Walishtuka baada ya kuniona mbele yao nikiwa nimesimama kimya, mikono yangu ikiwa imeshikilia mfagio na deki macho yangu yakiwa yameelekezwa moja kwa moja kwao.
Ukimya ulitanda kwa sekunde chache, kisha mama wa Loveness akageuza uso kwa dharau kama vile hakuwa amesema chochote.
Loveness naye alijaribu kuficha aibu kwa kuchezea nywele zake, lakini macho yake yalionyesha wasiwasi
Nilitoa tabasamu dogo la mwanaume aliyejifunza kuishi katika dunia ya mawe na miiba, kisha nikasema kwa sauti ya staha:
“jamani sio vizuri mi nadeki, halafu nyinyi mnachafua..”
Mam loveness alijibu" kijana mbona unavoongea kama una miliki hii nyumba? Au ushakuwa baba mwenye nyumba?
" Hapana si maanishi hivo mama ?
" Ooooh koma mimi mama yako toka lini? Punguza shobo".
" Mama kosa langu ni lipi ? mpaka mnanichuki hivo? .
" Neno mama litowe kichwani mwako mimi sio mama yako. Yaani kosa lako ni kuishi hapa
" Lakini mama....
" Lakini nini? hebu toka huko,kaendelee na kazi"
Niligeuka na kuondoka polepole, Sikuwa na nguvu wala kauli kwa familia kwa sababu am just a servant.
Lakini nilihisi kama moyo wangu unazidi kupasuka.
Kila siku hapa ilikuwa ni kipimo cha uvumilivu.
Kila saa ilikuwa ni vita ya heshima.
Na kila dakika, ilikuwa ni somo la maisha.
Nilirudi sebuleni na kusafisha tena na niliwasikia wakicheka na kusema " huyu ataondoka mwenyewe usijali mwanangu " nilisikia sauti ya makofi yaani kunitesa kwao ni sherehe ....
Siku zilizidi kwenda siku zilizidi kukatika na mwisho wa mwezi ulifika mzee akanipa hela yangu siwezi kuitaja ni siri yangu. Basi nilifurahi na kuona ninachoingiza sasa ni kikubwa tofauti na kile cha mara ya kwanza . Nikawa natumia nusu na nusu naweka benki....maana hata wahenga walisema akiba haiozi
Lakini mategemeo yangu,ni kwamba labda tukikaa muda mrefu chuki yao itaoungua kwangu lakini ilikuwa ni sawa na kuzima moto kwa petrol. Daima moto utaendelea kuwaka tena sio tena ule ule utakuwa zaidi.
Licha ya chuki, nilizidi kujituma.
Nilifua, niliosha, nilipika, nilitengeneza wiring ya taa ya korido iliyokuwa ikizimika-zimika, nikabadilisha fuse box ya jiko, hata gate la umeme lilipoharibika, nililitengeneza kwa ustadi hadi mzee Makani aliponipongeza:
“Maiko, sihitaji mafundi wa nje tena, nawe unanipunguzia gharama kubwa.”
Loveness alianza kunitazama kwa macho tofauti kidogo.
Hakuniambia kitu, lakini alikuwa akinipita karibu na kucheka chini kwa chini.
Lakini mama yake bado alikuwa ngumu kama mawe ya milimani
Hakuwa na hata tone la huruma, na kila nilichofanya kwake kilikuwa makosa.
Mpaka siku moja aliponifokea kwa kusema:
"Unafikiri kwa sababu unaonekana una akili na bidii, basi utanunua heshima? Kumbuka, hujazaliwa hapa!”
Nilimwangalia na kusema kwa sauti ya upole:
"Sijazaliwa hapa mama, lakini sihitaji kuzaliwa hapa ili niishi kwa heshima. Heshima haizaliwi hufundwa na huonyeshwa.”
Mama yule alicheka sana na kusema kwa kejeli " kweli mbwa ni mbwa hata umpe jina.saizi tumemlea sasa anapata mpaka jeuri ya kunijibu. Aligonga mikono yake na kucheka
Nilishindwa hata nimwambie nini ,maana kwake kila kitu nakosea.Sijuwi nini nitafanya anipende yaani hata mpango wa kumtongoza binti yake uliishia njiani. Inanibidi sasa nitafute namna kwanza familia inielewe ....
🌓 Usiku mmoja wa saa saba...
Nikiwa nimeamka kwenda kunywa maji, nilipita sebuleni na kukutana na mtu...
Loveness!
Alikuwa amekaa peke yake, macho yakiwa mekundu kana kwamba alikuwa akilia.
Nilisita, nikamwuliza:
“Uko sawa?”
Hakujibu mara moja. Kisha akasema kwa sauti ya chini:
“mi niwe sawa au nisiwe sawa wewe kinakuwasha nini . Hebu fanya mambo yako"
Lilinishuka mmmmh yaani lile jibu lilinifanya nijione mjinga.nilienda nikanywa maji na kurudi chumbani. Lakini nilipita palepale na kumwambia " usiku mwema"
Akanijibu tena " kaka mbona una shobo hivyo au unanitaka? Usiku mwena? Wa nini ? Na kwanini? Hebu nitoke hapa.Niliondoka haraka haraka kuelekea chumbani lakini maumivu niliyoyasikia ndani ya moyo wangu duh nashindwa hata kuyaelezea maana ni maumivu makali.
Nililala chali nikawaza sana niligeuka kila upande usingizi hauji . Niliamua kuamka na kutoka nje angalau nipunge upepo . Nilipofika sebuleni nilikuta taa imezimwa nikajua tayari kaenda kulala . Hivyo hata mimi ilinibidi tu nikaulazimishe usingizi.
Siku iliyofuata kwa kuwa nilichelewa kulala hata kuamka nilichelewa . Nilipitazama nje tayari ni kweupe niliamka haraka na kutoka nje nilikuta nyuma imedekiwa kwenda bafuni masink yamesuguliwa kwenda jikoni vyombi vimeoshwa. Niliogopa sana nakusema kimoyo moyo" mmmmh kama nimama kisirani hapa nimeisha"
Mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio sana ghafla sauti ya mama loveness ilisikika" baba mwenye nyumba pole na uchovu chai tayari. Wafanyakazi tumeshapika .
Niliogopa daaaaah......
FULL1500
099286085.