Tulipofika usawa ule ambao amesimama yule mwanamke, Yule mwanamke akatuita kaka zangu habari zenu, Tukamjibu poa, Akasema naombeni msaada wa mnisaidie kubadirisha spea tairi maana tairi moja limepata pancha. Tulitazamana mimi na marafiki zangu sababu hakuna hata mmoja kati yetu ambaye alishawahi kutengeneza gari wala kuziba pancha. Kisha rafiki yangu mmoja akasema sisi hatuwezi labda tukakuitie mafundi pale senta ili waje wabadirishe hilo tairi. Lakini mimi nikawaza kama niliweza kutengeneza kengele na watu wakaipenda hivi kweli nishindwe kubadirisha tairi la gari,
Nikamwambia yule mwanamke hakuna shida tutabadirisha tairi sisi wenyewe, Yule rafiki yetu ambaye alisema hatuwezi yeye akakataa na kuondoka, Mimi na rafiki yangu mmoja tukaongozana na yule mwanamke mpaka pale alipopaki gari lake, Akatupatia vifaa na tukaanza kazi, Mimi nikiwa na rafiki yangu mmoja tukafanikiwa kubadirisha tairi la gari tukatoa lile lenye pancha na kuweka tairi lingine,
Tulipomaliza yule mwanamke alishukuru na akatoa pesa kunipa, Mimi nikamwambia madam hakuna shida kaanayo tu hiyo pesa, Lakini akalazimisha tuchukuwe ile pesa kama sehemu ya shukuran. Kwakuwa mimi ndio nilionekana kama fundi pale, Ikabidi nimwambie rafiki yangu chukuwa hiyo pesa.
Kwakuwa yule mwanamke alikuwa anaelekea kushoto na sisi kulia hapakuwa na haja ya kupewa hata lifti, Tulimsaidia kurudisha vitu vyake kwenye gari, Na yeye akaingia kwenye gari lake akawasha na kuanza kuondoka huku akituaga (kwaheriniii) Lakini alisogea mbele kidogo na kusimama kisha akatuita nikaenda na kumuuliza au kuna kitu umesau pale ilipokuwa gari, Akasema hapana lakini samahani unaitwa nani jina ili hata siku nyingine tumekutana mjini uko niwe najua yule ni fulani, Nilitabasamu nikamwambia naitwa David, Alichukua card ambayo ilikuwa na namba ya simu akanipatia na kuniambia haya ni mawasiliano yangu siku labda una shida na wewe unaweza ukanitafuta. Kisha akaondoka. Mimi niliogopa hata kumuuliza jina lake.
Ikabidi na sisi tuendelee kwenda nyumbani lakini rafiki yangu akaniuliza mbona yule mwanamke kama kuna kitu amekupa, Nikamwambia hapana nilikuwa namuelekeza akifika njia panda aelekee kulia, Sikumwambia kama nimepewa card yenye namba za simu. Ile pesa ambayo ametupatia yule mwanamke ilikuwa ni kiasi cha elfu ishirini, Ilibidi tugawane elfu kumi,kumi Wakati tunaelekea nyumbani tulikutana na yule rafiki yetu ambaye alikataa kushiriki kwenye ubadirishaji wa tairi, Alituuliza vipi mlifanikiwa? Tukamwambia ndio tumefanikiwa na pesa tuliyopewa hii hapa, Tulimuonesha kwamba kila mtu katoka na kumi,kumi Alitamani tumnunulie hata soda lakini tukamwambia hilo haliwezekani.
Nilifika nyumbani nikawa naiangalia ile card ya namba za simu, Nilikuwa namfikiria yule mwanamke jinsi alivyokuwa mzuri lakini kwa mwonekano yeye ni mkubwa mimi ni mdogo, Lakini pia gari alilokuwanalo ni gari la gharama sana, Harafu kwa jinsi alivyokuwa inaonekana wazi yule ni mwanamke mwenye pesa, Nikafikiria labda atakuwa ameolewa na kama hajaolewa mbona anaonekana ana pesa nyingi, Kama yeye anapesa na mimi sina hata pesa ya kununulia simu ni kitu gani nitamwambia, Niliwaza nikaona huyu mwanamke hata kama nikimpigia simu sidhani kama anaweza akanielewa kwa chochote, Nikawaza au niitupe ile card, Lakini nikaona ngoja niiweke huwenza kuna siku itanisaidia. Lakini wakati huo mimi sina hata simu.
Maisha yakaendelea lakini sina hata mawasiliano na tina, Nikiangalia toka aondoke tina nimekuwa mpweke sina hata wa kunifariji, Pale nyumbani napo dada nae alishaolewa nimebaki na mama na baba, Wakati mwingine najikuta nafanya hadi kazi za kuosha vyombo. Maisha yakaendelea kibishi, Ikabidi nifanye mpango wa kununua simu, Kweli nikawa nimefanikiwa kununua simu ya batani,
Baada ya kuwa nimenunua simu nilitamani ningekuwa na namba ya tina, Nahisi tungekuwa tunaongea zaidi ya masaa nane. Nakumbuka kuna siku nilikuwa nafua lakini katika kukagua mifuko ya suluali yangu nikaiona ile card ambayo ina namba za simu za yule mwanamke, Niliacha kwanza kufua nikazichukua zile namba na kuzijaza kwenye simu yangu kisha nikaingia ndani na kumpigia,
Yule mwanamke alipoke simu na kuniuliza wewe nani? Nikamwambia mimi David yule ambaye alikurekebishia gari lako. Akasema Aah kumbe ndio namba yako, (mimi ndio) Bas sawa nitakutafuta badae kidogo maana nina kazi kwa sasa, Akawa amekata na simu. Nilichukia nikaona kama vile anaringa sana, Nikaitupia simu kitandani nikatoka nje na kuendelea kufua.
Zilipita siku kadhaa yule mwanamke akawa amenipigia simu tuliongea mengi akanitajia na jina anaitwa Sakina; Maongezi yakaendelea akawa ananipigia simu mara kwa mara, Lakini nilikuwa naogopa kumwambia kama nampenda, Sababu amenizidi umri mpaka na pesa,
Kadri tunavyozidi kuongea nikaona bora nimwambie ukweli maana nikizembea nitamkosa. Nilikaza Moyo na kumtongoza yule mwanamke, Nikamwambia ukweli kama nampenda. Alinijibu,Sawa unanipenda lakini nitakupa jibu lako wakati sahihi ukifika. Niliona afadhari maana nilikuwa nahofu anaweza akanifokea na kuniona kama kijana nisiyekuwa na adabu.
Nilikaa kama wiki bila maongezi na mwanamama sakina, Baada ya muda mrefu bila mawasiliano mwanamama sakina, Alinipigia simu na kuniambia tukutane kijiji cha pili kutoka pale kijijini kwetu. Mwanaume sikuwa na pesa ya kutosha ukizingatia naenda kukutana na mwanamke kama Sakina, Chap,chap ilibidi nikope pesa kwa washkaji ili niongeze kwenye pesa niliyonayo, Sababu alinipigia simu ghafla istoshe wakati huo sikuwa na pesa kiviile, Nikawa nimepata pesa kidogo kwa mshkaji wangu.
Nikaoga nikaangalia nguo ambayo ni safi na kali kuliko zote viatu vilikuwa na vumbi nikavisafisha kwa kitambaa, Nikatoka nje nimependeza hadi mama akaniuliza (wapi mwenzetu au ndio unaenda kumpokea tina maana nazisikia skia tu) Nilicheka na kujisemea kimoyomoyo wamama nao hawachelewi kujua jambo. Nikatoka na kuelekea kumuangalia mshkaji wangu mmoja wa bodaboda kwa ajili ya kupata usafiri,
Nikapata usafiri lakini wakati tupo njiani kuelekea kwa mwanamama sakina, Mshkaji wangu wa bodaboda akawa ananiuza kuna nini mwangu mbona umetupia kiaina, Nilicheka na kumwambia nyoosha barabara wewe...
Itaendelea...βπ»
~Daudi~.