Usiku usingizi haukuja Kabisa, nilikuwa nawaza huenda na huyu zakia alikiwa na shida na pesa wakapanga mipango yao kuja kupata pesaaa ,kwahiyo zakia kaja kutapeli tenaa??
Tulikaa siku mbili kuvuta subira lakini ilikuwa kimyaa, simu ya zakia haikuwa inapokelewa hata mara moja
Basi ile siku ya tatu , inno alikuja kasi chumbani kwetu yaan mule nilikuwa nalala na Alex na ilikuwa usiku akasema simu ya Zakia leo imepokelewa lakini nimeambiwa yupo hospital alipata ajali
Kila mtu alishtuka alex akasema piga embu ,inno akapiga
Ilikuwa ni sauti ya kiume akasema zakia aliletwa hospital siku ya Jumatano mchana alikuwa kwenye hatari baada ya piki piki yake kupamiwa na gari
Alex akauliza yupo hospital gani, akasema na hiyo siku ndio siku zakia alikuja nyumbani ina maana alipata ajali akitoka pale kwetu??
Alex ,inno na Subira waliondoka haraka kuelekea huko hospital ..
Nilibaki naomba mungu tu zakia bado awe upande wetu basii
Walirudi usiku sana lakini huwezi amini sikuwa nimelala, alex akanambia mke wangu unatakiwa kupumzika jamani,
Akanambia ni kweli tumemkuta zakia yupo hospital lakini anaendelea vizuri kwa taarifa za daktari
Tumelipia gharama zote na kesho tutaenda kumchukua kwahiyo usijali mke wangu nikasema sawa moyoni tu
Alinikumbatia aka akanambia salma wangu naona kabisa tunaenda kulea watoto wetu vile mungu alitaka tuwalee nasi binadamu
Hii ni njia mungu ametupa , tutaipita ili kesho tuwe imara zaidi ,salma wangu mimi nakuapia leo na hata kesho siwezi kuona mwanamke mwingine hata kwa bahati mbayaa hata iweje salma , usiku na mchana nitaomba mungu atulinde kama kufa basi nianze mimi mke wangu
Nilihisi kulia mana hayo ndio maneno haswa nayotamani kuyasikia kila sec kila dakika , saa na kila sikuuu
Najua Alex wangu ananipenda kupita maelezo yangu ...
Tulilala bwana pakakucha , Asubuhi na mapema Inno alikuja na Subira wakampitia Alex kwenda hospital , nilikuwa naomba tu Zakia aje hapa jamani afanye kama alivyosema mie niluahidi nikipona nitampa mungu sadaka kubwa iliyokubwa zaidi
Nitampa mungu mwili na roho yangu aviongoze yeye mpaka mwisho wa uhai wangu ambao yeye ndie amepanga ..
Walirudi nyumbani mida ya sa 6 mchana familia yote ipo tulikuwa sebleni anasubiriwa zakia nakwambia kama Queen vilee ,mama mkwe alikuwa anapiga maombi kama yotee
Mama yangu anasali na kumaliza dua zotee
Baba mkwe ndio usiseme anasali tuu yaan mie nae naomba moyoni na machozi kabisaa
Zakia alihudumiwa pale nyumbani karibu wiki zima ndio anapata kidogo afya yake
Wakati wote anaugua pale hakuna alie wahi kumuuliza kuhusu Juddy hata mmoja
Baada ya yeye kuona yupo vizur, siku moja alikuja chumbani , nilikuwa peke yangu aka akanambia Salma nakuahidi hii nimeteleza mara moja dada angu naomba unisamehe ,ulinisaidia mengi sana lakini mie nilikuangusha kwa wivu wa kipuuzi nakili nilikuonea wivu baada ya kuona umepanda na umepata nafanikio ya haraka kiasi kile
Nikiwa kama bint mpuuzi nilikuchukia na baada ya juddy kuja akatumia zile chuki zangu za kipuuzi kama faida kwake
Nakiri hapa nataka msamaha wako
Nilipo kuwa hospital nilihisi nakufa nilimuomba sana mungu anipe japo lisaa limoja tu.kwa ajili yakooo
Naamini nili ni lisaa limoja nililo pewa na mungu nitalitumia vizuri saanaaa, naomba unisamehe haukuwa na ushoga na mtu yeyote isipokuwa mie ukaniamini lakini mie nilikuangusha naomba unisamehe...
Zakia aliongea mengi sana yenye kujaza moyo wangu, nilihisi kupata nguvu kabisa
Zakia alinikiss kwenye paji la uso, niliomba mungu ampe afya ili alilokusudia likamilike na tulimalize
Alienda akamuita alex akaja mule chumbani, akachukua simu yake akampigia juddy
"We mwanamke hee ,mbona ulikuwa hupokei simu??" Juddy alipokea ile simu kachangamka akasahau hata kusalimiana
"Mwenzangu ile siku nakuja kwako wakati tunachat Nilikuwa kwenye boda nikapata ajali yaan hivi leo ndo natoka hospital "
"Weee pole jamani itakuwa mke mwenzio kakuwahi na unamungu wewe yaa hee ushkuru aisee"
"We acha tu, enhee nipeleke basi kwa yule babu nikammalize kuleee"
"Shoga hela unayo mana unasema ndo umetoka hospital hivyo mi nataka hela!!"
"Acha upuuzi we nambie nikukute wapiii , twende pesa ipo"
"Wee laki tano??"
"Nakupa.sita kabisa haki tena"
"Asante zakia usinifikirie vibaya et siwezi kukusaidia hapana mpenzi ,nataka mtaji nianze upya maisha nikamchukue na mwanangu roho inaniuma yule maraya yule kumchukua mwanangu basi tu aisee"
"Usijali nakuja japo tunaenda "
"Twende kesho asubuhi sana sawa"
"Sawa..."
Zakia alikata simu akamtazama alex , alex alichukua simu yake akampigia inno akamwambia njoo haraka huku chumbani , haikupita muda inno akawa amekuja
Aliambiwa maongezi ya zakia na juddy , alex akamuuliza tunaanzia wapi , inno akasema kila hatua kesho tutakuwa nyuma yenu zakia hakikisha unafanya kama tulivyokubaliana yaan muhimu tumjue kwanza huyo babu ndo wa muhimu kwa sasa tutamtumia huyoo
Zakia akasema naamini tutafanikiwa tu , niliwatizama wote huku naomba mungu mambo yafanikiwe mana ni kama vile uhai wangu kwa sasa unawategemea wao tuu kwa sasa
Mungu awaongoze vyema kabisaaa ...
Asubuhi na mapema zakia alimwambia juddy sehemu ya kukutana , Pale nyumbani walitoa gari moja wakampa Dereva halafu zakia akaongopa ni gari ya mumewe
Mimi alex inno na subira, tulikuwa nyuma na gari ingine , moyoni nasema mie leo naenda kupona jamani napona miee eeh mungu weee
MSIONE JANA NILIKUWA KIMYA MIMI NI MMOJA WA WATIA NIA SASA JANA NILIPATWA NA STRESS SABABU JINA LANGU HALIKURUDI HIVYO NDIO MAANA NILIKUWA KIMYA JANAπππ
ITAENDELEA...
KWETU morogoro.