Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

Riwaya: MAPEPE Na Mtaalam wa Simulizi SEHEMU YA KWANZA **

16th Jul, 2025 Views 21


UTANGULIZI.
"Kwa majina naitwa Kelvin Peter Lucas,wengi wanapenda kuniita 'Kevoo',Umri wangu ni miaka 29 tu,lakini yaliyomo moyoni mwangu ni zaidi ya huu umri nilionao,huenda nisingelikuwa na uvumilivu Leo hii nisingelikuwa duniani nakusimulia kisa hiki cha maisha yangu"

"...Nikiwa na umri wa miaka 25 ndio ilikuwa mara yangu ya mwisho kukanyaga ardhi ya mkoa wangu wa Mara, sehemu ambayo niliyozaliwa.Kiukweli sitamani kabisa kurudi tena nyumbani kwa sababu Moyo wangu utaumia zaidi ya sasa".

" Tangu niingie jijini dar es salaam na kujichanganya na wauza madafu wa kariakoo,uchungu wa yaliyonikuta umeanza kupungua kidogo,huenda ninayokueleza ukashindwa kunielewa na kuniona nimerukwa na akili".

"Pesa ninayoipata kupitia uuzaji wa madafu naitumia kujikimu Mimi mwenyewe,nilisema na nitaendelea kusema kwamba,sitamani tena kumpenda mwanamke,ni bora nikachukue wanawake wanaojiuza sinza na riverside(riva saidi)".

" Wazazi wangu wameshatangulia mbele ya haki,Baba alifariki nikiwa na umri wa miaka kumi na sita,akatuacha watoto watatu ambao ni Mimi,kaka yangu Paul Peter na mdogo wangu wa mwisho Rebecca peter"

"Chumba changu kidogo kinafanana na stoo ,maana ndani nimetandika godoro chini,pembeni kuna tenga mbili za kuhifadhia madafu na ukutani nimebandika picha ya zamani ya marehemu Mama yangu,kila nikiamka asubuhi naumia Sana kwa sababu sikurudi nyumbani kumzika Mama yangu,siyo kwamba sikuwa na nauli,la hasha,lakini kuna sababu kubwa ambayo ndiyo imenifanya mpaka siku ya Leo nikuhadithie kisa hiki cha maisha yangu"

**
MWANZO.
Ilikuwa siku ya jumatatu majira ya saa moja kamili asubuhi,niliamka kwa kukurupuka maana nimechelewa Sana siku ya Leo kutokana na pombe nilizokunywa usiku wa Jana.
"Dah,nimechelewa" (niliongea peke yangu huku nikiwahi ilipo ndoo ya maji).

Chumba ninachoishi nimekipangilia kawaida Sana,siyo kwamba sitamani niishi maisha mazuri Kama wenzagu bali sina uwezo wa kulipia chumba cha gharama,hapa penyewe nilipo ninadaiwa kodi na mwenye nyumba.

Nilichukua mswaki wangu uliotumika kwa muda mrefu,nikachukua kopo la dawa ya meno.
"Dawa nayo imeisha" (nilianza kuichana dawa ya meno ili nichokonoe kwa ndani)

Nilifanikiwa kupata dawa ya kuswaki asubuhi ya Leo,nikachota maji kwenye kikombe na kutoka nje,nyumba niliyopanga tunaishi watu watano,wawili wa kike na wakiume tupo wa watatu, mwenye nyumba anaishi jirani na hapa.

Nilitoka nje nikiwa na bukta pekee,kifua changu kilichojazia nilikiacha wazi bila ya kuwa na aibu.Nilinawa haraka haraka nikarudi ndani kwa ajili ya kujiandaa na siku ya Leo.

Nilivaa nguo zangu za kazi,nikabeba mfuko wa madafu nikatoka nje,nilielekea ulipo mkokoteni wangu nikayaweka madafu.
"We Kevo,unataka kuondoka bila kudeki chooni!" (ilikuwa ni sauti ya mpangaji mwenzangu wa kike anayefahamika kwa nina la Irene)

Irene ana gubu Sana,kelele kwake ni jambo la kawaida,mtaa mzima anajulikana kwa kuwa na mdomo mrefu Kama chiriku.
Niligeuka nikamuona Irene akiwa amesimama nje ya mlango wake na kanga moja.
"Aah za asubuhi Dada"

"Nani dada yako kevo?Kama huwezi kunipatia mambo bora uache"

"Samahani Irene"

"Haya,mwenzangu unaenda kazini bila kufagia chooni?"

"Irene,Mimi ni mtoto wa kiume"

Irene akashika kiuno,akaanza kutikisa mguu mmoja kwa dharau
"Kwahiyo ukiwa mtoto wa kiume ndio usisafishe choo?Mimi nimeamka zangu asubuhi nakuta choo kichafu,nenda kadeki kwanza ndio uende lasivyo hatuelewani hapa" (Irene aliongea kwa sauti ya juu mpaka nikaona aibu).

"Mimi nakuelewa Irene unachotaka,nitakueletea jioni nikirudi"

"Hayo ndo maneno sasa,kumbe unaelewa unajikuta mjanja"
Irene akaingia ndani.

"Huyu anapenda Sana hela" (niliongea huku nikianza kuusukuma mkokoteni wangu)
Irene ni mpangaji mwenzangu,anapenda Sana pesa,huwa namuachia pesa anisaidie kudeki,sasa siku ya Leo alivyosikia najiandaa kutoka bila kumpatia dili la pesa akaona atoke nje.

ingawaje hapa nina mwaka mmoja na nusu lakini sijawahi muona Irene anaelekea kazini,kuanzia asubuhi mpaka usiku huwa ni mtu wa kulala tu,hatujui pesa anatoa wapi,ila anakula na kulipa kodi kwa wakati.

Nilianza kuusukuma mkokoteni nielekee sokoni kariakoo,nilikuwa napishana na magari ya kifahari.
"Mh,haya maisha jamani,wengine wanatembelea Gari Mimi nakokota mkokoteni" (nilikuwa naongea peke yangu barabarani).

**
Kando mwa barabara inayoelekea sokoni kulikuwa na vijana watatu wafanyabiashara wakiwa katika mazungumzo.
Mmoja anajihusisha na biashara ya kuuza magazeti,Mwingine ni muuzaji wa Karanga na watatu ni muuza matunda.

Muuza magazeti anafahamika kwa jina la Daniel.
Daniel akasikika akisema
"Leo Kevo amechelewa sana" (akachukua gazeti moja la michezo)

Muuza karanga anayeitwa Hamis akajibu
"hata Mimi sielewi,labda tumuulize rafiki yake john atuambiie ni wapi alipo Kevo msomi aliyeangukia kuuza madafu"(akawa anacheka).

John Muuza matunda ni rafiki yangu,yeye ndiye aliyenisaidia kupata mtaji wa kuuza madafu.John amekuwa zaidi ya ndugu wa damu,ananipatia msaada wa mawazo pale ninapokwama.

John na Mimi huwa tunaelewana sana gengeni,nipo radhi kusimama kwa ajili yake na yeye hivyo hivyo hapendi kuniona nikiwa mnyonge mbele zawatu.

Maneno ya Hamis yakamfanya John awatazame kwa jicho la pembeni kisha akasema.
" Asubuhi asubuhi mmeshaanza umbea wenu,nyie ni watoto wa kiume mtavalishwa sketi kuweni makini"(akaendelea kupanga matunda).

Hamis na Daniel wakakaa kimya,biashara zetu wanne zimepangana,wote huwa tunauza eneo moja tofauti ni biashara tunazozifanya,Mimi nauza madafu na wenzangu wanafanya biashara zao ambazo zinawaingizia kipato.

**
Niliusukuma mkokoteni wangu wangu(haraka haraka) mpaka nikafanikiwa kufika sehemu ninayoweka mkokoteni wangu siku zote.Niliwakuta wenzangu wakiwa wameshafika muda mrefu Sana.

"Oya Daniel niaje?"

"Kwema kaka msomi"(Daniel aliitikia salamu yangu kwa kuniachia dongo moja)
Maneno ya Daniel yaliniuma sana,kwakuwa sikutaka kuonesha hisia zangu nikaendelea kuwapatia salamu.

" Hamis za asubuhi "

"Salama,karibu Sana Mzee"

"Asante ndugu yangu,ngoja niweke mkokoteni vizuri" (nikaupaki mkokoteni karibu na genge la matunda ya John)

Sikumuona John wakati nimefika ikabidi niwaulize Hamis na Daniel
"John kaenda wapi?"

Hamis akajibu
"Mmepishana sekunde tatu tu,ila usijali,kaka ameenda kujisaidia si unamjua mambo yake"

Nikatabasamu,John huwa anapenda kujisaidia haja kubwa kila siku asubuhi, tabia yake ameshindwa kabisa kuizuia.

**
Baada ya dakika kumi kupita nikamuona John akirudi kutoka chooni, alifika mpaka nilipokaa
"Mdogo wangu za tangu Jana"

"Salama kaka,ila kichwa kinauma"

"Hahahah...Jana ulikunywa sana"

"Dah,haya mambo yanahitaji mazoea" (niliongea kwa sauti ya chini)

"Hahah,usijali kevoo utazoea"

Usiku wa Jana Mimi na john tulienda kunywa pombe, uchovu wa siku ya Jana ndio unaopelekea kichwa changu kiume,upande wa john hakuwa na tatizo kwa maana ameshazoea kunywa pombe.

John na Mimi tukaanza kupiga stori za hapa na pale,upande wa Hamis na Daniel walikuwa wamejitenga pembeni peke yao.
Daniel na Hamis ni wambea,wakishagundua jambo lako watalisambaza kwa kila mtu wanayeonana naye,kuna muda wanatoa umbea hata kwa wateja wao.

John na Mimi tukaendelea kupiga stori ,tukiwa katikati ya mazungumzo yetu yenye Furaha, mara ghafla mazungumzo yetu yakasimama,mbele yetu kuna jambo ambalo limetushangaza kweli kweli.Siyo Mimi na john pekee ambao tulishangaa,bali Hamis na Daniel na wao waliyatoa macho mbele.

Itaendelea.....
💥IPI SABABU YA KEVOO KUTOKWENDA NYUMBANI? KWANINI HATA MAZISHI YA MAMA YAKE HAKUHUDHURIA?.

Soma mpaka mwisho wa simulizi kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Riwaya: MAPEPE Na Mtaalam wa Simulizi SEHEMU YA KWANZA **  >>> https://gonga94.com/semajambo/riwaya-mapepe-na-mtaalam-wa-simulizi-sehemu-ya-kwanza
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

TREVOR CHALOBAH 🫡

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 28💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

🌹I MISS YOU 🌹

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 22💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA🙈3~4

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 11.

majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest