_________________________________________
Niliona anaongea ujinga tu niliingia bafuni nikavaa, nikatoka kuja kulala uku natetemeka vibaya mno, aliona ninavyoogopa, akasema” acha uoga utanizoea tu lala leo ata sikukugusi, sikuwa namuamini ata kidogo, nililala kwa mashaka mno, kuna muda ilikuwa usiku wa saa 8 lakini Kwa ule uoga bado sikuwa nimelala kabisa…
Alijigeuza tu ivi kidogo nikapiga kelele mpaka akashtuka na kunitizama Kwa mshangao, vipi unatatizo gani, nikamtizama chini kwanza ndo nikajibu nilizani unataka kunivuta, �� Mariam ivi uko sawa kweli wewe, yaani muda wote huo wewe hujalala unawaza kuvutwa? …
Unahitaji msaada sio bure wewe, Mimi najua umelala kumbe mwenzangu uko LINDO, ebu lala nimeshakwambia sikugusi leo, ningetaka ningeshakula muda sana, alivyoona bado ninauoga aliniminya shingo Kwa kushitukiza, nikazima…
Nakuja kuamka asubuhi, Niko peke yangu kitandani kucheki saa saa 5 asubuhi, nikaingia bafuni kuoga nakuta kabati yangu, imefuliwa ilihali Mimi nilishindwa kufua Kwa sababu ya mikono nikaihifadhi tu, nikiwa nashangaa bafu likafunguliwa akaingia Mudy…
Akaingia na kibra changu kaja kuanika inamaana yeye ndo kafua tobaaaa��, nilijifunika macho Kwa aibu, ajabu akaja nakunikumbatia, usinionee aibu ni moja ya wajibu wangu kama mme, mikono yako ina shida hivyo nitakufulia mpaka itakapokaa sawa, natamani hata kukuogesha pia lakini ulivyombishi tutaishia kugombana tu…
Nilivyokumbatiwa niliogopa, alivyomaliza kuongea akaanika, akaniambia nioge nije kunywa chai kashaandaa, tunywe twende kwa mzee wake tunaitwa tukapate chakula upajue na ukweni kwako…
Sikutaka makuu nikavunga tu ila moyoni nimeshamtukana matusi mia kidogo, nilichofanya nilimuomba tu atoke nioge, nilioga kibkibishi leo kidogo mkono ulikuwa umeachia, nilitoka nimevaa kabisa, nikanywa chai, tukaondoka kwenda huko kwao, ila umo kichwa nilikuwa napiga hesabu kibao, nyumbani wameshanitafuta mpaka wakaanza kuingia na hofu, nikaomba simu niwatafute…
Akageuza gari mpaka kwake tena akaingia ndani na kutoka na Ile simu ya usiku, ilikuwa sumsung, nilisahau kukukabizi jana, hio ni simu yako, moyoni niliifurahia simu mno, ila alienipa sasa ndo tatizo lilipo…
Niaiweka line yangu, nikampigia shangazi alipokea Kwa hofu, nikamtuliza nakumwambia Niko sawa kabisa ni simu tu iliharibika, ila mzazi ni mzazi tu alihisi sina uhuru, akasema ukiwa free nitafute…
Tulienda mpaka mitaa flan ivi imepoa, nakutana na mjengo ghorofa moja kali vibaya mno, tukaingia Kwa rimoti, kuingia tena ndani ni Kwa kujitambulisha kwenye camera ya mlangoni, ndo ufunguliwe…
Tulivyofunguliwa tu Amina wangu akaniwao Kwa furaha, alikuwa kashanimiss tayali, baba ake alisubili nae kumbato kutoka Kwa binti yake lakini hakuambulia zaidi ya salam tu, tena salamu inatolewa huku Amina wangu ananishika mkono kunipeleka mpaka sebuleni…
Nilipigishwa story mpaka nikakoma, alionekana kuwa mwenye furaha kuliko siku zote, aliona mikono yangu kama inamajeraha, alimfata baba ake baba usinambie wewe ndio umempiga mama angu mikono yake…
Nilishtuka Amina anaongea nini mwisho na wengine humu wasikie, Mudy alimbeba binti yake akaja nae mpaka kwangu, Amina Mimi sijampiga mama Ako, Yani Mimi nikimpiga ujue kabisa siku hio hataweza ata kutembea, ni ukorofi wa mama ako tu muulize vizuri kajikwaa wapi…
Mmmh baba Mimi mama angu na mjua vizuri sana, sio mkorofi, ni vyema uniambie mapema kabla sijajua ukweli mwenyewe, lilivyo limbwa likasema ukweli ety, lilikuwa na makosa Mimi nikawa nalipiga mpaka nikaumia…
Nilijua tu baba wewe ndo mkorofi, ulivyokuwa mzembe sasa, ukaacha atumie tu, wewe mwanaume bure kabisa, sijui ata kama unajua kutongoza baba, nikajikuta ninedakia ajue wapi anachojua tu nikupigana na kutoa amri kama yuko jeshini…
Dah kumeshakucha, ila wanawake, hii midomo yenu hii hapana, hapa nisipoondoka mtanitafutia kesi, mtanichokoza muda sio mlefu…
Itaendelea…��
Full sh 1000
Njoo WhatsApp katika namba 0683944333.