Endelea ๐ป
"Flash?..... kwanini wanaweka flash kwenye keki au ni zawadi kwa wateja?" Sultana alijiuliza
Aliitoa flash kwenye keki akaitia mfukoni mwake kisha akaendelea kula
Baada ya kurudi Ndani Ya Jumba La Dhahabu alipitiliza chumbani kwake, nyumba ilikuwa kimya sana na hata hakuelewa watu wameenda wapi
Kabla hajajitupa kitandani alikumbuka kuhusu Flash iliyokuwa kwenye keki. Taratibu aliingiza mkono wake kwenye suruali, baada ya kuitoa aliichomeka kwenye TV iliyokuwa ukutani
๐ฉธIkitokea nimekufa kabla ya harusi yangu naomba unisamehe sana Liam, nina wasiwasi sana na Sona lakini kwa kuwa bado namuamini kwa kiasi fulani acha niende kukutana naye, kama sitarudi salama Sona ndio atakuwa mhusika wa kifo changu....๐ฉธ Sauti ya Marmar ilisikika
Sultana alichomoa flash haraka akiwa anatetemeka mikono.
Alijikuta akipata maswali mengi kichwani mwake kwanini flash hii imeishia mikononi mwake
Machozi yalimtoka asiamini kama mdogo wake anaweza kuwa katili namna hii kwa mtu anayedai ni rafiki yake
Baada Ya Wiki Moja๐ป;
Rayuna (Dada wa Liam) alirejea nyumbani....watu wote walionekana kumfurahia
"Kwanini una tabasamu baada ya kuniona, sina uhakika kama tumewahi kuonana hapo nyuma katika ulimwengu huu tofauti na siku ya leo" Rayuna alimuumbua Sultana
Sultana hakumjibu, badala yake alimzomea paka aliyekuwa amekaa juu ya meza
"Tabasamu lake lilikuwa ni kwa ajili ya huyo paka na si wewe" Sona alimtetea Dada yake kwa unafiki wa kistaarabu
"Ni mrembo sana naweza kujua kwanini yuko hapa" Rayuna aliuliza
"Muda si mrefu atakuwa mke wangu halali... nampenda" Liam aliongea mbele ya familia yote
"Nimepitisha hilo...." Bi. Fatma alipiga kura
"Nimepitisha hilo pia...." Sona aliongea,
Rayuna alirudia kumchunguza Sultana kwa umakini mkubwa
"Nimepitisha pia....lakini usijihesabu mshindi kwa sababu Ali hayuko hapa hivyo tutasubiria kura yake" Rayuna aliongea kisha akaelekea chumbani kwake
Sona alimcheka kimtindo Sultana bila wengine kuona. Ni kama alikuwa ana muambia safari ndio imeanza.
"Ali alienda kusalimia kwao....nina uhakika leo au kesho atakuwa hapa, si mtu wa changamoto kama Rayuna hivyo naamini kila kitu kitaenda sawa" Bi. Fatma alimuambia Liam
๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป๐ป
Rayuna akiwa chumbani kwake aliangua kilio baada ya kuiona picha ya Marmar ukutani
Alijikuta akikumbuka vitu vyote walivyowahi kutenda pamoja.
"Sona, kwanini ulishindwa kuzuia kifo cha Marmar.....hakika wewe ni mtu usiyekuwa na shukurani, ulitoka Kijijini ukiwa hujui kuvaa wala kuoga. Kupitia Marmar maisha yako yalibadilika ni kama ulikuwa unatumia nyota yake.... hainiingii akilini kuwa kifo chake kilikuwa ni bahati mbaya...." Rayuna aliongea huku akilia
"Ni kama unaniambia Mimi ndio nimemuua!....kwanini unipe jukumu kuhusu kifo chake, alikuwa ni kipenzi cha roho yangu ni dhambi kunitamkia maneno magumu namna hiyo" Sona aliongea huko machozi yakimlenga
Rayuna aliachia kicheko baada ya kuona Sona anataka kulia
"Nakutania tu.....sasa nimeamini ulimpenda Marmar kuliko kitu chochote"
"Ni kweli umelipenda chaguo la Liam" Sona alibadilisha maada
"Wakati wakiwa wanat*mbana sitahusika kuwashikia chupi, sasa kwanini nijali kuhusu wao. Nimekuja hapa kupumzika na si kufatilia mambo ya mtu..." Rayuna aliongea kisha akajitupa kitandani....
"Rayuna kabadilika....ni kama ananivamia kiakili bila Mimi kujua..." Sona alijisemea ndani ya moyo wake kisha akaondoka kwa gia ya kushikwa na haja ndogo
๐ฉธKeki ulizonipatia kuuza siku kadhaa zilizopita ziliisha ๐ฉธ Ujumbe uliingia kwenye simu ya Rayuna
Aliachia tabasamu kisha akaitoa laini kwenye simu....aliivunja vunja kumaanisha haina matumizi tena.
Alifumba macho yake, taratibu alijikuta akiikumbuka ile siku amemsaidia Sultana alivyozama kwenye kina kirefu cha bahari, baada ya Meli ya Star kupata hitilafu.
Aliikumbuka pia ile siku aliyomtumia mtoto kumdanganya Sultana kuwa Jumba La Dhahabu ni hekalu, lengo lake lilikuwa ni kumtanisha tu na Liam
Kwa kipindi chote familia yake wameishi wakiamini alikuwa Japan, lakini ukweli ni kwamba alikuwa Jijini Odes.
Mida ya Jioni watu wote wakiwa mezani wanakula, mlango uligongwa kisha ukafunguliwa watu wote waligeuza shingo zao kumpokea mgeni
Itaendelea ๐ฅ.