Simulizi za john
0789 824 178
1000
Usiku ulikuwa mrefu kwa Leila. Alilala akiwa na mawazo mengi kichwani. Hakukuwa na tumaini lolote kutoka kwa Zayn. Na kuhusu kumpigia Mr Ghali hakutaka hata kufikiria. Alijua wazi itamfanya aonekane mbaya zaidi machoni pa Zayn😩.
Alichukua chupa ya maji, akamimina kwenye kikombe kidogo, kisha akameza mkate mkavu uliokuwa umebakia kama slesi mbili ivii.
Hicho ndicho kilikua chakula chake cha kila wakati. Zayn alikata kila aina ya manunuzi nyumbani. Hakukuwa hata na sukari, achilia mbali mchele au unga. Trust me ninapo sema Zayn alijua kumkomesha Leila💔.
Asubuhi ilipofika, Leila aliamka kabla hata ya jogoo kuwika. Alikuwa tayari amefanya maamuzi ambayo hayakua mazuri ilimradi tu Lulu aishi.
Alioga harakaharaka, akavaa nguo nyingine safi, kisha akajiandaa kwenda hospitali. Bi Salma, mama yake, alikuwa anamsubiri nje ya wodi ya wagonjwa.
Alipofika Bi Salma hakutaka hata salamu alimuuliza
“Leila, haya mambo ya hela yanachukua mda mrefu sana. Si ulisema jana usiku kila kitu kingekua tayari?? Matokeo yake sijaona chochote”🤨
“Hela ilishatoka mama, tatizo benki wanayotumia ipo kwenye matengenezo. Tena waliniambia hadi kesho mambo yatakua sawa”
“Mpaka kesho?? Unadhani Lulu ataweza kuvumilia maumivu mpaka kesho? Jana ulisema jioni unamalizia process, sasa ivi unaniambia kesho sijui benki ipo kwenye matengenezo”
“Mama ni kweli, tuvumilie mpaka kesho kila kitu kitakua sawa! Mapema kabisa nitaleta hela ya Lulu”
“Na Zayn je? Hata haji kumuona mgonjwa??” Bi Salma alimkazia macho Leila
“Amesafiri kikazi. Lakini akirudi tu atakuja… usiwe na wasiwasi mama. Lulu atapona” Leila alidanganya kwa mara nyingine tena
“Kwaiyo akisafiri anashindwa hata kupiga simu ya kutoa pole??”
“Mama yupo busy hata mimi nampata kwa shida, ndo maana nakuambia akirudi safari atakuja kukuona”
“Na aje anione mapema maana toka akuoe sijawai ona sura yake! Anajificha ficha nini kama bangi!”🤣
“Yaishe mamaa, achana na mambo ya Zayn tuwaze kuhusu Lulu kwa sasa”
Mama yake hakujibu zaidi Alimtazama tu kwa jicho lenye mashaka mengi. Kama mtu mzima alihisi tu Leila alikua anamdanganya ni vile hakutaka kuendelea kuuliza.
Basi Baada ya kutoka hospitali, Leila alienda moja kwa moja hadi kwa Sinyati. Alipo fika tu hakutaka hata kuingia ndani, alisimama pale mlangoni na kusema
“Sinyati… nimekubali”
“Kukubali nini?”😳
“Kudansi. Kama kuna nafasi, nipeleke club. Hii hali ya kushindwa kumhudumia mdogo wangu inanitesa”😔
Sinyati alishindwa hata kusema neno. Alimkumbatia Leila kwa nguvu.
“Rafiki yangu najua sio rahisi. Lakini najua utafanya vizuri. Club One ni sehemu kubwa sana, ukicheza vizuri usiku huu unaweza kupata hata milioni ni wewe tu! Na nafasi zipo za kutosha! Acha nivae ili twende tukaongee na Boss”
“Ok kipenzi”
Sinyati alirudi ndani akabadili nguo haraka haraka kisha akamchukua Leila hao mpaka Club ONE. Club ONE ni club maarufu yenye hadhi, wateja wake wakubwa ni maboss wa maduka makubwa, matajiri wa Dar, na wanaume wenye fedha chafu💰.
Walipofika, Sinyati aliongea na Boss wake, ni jamaa flanii ivi mwenye tumbo kubwa kama pakacha, mfupi mweusiiii anapendelea kuvaa pete za dhahabu vidoleni.
“Huyu ndiye Leila? Mhmmm… anafaa. Mwili wake ni biashara tayari. Leila, utacheza leo kama majaribio tukikupenda leo nitakupa nafasi moja kwa moja. Usiniangushe” Alisema Boss akizidi kumkagua Leila juu mpaka chini
“Sawa Boss Asante” Leila alishukuru japo hakuonyesha furaha sababu sio kazi ambayo alidhani atawai kuja kuifanya😫.
Baada ya pale Sinyati alianza kazi. Alimfundisha Leila step chache za kucheza nyimbo za Kizomba, Bongo Fleva na Afrobeat kwa haraka. Walijifungia kwenye chumba cha wafanyakazi ambapo madansa wengine hutumia kufanyia mazoezi.
“Usijali sana kuhusu staili. Muhimu usione aibu. Cheza na moyo. Ukiona mwanaume anakutazama, tabasamu. Ukiona anatoa pesa, mkaribie jitikise vizuri. Ukumbuke ni kwanini upo hapa na unafanya ivi kwaajili ya nani”
“Daah, sio poa”
“Najua sio rahisi, shika step chache tu nyingine tutajifunza zaidi iwapo utahitaji kuendelea kuwa dansa”
“Ok”
Leila alijikaza na kuendelea na mazoezi! Hadi Kufikia jioni, alikuwa tayari kajua angalau step chache. Ndipo walipoanza maandalizi ya mwisho.
Sinyati alizibana nywele zake na kumpa wigi refu lenye mawimbi ya brown. Kisha akampa gauni fupi lililombana vizuri likionyesha mgongo, kiuno na mapaja. Yani ile nguo haifai hata kupita nayo barabarani maana watu watakupiga mawe🤣.
Sinyati pia Alimuongezea hereni kubwa, lipstick nyekundu, na perfume yenye kaharufu kazuri.
Leila alipojitazama kwenye kioo Hakuamini kama ni yeye.
“Mara ya mwisho niliwaka namna hii siku ya harusi yangu” Alisema akitabasamu na taratibu akavua pete yake na kuiweka ndani ya pochi.
Uko nje ya club sasa Sauti za muziki zilianza kusikika. Club One ilikuwa imeanza kujaa. Watu walikuwa wanaingia kwa makundi na wengi wao wakiwa wanaume! Walinunua vinywaji na kulipia kiingilio ili kuingia ndani.
Leila alimeza mate kwa woga. Alisimama nyuma ya pazia, akachungulia kwenye steji ambapo ndo alipaswa kwenda kucheza dakika chache mbeleni nguvu zikamuishia.
“Hapana siwezi! Siwezi mimi!”🙅♀️
Je, Leila ataweza kupanda jukwaani?
Nakuja………
SEHEMU YA : 09
“Nashindwa Sinyati… siwezi” Leila alizidi kusema kwa sauti ya hofu na mara hii alimgeukia rafiki yake.
“Kwani unacho ogopa ni nini?”
“Watu wakiniona je? Wakienda kumuambia mama yangu?? Habari zitamfikia mpaka Mr Ghali south Africa! Hata ivyo Sinyaa wanaume ni wengi mno mimi naogopa! Nilidhani nitakua jasiri ila kumbe nilikua nikijidanganya” 😰
“Skia, acha uoga Hakuna atakae gundua ni wewe. Ona hii…” Sinyati akatoa mask nyeusi inayo ng’aa vizuri kwenye taa🎭 kisha akaendelea kuongea akisema
“Ukivaa hii mask hakuna mtu ataijua sura yako! Also wakikuuliza unaitwa nani utajitambisha kama Luna. Luna ndo litakua jina lako la kazi, okay??”
“Okay” Leila alivaa ile mask na ilifunika sura yake nusu kasoro sehemu ya mdomo tu. Na jinsi alivyo vaa ile mask ndivyo alivyo zidi kupata confidence ya ajabu.
“Uko tayari sasa Luna?? Au bado unaogopa ogopa?”Sinyati alitabasamu😊
“Ndipo tayari!”
“Nice, nakuja”
Sinyati alimfuata Dj akamnong’oneza kitu sikioni ndipo Dj akachukua maiki na kusema kwa mbwembwe
“Ladies and gentlemen, nimeambiwa hapa tuna mali mpya! Mali safiiiii! Mtoto mbichiii kabisa. So for the very first time, give it up for… LUNA!!” 🗣️🗣️🥳🥳
Ghafla taa zilimulika stejini, na kwa mara ya kwanza, Leila alikanyaga steji iyo. Mask aliyokua ameivaa iliwaka hatari plus alivyo na body nzuri weee alivutia hatari🤌. Sijui hata kwanini Zayn hakugundua ilo mapema🥱.
Awali Leila alitetemeka Lakini mziki ulipoanza kumkolea akazidisha maringo na kuzungusha kiuno kana kwamba hakina mfupa!
Kwa kusudi akainama kidogo na kutingisha nyama nyama zake alizo pewa na Baba Muumba basi weee, Wanaume waliojazana kule club walianza kupiga kelele
“Weeeh Lunaaaa! Weee utatutoa rohoo”🗣️
“Lete viuno hivyo mamaaa! Tupe tusahau wake zetu mrembo” kelele zilikua nyingi kweli na miluzi ya kutosha
Mabunda ya noti yakaanza kurushwa juu, wengine wakimfuata karibu jukwaani na kumtunza moja kwa moja kwa mikono. Wengine walikuwa wakimrekodi, wakishangaa ni nani mwanamke huyo aliyekuwa nyuma ya ile mask mwenye kiuno bila mfupa🤔
Leila, ambaye sasa alikuwa Luna, alikua amejikuta kwenye ulimwengu mwingine kabisa. Ile aibu ya mwanzo ikapotea. Kwa dakika zile, alizidi kuzidisha mbwembwe ili wazidi kumiminia pesa za kwenda kumtibu Mdogo wake!
Alipomaliza kucheza maana nikwa dakika 10 tu, Alishukuru kwa kuwarushia mabusu ya hewani😘 kisha alishuka stejini akitabasamu. Haraka Alimkumbatia Sinyati kwa furaha, na wote wakacheka🤣👌.
“Umeweza shosti! Kumbe ndo unabalaa ivi?? Aisee sijawai ona striper alie amsha club nzima kwa mara yake ya kwanza” Sinyati alisema huku akimpa taulo ajifute jasho.
“Hadi mimi najishangaa! Nilipata nguvu ya ajabu”
“Tuachane na hayo, hela zako wamekukusanyia! Twende tukahesabu tujue umepata kiasi gani”
Walikwenda haraka kwenye chumba cha kupumzikia na Leila akaanza kuhesabu hela zake. Pesa zilikuwa nyingi, mpaka akafikiri labda anaota. Alizikusanya vizuri, akazihesabu na jumla zilikua shilingi 900,000 (laki tisa).
“Weee siamini!! Laki 9?? Hapa sasa Lulu atapata matibabu na hela ya dawa juu! Sinyaa siamini” alisema kwa sauti ya chini, machozi yakimlenga lenga🥺
“Huo ndo utamu wa kudansi! Nilikuambia mimi! Tena na style ya kuvaa mask ndo inafanya uwe unique! Watahitaji kujua ni nani mrembo nyuma ya mask”
“Na hawatajua ni nani kamwe” Leila alitabasamu😊
“So utapenda kuendelea kudansi?? Ama baada ya kupata kiasi unacho kihitaji mambo ndo yameishia hapa??” Sinyati alimuuliza Leila na kabla Leila hajajibu aliingia Boss akiwa anatabasamu hadi jino la mwisho😁
“Hey Leila! Ama nikuite Luna, What you did tonight was magic! Wateja wamekuchangamkia balaa. Nitakuhitaji kila wekeend hapa! Jumamosi na Jumapili usiku nikwa ajili ya Luna pekee! So uko tayari??”
Leila alimwangalia Boss halafu akamwangalia na Sinyati, Alitaka kusema hapana, alitaka kusema kuwa alienda kucheza pale kwa usiku mmoja tu
Lakini alikumbuka tena yale maisha ya kunyimwa hata hela ya chakula. Alikumbuka dharau za Zayn na jinsi biashara yake ya madafu ilishindwa kumpa maisha ya unafuu aliyo taka.
Baada ya kufikiria Alitabasamu, akasema kwa sauti iliyojaa ujasiri
“Nipo tayari! Nitakua nakuja kucheza kila weekend!”
“Fantastic! Endelea kuchukua mazoezi na najua ukiendelea ivi utafika mbali sana! All the best Leila na karibu Club ONE” alisema Boss
“Asante Boss”
Basi Boss alipomaliza kuongea na Leila akatoka na kuwapisha, acha Sinyati asianze kuruka ruka kwa furaha.
“Nilijua tu lazima ukubali kufanya kazi hapa! Umeona sasa? Maisha yako yatakwenda kubadilika trust me Leila”
“Na yote nikwa sababu yako! Umenisapoti sana Sinyaa nashukuru! Na idea yako ya mask imebusti confidence yangu”
“Usijali ndo maana mimi ni rafiki yako” Sinyati alitabasamu huku wakikumbatiana🫂❤️
Je nini kitaendelea?
Nakuja.