Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

NDOA YA MKEKA* 02👰🤵🤟💗

16th Jul, 2025 Views 2


Mwandishi; Kitty Fefe

Nilioga na kubadili nguo,nilikuwa nazo chache.....nilishawaambia nikachukua simu kuona kama hata nilipigiwa lakini sikukutaka kitu😩😩😩 yaani wazazi hata kuulizia kama nimefika..?? Kweli wamejua kunitupa🤣👐 niliona ngoja tu niwapigie jamani,nilitafuta namba ya mama na kupiga, akapokea
"Shikamoo mama"
"Marahaba,mmefika salama?..maana nilikuwa nimemuagiza mtu vocha nikupigie" nikaona kumbe mama ananijali😲😍
"Tumefika salama mama"
"Vipi mazingira ya huko?"
"Yako vizuri tu"
"0oooh....! Basi tutaongea zaidi"
"Sawa mama,ila....!"
"Nini tena?"
"Au basi"🙏🏻🙏🏻 nilitaka nimlalamikie lakini nikaona kama alishindwa nitetea huko nyumbani,sasa hivi ndo itasaidia nini....?😁😁😁 niliona nimuache tu,ila humu ndani simalizi mwezi Hakim atanirudisha tu kwetu 🤸🏻‍♀️🤸🏻‍♀️🤸🏻‍♀️

Nilitoka mule chumbani na kwenda sebuleni alipo Hakim,
"Kulthum njoo tule sasa"
"Sawa,ila naomba kuuliza"
"Niulize tu,be free"
"Mimi nitalala wapi?"😢
"Mule chumbani kwangu"
"Mimi siwezi kulala chumba kimoja na wewe"
"Kwanini? Kwani kuna tatizo"
"Nimekwambia tu siwezi"🤦🏼‍♀️
"Sawa,hamna shida vyumba vipo utalala kingine.....najua hujapenda hili lakini kiukweli mimi nimeridhia tu🙏na nakupenda sana....samahani pia kwa kilichotokea sikuweza kupinga uamuzi wa baba ako,hivyo usiwe na shaka usijione umepoteza....kesho nitakupeleka ukamuone mama yangu,anakaa sehemu ingine,hivyo nikuombe uwe na amani tu"
"Poa"
"Haya tule sasa"
Tulipakua chakula na kuanza kula,kidogo mjomba ake kutoka Tanga akampigia na kumuuliza habari za safari akamwambia ni nzuri tu tulifika salama,tulikula tukamaliza.....nikatulia tu nikawa nachati na braza angu(Mustafa )ninayemfuatia ndio nilikuwa naelewana nae sana.....akawa ananisisitiza niwe makini tu kama kukiwa na tatizo nimwambie🌝🌝nikaona afadhali hata kaka Mustafa ananijali kuliko wazazi na hao Salum na Khalid😔😔😔tulichat sana yaani nikamwambia
"Kaka naomba tu nichat maana najihisi upweke sana😔huku nahisi kama familia imenitenga"
"No usiseme my sis mimi niko hapa usijione mpweke kabisa"😢
"Sawa kaka,nitashukuru kama kila siku utakuwa angalau unanikumbuka"🙏
"Kuhusu hilo wala usitie shaka kabisa"
Tulichat sana jamani mpaka simu ikaisha chaji,nikawa najifikiria nitaanzaje kuweka chaji maana Hakim na joel walikuwa wanaangalia TV hapo sebuleni na sitaki kuongea nao😂😂😂nikasema nitaenda kuchaji nikienda kulala🚶🏼‍♀️ natamani kumwambia Hakim muda unaenda mbona hata hanionyeshi chumba cha kulala ila nikawa naona soo kumwambia jambo hilo mbele ya joel🥲nikavunga tu.....tukala kwa pamoja na tukaendelea kuangalia tv

Nashukuru sana joel akajiongeza na kuaga kuwa anaenda kulala🙏akatutakia usiku mwema na kuondoka,,,
"Kulthum hivi haujachoka ukapumzika?"
"Nimechoka" sasa hapa anauliza swali au anajibu😏
"Ndo unahitaji kulala chumba kingine?🥲anyway ngoja nije" akanyanyuka na kwenda chumbani kwake akarudi na funguo ya chumba kingine na kunipeleka akafungua na kuniambia nilale humo,kulikuwa pasafi sana ila akanambia nibadili shuka tu zipo kwenye kabati na kunitakia usiku mwema,nikaweka kwanza simu chaji na kumtakia kakangu usiku mwema kisha nikalala

Kutokana na uchovu wa safari usiku sikushtuka hata kidogo mpaka asubuhi kulipokucha🥱 kijua cha asubuhi kilikuwa kishachomoza😨nilienda oga kwanza nitoke nje nifanye kazi japo siipendi hii ndoa lakini lazima nijishughulishe buana na kazi za nyumbani😹😹😹cha ajabu nilikuta Joel kashafanya kazi zote hadi chai tayari🙄aibuje....!?😹🙈nikaanza jibaraguza pale mara ungeniamsha akanijibu eti nisijali mimi ni mgeni bado....au alidhani nilikuwa na shughuli usiku na Bro ake...!? wapi...!?😹😹😹 siliwi kizembe shenzzz😂😂😂🤸🏻‍♀️

Hakim nae akawa ameamka akanambia kuwa tunywe chai kisha twende mjini kwa ajili ya kununua nguo na vitu vingine na twende akanitambulishe kwa mama yake🌝nikawaza hivi mtu mwenyewe simpendi jamani nikanunuliwe nae vitu ni sawa kweli....!? ila nikikataa nitakuwaje navaa nguo zile zile nilizokuja nazo kama Ben Ten jamani....!? nyieee kuweza...!? kwanza sijamuomba akaninunulie ni yeye mwenyewe kanishobokea......!😹😹😹🤸🏻‍♀️🤸🏻‍♀️🤸🏻‍♀️

Tukiwa tunakunywa chai Joel akapigiwa simu na kupewa taarifa za msiba kuwa baba yake amefariki😢😢😢very sad....! tulimpa pole na Hakim akamwambia inabidi tukiwa huko mjini amkatie tiketi kabisa na kesho asafiri kwenda msibani mbeya,anatamani kwenda nae ila likizo yake imeisha na kesho kutwa anatakiwa aripoti kazini,hivyo Joel aende tu halafu yeye ataenda mara moja kuwapa pole weekend ijayo🙏🙏🙏Joel alielewa mimi na Hakim tukatoka pale nyumbani na kuelekea mjini,Joel akabaki nyumbani ili pia ajiandae na safari

Tulifika mjini na kununua nguo,viatu na vitu vyangu vingine..... kisha tukaenda kwa mama yake alitupokea vizuri mno🥰🥰🥰mpaka nilimpenda,ila mwanae SIMPENDI KABISA HILO MKUMBUKE😹😹😹 akanambia niwe na amani na atatuandalia sherehe maana ana vikundi vya wamama wenzie haiwezekani harusi ya mwanae iwe kizembe,japo imepita ya ghafla ila nisijali kabisa,tena na kwetu mahari lazima itolewe ndoa iende kisheria zaidi, nilimuitikia tu kwakweli siwezi mueleza yaliyomo moyoni mwangu🤪🤪🤪

Tukarudi nyumbani Joel akapatiwa tiketi yake na pesa,nilichogundua tu Hakim.ni mpole halafu ana moyo wa upendo sana,akamtakia Joel safari njema🙏🙏🙏Mimi nikaingia na mizigo yangu chumbani nikaanza jaribisha moja moja🥱🥱🥱maana huko dukani sikujaribu vizuri💃❤️‍🔥❤️‍🔥❤️‍🔥zilinitoa vizuri❤️‍🔥❤️‍🔥❤️‍🔥 yaani zote zilikuwa zipo bomba huwezi kujua kabisa kama mwenye ameninunulia simpendi 😹😹😹tena zingine alinichagulia yeye kabisa😂😂😂lakini ndo kumpenda simpendi 🗣️🗣️🗣️

Siku iliyofuata asubuhi tena nilikuta Joel kashaamka na kuandaa hadi chai🌝na akaniaga kuwa ananikimbia kidogo ila atarudi akimaliza msiba,nilimuomba namba yake akanipatia,Hakim nae ndio alikuwa anaenda kazini muda huo akanambia nibaki salama,na nimsamehe sana ananiacha mwenyewe🙏kila kitu kipo nitapika🥣aende tu babuu mimi hainiumi wala kidogo, akaniambia nimpe namba yangu atanipigia au kukiwa na kitu nahitaji nisisite kumtafuta..... nilimpa simu aandike namba yake nitambip apate yangu ila alivyoondoka sikumbip wala kusave namba yake nikacancel tu..... sitaki mazoea nae buana😹😹😹nikakaa zangu kuchat na kaka,tatizo likaja nilipojigundua natakiwa kupika na kuangalia vitu vya kupika vipo kwenye friji ,samaki,nyama hadi unga na mchele ,viungo sijui mafuta vipo halafu siwezi kuwasha jiko la gesi🙀🙀🙀na ushamba wangu naumbuka mimi nikatafuta mkaa humo ndani mpaka nilikonda,jamani kwani hawapikii mkaa sijui🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️namba ya Hakim nimefuta nikaona nimpigie Joel nae hapokei😭😭😭😭😭njaa inaniuma,kiburi kimeniponza😭😭na huko.Hakim si atarudi akidhani kuna mtu kapika huku😢😢😢 nimeisha😔😔😔😹

ITAENDELEAAA

FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NDOA YA MKEKA* 02👰🤵🤟💗  >>> https://gonga94.com/semajambo/ndoa-ya-mkeka-02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

TREVOR CHALOBAH 🫡

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 28💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

🌹I MISS YOU 🌹

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 22💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA🙈3~4

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 11.

majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest