Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

πŸ“πŸ“ ILA KWA MPARANGE 😒 Sehemu ya Saba. πŸ‘‰ Nipe jibu basi halima tutakuwa wapenzi wa kimya kimya?...πŸ‘‡

27th Jul, 2025 Views 136



" Baba mimi ni mke wa mwanao.

( Kabla mzee ajaongeza neno mama mkwe kaingia katoka sokoni anamwambia halima)

" Huo mchicha utapika ndio mboga yako uongeze damu si unajua mchicha unaongeza damu alafu iyo nyama utapika kwa ajili yetu Sawa.

" Sawa.

( Halima akawa anawaza mama mkwe ndio njaa au roho mbaya yani yeye ale mchicha wao wale nyama...akawaza uku anachambua mchicha...anamsikiliza baba mkwewe anavyosema pale)

" Halima kanichua vizuri kidogo nasikia afadhali.

" Sawa mume wangu acha nimsaidie kupika nyama kwanza mchicha atapika mwenyewe.

" Ila kwanini na yeye asile nyama.

" Kala sana kwenye harusi yake ukumbuki nyama sio nzuri kiafya acha ale mchicha.

" Sawa.

( Halima kimya anachambua zake mchicha...upande wa sauda mumewe akawa anamwambia)

" Mke wangu sasa wewe ujitambue ni mke wa mtu mambo ya ngoma sijui kigodolo ayo achana nayo kwa sasa ivi nakuomba.

" Mume wangu shida inakuja mimi ni mwanachama kabisa yani pale kwa mpalange tuna kikundi chetu cha shida na raha sasa nikisema nitoke haraka ivyo kwa sababu ya ndoa naweza kusababisha mpasuko nakuomba uvumilie miezi mitatu tu.

" Dah aya poa.

( Jamaa akatoka akaenda kwa rafiki yake kuomba ushauri)

" Rama Samahani japo kwenye jando tunafundishwa mambo ya ndani usitoe nje ila ili naona nikuombe ushauri ndugu.

" Niambie.

" Mimi nimeoa mke sehemu moja inaitwa kwa mpalange sasa mke wangu yupo na kundi la ajabu Sana la ngoma na anasema awezi kuacha ghafla.

" Sikia nikwambie wewe mtie mimba mkeo alafu kaonge na Dokta amwambie mimba aitaki heka heka mwenyewe atatulia ila kwa mdomo tu ni ngumu kuna wengine ndio tamaduni zao izo.

" Kwaiyo nikimpa mimba atatulia.

" Yah.

( Jamaa akaondoka na wazo la kumpa mimba mkewe...anarudi Kwake anaona dada zake nao wamefika...mmoja akamwambia kaka yake)

" Kaka Samahani nakuomba uyu wifi asiende kwenye ngoma kumbe kwenye ngoma mpiga ngoma anaweza kutembea na mwanamke yoyote yule atayemchagua.

" Unasema ukweli?

" Ndio nimesikia uko ya ngomani yabaki ngomani kumbe ndio wanachofanya wapiga ngoma.

" Kuanzia Leo mke wangu sitaki kusikia ngoma yoyote umeenda nasema kwa sauti kubwa kabisa KUANZIA LEO SITAKI SITAKI NARUDIA SITAKI.

( Sauda kanyamaza uku simu yake inaita anapiga mama yake akaingia chumbani kupokea)

" Haloo mama.

" Nakaribia kwako ivi jiandae unisindikize mvuti kuna ngoma ya shoga yangu yule aliyekupa kitanda siku ya harusi yako Leo anamtoa mwanawe jiandae mwanangu.

" Mama mume wangu kanikataza kwenda kwenye ngoma.

" Anawazimu uyo nakuja hapo kukuchukua asitake kukupanda kichwani.

" Mama sikia.

( Mama yake alikata simu na akaizima anaenda kimya kimya uku sura kakunja anasema)

" Mwanangu mwenyewe anipangie mtu yani asinisindikize kasema nani nilienda mwenyewe leba natukanwa kule tanua ulivyokuwa unaikatikia ulikuwa aujui itakatikia nayo ndani aya tanua ulete mtoto hapa...nilikuwa peke yangu"

( Anamaliza kuongea peke yake anafika kwa mume wa sauda anagonga hodi)

" Hodii.

( Mume wa sauda akafungua mlango anakutana na mama mkwewe)

" Karibu mama.

" Asante.

" Shikamoo mama.

" Marhaba nimekuja kumchukua mwanangu anisindikize mvuti mala moja.

" Kuna nini mama?

" Ngoma.

" Mama Samahani mke wangu nimemkataza kwenda kwenye ngoma.

" Unasemaje?

" Mke wangu nimemkataza kwenda kwenye ngoma.

" Kama kwenu akuna ngoma nyinyi uyu kwao kuna ngoma tena ndio hasiri yetu naomba niende nae kwenye ngoma sijataka nikuongope naenda nae wapi sijui wapi tunaenda kwenye ngoma mvuti mpe ruxsa mkeo..mama mzazi nimesema.

( Jamaa anaona sura ya mama mkwewe imebadilika uku dada zake wanatamani kujibu wanamsikiliza kaka yao atasemaje)

Dah yani..

ITAENDELEA.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

πŸ“πŸ“ ILA KWA MPARANGE 😒 Sehemu ya Saba. πŸ‘‰ Nipe jibu basi halima tutakuwa wapenzi wa kimya kimya?...πŸ‘‡  >>> https://gonga94.com/semajambo/ila-kwa-mparange-sehemu-ya-saba-nipe-jibu-basi-halima-tutakuwa-wapenzi-wa-kimya-kimya
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest