Mayner alipofika chumbani, aliangua kilio kisichokuwa cha kawaida. Alianza kwa kwikwi, lakini maumivu yalipomzidi, alilia mazima.
โIna maana mimi huyu mtoto si wa mume wangu kweli? Si wake huyu? Lini ameniona mimi nikichepuka? ๐ข Lini ameona nikimleta mwanaume humu ndani?โ alijiuliza, lakini majibu ya maswali yake alikosa.
Amani katika moyo wake ilipotea. Alijiona ni mwanamkiwa aliyetengwa na wazazi. Alijiona ni mmoja wa watu ambao wanapaswa kuchukua maamuzi magumu, maamuzi ambayo yangeweza kumtengenezea furaha, lakini hakujua aanzie wapi?
Mtu pekee ambaye alihisi angeweza kumsaidia kwa wakati ule alikuwa rafiki yake, yaani Laila. Alipapasa simu yake katika mkoba. Alipoiona, alimtumia meseji kama ingewezekana basi aende chumbani ili wazungumze.
Laila naye alipopata meseji alifika haraka chumbani na walianza kuzungumza huku machozi yakimdondoka kila sekunde.
โNawaza hatima ya maisha yangu katika hii nyumba, namuwazia mwanangu, na huenda nawaza hata kuondoka ๐. Lakini itakuwaje? Nitaenda wapi wakati bado nampenda Garma?
Moyo wangu na kila kitu kipo kwake, lakini ona nacholipwa na mama yake!โ alisema huku akilia mno.
โNimemsikia mama vizuri tu. Pia nimemsikia Garma kwa masikio yangu. Anaonekana bado yupo na mapenzi ya dhati kwako ๐. Kwa hiyo ni mapema sana kusema kwamba unataka kuondoka hapa. Utaenda wapi na huyu mtoto mdogo?โ
โLaila, wewe ni rafiki yangu. Umekuwa kama ndugu kwangu. Vuta picha, mama anaongea kabisa kwamba mimi si mzuri, malaya na natoka nje! ๐ก Sijui mwanae sijui amekosea kuzaa na mimi, alienda akarudi. Kwa hali ya kawaida unachukuliaje? Eh! Unachukuliaje? Nami nina moyo! Nina moyo ambao unabeba maumivu au anataka nami nilipize vile ambavyo anafanya ndiyo ajue kwamba ninaumia?โ Mayner aliendelea kulia.
Mdomo wake ulikuwa ukitamka maneno huku mwili ukitetemeka. Kila neno ambalo lilitoka kinywani mwake liliambatana na machozi yaliyodondoka katika nguo yake.
โNateseka, naumia, nakosa amani katika maisha yangu. Hapa sijaolewa, na vipi nikiolewa? Si ndiyo mateso yatazidi? Nitanyanyaswa kwa kigezo kwamba nimelipiwa mahari.โ
โUnayoyaongea hata mimi yananiumiza, tena sana tu ๐ข. Lakini nikuombe ukubali kuteseka ili mtoto aishi kwa amani. Kumtenga mtoto na baba ni kumuumiza. Ona alivyokuwa mzuri, alelewe na mama peke yake kweli?โ aliuliza Laila.
Mayner hakuwa na la kusema. Alimtazama mtoto wake ambaye hakuwa anaelewa lolote. Chozi lake lilidondoka katika paji la uso la mtoto yule, kisha alilifuta.
โFazma mwanangu, bibi yako ananitesa. Bibi yako ananipa maumivu ambayo hata kukuambia naogopa,โ alisema huku akiendelea kumtazama mtoto.
โNdio hivyo mwaya, endelea kukomaa tu ๐ช. Kumbuka mmepanga nini na Garma, kumbuka wapi mmetoka. Kama kweli mna mapenzi ya dhati, na kile ambacho yeye amekiongea pale nje anamaanisha, sidhani kama mtashindwa kufikia malengo yenu.โ
โMh! Ahsante rafiki yangu, ahsante kwa ushauri wako. Nitajaribu,โ alisema Mayner.
Walijikuta wanazama katika maongezi mengine ambayo yalihusu stori za malezi na mambo mengine ya hapa na pale. Mwisho, Laila aliomba kuondoka ili kwenda kupambana na jua huko nje. Hakukuwa na namna zaidi ya kumruhusu ili kesho kama kungekuwa na uwezekano aweze kuja tena.
Laila aliondoka hadi sebuleni ambako alimkuta Garma akiwa amejiinamia katika sofa, kichwa chake kilikuwa kinatunga sheria mithili ya kobe.
โShem, naondoka,โ alisema huku akijiweka sawa. Garma aliinua kichwa chake na kumtazama Laila, akasema:
โMapema mbona? Nikajua kwamba utakaa labda?โ
โMh! Hapana, ila kesho nitakuja. Si unajua nimeshinda hospitali, halafu pia nanuka jasho kama nini?โ ๐
โAnha! Sawa basi, shika hii hapa ya usafiri. Maana nimechoka mno ningekupeleka kwa gari,โ alisema Garma huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa waleti. Kisha alichomoa elfu 20 na kumkabidhi.
โAhsante. Mama yupo wapi?โ
โMama! Mama, walitoka na yule mpumbavu wake nje,โ alisema Garma.
โOk, basi kwaheri,โ Laila alizungumza na kuondoka mahala pale.
Alipiga hatua hadi nje ambako alikutana na mama Garma akiwa na Ninah, wanazungumza. Mazungumzo yao yalikuwa ya siri kidogo, maana walipomuona ilibidi wakae kimya. Naye aliamua kuwapita bila hata kuwaaga.
โWewe binti, njoo hapa!โ alisema mama Garma huku akiweka kaukali kidogo katika kauli yake.
Laila aliwaza kwa muda kama aende au arudi, mwisho aliamua kurudi ili apate kumsikiliza anataka kusemaje.
โHivi rafiki yako ana nini?โ aliuliza mama Garma.
โKwanini?โ
โKawa kingโangโanizi kwa mwanangu, anatuletea zombie katika familia yetu. Hivi tukisema watu wenye watoto watoe watoto wao mbele, kale alikokatotoa yeye sijui kukinya ni katoto kale?โ
โMama, mbona unafika mbali hivyo?โ
โNyoko! Mbona unafika mbali hivyo? Kumbe nawe zuzu, enh? Ndio mnakaa na mwenzako mnasema mumsingizie mwanangu mtoto, si ndio? Nakuambia hivi, kesho njoo uchukue maiti ya yule mtoto. Aya, ondoka ila habari ndio hiyo,โ mama Garma alizungumza kisha akabetua midomo yake na kumruhusu Laila aondoke.
Moyo wa Laila ulidunda mno ๐. Akawaza kuhusu kauli ya mama Garma na neno ambalo amelisikia, akapatwa na wasiwasi. Alitamani arudi tena ndani ili kuzungumza na Mayner lakini alihisi kama hakuwa na sababu ya kufanya hivyo. Mwisho aliamua kuondoka bila hata kumsemesha.
Mama Garma na Ninah waliendelea na mazungumzo yao. Walipata kuongea kuhusu mpango wao.
โNilikuja hapa kuangalia kama tayari, lakini huyu Garma sijui kawaje, khe,โ alisema Ninah.
โUsijali bwana, yule mtoto mbona anakufa. Si sindano umesema tayari au?โ
โNdiyo.โ
โBasi ondoa shaka, na jioni kuna jambo nitamfanyia. We subiri tu,โ alisema mama Garma.
โLipi hilo?โ
โNitakuambia.โ
โMh!โ
โNdiyo. Sisi si tunajua, ni wakongwe kwenye hizi kazi bwana,โ alikazia kauli yake.
Kuanzia leo hakikisha unanifollow ili usome simulizi hizi hapa.
1. Nilimuua Mama ili niolewe na Baba
2. Alizaa na shemeji yake
3. Mume wangu akitaka nimuue.
Ninah hakuwa na jinsi. Walipata kuongea mambo mbalimbali hadi pale ambapo waliagana, huku Ninah akiondoka na mama Garma akirudi tena ndani. Uso wake uliweka tabasamu kuona kwamba jioni kama si usiku wa siku ile, kuna jambo ambalo anatakiwa kulifanya.
Hatimaye masaa yalikimbia, na jioni iliingia huku ikiwa na kiubaridi hivi.
Jukumu la kumuogesha Mayner lilikuwa kwa Garma ambaye alienda naye bafuni. Hakutaka kumpa jukumu lile mama yake kwa hofu aliyokuwa nayo juu ya mke wake.
Bafu lao lilikuwa chumbani kwao, hivyo ilikuwa rahisi kuoga huku wakiwa na uhakika kwamba mtoto wao alikuwa sehemu salama. Kwa bahati mbaya, mlango wa chumba waliacha wazi bila hata kujua. Wakati wapo chooni, wamefungulia bomba la maji huku maji mengine ya moto yakiwa katika ndoo.
Ndipo mama Garma aliingia chumbani na kumchukua mtoto. Alimwingiza shuka mdomoni ili asipate kupiga kelele. Akamshika miguu juu, kichwa chini mithili ya Pazi wa kwenye simulizi ya darasa la tatu kwenye kitabu cha Kiswahili simulizi inayoitwa Jogoo Aliyesema.
Baada ya kumshika, alianza kumrusha rusha kama anashindilia roba la mpunga hivi. Kwa zaidi ya mara nne alifanya, na mwisho alimuachia kwa kumweka sawa kama ilivyokuwa mwanzo, na kuondoka katika chumba kile.
โKufa mbwa wewe, mwanangu anazaaje mtoto mweusi?โ alijisemea akiwa mlangoniโฆ
Nunua simulizi hii kwa 1000Tsh. Njoo WhatsApp, namba ni 0717255498.