Ameelekea wapi nilianza kumtafuta maeneo yale lakini sikufanikiwa kumpata, Niliamua kwenda hadi nyumbani kwao na tina, Nilifika na kumkuta mama yake na tina anapika, Ilibidi nimdanganye kwamba tina nilimpatia vitabu vyangu anishikie lakini akaondoka navyo kama yupo huku nyumbani mwambie naomba anipatie,
Mama yake na tina akaniambia, Tina bado hajafika nyumbani nahisi atakuwa amelala hukohuko bweni,sababu sio kawaida yake kufika nyumbani mida kama hii. Dah! Nilimwambia mama ahsante nitavichukuwa hata kesho huko shuleni. Nikawa nimeondoka lakini kichwa kinaniuma huyu tina yuko wapi,
Nilianza kutapatapa kama nimechanganyikiwa, Nilirudi pale shuleni nikiwa kama mwendawazimu, Walinifuata wale marafiki zangu ambao tulitengeneza nao kengele, Walifika na kuniuliza (unamtafuta tina maana tulikuona unacheza nae harafu badae tulimuona tina akiwa na side). Palepale nilianza kumtafuta side maeneo ya pale shuleni lakini sikumuona, Niliondoka na kuelekea kwenye geto la side na wale marafiki zangu wakanifuata wakitaka kujuwa kuna nini.
Tulifika kwenye geto la side lakini hapakuwa na mtu na geto lilikuwa limefungwa na kufuri tukajaribu kuchungulia ndani lakini hatukufanikiwa kuona chochote, Ikabidi mimi na marafiki zangu tupange mpango wa kwenda kwa mwalimu jose, Lakini lazima tuwe na sababu za kufika pale kwake, Tukaona kwaku side hayupo kwake basi tukamuulizie kwa mwalimu jose,
Tukapanga tukifika kwa mwalimu jose tuseme kwamba side alituaga na kusema anafuata vitabu vya history kwa mwalimu jose, Ndio mana tumeamua kumfuata.
Kweli ikabidi tuelekee nyumbani kwa mwalimu jose, Tulifika nyumbani kwa mwalimu jose tukamkuta mke wake tukamuuliza, mwalimu jose yupo? (akatujibu hayupo) Tukamwambia hata hivyo tulikuwa tunataka tumuulize kama side amefika huku maana alisema anakuja kuchukuwa vitabu vya history, Lakini kama mwalimu hayupo sisi tunaondoka. Tukawa tumeondoka,
Lakini yote ni kutaka kujuwa tina yuko wapi na yupo na nani maana side tumemkosa na mwalimu jose tumemkosa, Dah,,,π₯ Mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio nilianza kuuona uchungu wa mapenzi,
Wale marafiki zangu wakasema twendeni kwa side tukamuangalie mara ya mwisho kama hatokuwepo bac tukalale, Tukawa tumerudi kwenye geto la side, Kufika tukakuta side yupo, Tulimgongea mlango na alipofungua niliingia ndani na kuanza kutafuta kama nitamuona tina, Lakini ndani mwa side sikuambulia chochote, Nikamuuliza side tina umemuacha wapi side akasema (niliagizwa na mwalimu jose nimpelekee vitabu tina na nilimpatia vitabu na kuachana nae na sijui tina alipo)
Tulitoka pale na marafiki zangu wakasema tukalale tutaonana kesho, Tukaachana na marafiki zangu, Lakini mimi moyo haukuridhika kwenda kulala bila kumuona tina, Nilipita hadi shule labda naweza nikamuona tina lakini sikumuona na nilikuta pale shuleni wameshasambaa, Nilienda zangu nyumbani kulala lakini usingizi haukupita sababu muda wote nilikuwa macho nikimuwaza tina.
Kwakuwa ilikuwa ni J-mosi, Asubuh niliamka dada yangu Zai akawa ananitania mbele ya mama, Akiniambia mbona macho umevimba utazani usiku ulikuwa unalia au jana wifi kakuzingua eti. Niliona dada anazingua nikaachana nae.
Ilipofika mida ya jioni nikawa nimeonana na tina, Nilimuuliza jana ulikuwa wapi mbona sikukuona wakati tulipanga kuonana. Tina akaniambia kwamba alikuwa anajihisi homa na alienda kulala bweni, Nikamwambia mbona nilisikia ulipeleka vitabu kwa mwalimu jose harafu mimi nilifika hadi kwa mwalimu jose lakini sikukukuta.!? Nilipoongelea habari ya mwalimu jose tina alianza kuwa mkali na kuanza kuniambia ( kwahiyo ukisikia nilienda kwa mwalimu jose tayari unaanza na kuhisi mimi ni malaya saana, kwanza unanichukuliaje maana naona unanifuatilia utazani wewe ni baba yangu Why!)
Ilibidi niombe msamaha kwa tina wakati yeye ndiye amenikosea, Hata hivyo hatukuelewana vizuri. Lakini pia siku ya kufanya mtihani ilikuwa inakaribia,
Ikafika J-tatu tukiwa darasani tina aliomba ruhusa aende chooni nilipoona tina anatoka nilivunga dakika chache na mimi nikaomba ruhusa niende chooni, Nilikutana na tina huko chooni tukaanza maongezi, Tina akaniambia kuna vitu vya mtihani hajakamilisha kununua, Kwahiyo akawa ameniomba pesa kidogo kwa ajili ya kukamilishia vifaa vya mtihani, Nikamwambia hakuna shida nitakupatia hiyo pesa ya kununulia hivyo vitu.
Lakini wakati tunamalizia maongezi alifika mwalimu Jose na kuuliza mnafanya nini huku?
Itaendelea...ππ»
~Daudi~.