Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI; NURU HALISI SEHEMU 10

1st Aug, 2025 Views 10



ENDELEA........
Ugomvi wao ulitapakaa kila kona, Sabrina akiwa kavaa nguo za kulalia aliwakalisha chini kujua shida nini.

"Naweza kujua kwanini umeingia chumbani kwa Anjeli"

"Nilienda kumkumbusha majukumu yake cha ajabu aliniwasha kibao" Hilda aliongea.

Sabrina alimgeukia Anjeli kusikia ni kitu gani ataongea. Cha ajabu Anjeli alimgeukia Osman.

"Kwanini una muangalia Osman! kwanini yeye ndio sababu ya wewe kuchelewa! kuamka" Asha aliongea.

"Naweza kuonekana kichaa mbele yenu lakini Mimi si mtu wa kupenda kuzungumza uongo, usiku wa jana niliamka kumpikia Osman chakula. Nadhani mnaelewa changamoto za kuchoma chapati, nilichelewa kwa sababu hiyo".
Anjeli alitumia akili kubwa kumfikishia ujumbe Sabrina kuhusu chanzo cha ugomvi.

"Sitarajii kuona hii nyumba imegeuzwa kuwa uwanja wa mieleka..... Hilda naomba unifuate chumbani kwangu" Sabrina aliongea.

Osman, Asha na Victor waliondoka kwa sababu muda wa kwenda kazini ulikuwa umefika.

Kitendo cha Hilda kuingia tu chumbani kwa Sabrina alikula kibao.

"Nilipendekeza uolewe na Kijana wangu kwa sababu niliamini wewe ni mwerevu kuliko mabinti wote hapa Jijjni Mwanza. Ni aibu kuona una shindana na Mfanyakazi. Jitahidi kumzuia Osman asielekeze macho yake kwa Binti mwingine. Nitafurahi ukianza kuhudhuria clinic na si kujitia mcheza mieleka" Sabrina aliongea.

"Unaweza kuwa ni mkwe lakini sitavumilia kuona unatetea usaliti, naomba uniache niitetee ndoa yangu hata kama ni kwa kumwaga damu. Ile siku unaniomba niwe mke wa mwanao nilikueleza kuhusu kichaa changu, misimamo yangu pamoja na imani yangu kuhusu mapenzi. Nitafurahi kama utakuwa mtazamaji, kuhusu swala la kwenda clinic si jukumu langu pekee yangu....mkumbushe mtoto wako atimize majukumu yake ya kitandani" Hilda aliongea kisha akaondoka akiwa kakunja sura yake.

Anjeli akiwa bado amekaa sebuleni aliitwa kwa ishara na Hilda mfano wa binadamu anavyoitaga mbwa..
Hakuona nouma alimfuata,

"Sikiliza msichana, huenda ukawa ni Dada poa uliyehitimu mafunzo katika Chuo Cha maka....haba, lakini naamini una akili timamu.
Siku ya leo nitaisahau.... naomba usirudie kutembea na Mume wangu, endapo utafanya hivyo utaishi jehanamu maisha yako yote, nenda ukaandae chai umpelekee Osman " Hilda aliongea kisha akaendelea na shughuli yake.

Kuna namna Anjeli alijisikia hatia ndani ya moyo wake alijiahidi kukaa mbali na Osman. Ndiyo, hili swala limo ndani ya uwezo wake kwa sababu hakuwa amempa moyo wake Osman.

Aliingia jikoni akaandaa chai, baada ya kumaliza alielekea chumbani kwa Sabrina.

"Sababu uliyonipatia leo siyo ya kishujaa hata kidogo ni kama ulikuwa unaniambia ni kukate vidole vyako vyote.....Osman anaweza kuwa na tabia ya umalaya lakini jitahidi kukaza na si kuonekana kama Dada poa wa kiwango cha chini. Naomba usisahau hata Dada poa huwa na mipaka na heshima yake.... unaweza kwenda" Sabrina aliongea.

Anjeli alielekea kwenye Kampuni la DreamCloud akiwa kapendeza, kila mtu alimkodolea macho kutokana na uzuri wake.

Osman akiwa anaongea na Victor, alijikuta akipoteza ujasiri wa kupangilia maneno yake.
Kumbukumbu ya kilele alichofika usiku wa jana kupitia Anjeli ilimchanganya zaidi.

"Tutaongea baadae" Osman aliongea kisha akaelekea ofisini kwake.

Victor alijikuta akicheka pekee yake kimtindo.

"Kitu gani kina kufurahisha .." Asha aliuliza baada ya kumfuma akicheka

"Sikuwahi kufikiria kama Osman anaweza kuzagamua Dada wa kazi tena nyumbani!....ni heri wangeenda hata Lodge. Hakika hisia ni kitu cha ajabu...na hata hivyo Anjeli ana kila sifa za kumtesa Osman" Victor aliongea.

Asha alitaka kuachia ngumi lakini siku ya leo hakuwa na bahati mkono wake ulidakwa.

"Husikii aibu kumpambania Mwanaume ambaye hana taarifa kama unateseka kwa sababu yake!...hakika unajidhalilisha mwenyewe" Victor aliongea kisha akaondoka.

Upande mwingine, Osman alifurahia chai aliyoletewa.

"Naomba usije kurudia kuzungumza kuhusu mapenzi, moyo wangu unauma kwa sababu nimemkosea sana mke wako" Anjeli aliongea.

"Nafikiria kukuondoa nyumbani kwetu.....nataka nikupangishie nyumba. Najua unaweza kunifikiria tofauti lakini Hilda hakuwa chaguo langu. Ni chaguo la Mama..... nashindwa kuvuta hewa vizuri kwa sababu yako" Osman aliongea.

"Una shindwa kuvuta hewa?... pole kwa hilo itapendeza kama utamueleza mkeo kuhusu hili, naomba niondoke kwa sababu umemaliza kunywa chai" Anjeli aliongea akikusanya vyombo.

Osman kafikia hatua mbaya hakika, alihitaji kumkumbatia Anjeli kabla hajaondoka.

Anjeli hakuwa tayari kwa hili.... walianza kusukumana huku na kule.

Asha aliingia bila hodi baada ya kuchoka kusikiliza mazungumzo yao.
Osman ndio kumuachia Anjeli....

"Ni kitu gani kimekupata kwenye akili yako?....kama unahitaji kimada niambie ni kutafutie lakini ai kutembea na Dada poa, hakika nasikia aibu. Una mdhalilisha mkeo" Asha aliongea baada ya Anjeli kuondoka.

"Kuwa Mlinzi wangu wa karibu haimaanishi unaweza kuongea chochote kuhusu mambo yangu, kuna muda huwa nahisi kama umekuwa Mama yangu hivi. Jaribu kuishi kama Victor" Osman aliongea.

Asha alijitoa ufahamu akamkumbatia Osman.

"Naomba unipe nafasi pia kwenye moyo wako....kuna namna nateseka, nimekuwa nikiteseka na nitaendelea kuteseka endapo utaendelea kunipuuzia" Asha aliongea.

Osman alimsukuma kwa nguvu, kama si kujishikiria kwenye meza angeumiza kichwa chake vibaya.

"Kumpenda Anjeli haimaanishi namdharau mke wangu, haimaanishi hata wewe uanze kuzungumza vitu vya ajabu. Hilda ana heshima yake katika moyo wangu naomba usije kutafuta sababu ya kumuona hafai, sioni hasara kukufukuza kazi..... naomba ukae na Victor akufundishe namna ya kuishi na boss....ingawa sijawahi kumuambia lakini anajua kuishi kama Mlinzi na si Kaka wala Baba kwangu" Osman aliongea.

Victor akiwa mlangoni aliachia tabasamu kwa sifa nzuri alizokuwa anazisikia.
Siku zote huwa anajichukulia poa lakini leo alijipigia makofi baada ya kusikia ana kubalika kinyama.

Aliondoka kwa haraka, hakutaka kuonekana.

Upande wa Anjeli akiwa chumbani kwake, alijikuta akikosa amani ya kuendelea kufanya kazi hapa.

Akili yake ilimuambia kama ataendelea kukaa hapa basi anaweza kupoteza maisha.

"Nitamuuzia utu wangu Osman kwa mara nyingine..... pesa atakayo nipatia itanisaidia kurudi Jijini Dodoma, hapana nitaenda Morogoro....nina uhakika nitafanya vizuri nikiwa huko" Anjeli alijisemea moyoni mwake kisha akasubiria kufatwa na Osman..............Kumeanza kuchangamka. Hii story kuisha bado sanaaaaa. Kwa bei ya 1000 utaisoma yote.....

NAMBA YA MALIPO 0743770612 JINA JOFREY.

UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP KWA NAMBA 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI; NURU HALISI SEHEMU 10  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-dada-poa-wa-usiku-mmoja-mtunzi-nuru-halisi-sehemu-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest