Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA *__________________________________* SEHEMU 03 na 04

8th Jul, 2025 Views 38

03

ENDELEA......
Victor mpeleke ndani Osman, nina mengi ya kuzungumza na Asha" Sabrina aliongea huku akimtazama Asha kwa kumkadiria.

"Kuhusu kuondoka kwangu bila kutoa taarifa Asha hauhusiki itapendeza kama hata bebeshwa lawama katika hili" Osman aliwahi kutetea ukorofi wa Mama yake anauelewa.

Sabrina aliachia tabasamu kwa namna Osman anavyo hangaika kumtetea Asha.

"Mkeo ana kusubiria ndani naomba uachane na mambo ya Wanawake....'' Sabrina alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo.
Asha alitambua kosa lake alipiga magoti chini.

Osman alitaka kuongea Victor alimkatalia
"Mambo ya Wanawake hupaswi kuzungumza... naomba tuondoke"

Osman alimsikiliza Victor waliingia ndani...moja kwa moja alielekea chumbani kwake.

Alipokolewa na harufu nzuri ya marashi....Hilda alikuwa kapendeza sana siku zote alijiweka vizuri kumsubiria Mumewe.

"Mama yangu yupo na hasira naomba umsaidie Asha..." Osman alimuomba Hilda kisha akamkumbatia
Anafanya hivi kama wajibu tu lakini mpaka sasa moyo wake haujapata Mwanamke wa kuutikisa.

Hilda hakutaka kuonekana na roho mbaya alivaa mavazi ya heshima kisha akaelekea nje.
Asha alikuwa kapiga magoti chini. Yeye na Hilda walitazamana.
Kila mtu alimuona mwenzake hana maajabu yoyote hasa kwa swala zima la urembo.

"Nilitarajia atakuwa ni mrembo kuliko hata Mimi...." Asha alijisemea huku akicheka ndani ya moyo wake.

Hilda alisogea taratibu huku akimtazama Asha kwa jicho la dharau, alivyoona anamudu alikaa kwenye kochi.

"Mkwe, naomba Asha atanifulia mashuka yangu nitakayo yatumia usiku wa leo na Osman" Hilda alizungumza.

Ilikuwa ni adhabu kubwa sana kwa Asha ni heri hata angetolewa jicho juu hata Sabrina mwenyewe alishtuka, hakutarajia kama huyu Binti anaweza kuwa gaidi namna hii.

"unasubiri nini kusema ndiyo...pokea adhabu" Sabrina alimshtua Asha aliyekuwa kwenye mshangao.

"Ndi...Ndi....ndiyo nitatekeleza" Asha alijibu.

"Naamini utafanya kwa moyo mmoja...." Hilda alizungumza kisha akaondoka.

"Naamini hautaenda kinyume na maagizo uliyopatiwa, amri ya Hilda haina tofauti na ile ya Osman... mshukuru kwa huruma zake. nilipanga kukupokonya vidole vyako vyote" Sabrina aliongea kisha akaondoka, ndani ya moyo wake alimpigia saluti Hilda kwa adhabu aliyoitoa.

Asha aliachia tabasamu lililojaa maumivu kwa adhabu aliyopatiwa. Alikusanya nguo akaenda chumbani kwake kupumzika.
Alijikuta akiumia ndani ya moyo wake baada ya giza kuingia, udhaifu wa Wanaume anaujua. Aliamini kwa vyovyote vile ni lazima Osman amzagamue Hilda.

Usiku ulivyo wadia Osman hakuonesha ushirikiano wowote kwa Hilda....hisia zake zilirudi Jijini Dodoma, alikumbuka tukio alilolitenda na Anjeli... alijikuta akitamani kushiriki na msichana huyo anayejikuta Malaika mchana lakini usiku ni kubwa la makahaba.

Hilda alijisikia fedheha sana, alivaa nguo akajifunika blanket

"Nisamehe....sijisikii vizuri" Osman alijitetea
"Naelewa...." Hilda alijibu kwa ufupi.

Kulivyo pambazuka Asha alisimama mlangoni kwa Hilda kuchukua mashuka kama alivyopatiwa agizo siku ya jana.

Hilda ni Mwanamke mjanja, alimwagia kimininika cha alovera kwenye shuka ilimradi tu ionekane mechi ilipigwa tena hata tembea yake ilikuwa ni ya kuchechemea.

Moyo wa Asha uliumia sana kana kwamba alikuwa anasalitiwa. hakuelewa kama Hilda hakuambulia chochote usiku wa jana.

"Naomba ufue haya mashuka kwa mikono yako, endapo utavaa gloves au kufulia mashine nitahesabu unanidharau" Hilda aliongea kisha akaweka mashuka chini.

Asha aliinama akaanza kuya kusanya bila kuongea chochote.

Siku zilizidi kwenda Hilda na Osman walianza kukutana kimwili.....japo walitenda hili tendo lakini moyo wa Osman ulikuwa umefungwa bado hakuwa na hisia na Hilda hata kidogo.

Moyo wake ulikuwa una mkumbuka Dada poa aliyekutana naye kwa usiku mmoja.
Japo alimuibia vitu vyake lakini kuna namna aliweza kumfikisha katika kilele ambacho hajawahi kufika tangu aanze kukutana na wanawake.

Upande mwingine, Maisha ya Anjeli yalizidi kuwa magumu, hakuona sababu ya kuendelea kukaa Dodoma. Alihitaji kwenda Mwanza amkabidhi Osman boksa yake anayoamini ni chanzo cha ugumu anaokutana nao.

"Nataka kwenda Jijini Mwanza kujifunza kutengeneza viatu naomba mnichangie pesa ni kirejea nitawarudishia wote kwa sababu nitakuwa na uhakika wa kuingiza pesa" Anjeli alizungumza na Baba mmoja anayependa kumuita Malaika.

Ombi lake lilitembea kwa haraka, Malaika ndio alikuwa na uhitaji basi kila mtu aliguswa hawakutaka ateseke hata kidogo.

Anjeli alijilaani vikali ndani ya moyo wake kwa sababu watu hawa wana mtendea mema sana lakini yeye ana wadaganya.

Pesa ilipatikana ya kutosha, kulivyo pambazuka walimpeleka akapanda gari iliyokuwa inaenda Mwanza. Walimtakia mafanikio mema.... Anjeli alizidi kulia machozi ya majuto kwa sababu lengo lake ni kumtafuta Osman akambidhi boksa lake kisha waongee kuhusu mikosi aliomwachia na si kujifunza kutengeneza viatu...........ITAENDELEA......

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA
*__________________________________*
SEHEMU 04

ENDELEA..........
Akiwa ndani ya gari aliwaza mambo mengi kuhusu maisha yake.

Alijitahidi sana kubana matumizi, hakuwa tayari kununua vitu hovyo japo nja ilikuwa inamkandamiza lakini alijikaza.

Baada ya masaa nane kupita alifika Jijini Mwanza.
Hakujua anaanzia wapi, stendi ya nyegezi ilikuwa imechangamka kuliko hata ya Jijini Dodoma.

Anakuja kushtuka akiwa hana begi, aliangua kilio cha uchungu kwa sababu hakuwa na akiba yoyote ya pesa.

Zaidi ya kupewa pole hakukuwa na msaada mwingine kwa ajili yake.

"Siku hizi binadamu ni mafundi wazuri wa kuigiza, juzi kati tumetoka kumchangia binti Mmoja akijitia katelekezwa kumbe alikuwa ni bonge la tapeli tu, hata huyu na mashaka naye" Mama Mmoja alizungumza akionekana kukwazika na namna Anjeli anavyopiga kelele za kuibiwa.

Upande wa Osman moyo wake ulizidi kufurukuta kila akimkumbuka Anjeli mfano wa mtu aliyekolezwa na madawa.... alishindwa kuvumilia alimshirikisha Asha Mlinzi wake wa karibu.

"Una mkumbuka yule binti aliniibia nguo zangu kisha akaziuza tulivyo kuwa Dodoma"

"Nakumbuka...." Asha aliongea huku akimtengenezea koti lake.

"Naomba umtafute kwa ajili yangu..."

"Kuna nini?...."

"Kuna jambo hatukumalizana ukimpata nitafurahi sana.... naomba ufanye kwa siri" Osman aliongea kisha akaondoka.

Asha hakuelewa kwanini Boss wake anataka kuonana na Anjeli,,,

Osman aliingia kwenye kikao, kulikuwa na haja ya kufanya mabadiliko katika magodoro yanayozalishwa na kuuzwa na Kampuni lake. Kwa wakati huu walihitaji kuwafikia hata watu wenye kipato cha chini kabisa.

Upande mwingine japo Victor ni Mlinzi wa Osman mara nyingi anatumika na Sabrina.

"Nipeleke Supermarket kuna vitu naenda kununua"

"Sawa...."

"J
Kabla hujaenda kujiandaa naomba nisikie kutoka kwako.. "

"Kitu gani mkubwa?"

"Ni kitu gani kilitokea mlipokuwa Dodoma?"

"Tofauti na kuhakikisha Boss anapata amani ya moyo hakuna kitu kilitokea"

"Akili yake ni kama haijatulia hivi...tuachane na hilo huenda nimekuuliza swali gumu" Sabrina aliongea kisha akaenda nje kumsubiria Victor.

Wakati anataka kuingia ndani ya gari Hilda alijitokeza

"Naomba tuambatane wote...." Aliongea.

"Usiwe na shaka ingia kwenye gari" Sabrina aliongea.

Safari ya kwenda Supermarket ilianza, hadithi za hapa na pale ziliendelea.

Upande wa Anjeli hakujua anaanzia wapi hivyo alikaa kwenye bench kubwa lililokuwa mbele ya duka la Mangi.

Asha alipita sehemu hii akielekea airport, laiti kama angegeuza shingo yake mkono wa kulia basi angemuona Anjeli hivyo zoezi la kwenda Dodoma lingeishia hapa.

Anjeli alijikuta akikumbuka kuhusu kitambulisho cha Taifa cha Mtu anyemtafuta.

"Haya maeneo kuna mtu anafahamika kwa jina la Osman!" Anjeli alijikuta akimuuliza Mangi.

"Unaongelea Osman CEO wa Kampuni la DreamCloud au Osman yupi" Mangi aliuliza.

Anjeli alijaribu kutoa sifa za Osman anaye zungumzia yeye.

"Bila shaka una muongelea Osman niliyekuelekeza Mimi..."

Wakati Asha anapanda ndege kuelekea Jijini Dodoma, Anjeli alipanda bajaji kuelekea ofisini kwa Osman.

Kampuni la DreamCloud lilikuwa limechukua eneo kubwa sana, hii haimkutisha Anjeli alipiga moyo konde. Kuonana na Osman haikuwa rahisi kama anavyo fikiria, hakuna aliyemsikiliza kwa sababu hakukuwa na makubaliano ya kuonana kati yake na Osman.

"Cha kukusaidia sana nenda kakae hapo getini, kama atapita hapo atakutambua. Ndio kwanza nimeajiriwa jana siwezi kufanya makosa," Dada wa mapokezi aliongea.

Anjel hakukata tamaa alikaa getini kwa Mlinzi akaendelea kumsubiria Osman.

"Angalia usije kukata gogo hapo kwa namna ulivyokaa na hofia usije leta ajali ya kinyesi hapo" Mlinzi aliongea.

Akili ya Anjeli ilikuwa mbali sana hakuwa akimsikiliza Mlinzi.

Osman akiwa anatoka ofisini kwake aingie kwenye gari alisikia sauti ya Mwanamke ikimuita.
Japo kulikuwa na umbali kidogo lakini alifanikiwa kuiona sura ya Anjeli.

Mapigo ya moyo yalienda mbio sana kana kwamba ameona joka mkubwa..................
Soma mpaka mwisho kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA *__________________________________* SEHEMU 03 na 04  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-dada-poa-wa-usiku-mmoja-__________________________________-sehemu-03-na-04
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
bei kitonga
bei kitonga

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA🙈3~4

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 11.

majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA EPISODE 2

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE...5...6

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 3...4

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA 1

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈21

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈20

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 8

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 7

majario rewards 100 Comments 0
 

Life in a Year (2020)

majario rewards 100 Comments 0
 

Kenya, Tanzania, Congo

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 40

majario rewards 100 Comments 0
 

POSHY QUEEN:

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 39

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈19

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈17

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈16

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈15

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 05 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 04 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 03 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 02 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 01 ❤❤.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 34

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈10

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest