Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Lakini wakati huo ndoa ya tina na sakidi ambaye ni mtoto wa sakina imestopishwa kwanza... Inaendelea... Sehemu Ya 18

31st Jul, 2025 Views 3



Baada ya sakina kwenda mahakamani, Kesi ikaanza kusikilizwa sakina na mumewe. Sakina alikuwa anataka talaka, Mzee alijaribu kukataa lakini ikashindikana, Mzee ikabidi akubali kutoa talaka, Lakini kabla hatoa talaka sakina akasema inabidi mzee kabla hajatoa talaka agawanye urithi kwa watoto wake wote sababu yeye umri umeshaenda hivyo anaweza akatangulia mbele za haki,harafu watoto wakadhurumiana kwenye kugawana mali.

(Sakina aliamua kufanya hivyo ili mwanae apate urithi mapema sababu yule mzee watoto wake ni wale wengine ni wakubwa kuliko Sadiki, na yule mzee hadi umri ule tayari ana wajukuu wakubwa tu, Kwahiyo sadiki ndio mtoto wa mwisho kwa yule mzee)

Wakati huo kesi inaendelea ya sakina na mume wake, Mimi huku nazidi kupambana na kazi ya kuuza mihogo niliongeza juhudi katika kazi hadi pale nyumbani kwao na Edina wakanielewa, Nilipiga kazi hadi na mimi nikawa naweka kamzigo kangu kadogo kisha nauza napata faida huku na kulipwa nalipwa, Lakini nikaona kuna vijana wameanza kumnyemelea edina Dah nikaona nikichelewa huyu mdada nitamkosa harafu nimeshaanza kumpenda, Nikaona nijitoe muhanga kama kunikataa anikatae lakini ukweli niwe nimeshamwambia, Ilibidi nikaze moyo kama mwanaume,

Nakumbuka ilikuwa ni jioni kwakuwa nilikuwa naelewana vizuri na Edina nilimuomba anisindikize kwenye shamba la jirani ili nikaangalie kama naweza nikapata mihogo ya kuongezea ili kesho yake nipeleke mjini, Tukiwa njiani nilianza kumpigisha story za mapenzi Edina alionekana kufurahi maana alijikuta anacheka na kuhuzulika kuotaka na vile ninavyomwambia na kumuuliza, Nikaona huu ni muda ambao ninapaswa niutumie vizuri wakati edina anafurahia story zangu nikamwambia na swala langu kwamba nampenda na ninataka nimuoe tuwe mke na mume, Edina alikaa kimya sekunde kadhaa kisha akaniambia sawa nimekuelewa lakini twende kwanza tukaangalie uwezekano wa kupata mihogo harafu kesho jioni ukirudi kutoka mjini natumaini nitakuletea kitu kizuri, Dah nikaona nisiwe na haraka sana sababu edina anaonekana kunikubali ingawa bado hajanipa jibu. Hiyo jioni nikiwa na Edina nikafanikiwa kupata mzigo na ikabidi kesho yake asubuh nikabebe na kuupeleka mjini,

Wakati huo kesi inaendelea mahakamani, Yule mzee akawa amekubali kugawa mali yake kwa watoto wake wote watatu na akimaliza kugawa mali kwa watoto atoe na talaka kwa sakina, Mzee akasema mali zote ziorozeshwe ili apate idadi kamili na namna ya kuzigawa, Mali ziliorozeshwa hadi zile za sakina ambazo zinahusiana na mali za mzee, Sakina alifurahi sababu aliona hata kama yeye atakosa lakini atakula kupitia mwanae, Mzee baada ya kuwa amepata idadi kamili ya mali zilizopo, Akasema ili ugawaji uwe wa haki inabidi akapime DNA na watoto wake wote ili kuthibitsha kama kweli wale ni watoto wake na kile anachokifanya ni sahihi.

Asubuh niliamka mapema na kwenda kuchukuwa mihogo ambayo nilienda kutafuta nikiwa na Edina nilifunga mzigo wangu kwenye guta na kuelekea sokoni kwenda kuuza, Nilishukuru Mungu sababu nilimaliza mzigo mapema, Lakini wakati nipo barabarani natoka katikati ya mji kurudi nyumbani ghafla ilikuja gari na kupaki mbele yangu, Na alishuka tina, Tina akaniambia niachane na guta langu ili yeye anipe lifti. Nilihisi amenidharau pakubwa sana,nikamwambia tina kabla ulimwengu haujaweka hadharani maovu ya sakina ni bora wewe ukaondoka sababu utaaibika bila hatia. Tina akanijibu hayo ni maneno ya mkosaji,kama wewe ulikuwa unaigiza sisi tunaishi, Aliingia kwenye gari na kuondoka.

Sakina aliposikia swala la kwenda kupima DNA alikuwa kama mwendawazimu, Akasema kama ni swala la DNA bora mpango wa yeye kupewa talaka uahilishwe kwanza, Mzee akasema hapana mpango wa sakina kupewa talaka uko palepale, Sakina alianza kupata kiwewe baada ya kuambiwa neno DNA sakina alijikuta hadi anashindwa kuelewana na mwanae, Sakina alikosa namna ya kufanya ikabidi aanze kunitafuta ili angalau nikamsaidie.

Wakati nimetoka kuongea na tina nikawa nimefika nyumbani, Lakini nilikaa siku zaidi ya tano bila Edina kunipatia jibu langu, Hadi nikawa naona kama vile Edina ananizingua, Siku ya sita wakati nimetoka kwenye mizunguko yangu ile nafika nyumbani bahati nzuri na Edina na yeye akafika pale kwangu, Tukapiga story mbili tatu mwisho Edina akaniambia unakumbuka nilikwambia nitakuja na kitu kizuri kwa ajili yako bac kuanzia leo nitakuwa wako hivyo naomba na mimi nibaki kuwa wako siku zote,❤️ Mwanaume nilifurahi sana na kuanzia hapo nikawa na mahusiano na Edina,

Baada ya kuwa edina amenikubali siku inayofuata nilienda kuuza mihogo nikiwa na furaha kweli, Nilifika na kuuza mzigo wangu lakini nikawa nimebakisha kidogo ikabidi nianze kutafuta mteja wa kununua mzigo uliobaki, Lakini wakati naendelea kutafuta mteja nikakutana na sakina, Mwanamama sakina akaniambia kila kitu kuhusu kesi yake na mume wake, Akaniomba nimsaidie niende kwa mzee nikamshauri aachane na mpango wake wa kwenda kupima DNA, Nikamwambia sakina kwa sasa siwezi tena kushiriki kwenye mambo yako, Sakina alianza kunilazimisha ikawa kama vile ni ugomvi, Hasira zilinipanda nikamsukuma akaangukia kwenye dimbwi la maji machafu, Watu wote pale sokoni walishangaa kuniona muuza mihogo kama mimi namsukuma mwanamama tajiri kama sakina, Nilimuacha akiwa chini mimi nikaondoka,

Nilifika nyumbani nimechoka na mawazo mengi nikapitiliza kulala, Siku inayofuata ikabidi nionane na Edina tulikaa na kuongea mengi hadi tukapanga kufunga ndoa, Ikabidi nianze kuandaa mahari, Nikawa kila nikipata pesa kidogo naihifadhi kwa ajili ya mahari ya kumuoa Edina, Nikapamba hadi nikawa nimepata kiasi cha laki nne, Nikaona kwa hii pesa niongeze angalau ifike laki tano ili kama nitaelewana na wazazi wa Edina nitoe mahari nusu harafu nyingine nitamalizia,

Lakini wakati huo mwanamama sakina maji yapo shingoni, Mzee hataki kusikia chochote kutoka kwa sakina, Sakina hakuwa na ujanja wa kumzuia mzee, Ikabidi watoto wote wa mzee waende hospitali kwa ajili ya kwenda kupima kipimo cha DNA.

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Lakini wakati huo ndoa ya tina na sakidi ambaye ni mtoto wa sakina imestopishwa kwanza... Inaendelea... Sehemu Ya 18  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-lakini-wakati-huo-ndoa-ya-tina-na-sakidi-ambaye-ni-mtoto-wa-sakina-im
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest