimesimama kwa hasira sijui alihisi nini ama aliona nini, nilishangaa ameondoka bila kunisemesha wala kunigusa.
Sikutaka nami nimuache aondoke hivyo,
Niliongea, Sikia, nakuambia hivi, koma tena ukome kabisa kunipiga, kama umepata huyo Malaya wako ambaye anatamani hata nife kesho muwe huru, mniache nife kifo cha Mungu lakini sio kwa ajili yenu.
Mume wangu alinitazama na akatabasamu. Kisha akaniambia naona umeshakuwa mwehu.
Aliniambia hivyo, nami nikacheka, Mwehu mama yako aliyekuzaa akakupa roho mbaya ya kuniolea ndugu yangu.
Kabla sijamalizia kuongea nilishangaa nimekatwa mweleka mmoja chini, sikukubali, nami nilijiambia Mungu nisaidie nisimame hapa, Haikuchukua round nikiwa pale chini alinipiga mateke mengi mfululizo ya mbavuni bila kujali.
Watoto walikuwa tu wakisema mama anakufa , mama anakufa.
Nilikuwa tu navizia nipate nguvu ya kusimama pale na niokote chochote nimponde nacho kichwani. Watoto waliendelea kulia na majirani sasa walikuwa wakija na kutuamua. Nilibahatika kuokota chupa ya soda, iliyojaa soda. Eee Mungu nisamehe dhambi zangu zoote, nauaaaa… nilikuwa nikisema hivyo, na wakati huo nilipiga chupa paaaa, na kwa bahati jirani mmoja akasema Kisimaaa unakufa inamaaaa… Mume akainama ile chupa ikapiga ukutani paaa vipande vikatapakaa chini.
Mume wangu alipata hasira sana, na uzuri watu walikuwa wako hapo,,,, hivyo walikuwa wamemshika , mimi nikiwa nimechakazwa kwa kipigo.
Unataka kuniua? Unataka kuniua , mwanamke fedhuli mkubwa wewe,unataka kuniua? Aliendelea kufoka, na wakati huo nikiwa bado natamani kumvizia ili nijue namfanya la kumfanya.
Ila wanaume jamani, yani kamuolea mdogo wake alafu anampiga, si akadinyane huku amuache mama wa watu jamani….. alisema mama mmoja.
Mwingine alidakia,,,, Yani jamani huyu mama uzuri wake woote umeisha, ila wanaume Mungu anawaona……
Pembeni nilisikia mwingine akisema, hivi kwani mwanaume ni huyo Kisimati tu, si kuna wanaume wengi,si aondoke?
Aondoke ya nini? Hakuna haja yakuondoka, dawa ni akae hapo hapo atafute kipoozeo chake , huyu mwanaume akitoka kwa hawara yake nay eye anakuwa katoka kwa hawara yake ngoma droo.. haloooo ya Mainda. Mimi jamani huu ujinga sifanyi, yani watu wakatikiane huko mimi nikonde akaaa, na mimi ni mwendo tu wa kukatikia na kukatikiwa ha ha hahaaaa halulaaaaa.
Alisema Mainda mwanamke jirani ambaye ni mrembo sana na anajipenda sana licha ya mume wake kuzaa na wanawake watatu mtaani hapo.
Nilisikia kila mwanamke aliyekuwa akiongea, nami nikajiambia sasa sijui nachukua ushauri wa nani, nani nichukue ushauri wake.
Nikiwa nimekaa pale chini kitako sebuleni, nilimkumbuka Filex. Nilijikuta natabasamu na kusimama.
Unaenda wapi jamani? Kajiandae hata uende polisi ukamshtaki tu upewe fomu ya kwenda kujitibu. Alisema mama mmoja.
Wala sijaumia, nilijibu, sijaumia.
Mhhh… hivi yale mateke unadhani utajua sasa hivi kama hujaumia? Nenda hospitali jamani, nenda unaweza kukuta hata kapasua bandama… kisha akacheka ha ha ha.
Samahani nacheka ila sichekei mazuri, nenda hospitali mama yangu.
Asante kwa ushauri. Nilisimama na kuingia ndani chumbani.
Nilikumbuka Filex alinipa namba zake za simu nikaziandika na kuficha kile kikatasi kwenye brazia. Nilifuata mahali nilipokuwa nimeweka kile kikaratasi. Nilikuta zile namba na nilizikariri kwenye akili yangu. Na kujiahidi ninaoga kisha ninaelekea kumpigia Filex simu.
Nilimaliza kuoga, na nikaaga watoto kwamba ninaelekea hospitalini. Njiani dereva wa bajaji nilimuomba anipatie simu yake ili nipige kwa Filex.
Filex alipokea na nikamueleza kwamba nimepigwa sana naelekea hospitali.
Sasa kama umepigwa hivyo Lulu jamani, si uende polisi kwanza? Alinishauri.
Hapana, hata nikienda polisi kwani ndio itakuwa hajanipiga? Nilimjibu.
Hapana walau ataonywa, haitabadilisha wewe kuwa hujapigwa lakini walau atapata hofu kwamba siku nyingine asikupige, atakuua ujue mimi nitakukosa,, Filex aliongea kwa huruma sana.
Uko wapi sasa? Naweza kuja? Aliniuliza.
Ndio, wala lengo halikuwa mimi kuja hospitali, kweli amenipiga lakini sina maumivu makali ya kuja hospitali , lengo langu ilikuwa ni nitoke ili niweza kukupigia simu tu basi. Nilimjibu.
Oooo, jamani, asante sana mnooo , nashukuru mno mno mno. Basi nikuombe nikukute pale kituo cha mafuta nakuja hapo ndani ya nusu sasa Lulu wangu, nikuone alafu tuongeee kidogo, nione nakusaidiaje mama yangu, sawa eeee. Filex alisema.
Sawa , nitakuwa hapo ndani ya nusu saa. Nitakuwa hapo.
Nilijikuta navutiwa na Filex. Liwalo na liwe. Nilijisemea. Hivi kweli nitaendelea kuteseka hivi mpaka lini? Nitaendelea kuteseka hivi mpaka lini lakini? Nilijiulilza.
Nilimuelekeza dereva wa bajaji anipeleke mpaka kwenye kituo cha mafuta aliponielekeza Filex nami nikaelekea hapo.

*SEHEMU YA TISA*

Kwa hulka za Kitanzania, imezoeleka mtu ama mwanaume akipata pesa basi atajulikana sana na kupewa heshima haijalishi anakosea ama hakosei. Na hii kwa mume wangu sasa ilikuwa ni jambo la kawaida kwake kupata heshima. Pesa zake na utajiri wake haijalishi alikuwa kijana mdogo tu lakini zilimpati heshima na sifa nyingi sana, alikuwa akijulikana kila mahali. Lakini pia gari zake ambazo alikkuwa akitembelea na gari ambayo alimnunulia mdogo wangu(Mwanamke aliyenikwapua mume) Yalikuwa ni magari ya kifahari sana na sio rahisi kama ungeona gari ya aina hiyo kwa mtu mwingine, labda kama ungetoka na kwenda miji mikubwa kama Mwanza ama Dar es salaam Tena ukutane na wanaume wenye pesa hasa ama wanawake wenye pesa hasa.

Mali zake na utajiri wake ulimfanya akajulikana hasa na hata angekosea basi hapakuwa na wakumrekebisha. Alitoa michango mikubwa sana kanisani kwenye shughuli za ujenzi wa kanisa, na sio kanisa ambalo tunaabudu, bali alipata mialiko mingi sana kwenye makanisa mengi kwa ajili ya kuchangia, na tayari alishaanza kuwa mgeni rasimi. Na kama basi angetoa mchango kidogo sana basi ni shilingi milioni tano tena cash. Na michango yake mingi ilikuwa ni shilingi milioni kumi mpaka ishirini kulingana na aina ya sehemu anayoalikwa.

Sijui kwa nini hakukuwa na mtu wa kumkaripia kwa alichokifanya, sijui kwa nini hata viongozi wa kidini kwa nini hawakumkaripia kwa alichokifanya, na zaidi sana mtoto wao alikuwa akipata huduma zote za kiroho kwa kile kinachodaiwa mtoto ni malaika tu hana kosa.

Wana familia nao hakuna aliyemkaripia wala kumuonyesha alichokifanya ni kosa. Ama kweli wanasema penye uzia penyeza rupia. Hii kwake ilishika hatamu.

Niliendelea kuonekana mimi ndiye mwanamke msaliti kwa kuuza mali za familia na kujiuzia. Kila niliyejaribu kumueleza kosa langu aliniambia hilo ni kosa kubwa sana.

Nilibaki najilaumu sana kwa nini ile siku nilifanya maamuzi yale, lakini wanasema kujua huwa hakutangulii lakini majuto ni mjukuuu. Nami sasa naendelea kuwa na majuto.

Dakika kumi na tano zimeisha tangu nifike kituo cha mafuta kama Filex alivyonielekeza. Nimeshamua liwalo na liwe.

Nageuza shingo kuelekea inapotoka sauti ya kuite jina langu. , nah ii ni baada ya kusikia sauti ya kiume ambayo niliweza kuitambua ikiita Lulu, Luluuuu… Nilieuka na kukutana macho kwa macho na Filex. Aliachia tabasamu lake na kuashirikia kwa mikono na macho kwamba nimfuate pale alipokuwa. Nilisogea na aliniam bia,

Ingia kwenye gari bibie.

Nilipanda kwenye gari na aliondoa gari.

Pole sana Lulu, pole sana. Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi.. Hivi wewe ni mwanamke wa kupigwa kweli? Ila jamaa pesa inampa kiburi. Pole sana Lulu . Binafsi nakupenda sana, na ukinihakikishia uko tayari kuwa na mimi niamini nitakuoa kabisa. Ila ninajua unaogopa sana, lakini usijali. Nitahakikisha nakusaidia, nakupenda sana Lulu. Nihakikishie tu unanipenda niwe na amani ya moyo.

Ndio nakupenda Filex, nilisema bila kufikiria, kutafakari wala kushauriwa. Nilipokuwa napigwa na Mume wangu, nilikuwa nasikia wanawake wakisema maneno mengi nikiwa pale chini. Yale yalitosha kunionyesha mimi ni aina gani ya mwanamke na ninapaswa kuchukua maamuzi gani lakini pia nilijua jinsi ambavyo ndoa nyingi zimewachosha wanawake na wanaishi vivuli vya ndoa na sio ndoa.

Kweli Lulu unamaanisha? Filex aliniuliza tena.

Ndio, ninamaanisha na ninatamani hata kesho niondoke kwenye ule mji nirudi kwetu, ni vile tu yani sijui natakiwa kufanya nini. Nilianza kulia tena.

Usilie, usilie, niko hapa kwa ajili yako. Nataka kwanza nijiridhishe kama kweli naweza kurejeza, tabasamu lako, sura yako, urembo wako na rangi yako,, nataka kwanza nijihakikishie hilo. Filex alisema. Kisha akatoa simu kwenye boksi lake.

Chukua simu hii. Na line nimesajili kwa jina langu mpenzi. Hii ni kwa ajili yangu na wewe tu,. Mimi sitakuwa nakupigia bali wewe muda wowote nipigie. Muda wowote nipigie nimekuruhusu. Umesikia mrembo? Filex alisema.

Ndio nimesikia.
Alinipatia simu, nilifungua na kuiangalia, ni simu nzuri sana ilikuwa na risiti yake kabisa.

Asante sana Filex, asante sana. Nilisema.

Bado hujashukuru, bado, Utashukuru sana Mmrembo. Yani nataka nikubadilishie usemi wako, kila unaponiona useme tu asante. Ndicho ninachotaka. Filex alisema kisha akatabasamu.

Alinifanya na mimi nikatabasamu pia.

Alifika mahali kisha akaniambia, nataka tuegeshe gari hapa hapa, kwani tukishuka watu wengi wanakufahamu hapa sio mahali sahihi. Hivyo nataka kukuagizia chakula ule ushibe, nikupe na fedha kidogo za kwenda hospitali kesho kupata matibabu sawa mpenzi? Kisha nikurudishe nyumbani umesikia mpenzi?

Ndio nimesikia. Nilikuwa niaitikia nikiwa sijali lolote lile. Na nilikuwa natamani sasa hata niachike tu niwe huru na maisha yangu. Kumbe hata ukiwa na watoto unaweza kupendeka? Nilijihoji na kujiambia na kujiaminisha kupendwa kupo tu.

Kililetw chakula. Tulikula kisha akaniuliza unatumia kinywaji gani?

Niitulia kidogo nikamambia soda.

Hapana soda sio nzuri, unaonaje kama utakunywa mvinyo glass moja tu? Glass moja tu kwa ajili yangu.

Niliguna kidogo kisha nikamwamb ia basi sawa niagizie.

Sijanywa pombe muda mrefu sana, kama miaka mitatu, leo nakunywa nini kitatokea?

Nilikuwa najiuliza kimya kimya. Glass yangu ya mvinyo ilifika na niligugumia kap kap. Filex aliachia tabasamu kisha akasema ngoja upewe ingine.
Tayari muda ulikuwa umeshasogea sana, ni jioni kabisa.
Nilikunywa tena glass ya pili. Na ya tatu na sasa ni kama nilikuwa nimeanza kulewa Fulani hivi. Haikuwa kulewa ya kutojitambua, ila nilikuwa nimelewa kiasi.
Tulimaliza kuongea na anilirudisha mpaka pale pale kwenye kituo cha mafuta na kuniacha pale. Niliita bajaji ili inipeleke nyumbani. Ilikuwa ni saa mbili kasoro dakika ishirini nilipokuwa naingia nyumbani .
Kaka alinifungulia geti, na akaniambia baba kasema ukirudi nimpigie simu ajue umefika saa ngapi. Kijana aliniambia
Sawa mpigie mwambie ndio naingia.

*SEHEMU YA KUMI*

Kaka alimpigia mume wangu simu na alimtaka kaka anipe simu niongee naye.

Umeanza kiburi eee? Yani naondoka na wewe unaondoka na unanirudia usiku nyumbani kwangu, ulikuwa wapi? Mr alihoji.

Mh… niliguna kwanza,, sikia alafu naomba unisikilize vizuri sana.

Wewe kuniona sifai haina maaa sifai kweli, ninafaa sana na ninapendeka, umeshaamua kuwa na mke wako si utulie, mimi kutokuwepo kinakuuma nini? Si una mkeo mwenye kismati kama ulivyosema? Huyo ishi naye, huyo ndo akichelewa nyumbani mhoji. Ila mimi niache na ratiba zangu , najitafuta nikijipata hutaniona hapa kwako. Nilimjibu mume wangu hivyo.

Ni wewe unaongea hivyo? Ni wewe? Unatoa wapi kiburi cha kunijibu hivyo?

Sio kiburi, sio kiburi kabisa, ni uhalisia, wewe umeshaoa mke wako mwingine, umenifanya mimi punching bag, sasa nikiwa sipo ama nachelewa kurudi nyumbani kinakuuma nini? Kwani nia thamani tena machoni pako? Si una mwanamke wako?

Anza kujifunza kunichukia maana hii ndiyo itakuwa ratiba yangu mpaka nijipate. Nimechoka kusimangwa, nimechoka.

Nilisema hivyo kisha nikazima kabisa na simu.

Mr najua ni kama hakuamini. Niliingia ndani na kupitiliza chumbani moja kwa moja. Ninajua anapenda kunikagua. Sikuoga ila niliswaki tu. Nikachukua chai yangu nikanywa nikawa tu tumejilaza chumbani natafakari. Halikupita lisaa naye aliwasili.

Ulikuwa wapi? Ndilo swali la kwanza alilonihoji.

Nilitoka kwenda hospitali kucheki afya yangu. Nilimjibu.

Mh… aliguna. Eenhe umeambiwaje?

Nilicheka kabla sijamjibu, kisha nikamwambia nimeambia siumwi popote ni mzima wa afya njema. Nilimjibu.

Alisimama na kuniambia haya nenda chumbani kwangu nikakukague.

Namjua, ni mwanaume wa kupenda ugomvi na kupiga. Kama ningekataa ni lazima angenipiga sana. Yani nilikuwa na hasira lakini nilisema ngoja tu nivumilie. Lakini pia nilijipongeza kwa kutokuoga maana lingezuka tafrani la mwaka.

Niliongoza chumbani kama ilivyo ada. Nilifika na nilikaguliiwa. Alijiridhisha na kunichia.
Moyo wangu ulikuwa na hasira na uchungu sana. Nilijiambia lazima hii tabia niikomeshe. Ni karibia miezi mitano hatujafanya kabisa tendo la ndoa. Licha ya kulala chumba kimoja . Hivi hii ni ndoa ama ni maigizo? Nilikuwa najiuliza.

Itaendelea.......
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Niliolewa na mwana ume mwingine nikiwa kwenye ndoa *6-10* *  >>> https://gonga94.com/semajambo/niliolewa-na-mwana-ume-mwingine-nikiwa-kwenye-ndoa-6-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest