Story na Nash
Tsap 0773792227
(Location; Kigali, Rwanda)
Japo mvua ilikuwa inanyesha lakini Paulina alimhimiza Binti yake waongozane sehemu aliyokusudia 😒😒😒
"Mama, mvua ni kubwa kwanini tusisubiri ikatike kwanza😒" Mariah alizungumza kwa sababu hawakuwa hata na mwamvuli🙄🙄.
Kitu kingine alikuwa na uchovu kupita kiasi usiku wa jana alikesha akitumbuiza😇😇 kwenye Casino linalojulikana kwa jina la SUPER IVY😇
"Acha kuwa msumbufu, tembea🤨🤨" Paulina alizungumza huku akiongeza kasi kwenye miguu yake hakujali kama binti yake kavaa chupi na tisheti kubwa🙄
Mariah alimfuata Mama yake kwa nyuma.😒😒
Radi na ngurumo zilivyo sikika alijificha nyuma ya Mama yake😔😔
"Mwanamke kabisa unaye tarajia kuitwa Mama miaka ijayo unajificha kwenye mgongo wa Mama yako🤥! hakika wewe ni kichaa🤨" Paulina alizungumza kisha akaendelea kutembea😌
Mariah alizidi kumfuata nyuma asielewe wanaenda wapi🙌🏾. Magari waliyopishana nayo yaliwarushia tope🤥....
"Tunajitahidi kukaa mbali lakini bado wanaturushia tope☹☹" Mariah alilalamika akionekana kukasirika
"Acha kuongea sana nifuate tumekaribia kufika🧐🤔...." Paulina alizungumza
Baada ya dakika 25 kupita walifika sehemu wakasimama🙌🏾.
Mariah aliangalia sehemu waliyosimama kwa umakini mkubwa akafanikiwa kuona bonge la nyumba😬😬, hakuelewa kwanini Mama yake kamleta sehemu hii.🙄
"Hii nyumba kwa kukadiria unahisi imegharimu kiasi gani cha pesa🤔🤔" Paulina aliuliza
"Laki tisa😬...." Mariah alizungumza bila kufikiria
"Pumbavu🤨! kwa jibu lako hilo inaonekana unawaza kumiliki laki tisa maisha yako yote😏😏....naomba uangalie kwa umakini muonekano wa nyumba hii kisha uniambie ni kiasi gani cha pesa kitakuwa kimetumika🤔🤔'' Paulina aliongea huku akimtazama Mariah kwa macho yaliyobeba msisitizo🧐
"Milioni 450🤔🤔....." Mariah alijibu bila kufikiria ni vile tu macho ya Mama yake yalimtisha😥
"Umekosea kidogo nitakusahihisha🙄, milioni 500 zimetumika hapa🤔🤔" Paulina alizungumza akionekana kuwa na machungu😥😥
"Kwanini umenileta hapa🤔" Mariah aliamua kuuliza
"Hii nyumba ilikuwa ni ya kwetu ila sababu ya upumbavu wa Baba yako alibadilisha kila kitu akampatia Mwanamke😒😒.....nilifukuzwa sehemu hii nikiwa na ujauzito wako😥, mpaka sasa tunaishi maisha magumu sababu ya Mwanamke anayeishi humu ndani☹" Paulina alizungumza
Mariah aliamini Mama yake anaumwa akili kwa sababu tangu jana usiku hakuwa akimuelewa kabisa🧐
"Mama naomba tuondoke🥺...." Mariah alishauri
"Hii nyumba imeghalimu milioni 500 halafu unataka tuondoke tena bila hata kuuliza maswali mengi😳😳! hivi wewe ni mwanangu au nilibadilishiwa hospitali😥! hii ni nyumba yetu Mariah😔😔" Paulina alizungumza huku machozi yakimtiririka 😪
Baada ya Mariah kuona machozi kwenye macho ya Mama yake alielewa anamaanisha🥺
"Mama, milioni 500 ni pesa nyingi sana🙌🏾.... inawezekanaje sisi tuishi maisha magumu wakati unadai hii ni nyumba yetu😥😥 " Mariah aliuliza
"Sasa naona umeanza kuwa na akili🤔, hayo ndio maswali niliyotegemea uniulize😒" Paulina alizungumza akajifuta machozi kisha akamshika mkono Binti yake😔
"Kabla sijaingia kaburini naomba uirudishe hii nyumba mikononi mwetu😪😪....ndani ya hiyo nyumba kuna Kijana mzuri naomba ufanye juu chini awe rafiki yako🙌🏾. Wanawake na Wanaume ni watu dhaifu sana katika mapenzi endapo utafanikiwa kuuteka moyo wake kila kitu kitakuwa chetu🤨🤨"
"Bado sijaelewa hadithi yako🧐...." Mariah alimuambia Mama yake
"Ulisema unaweza kukimbia umbali mrefu bila kuchoka si ndiyo🤨? basi naomba uende sehemu anayouza karanga Mjomba wako🤌....muombe akusimulie kuhusu hii hadithi nina imani kubwa utamuelewa yeye kuliko Mimi🧐" Paulina alizungumza
Mariah alikuwa na shauku ya kujua kila kitu hivyo aliondoka kwa kukimbia mpaka sehemu anayouzia karanga Mjomba wake😟😟.
Alisimuliwa kila kitu kama alivyoomba🤌....machozi ya uchungu yalimtiririka kwa uchungu😥😥.
Kwa haraka aliweza kuelewa kwanini Mama yake kawa mtu wa hasira muda wote☹☹. Laiti kama Baba yake angekuwa hai basi angemkata kata panga kisha akatokomea na Mama yake kusikojulikana🙌🏾.
"Kwahiyo Kampuni la green tea ni la kwetu🤔🤔?....yaani hizo mali zote ulizonitajia kwa haraka haraka zote ni zetu🤨?...kwanini Baba amthamini kupita kiasi mtoto wa mchepuko ambaye siyo hata damu yake🙌🏾!..." Mariah alilalamika
"Nina uhakika mkubwa Baba yako alimpenda Mama yako kupita kiasi🤌. Yule mchepuko alitumia nguvu ya ziada kumlaghai Baba yako🤨🤨. Sijui ni kwanini Mama yako kaifufua hii hadithi iliyokwisha kupita🙌🏾. Naomba usifanye kitu chochote🤌" Mjomba aliongea
Mariah aliondoka bila kuongea chochote😥, anafika nyumbani kwao akiwa kalowa tepe tepe☹☹.
Paulina alimuonea huruma Binti yake kwa namna anavyo huzunika😥😥
"Kama si ujinga wa yule mchepuko🥺, Kampuni la green tea lingekuwa chini yako🥺, cha ajabu umeishia kuwa mwimbaji wa Casino😥"
"Mama naahidi kurudisha kila kitu kilicho chetu mikononi mwetu😥..... nitahakikisha huyo mchepuko na Kijana wake wanaishi maisha magumu kuliko hata ya kwetu🙌🏾" Paulina aliongea kisha akaelekea chumbani kwake kubadili nguo🧐.
Muda wa kwenda kazini ulikuwa umewadia🤔. Hakuona sababu ya kupumzika ile anataka kufungua mlango Mama yake alimsubirisha🙌🏾
"Hii ndio picha ya mtoto wa Mchepuko🙌🏾, jina lake anaitwa Max😒. Kama Mama yake aliweza kumshawishi Baba yako mpaka akatusahau sisi jitahidi kumshawishi pia aweze kukupatia kila kitu chetu🙄🙄"
Mariah alipokea picha akaiweka ndani ya begi lake😒, alimuonesha Mama yake tabasamu kumaanisha kila kitu kitakuwa sawa🙌🏾
Paulina alimsindikiza Binti yake kwa macho ya huruma😔😔....kazi anayoifanya ni ngumu kuliko zote😥. Lakini ili waweze kula ni lazima Mariah akawaburudishe watu kwenye Casino la IVY☹☹.
🎵Chai ya maajabu imegundulika,
tumia kwa Mwanaume tajiri
Kama ni masikini achana naye mwaya atakusumbua tu🎵
Mariah aliimba wimbo huu huku akicheza kiuno chake😅😅😅
Nje ya Casino hili Max, CEO wa kampuni kubwa ya green tea, alipark gari lake😌. Alikuja mahali hapa kupumzisha ubongo wake kutokana na uchovu wa kazi🙌🏾.
Kitendo cha kugusa mlango wa Casino la Ivy, alikutana na sauti ya Mariah😌😌. Alivuta kiti chake kisha akakaa🙌🏾 ....akili yake yote aliielekeza kwenye wimbo wa Mariah😅😅
"Chai ya maajabu!" Max alijisemea huku akishushia wine🍷
Itaendelea
Nash stories
Tsap 0773792227
Full 1000.