Katika Qur-aan na Hadiyth kumetajwa moto kuonesha mazingira mabaya watakayoshukiwa watu waovu, Waliompinga Allaah na kuendesha maisha yao ya hapa duniani kinyume na kanuni na taratibu alizoziweka Allaah (Subhaanahu Wa Taβala).
Maisha ya motoni ni kinyume na maisha ya Peponi ambayo picha yake tumeshaiona. Tunafahamishwa katika Qur-aan kuwa motoni kuna Daraja au Milango saba, na kila mlango iko sehemu iliyogawanywa.
βNa bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipoahidiwa wote. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewaβ. [Suratu-Al-Hijr:43-44].
Daraja hizi za moto zimepewa majina kama tusomavyo katika Qur-aan:
1οΈβ£ πππππ‘π‘ππ :
Katika Aayah nyingi jina hili limetumiwa, Kama jina la ujumla la maisha ya Motoni. Kama katika baadhi ya Aayah hizi Allaah Aliyetukuka Anasema:
βHakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tuβ [Al-Anbiyaa: 98].
ββ¦kisha Tutawahudhurisha pembezoni mwa Jahannam, wapige magoti (hapo)β [Maryam: 68].
2οΈβ£ πππππ: Moto wenye muwako mkubwa kabisa.
βAtauingia Moto wenye mwakoβ. [Suratul-Masad: 3].
3οΈβ£ ππ¨π§πͺππ ππ: Moto wa kuvunja vunja-Moto uliowashwa kwa ukali.
βHasha! Atavurumishwa katika Hutwamahβ. [Suratul-Humazah: 4].
4οΈβ£ π¦πβππ¬π₯π: Moto mkali wa kuunguza.
βBasi wapo miongoni mwao waliyoyaamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni (Saβiyra) moto wa kuwateketezaβ. [Suratun-Nisaa: 55].
5οΈβ£ π¦ππ€ππ₯π: Moto unaobabua.
βNitakuja mtia kwenye Moto wa Saqarβ. [Suratul-Mudaththir: 26].
6οΈβ£ πππππ¬π : Moto mkali.
βNa Jahiym itadhihirishwa kwa wapotovuβ. [Suratush-Shuβaraa: 91].
Basi bila ya shaka mtaiona Jahiymβ. [Suratut-Takaathur: 6].
7οΈβ£ ππππͺππ¬ππ: Moto uokwao kwa ukali.
βHuyo maskani yake yatakuwa Moto wa Haawiyahβ. [Suratul-Qaariβah: 9].
Wakosaji wataingia katika aina hizi za Moto kulingana na makosa yao. Kwa ujumla aina yoyote ya moto ulioandaliwa kwa ajili ya makafiri na wakosefu hata ukiwa na daraja ya chini namna gani, Utakuwa ni mkali usio na mfano na usiovumilika hata kwa muda mfupi sana kama Allaah (Subhaanahu wa Taβala) Anavyotufahamisha:
βHakika hiyo (Jahannaam) ni kituo kibayana mahali (pabaya kabisa) pa kukaa (hata kwa muda mfupi.β [Suratul-Furqaan: 66]
Kiufupi maisha ya motoni yatakuwa magumu sana kwa wakazi wake. Chakula chao kitakuwa cha moto wa kuunguza kila kitu tumboni, Mavazi yao yatakuwa ya moto, Kinywaji chao cha moto kitakachochemsha matumbo yao kama maji yachemkavyo kwenye sufuria ya shaba.
Tunamuomba Allaah (Subhanahu wa Taβala) Atukinge na adhabu ya moto, sisi na vizazi vyetu na Waislam wote kwa ujumla, Aamiyn.
Kwa faida zaidi
ππ’πππ’πͺ ππ π£πππ Naupenda Uislam
Wabillaahi at-Tawfiyq..