Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Lakini cha ajabu nilimkuta mtu mwingine kabisa ambaye simfahamu, Na alikuwa ni mwanaume. Inaendelea... Sehemu Ya 8

31st Jul, 2025 Views 3



Lakini mkononi mwake alikuwa ameshika bahasha, Nilitaka kurudi sababu niliogopa huwenda akawa ni mtu mbaya, Yule jamaa akaniambia usiogope kuna mtu kanituma naamini wewe ni David, Nikajiuliza amelijuwa vipi jina langu au huyu mwanamke ameolewa. Yule jamaa alipoona nazidi kuwa na hofu akanipatia ile bahasha na kuniambia nadhani unamfahamu aliyenituma, Niliichukuwa ile bahasha huku naogopa. Jamaa aliponipatia bahasha aliingia kwenye gari na kuondoka.

Nilibaki nimesimama huku mkononi nimeshika ile bahasha, Muda kidogo sakina akanipigia simu, Nilipokea simu huku sielewielewi kinachoendelea, Sakina akaniambia kuna bahasha hapo umepewa lakini usiogope ni mimi nimemtuma akuletee sababu kuna kazi kidogo hapo kama utaiweza utanisaidia,lakini kwa sasa wewe nenda nyumbani ukipata muda ukatulia bas nitafute nikupe maelekezo. Kidogo wasiwasi ukawa umepungua maana nilihisi naweza kutekwa.

Nilifika nyumbani muda umeenda ilibidi nile na kuingia kulala, Lakini kabla sijalala nikaona ni vyema nikampigia sakina ili nielewe ni kazi gani anataka kunipatia, Nilimpigia akaniambia fungua kwenye hiyo bahasha kuna majina na maelezo baadhi yameandikwa humo kwahiyo inabidi uyapange yakae kimpangilio ukimaliza kesho nijulishe. Nikamwambia sawa.

Lakini wakati naongea na sakina, Tina nae alikuwa anapiga simu na kuambiwa inatumika, Ile namaliza kuongea na sakina, Tina nae akapiga akawa ananiuliza muda wote napiga simu yako inatumika ulikuwa unaongea na mtu wako eti,harafu nimesikia umeondoka, Nikamwambia hapana mimi nipo tina akagoma akasema kama kweli upo njoo nyumbani kwetu sasa hivi sije nikuone kama kweli upo. Dah nikaona haya mambo ya bahasha nitashughulika nayo kesho, Ikabidi nitoke usiku ule kwenda kulala kwa tina, Sababu hata hivyo nilikuwa nimemkumbuka sana, Maana tangu kipindi kile aondoke ndio hivyo tena.

Nikalala kwa tina mpaka asubuh jua linachomoza bado nimesinzia, Lakini nikawa kama naota nasikia sauti ya mama yake na tina akimuamsha tina afanye usafi pale nyumbani, Nilishtuka ile kuchungulia dirishani jua tayari limechomoza, Tina aliamka na kuniambia jifiche uvunguni haraka mama kila siku lazima aingie humu chumbani kwangu, Nilizama uvunguni tina akachukuwa na nguo zangu akanitupia hukohuko uvunguni na kuniambia nitulie. Tina alipofungua mlango mama yake aliingia hadi ndani, Kisha Akauliza, tina siku hizi una simu mbili? Tina ikabidi amdanganye mama yake kwamba ile ni simu ya rafiki yake lakini imeharibika na ataiijia mwenyewe ili aipeleke kwa fundi. Mama yake na tina akasema haya toka ukafanye usafi.

Tina alitoka nje na kuanza kufanya usafi wakati huo mimi nikiwa uvunguni mwa kitanda, Nilitulia uvunguni mwa kitanda hadi mida ya saa nne asubuh, Tina aliniletea chakula na kunipatia, Nilikula chakula nikiwa uvunguni mwa kitanda, Lakini nikakumbuka sakina anaweza akanipigia harafu mambo yanaharibika, Ikabidi niichukuwe simu yangu pale mezani na kuizima kabisa,

Nilijificha chini ya uvungu mpaka saa tisa, Kwakweli niliona kama ni adhabu nimeipata hata hivyo tina alikuwa analala nyumba tofauti, Niliogopa kutoka sababu wangeniona wazazi wa tina ingekuwa ni kesi nyingine, Wakati mwingine tina alikuwa anaingia mule ndani na kuanza kunicheka, Nilikuwa nachukia. Nilikaa ndani hadi mida ya saa kumi jioni,tina akaniambia jiandae kutoka sababu wazazi wangu kuna sehemu wanaenda kwahiyo itabidi utoke.

Wazazi wa tina walipotoka na mimi ikabidi nitoke mule ndani na kuelekea nyumbani. Nilifika nyumbani nikaingia ndani mwangu huku nawaza upuuzi ulionitokea,ile nawasha simu sakina nae akapiga nilipo pokea simu akaniuliza kama nilimaliza kazi yake, Nikamwambia ndio namalizia maana nilibanana na kazi za nyumbani. Ikabidi niifungue ile bahasha ambayo nilipewa na yule jamaa, Nilipoifungua nilikuta kuna michoro lakini katikati ya ile michoro kuna kiasi cha pesa kimeandikwa,

Mimi kwa akili ya haraka haraka nikagundua hapa inawezekana wanatafuta namna ya kugawana pesa au kama sio hivyo huwenda kuna biashara ya mzunguko wa pesa, Ambapo kila mzunguko unapoisha kuna mtu atachukuwa pesa na kugawana na wengine, Nikaona pengine hii ni hisa ya biashara, Ikabidi nianze kuifanyia kazi.

Nikachukuwa jina la sakina nikalijaza mara mbili harafu majina mengine kama matano hivi nikayaweka mara mojamoja. Mfano kama watu wanahitaji malipo kutokana na kazi ambayo wameifanya bas jina la sakina ndio litakuwa linagawa pesa ya malipo kwa wengine, Harafu na lenyewe linalipwa, Inamaana kwamba jina la sakina litakuwa linalipwa mara mbili, Ndani na nje, kwahiyo ndani litasimama kama mfanyakazi harafu nje litasimama kama boss.

Nilipomaliza muda ukawa umeenda hivyo simu ya sakina ikawa haipatikani, Lakini nilianza kuwa najiuliza mbona simu ya sakina mida ya usiku mara nyingi huwa haipatikani, Nikaona labda huwa anachoka na kazi,

Nikampigia tina na kuanza kuongea nae, Kwakweli mapenzi mimi na tina yakaanza kukolea tina akaonesha kunipenda sana hadi tukafikia hatua ya kuwekeana ahadi ya kuoana.

Kesho yake nikamtafuta mwanamama sakina nikamwambia kazi yako tayari, Akasema sawa kuna mtu namtuma aje kuchukuwa utamkuta pale baa. Ikabidi nianze safari ya kuelekea Kijiji cha jirani kupeleka ile bahasha. Nilifika lakini sikumkuta anayeiijia ilibidi nikae kumsubiri baada ya masaa mawili alikuja mwanaume mwingine tofauti na yule wa mwanzo, Kwakuwa alikuja na gari ya sakina nikaona hakuna shida nikampatia ile bahasha akaondoka.

Mwanamama sakina alipoipokea ile bahasha na kuikagua kwa mara ya kwanza alinipigia simu mida ya usiku na kunishukuru, Alionesha kufurahia kazi yake vile nilivyoipangilia, Alinisifia na kuniambia maneno ya mahaba hadi nikawa nashindwa kati ya tina na sakina nimpende nani. Sakina akawa ameniambia inabidi nifanye mpango wa kuhamia mjini...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Lakini cha ajabu nilimkuta mtu mwingine kabisa ambaye simfahamu, Na alikuwa ni mwanaume. Inaendelea... Sehemu Ya 8  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-lakini-cha-ajabu-nilimkuta-mtu-mwingine-kabisa-ambaye-simfahamu-na-al
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest