Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

ππˆπ“π€πŠπ”π†π€ππƒπ€πŸ˜ ⁽NΙͺα΄›α΄€α΄‹α΄œκœ°α΄œα΄€α΄›α΄€ α΄˜α΄α΄˜α΄α΄›α΄‡βΎπŸ₯° 3

27th Jul, 2025 Views 30



*______________________________*

𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 π‘Ίπ’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š

Kesho yake nikiwa kazini majira ya mchana Patrick alikuja akamkuta mama T walisalimiana hukuakiwa ananiangalia na Mimi nilimtupia jicho huku nikiwa naendelea kumuhudimia mteja Patrick alinikonyeza
" Yani huyu kaka anahangaika inamaana hajawahi kuwa na mwanamke au mihemko yake inampeleka vibaya . Walitaniana Tania a na mama T Kisha wakatoka pamoja muda uleule simu yangu iliingiza messeg lakini sokuhangaika nayo kwasababu nilikuwa na mteja .

Nilipomaliza kumuhudimia mteja nilichukua simu na kuangalia nilishangaa kuona message ya hela tena laki mbili niliamgalia mara mbili mbili huku nikijiulizs ni nani aloekosea na kunitumia Ile hela
" Jamani watu wanajua kunitega na hizi shida zangu alafu wanakosea kutuma hela nikapanga mpaka ikifika jioni hamna aliejotokeza napenda kutoa natatua shida zangu .

Nilipomaliza kutafakari na kutaka kuweka simu ili niendelee na kazi nyingine Patrick alikuwa anapiga
" Jamani huyu Kaka king'ang'anizi kwani hajiongezi . Nililalamika na kuipokea Ile simu kabla hata ya salamu nikamwambia
" huu Ni muda wa kazi tafadhali Kama huna Cha maana Bora ukate simu au nikate Mimi
" Hapana Tatiana usikate Kuna pesa nimekutumia umeiona . Nilishangaa
" Wewe kwanini umetuma Sasa na umetuma kwaajili ya nini?
" Ni yako kwaajili ya lunch
" Khaaa hata Kama ndio yote hii.
" Basi Kama umeipata endelea na kazi nitakupigia badae. Patrick alikata simu nikiwa bado sijamalizana nae.

Kila siku Patrick alikuwa anakuja kazini kwetu na kutaka huduma na kutaka ahudumiwe na Mimi tu kitendo hicho Cha Patrick kutaka huduma yangu kulikuwa kinamkera Paulina Ila hakutaka kuonyesha zaidi ya kuishia kusema mafumbo lakini hakuna aliemjali wakati mwingine alijinunisha na kuamua kucheka mwenyewe. Siku moja mama T alikuja na kuingia kwenye ofisi yake Kisha akaniita nilienda haraka na kusimama mbele yake akaniruhusu nikae nikakaa akaniuliza
" Unamfahamu Patrick?
" Ndio namfahamu
" Una ukaribu nae gani? Hili swali lilimshitua na kunifanya niwe na kigugumizi
" Sina ukaribu nae namchukulia Kama mteja tu.
" Kweli ?
" Ndio boss
" Kuna Mambo Patrick ameniambia kuhusu wewe . Mapigo yangu ya moyo yalianza kwenda Kasi huku nikimuita majina ya ajabu
" Huyu mshenzi atakua kamwambia ujinga gani mama T akiniharibia atanitambua kichaa Yule asiechagua jalala la kwenda kula .
" Hivi unajua Patrick ametokea kukupenda na anania njema Sana na wewe..mama T aliniambia na kufanya nione aibu
" Kweli huyu kichaa anaanzaje kumwambia maneno haya huyu mama inamaana ameshindwa kuniambia mwenyewe tukaelewana .
" Tatiana ... Mama T alimuita nikamuangalia
" Umenisokia nilichokwambia ?
" Nimekusikia na alishawahi kuniambia lakini naogopa kuwa kwenye mahusiano nae simfahamu vizuri.
" Patrick Ni mwanaume ambae katulia na mwenye msimamo na mpaka amekuja kuniambia Mimi amini kweli anakupenda Kama unampenda mchunguze
" Sawa nimekuelewa.
" Sawa Ila sikulazimishi na wewe una maamuzi yako
" Sawa. Niliondoka na kwenda kuendelea na kazi zangu huku nikiyatafakari maneno ya mama T. Zilipita wiki mbili Patrick hakuja pale barber shop na Wala hakunitafuta nikajikuta nateseka kwa kumiss kumuona nilikuwa namfikiria Sana mpaka nikawa najishangaa imekuwaje mpaka ikawa hivi Ina maana na Mimi nilikuwa nimeshampenda Ila nilikuwa namringia
ππˆπ“π€πŠπ”π†π€ππƒπ€πŸ˜ ⁽NΙͺα΄›α΄€α΄‹α΄œκœ°α΄œα΄€α΄›α΄€ α΄˜α΄α΄˜α΄α΄›α΄‡βΎπŸ₯° 4

*______________________________*

𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 π‘Ίπ’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š

Nilitamani nimpigie simu ilimradi nimsalimie ili nipate kusikia sauti yake lakini nikahofia huwenda kabadilishe maamuzi kapata mwanamke ambae wanapendana siku hiyo nilikuwa na mawazo Sana mpaka nikakosa Raha mpaka wenzangu wakaniuliza
" Tatiana unashida gani leo hujachangamka sijui unawaza nini au Shem kazingua Nini
" Mmmm mama kitu Kama hicho si unajua siku hazifanani .

Nilivumilia mwisho uvumilivu ulinishinda nikachukua simu yangu na bonyeza namba ya Patrick Ila nilipotaka kupiga nikajikuta najiuliza
" Sasa nikimpigia ndio nakwambia nini wakati nilikuwa najishauwa sitaki kuongea nae . Nikiwa bado natafakari nipige au nisipige alikuja mteja na kunisalimia
" Mambo .
" Safi . Niliitikia salamu huku nikiwa naweka simu kwenye mfuko wa suruali nilivyokuwa nimevaa kumbe simu ilikuwa imejipiga bila Mimi kujua na Patrick alikuwa kapokea Mimi nitaendelea kuongea na mteja
" Dada nahitaji huduma ya massage .
" Sawa karibu twende nikskuhudumie. Niliongozana na mteja mpaka chumba Cha massage na kuanza kumpa huduma baada ya dakika kumi mlango ulufunguliwa kwa nguvu nikashangaa kumuona Patrick kaingia huku akiwa kakasirika alinifuata na kujishika mkono na kutaka kunitoa nje Yule mteja alinyanyuka na kumwambia Patrick
" It's bro vipi mbona unazingua kwanza unaingiaje bila hodi hebu jaribu kuheshimu kazi za watu. Patrick aliniachia mkona na kumsogelea Yule Kaka na kumuangalia kwa dharau
" Wewe kwa pesa gani mpaka ufanyiwe massage na mpenzi wangu huyu yupo hapa kwaajili yangu tu. Nilibaki kumshangaa Patrick nikahisi kapagawa nilimsogekea na kumwambia
" Patrick usiniharibie kazi huyu Ni mteja anahitaji huduma yangu hata wewe ukitaka nitakupatia huduma Ila katulie kwanza nje nimalizie huyu . Patrick alichukua pesa mfukoni kwake akamtupia Yule Kaka wa watu usoni
" Shika hiyo hela kafanyiwe massage sehemu nyingine .alimgeukia na kutoka na Mimi mpaka nje
" Patrick unanipeleka wapi hebu niache bwana . Patrick hakujali alifungua mlango wa gari na kunilazimisha nipande huku saloon alikuwa anatushangaa na wengine wakiulizana Patrick kapatwa na Nini.

Patrick alipanda kwenye gari na kuliwasha
" Patrick unajua unaniharibia kibarua changu
" Acha kiharibike Nina uwezo wa kukulipa peza zaidi na unayolipwa. Patrick alionekana kuvurugwa nikaamua kumuacha afanye anachojisikia aliendesha gari na kwenda kulipaki pembeni ya barabara Kisha akaegamia kwenye kiti na kuangalia juu kwa sekunde kadhaa Kisha akamuangalia macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira
" Tatiana ukipiga simu ili kunijulisha kuwa unaenda kutoa huduma ya massage kwa mwanaume ? Nilishangaa maana yalikuwa mageni kwangu
" Mimi nimekupigia simu saa ngapi?
" Kwahiyo unakana hebu angalia simu yako mtu wa mwisho kumpigia Ni Nani. Nilitoa simu na kuangalia Mungu wangu Ni kweli Ilionyesha ningempigia
" Samahani itakuwa bahati mbaya ilijipiga . Patrick alicheka kwa dharau
" Hainiingii akilini inamaana hiyo simu yako unachagua mtu wa kumpigia alafu inajibonyeza na kunipiga yenyewe na kwa Nini owe Mimi na sio watu wako wa karibu ambao unawasiliana nao kila siku. Kwa hapo sikuwa na lakujitetea nikabaki na aibu Patrick alizidi kunikodolea macho .
" Tatiana naomba unipe jibu moja upo tayari kuwa na Mimi ? Jamani jamani linapokuja swala la kumkubali Patrick najikuta siwezi kuongea Wala sielewi nitoe jibu gani nabaki kujikanyaga Patrick alirudia kuuliza kwa Mara ya Pili nikajikuta nagunaguna .

Patrick aliwasha gari na kugeuza aliendesha kwa Kasi huku akiwa kakasirika hakutaka hata kuniangalia alinifikisha mpaka saloon akanishusha na yeye kuondoka zake niliingia saloon nikiwa mnyonge na kwenda kukaa kwenye sofa Paulina na Martha walinifuata na kuniuliza
" Vipi mbona kinyonge Patrick kakufanya Nini ?
" Hajanifanya chochote na sijui kwanini kanifanyia fujo mbele ya mteja . Joe kijana tunaefanyanae kazi pale saloon alimuangalia Kisha akasema
" Ukiona jogoo linakuzungukia sehemu ujue Kuna mtetea limeona kwahiyo Patrick amakuelewa Tatiana na anawivu na wewe usijifanye humuekewi kijana mwenzio. Martha alisapoti usemi wa Joe
" Nimekuelewa Joe Patrick huwa anamasihara Sana na wadada Ila kwa Tatiana naona Kama yupo serious. Paulina alibinua midomo na kusema
" Hana lolote umalaya unamsumbua Patrick akiona msichana mgeni anataka kupita nae Sasa ukijilegeza ukaona anakupenda kweli atakupitia na kukuacha hapo waulize wenzio. Martha aliguna
" Mmm Paulina acha kukuza Mambo una ushahidi na unayoongea
" Ndio unajifanya hujui Kama Patrick chovyachovya.

Maneno ya Paulina yalikuwa yananiumiza kwani nilikuwa nimeshaanza kumpenda Patrick na mama T alinihakikishia kuwa Ni kijana anaejitambua inakuwaje Paulina aniambie Yale maneno sikujua nimuamini nani.
Ilipita mwezi mmoja sijamuona Patrick nilitamani nimuone hata maramoja kila siku nilopoenda kazini nilijipa moja labda leo ata kuja lakini ilikuwa hola nilianza kujutia kwanini nilishindwa kumwambia ukweli Kama nampenda. Niliamua kuanza kufuatilia taarifa zake ili nijue Ni mtu wa aina gani nilifikiria muulize Martha kwakuwa ndio nilikuwa naelewana nae na nimtu wakuficha Siri za mtu japo alikuwa Ni muongeaji nilimfuata na kumuomba badae tuonane
" Martha naomba tuonane baada ya kutoka kazini Kuna Mambo Fulani nataka tuongee.
" Kuna Nini
" Mbona unaharaka tulia tutaongea badae
" Nidokeze kidogo maana Nina kimuhemuhe
" Tuliza hicho kimuhemuhe chako endelea na kazi.

Baada ya kutoka kazini Paulina aliondoka na sisi tulielekea kwenye mgahawa uliopo karibu na sehemu tunayofanya kazi tukaagiza sambusa na juice
" Haya maongezi yatakuwa mazito mpaka yumekuja kuongelea huku Tena tukipooza Koo kwa juice ya baridi . Ilibidi nitababasamu nilitafakari nianzie wapi kumuuliza nikaanza kwa kusema
" Martha Kuna Jambo nataka uniambie ukweli usinifiche kitu
" Nadhani unanijua vizuri shoga yangu Mimi huwa sizungushi Mambo huwa na nyooka Kama rula niambie unataka kujua Nini
" Nakujua vizuri shoga yangu nilikuwa nataka kumjua Patrick Ni mtu wa aina gani pamoja na tabia zake naomba unieleze unavyomjua . Nilishangaa Martha anaangua kicheko huku akiniangalia usoni . Kicheko chake kilinifa ya nijisikie vibaya na kuona aibu maana sikujua ananicheka kwasababu gani
Soma mpaka mwisho kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ππˆπ“π€πŠπ”π†π€ππƒπ€πŸ˜ ⁽NΙͺα΄›α΄€α΄‹α΄œκœ°α΄œα΄€α΄›α΄€ α΄˜α΄α΄˜α΄α΄›α΄‡βΎπŸ₯° 3  >>> https://gonga94.com/semajambo/nitakuganda-n--3
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest