.
Namba ya WhatsApp-0683944333
______________________________________
SEHEMU YA KWANZA
Naona tu mnaitana, kama ni majambazi poleni, cha thamani hapa ni roho yangu tu, simu niliyonayo nikipigiwa nikapokea tu imeisha charge, siwezi uza ata Kwa buku, mfukoni sina hela, Wala hata hio harufu ya Hela tu sina, nguo nazo nimeazima tu, ata hii roho yangu yenyewe inadhambi sijatubu, ata nikibatizwa ayo maji yatachemka moto Kwa hizi dhambi....
Niliongea Kwa kujihami, jamaa walikuwa wawili wamevaa vipensi uku wako vifua wazi,walinitizama mmoja akajibu, binti unajua hapa uko wapi? Na Kwa nini umeingia eneo lisilokuhusu umetumwa?...
Heee we jambazi vipi, Yaani nitumwe Kwa majambazi kwamba �� roho yangu siipendi au? Yaani roho yangu hata kama inadhambi siwezi iweka rehani, na MSISAHAU hii ni nchi huru, maeneo mazuri yote mnayatumia kuteka watu, afu eti nchi Ina jeshi looh ��...
" Binti unaelewa unachokiongea Yaani ukituangalia sisi unaona ni majambazi sio?
Sasa nyie nao Kuna Cha kuuliza, picha inajieleza kabisa, mnajaza vifua kutukaba mwisho vifua vipasuke, izo nguvu mlipaswa kutumia na wanawake zenu, mdomo koma mniache niende sina kitu jamani...
Binti naona kwanza tumekustahi mno, hapa uko Kambi ya jeshi, na tuna nguo chafu nafikili utazing'arisha, na but usisahau,
Nilijikuta nacheka Kwa sauti, Kuona majambazi wamejigeuza kuwa wajeda, ha ha ha ha, mbavu zangu jamani, Yaani nyingi mwe wajeda, ivi mnawajua vizuli wajeda nyie, Yani wale viumbe wa mapigo na mwendo ��, kwanza kukutana nao tu ni nuksi nahisi hata ningekuwa...
Kabla sijamalizia kuongea, nikawa nasikia wengi wanaimba tena kibaya zaidi wanamagwanda na hawako mbali, nyie nilihisi mkojo, umekaba mpaka Koo, sio tu kibofu...
Niliwatizama Kwa hofu mno, mmoja alinionea huruma masikini akanipa ishara nipotee, wee ata sikusubuli kuoneshwa njia, nilijua awa viumbe hawapendi maswali, binamu yangu aliuliza njia wakamuonesha njia ya kuingia zaidi kambini, alitusimulia akiwa mahututi, anapigania roho na Israel wanavutana, yote ayo ni adhabu za wajeda, nikajiongeza kichwani, sitouliza hapa ni miguu nisaidie...
Dua yangu, ilikuwa nikuombea miguu, mnisamee hata sijajitambilisha...
Naitwa Mariam, nimemaliza chuo Cha ualimu nasubili ajira, Leo nilikuwa na mawazo chungu nzima, nikaamua nikatulie zangu mahali peke yangu, huku ni Kwa mjomba wangu nimelelewa na mjomba Toka nikiwa na miaka 8, wazazi wangu wote walifaliki, na huku tulipohamia ni wageni kabisa...
Mjomba kajenga huku Musoma Makoko, tuna siku nne Toka tuhamie, Sasa mwenzenu nikaamua kwenda mahali nikapuge upepo wa ziwa, nikiwa nimetulia zangu nahasira mpaka saivi sijapata ajira, ghafla nahisi mijemba inakuja inakishindo nikajua mamaaaa wamekuja majambazi hao, nikaona niwasaidie tu kujieleza wasipoteze muda kunikaba mtu ambae ata mia mbovu sina, kumbe mwenzenu nimeyabananga, ni wazee wa mitutu, nilivyooneshwa ishara ya kupotea nyie hamkuwepo ila Mungu wenu alikuwepo....
Nilikimbia Kwa mara ya kwanza Toka nizaliwe Leo ndo nimegundua kumbe ninakipaji Cha kukimbia bila kuchoka tena Kwa kasi kubwa bila kupumzika��...
Itaendelea...��
SEHEMU YA PILI
Nilifanikiwa kuchomoka, nimekuja kufunga break jilani na nyumbani baada ya Kuona maduka ya bidhaa, ndio nikafunga break, lakini Sasa sikuwa na kiatu chochote mguuni na ata sikumbuki wapi nimetupa, nilikuwa na kiu ya hatali...
Moja Kwa Moja nikaenda duka moja, lilikuwa la jirani yetu na binti zake nimesoma nao sekondari, japo mitaa ilikuwa tofauti, niliwaona na mabinti zake, walinichangamkia ila nikawatuliza Kwa ishara ninywe kwanza maji..
Nilikunywa maji Lita Moja na nusu, yote Kwa mara moja, bila kituo nilimaliza kopo zima ndo nikashusha chupa...
Kila mtu alinishangaa, Sophia na Saphina wakaniuliza Kwa pamoja, Mariam kulikoni mwenzetu sio kawaida Yako na mbona uko hivyo?...
Nilishangaa, wamewezaje kuwaza Kwa pamoja, swali la kuniuliza, nilivyowauliza hivyo walinicheka nakusema " umesahau kama tumelala mfuko mmoja, hivyo mawazo yetu ni sawa...
Ilibidi tu nicheke hawa vichaa sitowaweza, ikabidi niwape mkanda oya mwenzenu Leo siyamenikuta bwana, nimepitia hii njia nikatokezea ziwani nikachaniza Kwa juu niliona kumetulia, Sophia akadakia tobaaaa, Kambi ya jeshi io umetoka salama kweli?
We acha, ata mimi mwenyewe siamini kama nimenusulika, yaani hawajanigusa hata unywere, na wamenikamata kabisa, Cha kushangaza wameniachia kizembe kabisa , Yaani kama ningekuwa ni gaidi wale tayali wangekuwa wameniuza, nilichogundua saivi nchi Haina tena ulinzi ni vile tu manyemela hawajasanuka...
Wajeda wa saiv ni milenda, midebwedo hawana mizuka kama wazamani, Yaani nimeshangaa mjue...
" Wee Mariam wewe acha kutupanga awawezi kukuachia ivi ivi we sema tu ukweli, umepewa adhabu umetoroka au umemraghai mjeda na utamu, lakini napo inagoma ivi, ata kama ni utam lazima adhabu ufanye, au umeshtuka Kwa mbali kabla hatujafika umeamua kutupanga��...
Niwapange ivi mnazani natania ee, ndio maana nimewambia Sasa hivi hakuna wajeda ni migwanda tu, wajeda wamejazia tu vifua sura Kaa yangu Yaani ni warembo afu wakiume, ukute ni pisi za watu, afu sie tumebweteka tunajua nchi inamajembe, kumbe majembe butu ya Karne ya utumwa....
"Heee Mariam mbona huna viatu na unamajeraha, kumbe ni kweli utakuwa umewatoroka...
Sophia elewa basi, sijawatoroka, wale midebwedo, wameniachia Kwa hiyali Yao wenyewe, mpaka mwenyewe nimeshtukia wale huenda wanakulana wale, mjua wamenikamata walikuwa wawili, afu walikuwa vifua wazi kabisa na vipensi tu vidogo, �� afu mmoja hakuwa anaongea kabisa, huenda yule mkimya ndo �� ebu ujue najaribu kuwaza ....
Nyie kumbe wakati naongea yule wale wajeda walikuwa hapo dukani wananunua maji, na wamenisikia Yaani ni Ile nageuka Ili niwape mkanda vizuli, nakuta jamaa wananitizama macho Kwa macho....
Yaani kulopoka Kule wajemba kumbe wapo nyuma yangu��, niliganda kama sanamu...
Itaendelea....
Full sh 1000
Njoo WhatsApp kupitia namba 0683944333.