Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MKE ALIYECHUMA NAYE MALI | EP 19

27th Jul, 2025 Views 29


Laila alitamani kupokea simu ya rafiki yake lakini mkwara aliokuwa amepewa ulizidi kumuumiza kichwa. 🀯 Alijikuta akidondosha chozi. 😒 Moyo wake ulimuuma kuona mtu aliyemwahidi kila siku jana kushindwa kumsaidia.

"Kama ameweza kumpa mtoto wake uchizi, atanishindwa mimi kweli?" πŸ€” alijiuliza moyoni.

Siku hii kwake ilikuwa kati ya siku ngumu zaidi kuwahi kumpata. πŸ˜” Alikabiliwa na maamuzi mazito ambayo hakutegemea kuyachukua. Urafiki wake na Mayner ulikuwa mkubwa mno.

Tangu utotoni walipocheza pamoja hadi ukubwani, ni hali ya kipato tu iliyowatenganisha, lakini siyo upendo. ❀️ Wakati mwingine Laila alikosa msaada kabisa, lakini kila alipomwendea Mayner na kumweleza, alimsaidia – hata kuongeza hela kwa ajili ya kukuza ofisi yake.

β€œKama nitakuwa nakosea, Mungu nisamehe...” πŸ™ alisema huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimdondoka. 😭

Dakika 30 mbele, Mayner alifika akiwa na Rasma, ambaye kwa muda ule alikuwa ametulia kidogo. Alipotokea tu, Laila alitaka kufunga ofisi yake.

"Kuna nini Laila?" Mayner aliuliza huku akitaka kukaa.

"Shoga toka hapa kwangu na huyo chizi wako sijui mwendawazimu, utajua mwenyewe!" 😠

"Laila mbona sikuelewi, kuna nini?"

"Usitake kuelewa bwana. Toka, toka, toka! Nenda kafuge dondocha huko kwingine, siyo hapa kwangu!"

Laila alikuwa mkali sana. 😀 Alijaribu kuficha maumivu ndani ya moyo wake, lakini aliyoyasema hayakuwiana na aliyoyahisi. Moyoni kulikuwa na vilio. 😒

Mayner alimtazama Laila kwa mshangao na huzuni. 😞

"Nimekuja nataka unipeleke kwa mganga. Ona anavyoteseka Rasma!"

"Khe! Sasa kuteseka kwake kunanihusu nini? Ndugu yangu huyo? Au tunajuana? Usiniletee nuksi hapa, nitakuitilishia mwizi!" 😑

"Laila, wewe siyo wa kunifanyia hivi mimi... Sikutegemea urafiki wetu ungeishia kwenye matusi hivi."

"Bibi wewe, kusoma hujui na hata picha huioni? Sitaki ushahidi wa mandondocha! Si ana ndugu zake? Peleka kule! Tokaaaaaaaaaaa!" πŸ”₯

Mayner alitikisa kichwa kwa huzuni πŸ˜”. Hakutegemea rafiki yake wa dhati angemgeuka hivyo. Alimgeukia Rasma ambaye alikuwa bado anatemetemeka na kutema mate hovyo. 😷

Watu waliokuwa karibu na ofisi walianza kukusanyika kushuhudia.

"Utu kwako umewekwa pembeni, si ndiyo? Hutambui umuhimu wangu kwa sababu nina shida? Upo tayari kuniaibisha? Asante, umenifunza!"

Akamshika mkono Rasma na kuondoka naye.

"Kuna nini Laila, si rafiki yako yule?" aliuliza mama mmoja jirani yake.

Laila hakujibu. Alirudi ndani, akafunga mlango. Kilio chake kilikuwa cha kutoka moyoni. 😭 Alilia kwa maumivu ya maamuzi aliyoyachukua, akijua yangeumiza wengine, lakini hakuwa na jinsi.

Alihitaji kuokoa maisha yake na kujiepusha na mgogoro uliokuwa unaendelea. Hakutaka kuwa upande wowote, ingawa alijua wazi kuwa Mayner angemchukia.

---

Mayner alirudi nyumbani akiwa amechoka sana. 😩 Alimuweka Rasma pembeni kisha akaanza kuangua kilio. Akili yake haikumpa nafasi ya kutafakari vizuri. Aliona dunia yote imeanguka juu yake. πŸ˜”

Alikosa nguvu ya kumsaidia Rasma, na alipoona jinsi alivyokuwa akiweweseka, moyo wake ulizidi kuumia. πŸ’”

"Nifanyeje? Nikamuombe mama yake msamaha?" alijiuliza.

Alijaribu kumpa chakula, lakini Rasma alimwaga chini na kuanza kukikanyaga, kisha kukila kwa mikono.

"Rasma mbona hivyo sasa?" 😟 Mayner alizungumza huku akimzuia, lakini alijikuta akipigwa.

"Acha! Achaaaaa!" 😠 Rasma alitamka huku akitikisa kichwa kama feni.

Mayner alimuachia, lakini moyoni alizidi kuumia. Hasira zikampanda. Alimshika mkono na kutoka naye nje.

Akiwa amefika mwisho wa uvumilivu, aliamua kumpeleka mbali kabisa. Alipungia bodaboda mkono.

"Wapi mnaenda?" bodaboda aliuliza.

"Misungwi."

"Mbona mbali, si mgepanda gari?"

"Nakupa hela."

"Ah, sawa! Nipigie 40 elfu basi."

"Acha tamaa bwana."

"No sister, mafuta yamepandishwa kila siku."

"Uwi, sawa. Tufanye 30."

"Unaua bendi aisee!" πŸ˜…

"Nisaidie tu ndugu yako."

Bodaboda akaangalia kushoto, kulia, kisha akasema:
"Kalia chuma tuondoke. Sina huyu chizi au?" 😬

Mayner aliumia sana kwa jina hilo. 😑 Alitamani kumjibu, lakini moyo wake ulijaa huzuni.

Wakafika Misungwi saa tano usiku. Mji ulikuwa umetulia sana. πŸŒ™ Alimuomba bodaboda asimamishe eneo kama msitu.
"Hapo nimefika," alisema Mayner kisha akampa hela bodaboda.

Yule boda aliondoka bila maneno mengi.

"Tunaenda wapi?" Rasma aliuliza kwa sauti ya kawaida kabisa.

Mayner alishtuka. 😲 Akajaribu kumuita mara kadhaa:

"Rasma? Rasma? Rasma?"

Hakujibu. 🀐

Mayner alihisi pengine lile lilikuwa ni bahati tu ya kusikia. Akaamua kuendelea na mpango wake.

Alisogea zaidi kichakani, akamuacha.

"Kaa hapa, nakuja..." alisema, kisha akaondoka...

Hivi ulishawahi kununua kitu kutokana na hela uliyokuwa nayo..!? Vile mfuko wako upo muda huo, ndivyo unafanya manunuzi ya kitu unachokipenda.

Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ALIFIRISIKA BAADA YA KUMUACHA MKE ALIYECHUMA NAYE MALI | EP 19  >>> https://gonga94.com/semajambo/alifirisika-baada-ya-kumuacha-mke-aliyechuma-naye-mali-ep-19
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest