Josephat alipotoka mochwari kuutazama mwili, alifika sehemu aliyomuacha mke wa kaka yake – mama Caro. Aliulizwa:
"Vipi, mume wangu anaendeleaje?"
Joseph alizubaa kama sekunde kadhaa, kisha alimjibu:
"Aah, hali ya kaka siyo mbaya sana wala nzuri sana..."
Mama Caro akazidi kuchanganyikiwa, akasema:
"Shemeji mbona mnanichanganya? Maana mume wangu aliondoka nyumbani akiwa si mgonjwa wa kuweza kuzidiwa. Hebu nipeleke nikamuone kwa macho yangu. Haiwezekani mtu aondoke nyumbani mzima, halafu niambiwe kazidiwa."
Akimshika mkono shemejiye na kumvutia kuelekea wodi walipo wagonjwa, alisema:
"Nataka nikamuone mwenyewe."
Josephat akamzuia na kumuuliza:
"Unataka kwenda wapi?"
"Nikamuone mwenyewe."
"Hapana shemeji, hatuwezi kumuona kwa sasa. Yupo chini ya uangalizi wa daktari na wamesema twende nyumbani, turudi baadaye."
Kwa shingo upande, alikubali akiwa na mawazo mengi kichwani. Walipokuwa kwenye gari, Joseph alikuwa bize sana na simu – kumbe aliwajulisha ndugu kwa meseji kuhusu msiba walioupata.
Walipofika nyumbani, mama Caro alishangaa kuona watu wamekusanyika. Pale pale, akili yake ilimtuma kitu fulani, lakini hakutaka kuamini. Akahisi labda mwanawe Caroline, aliyemwacha nyumbani, atakuwa amepatwa na tatizo.
Ghafla, mwili wake ulipatwa na mshtuko baada ya kumuona Caro akikurupuka kutoka mikononi mwa watu waliokuwa wakimshikilia, na kuanza kumkimbilia mama yake huku akilia:
"Mama... mimi ndo sina tena baba... nani atanisomesha mimi? Oooh baba, baba... babaaa! Mama, yuko wapi baba? Umemuacha wapi baba? Aaaaah!"
Mama Caro, mwili wake uliingiwa na ganzi – akapoteza fahamu. Watu walikuja kumbeba na kumwingiza ndani akiwa hajitambui.
Caro sasa akaanza kumlilia mama yake, akidhani naye amefariki. Hakika, ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwenye familia.
Kikao cha familia kilikaa. Wengi walihoji kifo cha ndugu yao kilitokana na nini. Joseph hakuwa na jibu sahihi; alitoa maelezo aliyopewa na Dokta Mery. Kila mtu hakuyaridhia maelezo hayo.
Mmoja wao akasema:
"Mi nafikiri twendeni hospitali, huko tutapata majibu kamili."
Msafara ukaanza kuelekea hospitali. Walipofika na kuhoji kifo cha ndugu yao, walipewa ripoti iliyoonyesha kuwa alizidiwa muda mfupi alipofika kwa daktari.
Hawakuridhika na majibu yale – wakaomba waonane na mganga mkuu. Walipofika ofisini kwake, hawakumkuta.
Dokta Mery akawaita kwenye ofisi yake na kuwaambia:
"Mimi ndiye niliyempokea ndugu yenu. Alifika kwangu na kunielezea kuwa kichwa kinamuuma sana. Wakati najiandaa kumchukua vipimo, akazidiwa, ikabidi nimpeleke wodini kwa matibabu zaidi. Nako, bahati haikuwa kwetu – ndipo akaaga dunia."
Mmoja wao akamuuliza:
"Daktari, ina maana ulishindwa kabisa kuokoa maisha ya ndugu yetu?"
Dokta Mery akajibu:
"Oooh... unajua, daktari kazi yake ni kutibu, si kuzuia kifo. Samahanini sana kwa kilichowatokea."
Akaulizwa tena:
"Sasa daktari, hamkubaini ni kitu gani kilichomsababishia kifo?"
Akaeleza:
"Kama ripoti inavyoonesha, tulimpiga picha na tukabaini alikuwa na hitilafu kwenye ubongo, iliyosababisha damu igande na kufanya ubongo ushindwe kufanya kazi."
Kiasi waliridhika na majibu yale, hivyo wakaomba kwenda kuangalia mwili wa ndugu yao.
Bado mzee Sixbert, anayedhaniwa kuwa marehemu, alikuwa pembeni ya mwili uliolazwa chini – mwili unaofanana kabisa na yeye. Wakati bado akiendelea kujishangaa, aliwaona ndugu zake wakiingia mle mochwari – akiwepo Josephat.
Walipofika, wakawa bize kuukagua ule mwili huku machozi yakiwadondoka. Mzee Sixbert alitaka kuongea – alishindwa kutoa sauti, alishindwa kunyanyua mguu wala kiungo chochote cha mwili. Yeye aliwaona, lakini wao hawakumuona.
Alitamani kuwasemesha – akashindwa. Alijiuliza:
"Hawanioni au?"
Basi, alibaki kuwatizama wakiangaika na ule mwili unaofanana kila kitu na yeye. Maskini, machozi yalimtoka – hakujua hatima yake.
Mara, ule mwili akaona ukigeuka na kuwa mti wa mgomba. Lakini kwa kina Josephat na wenzake – bado waliendelea kuona ni mwili wa ndugu yao.
Walifanya taratibu zote za kuuchukua ule mwili uliyoonekana kwa macho ya kawaida. Ila upande mwingine, haukuwa mwili – bali ni mti wa mgomba.
Mganga mkuu aliitisha kikao cha dharura kutokana na vifo vya kutatanisha vilivyotokea kwenye hospitali yao. Cha kwanza ni yule mtoto mchanga, pili ni yule mzee. Akasema:
"Hamuoni kama inatia doa hospitali? Kwanza, Dokta Mery yuko wapi? Atueleze, kwa kuwa ndiye alikuwa daktari wa zamu."
Kumbe muda huo, Dokta Mery – hamu ya kula nyama za watu ilimshika haswa. Alijizuia, akashindwa. Akaamua kuelekea mochwari.
Mganga mkuu alimuagiza Nesi Tina amwite Mery. Tina alikwenda kwenye ofisi ya Dokta Mery, akamkosa. Alipowaulizia wenzake, wakamwambia:
"Tumemuona akielekea mochwari kwa haraka sana."
Nesi Tina naye akaelekea huko. Alipofika, aliufungua mlango. Alichokiona – hakuamini. Na alishindwa kabisa kuzuia mshangao wake.
Akajikuta akisema:
"Haaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!"
✨ ITAENDELEA…
FULL 1000
📞 0699286085.