Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Siri Ya Mvuvi Na Bahari Lakini kabla ya kunijibu akaniuliza umesema unanipenda je una malengo gani na mimi... Inaendelea... Sehemu Ya 05

2nd Aug, 2025 Views 37



Nilimjibu kirahisi tu nitakuoa, mrembo Salha akawa amenikubali tukaendelea na maongezi, badae mambo yakawa mazuri nikatafuta nyumba ya kulala wageni, nikalala na Salha usiku ule mpaka asubuh, kwa mara ya kwanza nikajikuta nimemsaliti Latifa, lakini asubuh palipokucha niliamka na kujikuta nikiwa peke yangu, na mlango umefungwa kwa ndani, Mh! nilianza kujiuliza au niliamka na kufunga mlango baada ya Salha kuondoka!? nikawa sielewi ilikuwaje hadi Salha hayupo harafu mlango umefungwa! tena kwa ndani!? nilijiuliza maswali mengi lakini nikaamua kuachana nayo, badae nilikutana na Latifa lakini nilikuwa nikimtazama usini najihisi kumkosea sana,

Zile siku tatu za kuanza kazi zikawa zimefika lakini kabla hatujaenda kazini tukapata taarifa kwamba yule jamaa ambaye ni mmiliki wa ule mtumbwi, inasemekana kwamba amepotea sababu toka achukuwe ule mtumbwi hakufika hata nyumbani kwake,hivyo alipotelea njiani. watu waliingia baharini kujaribu kumtafuta labda watapata hata mwili wake lakini hakupatikana, na kwenye zoezi la utafutaji tulikuwepo na sisi, lakini hatukusema kama mara ya mwisho aliijia mtumbwi kwetu.

Baada ya kuwa amekosekama sisi tukaamua kurudi kwenye eneo letu la kazi, lakini ule mtumbwi tukaukuta upo pale tunapofanyiaga kazi Riziki alikuwa mtu wa kwanza kushangaa, lakini mimi na Goma tulikuwa tunaelewa kuhusu ule mtumbwi, tukamwambia Goma leo hali ya hewa ya bahari sio nzuri inabidi tukae angalau siku moja ndio tuanze kazi, Goma akasema hapana hali ya hewa ya leo ndio nzuri kuliko siku zote sababu bahari ikimeza mtu ndio samaki wanakuwa wengi, ikabidi tujiandae kuingia baharini, tukasogeza mtumbwi wetu ndani ya maji pamoja na vifaa vya uvuvi, lakini hali ya hewa ilikuwa ni mbaya sana sababu mawimbi yalikuwa ni makubwa sana,

Tuliingia baharini na kuanza kuyakata mawimbi tukiwa na mtumbwi wetu, lakini tunavyozidi kwenda ule mtumbwi ukaanza tena kuongeza kasi kuelekea katika kina kirefu cha maji, mtumbwi ulianza kuongeza mwendo, Goma akatuambia shikilieni msiachie, mimi kwakuwa haikuwa mara yangu ya kwanza hivyo nilichukulia ni kawaida tu, lakini mtumbwi uliongeza kasi Riziki alianza kupiga kelele akiogopa jinsi mtumbwi unavyoenda kwa kasi, mtumbwi ulikuwa unakimbia kama unataka kupaa, Riziki aliogopa sababu sio kwa kelele zile, ule mtumbwi ulipokaribiria sehemu yenye kina kirefu cha maji ukaanza kupunguza mwendo hadi ukasimama wenyewe,

Mtumbwi uliposimama hali ya hewa ikawa tuliva pakawa hakuna mawimbi hata kidogo yaani maji yakatulia tuliii, (kimya kikatawala) Goma alichukua kamba na kujifunga kiunoni kisha akatuambia tutulie wala tusiogope akamsistiza Riziki atulie sababu yeye ndiye alionekana kuogopa zaidi, Goma baada ya kufunga ile kamba kiunoni akaniambia niishikilie ile kamba na nisijaribu kuiachia kwa hali yeyote ile yaani chochote kitakachotokea nisiiachie ile kamba, Riziki akaambiwa yeye akae kwenye mtumbwi na asijaribu hata kidogo kujitupa ndani ya maji, Riziki akauliza kwani leo tunavuaje samaki maana sielewi, akaambiwa fuata kama nilivyokuelekeza,

Goma alitoka ndani ya mtumbwi na kuanza kutembea juu ya maji huku akinena maneno ambayo sisi hatuyaelewi, ilikuwa tayari ni usiku wa manane, mimi na Riziki tulianza kuhisi labda ni ndoto sababu sio kwa maajabu yale, Goma alitembea hatua chache kisha alisimama juu ya maji (na maji yametulia kama kwenye mtungi) Goma alianza kuzama polepole wakati huo mimi nimeshikilia ile kamba, Goma alizama mpaka akaacha kuonekana (hadi wakati huo sisi hatuelewi Goma anafanya nini) baada ya kuwa amezama ndani ya maji, sisi huku kwenye mtumbwi tukaanza kuvutwa, mtumbwi ukaanza kuyumba ghafla hali ya hewa ikabadirika bahari ikachafukwa yakaanza kuja mawimbi makubwa ule mtumbwi wetu ulianza kuwa kama vile unapaa, mtumbwi ukaanza kuvutwa kama vile tunaingizwa ndani ya maji, mtumbwi ulikuwa unaingizwa ndani ya maji na kupandishwa juu, Riziki alianza kuwa na wasiwasi, mwisho akajitupa ndani ya maji, alipojitupa ndani ya maji alianza kuzama, mimi wakati nataka kumuokoa Riziki, ile kama iliniponyoka na kudumbukia ndani ya maji, Goma akazama na ile kamba Riziki na yeye akazama, kutokana na hali ya hewa alishindwa hata kuogelea akajikuta amezama, mimi nikabaki peke yangu,

Nikawa nimebaki mwenyewe, nikawa kama nimechanganyikiwa sababu sijui cha kufanya, hali ya hewa ilianza kubadirika na kuwa ya kawaida, lakini wenzangu wote wamezama ndani ya maji, nilianza kuwatafita lakini sikuwapata, nilitafuta hadi nikaona panakaribia kupambazuka, ikabidi nigeuze mtumbwi na kuanza kurudi lakini huku nikiwa na hofu,kwamba nitasema nini kwa watu hadi wanielewe kwamba wenzangu wamepotea baharini,

Nilipoanza kurudi ule mtumbwi niliuendesha kidogo nikajikuta nimetokezea pale kwenye sehemu yetu ambayo huwa tunapaki mitumbwi, ule mtumbwi nikaufunga pale kisha nikaenda nyumbani lakini kichwa hakipo sawa sababu wenzangu wote niliokuwanao wamezama ndani ya maji tena kwenye mazingira ambayo sio ya kawaida, nilifika nyumbani na kujifungia ndani huku nikiwa na mawazo mengi. Nilikaa ndani hadi mida ya jioni, ilipofika mida ya jioni nikatoka na kwenda kutembea kule pembezoni mwa bahari huku nikiangalia kama naweza nikawaona wenzangu, hadi wakati huo hakuna mtu mwingine ambaye alikuwa anajuwa kama wenzangu wamepotelea baharini,

Lakini wakati naendelea kutembea huku nawatafuta wenzangu nikawa nimekutana na Salha, Salha akaniuliza umepoteza nini mbona kama vile kuna kitu unatafuta, kabla sijamjibu chochote, nikamuuliza ile siku tumelala wote ilikuwaje mbona uliondoka na kuniacha mlango ukiwa umefungwa kwa ndani" Salha akasema inaonekana ulikuwa na usingizi sana mbona nilikuamsha na ukainuka na kufunga mlango harafu mimi tayari nilikuwa nje" Dah, nikaona Salha ananichanganya, ikabidi niachane nae, lakini wakati naondoka Salha akaniambia ukikosa kile unachokitafuta jaribu kunitafuta na mimi ili nikupe msaada" siku,mjibu chochote, sababu kwanza naona kila kitu kimeharibika, nikamuacha Salha,nikaendelea kuwatafuta wenzangu,

Niliwatafuta mule pembezoni mwa bahari lakini sikuwaona mwisho giza likaanza kuingia, ikabidi nirudi kwanza nyumbani lakini wakati narudi nyumbani nikakutana na ndugu yake na Riziki, yule ndugu yake na Riziki akaniambia mama yake na Riziki anaumwa, kwahiyo wanamtafuta Riziki ili awapatie pesa ya kwenda hospitali, nikaona huu ni mtihani mwingine, ikabidi nitoe kiasi kidogo cha pesa na kumpatia, lakini yule ndugu yake na Riziki akaniambia kwamba ukimuona Riziki mwambie awahi hospitali kuja kumuona mama yake...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Siri Ya Mvuvi Na Bahari Lakini kabla ya kunijibu akaniuliza umesema unanipenda je una malengo gani na mimi... Inaendelea... Sehemu Ya 05  >>> https://gonga94.com/semajambo/siri-ya-mvuvi-na-bahari-lakini-kabla-ya-kunijibu-akaniuliza-umesema-unanipenda-je-una-malengo-gani-n
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest