Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI *SSEHEMUYA 10

27th Jul, 2025 Views 16



Chris alisimamisha gari kisha akamtaka ashuke. Alielewa fika mtu huyu hakuwa na ratiba za kwenda saluni hivyo alimpa shilingi elfu 50 bila kujali uwepo wa Dorin.
Hakutaka kusubiria shukurani aliwasha gari wakasepa.

"Kwanini ananipa hela mbele ya Dorin, huenda wakawa washikaji tu....lakini kwanini wawe na mazoea ya kuazimana majiko ilihali ni jinsia mbili tofauti...potelea mbali" Jamila aliongea ile anataka kuweka hela kwenye brazia yake Kibaka mmoja alipita nazo, kwa huruma alimuachia 2000 kama nauli ya aendako.

Jamila si mwepesi wa kutokwa machozi alijikuta akicheka tu, aliamini haikuwa ridhiki yake.

Upande mwingine Chris alisimamisha gari lake mahali wanapouza mitungi ya gesi ya kila aina.

"Nitakununulia mtungi mkubwa wa gesi....nina uhakika unachoka sana kuja kwangu kupika"

Dorin alitabasamu, siyo kwamba hakuwa na uwezo wa kununua gesi, ni vile alihitaji tu ukaribu na Chris

"Ahsante kwa ofa yako, inaonekana hutaki niwe nakuja nyumbani kwako, mwanzo nilihisi unafurahia vile navyokuja kwako lakini nimeona haufurahii hata kidogo"

"Mimi na wewe ni marafiki wakubwa, nina uhakika hiki kitu hakiwezi kubadilika. Napenda pia uwe unakuja kwangu kupika lakini kwa sasa inaweza kuleta shida kwa sababu kuna msichana nataka awe anakuja kwangu mara kwa mara. Nina uhakika atajisikia vibaya endapo kila mara atakuwa ana kukuta nyumbani kwangu" Chris aliongea

"Unaongelea msichana yupi?...yule muuza karanga au kuna mwingine" Dorin aliuliza

"Huyo huyo...."

"Ni kitu gani umefata kwake sasa, isije kuwa ana nyota kali ya mafanikio lakini kama ni kimuonekano mbona ni kama unajidhalilisha hivi"

"Nimevutiwa naye hivyo hivyo naomba usinivunje moyo.... ndiyo ni muuza karanga lakini kauendesha moyo wangu"

"Okay, ninunulie hiyo gesi niondoke.... nafurahi kuona umempenda muuza karanga" Dorin aliongea huku chozi likidondoka, Chris alinyoosha mkono akalidaka kabla halijafika chini

"Kwanini unalia hasa baada ya kusikia nampenda yule muuza karanga"

"Ni kweli hujui?....eti ni kweli hujui kama moyo wangu unakutaka wewe, nimekuwa ni kikupenda kwa muda mrefu sasa. Naumia kuona una mchagua mtu mwingine..."

"Mimi na wewe tunapendezea kuwa marafiki,...sina vigezo vya kumiliki mtu mzuri namna hii kama wewe"

"Emu ninunulie hiyo gesi kwanza niondoke zangu, naamini utapata wasaa wa kufikiria kuhusu ombi langu...." Dorin aliongea kisha akafuta chozi lake

Chris alimnunulia gesi kama alivyo muahidi, baada ya hapo alimpeleka mpaka nyumbani kwake.

Wakati wa kurudi anashangaa baada ya kumuona Jamila, hakuwa pekee yake alikuwa na Kijana mmoja hivi mtanashati akimpiga sound.
Kuna namna Chris alijisikia wivu hivi, wakati anawapita aliwarushia tope makusudi kabisa

Jamila aliporomosha matusi huku akilisindikiza kwa macho gari la Chris.
Hakuweza kumsikiliza tena Mwanaume huyu namna anavyo mtongoza.

Kuna hasira iliwaka ndani ya moyo wake, kurushiwa tope ilikuwa ni kama udhalilishaji kwake.
Isingekuwa rahisi kuacha hili jambo lipite.
Alitembea kwa miguu mpaka alipofika nyumbani kwa Chris

Chris hakuwa hata amepumzika alishtukia Jamila huyo hapo tena akiwa amekunja sura yake kabisa

"Mbwa wewe kwanini umenirushia matope hivi unajua ni kiasi gani umenidhalilisha....hii nguo utaifua siku ya leo" Jamila alionesha hasira zake waziwazi

"Mimi huyu nimekumwagia matope au una sababu zako tu...." Chris alivunga

Jamila hakuwa na subira, alimrukia wakadondoka wote chini, ukweli ni kwamba hakuwa na hasira tu za tope. Roho yake ilimuuma kwanini Dorin hupenda kuja kupika kwake.
Alifanya vurugu huku akijaribu kunusa pua zake kama atasikia harufu ya vitunguu vikikaangwa. Lakini kulikuwa kimya....

"Kwani huko jikoni hakuna mtu...." Aliuliza

"Kwahiyo uko hapa kujua kama kuna mwanamke mwingine na si kunihukumu kuhusu tope nilizoku mwagia si ndiyo!" Chris aliongea kisha akamgeuza Jamila akawa kwa juu yake

Mapigo ya moyo wa Jamila yalienda juu baada ya kuhisi maumbile ya Chris yana mgusa gusa

JE NINI KITAENDELEAAA!
FULL 1000
SIMULIZI HI IMEKAMILIKA MPK MWISHO KABISA
BEI NI 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BIASHARA YA KARANGA ILINIPA MUME DAKTARI *SSEHEMUYA 10  >>> https://gonga94.com/semajambo/biashara-ya-karanga-ilinipa-mume-daktari-ssehemuya-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest