Story………………...
Mtunzi……………..Simulizi Za Zooper
WhatsApp……....0613083801
Umri………………...18+
ILIPOISHIA.......
Furaha aliyokuwa nayo mwanzo ilipotea kabisa baada tu ya kumkosa binti aliyekuwa hamfahamu.
"Inatakiwa uwe na furaha Prince hii ni siku yako mhimu!"
"Najua!"
Malikia alibaki kumtazama kijana wake aliyemjibu kiufupi na wote walienda kukaa na baada ya mda kuna binti aliletwa aliyepambwa na kuvutia kwenye macho ya kila mtu aliyekuwa maeneo yale, Mfalme Leo alipiga makofi akifatiwa na wengine akiwemo Malikia wake lakini haikuwa hivyo kwa Prince Hayden, yeye aligeuka na kutazama pembeni kabisa kitu kilichozidi kumshangaza Malikia aliyekuwa akifatilia mienendo ya kijana wao.......
ENDELEA........
"Ni binti mrembo sana!"
"Ndio Mfalme wanangu karibu wote ni warembo, watazame na hao wengine!"
Baba mzazi alimwaga sifa kwa mabinti zake wote waliokuwa wamesimama mbele ya macho yao na Mfalme Leo aligeuka na kumtazama Malikia wake na kumkonyeza.
Malikia alisogeza mdomo wake mpaka kwenye sikio la Prince Hayden na kumnong'oneza na baada ya mda Hayden alinyenyuka kwenye kiti chake na kutembea taratibu akimsogelea binti aliyekuwa ameletwa.
Makofi pamoja na vigelegele vilizidi kusikika.
"Wameendana watazame!"
"Hakika wamependeza, Jasmine anasitahili kuolewa na mwana wa mfalme!"
"Tafadhali kila mmoja wenu akae kimya!"
Vigelele pamoja na minong'ono ilikoma baada ya sauti kusikika.
Prince Hayden alimtazama machoni Jasmine aliyekuwa ametawaliwa na aibu tele na kumnong'oneza kwa sauti ya chini na baada tu ya kumnong'oneza tabasamu alilokuwa nalo Jasmine lilipotea pale pale ila Prince Hayden alimshika mkono na kuongea kwa sauti ya chini.
"Zingatia kile nilichokwambia!"
Jasmine alikubali kwa kichwa na Prince Hayden alimpeleka na kwenda kumkarisha kwenye kiti na yeye kukaa pembeni yake na makofi yaliibuka kwa mara nyingine tena.
"Taratibu za uchumba zifanyike haraka!"
Prince Hayden na Jasmine walisimama lakini hakuna aliyekuwa na tabasamu kabisa kwenye macho yake, mpaka wanamaliza kuvalishana pete za uchumba bado hali ilikuwa ile ile kwenye nyuso zao na aliyeigundua alikuwa Malikia Luciana na baada ya kila kitu kukamilika Prince Hayden alifanya kitu kingine cha kushangaza kwa kutoka nje na kuondoka akiwa na dereva wake pamoja na walinzi wake pasipo hata kuwasubiri Malikia Luciana pamoja na Mfalme Leo.
"Malikia, Prince ameondoka!"
"Nini!?"
Malikia Luciana alishitushwa na taarifa alizofikishiwa na mlinzi wao hivyo alisogea mahali alipokuwa Mfalme Leo na kuzifikisha.
"Hii inawezekanaje!?, anaondokaje peke yake pasipo kukumbuka uwepo wetu!?"
"Sijui nini kimempata Prince kabadilika ghafra sana!"
"Maandalizi yafanyike haraka ya kuondoka!"
"Sawa Mfalme!"
Malikia Luciana alitoa maagizo kwa walinzi wao.
Jasmine hakutaka kukaa sehemu ya tukio hivyo alitoka na kuelekea kwenye chumba anacholala, alifika na kufungua mlango na baada ya hapo alianza kuvua nguo zake huku akiyatupa mapambo aliyopambwa kwa hasira akikumbuka alivyonong'onezwa na Prince Hayden.
"Samahani sana sitaweza kukuoa ila leo nitakuvisha pete ya uchumba tu!"
Baada ya kukumbuka alianza kuzungumza mwenyewe kwa hasira na mda huo huo kuna binti aliingia ndani ya chumba hicho.
"Mbona upo katika hali hiyo ikiwa leo ni siku yako ya uchumba!?"
"Prince Hayden hataki kunioa!?"
"Prince hataki kukuoa!?, kivipi wakati mpaka pete mmemivishana!?"
Jasmine alimweleze kiufupi ndugu yake aliyekuwa akiitwa Arabella.
"Kwanini ulikubali kuvalisha naye pete!?"
"Kwa sababu nataka kuolewa naye tu!"
"Lakini tayari ameshakataa!"
"Sijali alichokisema ila nachojua mimi tayari ni mchumba wake!"
Jasmine alikaa kitandani kwa hasira na Arabella alikaa pembeni yake na kuanza kumtuliza dada yake.
Prince Hayden alikuwa ndani ya gari na alitoa amri dereva aendesha haraka mpaka kwenye eneo alilomwonea Sierra kwa mara ya kwanza, dereva alifanya kama alivyoambiwa na baada ya mda gari iliweza kufika.
"Ndio hapa Mwana wa mfalme!"
"Sawa!"
Prince Hayden alishuka kwenye gari na walinzi wake walifanya vivyo hivyo.
"Asinifate mtu!"
"Sawa mkuu!"
Walimwacha mwenyewe na Prince Hayden aliondoka na kuanza kuzunguka akimtafta Sierra, njiani watu walimtazama na wengi walibaki kwenye mshangao mkubwa kuona mtoto wa mfalme anatembea pasipo kuwa na ulinzi wowote ule.
"Angalie kule!"
"Wapi!?"
"Kule!?"
"Ooooooh mu....ngu wangu, Prince Hayden!"
"Kwanini yupo peke yake na walinzi wake wapo wapi!?"
"Ingekuwa vizuri kama ungeenda kumuuliza mwenyewe!"
Kila mtu aliongea lake na Prince Hayden baada ya kuwaona aliwasogelea na ilibaki kidogo tu wakimbie.
"Msikimbie!"
Wote kwa pamoja walipiga magoti na kuinama chini kama utaratibu ulivyo kwa ajili ya kutoa heshima kwa Prince Hayden aliyewainua na kuanza kuwatazama kama atamuona Sierra lakini hakuwa miongoni mwao.
"Mnaweza kuendelea na kazi zenu!"
Baada ya kuongea alijiondekea na kuendelea na kazi ya kumtafta Sierra.
"Ohuuuuuuu nilihisi moyo kuchomoka!"
"Siamini kama leo nimeongeleshwa na Prince Hayden, najihisi mwenye bahati sana!"
"Hahahaha mimi ndiyo mwenye bahati zaidi kwani nilikuwa karibu yake na nilisikia harufu nzuri iliyokuwa ikisikika kwenye mwili wake!"
Mvutano ulikuwa mkubwa kwao wakati huo Prince Hayden akiwa ameshaondoka tayari kwenda kumtafta Sierra.
Huku barabarani msafara wa Mfalme Leo pamoja na Malikia Luciana uliweza kufika na kulishuhudia gari la Prince Hayden likiwa limepaki kando ya barabara huku walinzi wakiwa wamesimama pembeni yake.
"Simamisha gari haraka!'
Gari ilipakiwa pembeni na Mfalme Leo aliteremka akifatiwa na Malikia Luciana na kusogea mpaka walipokuwa walinzi wa Prince Hayden na raia mbalimbali walianza kurundika baada ya kuuona msafara wa Mfalme wao maeneo yale.
Kwa hasira Mfalme Leo alihoji alipo Prince Hayden na walinzi walijibu hata wao hawajui alipoelekea.
"Nyie ndiyo walinzi wake mnakubalije anaondoka mwenyewe!?"
"Tusamehe kwa hilo Mfalme, Prince alikataa tusiongozane naye!"
Aliwatazama kwa hasira lakini mda huo huo Prince Hayden alifika na kukuta mzozo ukiendelea na Malikia Luciana alisogea karibu yake.
"Wapi ulipokuwa na kwanini unahatarisha maisha yako Prince!?"
Prince Hayden hakujibu zaidi ya kukaa kimya na kitendo kile kilimkera Mfalme Leo ila kutokana na wingi wa watu alirudi ndani ya gari na wengine wote walifanya vivyo hivyo na baada ya hapo msafara ukaendelea kuelekea kwenye kasili la kifalme.
**************************
Licha ya kazi nyingi alizoambiwa kufanya ila zote alizimaliza kwa wakati na mda huo ulikuwa mda wa yeye kupumzika, Sierra aliingia chumbani kwake na kujilaza kitandani ila mwili wote ulikuwa ukiuma kutoka na viboko alivyopigwa, alijikuta akitokwa na machozi na kuachia kilio cha chini chini huku akiwaza kwanini ndugu zake wanamchukia bila sababu ya msingi, akiwa ametulia mlango ulifunguliwa na Mama yake mkubwa akiwa kabeba ndoo ya maji na kumwagia pasipo kujali kama yupo kitandani........ITAENDELEA.
Full Tsh 1000, WhatsApp 0613083801
Namba za Malipo 👇👇👇👇
0613083801 HALOPESA JINA JOHN
0748697173 M-PESA JINA JOHN..