Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SULTANA 06 (Ndani Ya Jumba La Dhahabu)

1st Aug, 2025 Views 33


MTUNZI; LIZY MICA

Endelea ๐ŸŒป
"Sona hayuko hapa.... jitahidi utoke salama, huenda hii Meli inazama kwa sababu ya dhambi zangu nyingi. Kama roho yako itakuwa salama naamini dhambi zangu zitapungua, I don't know wewe na Sona mna uhusiano gani lakini naomba usimuamini tena....hii Meli ilikuwa inaenda China" Polisi aliye kabidhiwa jukumu la kumfikisha Sultana China aliongea

"Una maanisha kusema hii Meli haiendi Kijijini Odes..." Sultana alijikuta akiuliza na hata akasahau kama yupo hatarini

"Meli kubwa kama hii haiwezi kufika Kijijini Odes... abiria wote walikaa kwenye siti pekee yako uliwekwa huku ukiwa hujitambui,.... naomba ujirushe kwenye maji" Polisi aliongea

"Si....si...sijui kuogelea" Sultana alipaniki

Polisi hakuongea tena, badala yake alimshika Sultana wakaruka wote ndani ya maji, bahari ilikuwa imechafuka kupita maelezo.

Kwa mara ya kwanza Sultana aliishuhudia nguvu ya maji ikiimeza chombo kilicho tengenezwa na binadamu.

Polisi alijitahidi kadri ya uwezo wake kumsaidia Sultana lakini ilishindikana....maji yalikuwa na nguvu kuliko wao hivyo walijikuta wakitapa tapa huku na kule

Baada ya dakika 40 kupita, bahari ilikuwa shwari kana kwamba hakuna kitu kilikuwa kinaendelea.
Japo ilikuwa ni usiku lakini watu wengi walifika eneo hili kutoa msaada....Sona akiwa na timu yake walifika pia.
Moyo wake ulivunjika baada ya kusikia hakuna hata mtu mmoja aliyesaidika

"Ni ngumu kuelezea lakini kila kitu kimetokea ghafla.... isingekuwa rahisi kwetu kufanya chochote, bado masaa machache tu kupambazuke naamini tutaweza kufanya chochote kitu" Mmoja wa mabaharia alizungumza

Sona alishikwa hasira, alijikuta akimtia kibao kana kwamba yeye ndio amezamisha Meli.
Hakujua anaanzia wapi kumtafuta Dada yake..... lengo lake halikuwa kumuua alihitaji tu kumuweka mbali na Kijiji chao pamoja na Jiji la Odes

๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป
Kulivyo pambazuka asubuhi, Liam alifika eneo la tukio akiwa kavaa nguo za kulalia.
Meli ya Star ilikuwa ni mali yake hivyo alihitaji kujua kwanini hakupatiwa taarifa usiku wa jana.

"Kila kitu kimetokea ghafla, tutajaribu kufuatilia chanzo cha ajali hii" Sona aliongea huku akizitazama maiti zilizokuwa zinatolewa ndani ya maji

Idadi yake ilitimia 200 lakini hakuweza kumuona Sultana.
Yeye pamoja na Liam walijitosa ndani ya maji... walihitaji kuwa sehemu ya msaada.

Mpaka jua linazama....Sona hakufanikiwa kuupata mwili wa Sultana, isipokuwa wa yule Polisi aliyemkabidhi Dada yake.
Aliangua kilio kikubwa ndani ya moyo wake

"Siku ya kesho unatakiwa upeleke miili ya wageni pamoja na Wauaji Israel.....timiza majukumu yako, kuhusu hili tukio nitawajibika kwa sababu Meli ya Star ni mali ya Kampuni langu. Ahsante kwa msaada wako" Liam aliongea

"Kila kitu kitakuwa sawa, nitajihidi kurudi mapema kwa ajili yako hivyo naomba usivunjike moyo" Sona alimkumbatia Liam kisha akaondoka huku akiwa na huzuni mkubwa ndani ya moyo wake. Aliamini Dada yake atakuwa kaliwa na nyangumi wa baharini

"Sultana kuliko uendelee kuwa kahaba wa kutembea na Wanaume tofauti ni heri kaburi liwe ndani ya samaki wa baharini....naamini wazazi wangu watanipongeza kwa hili" Sona alijisemea kisha akaingia ndani ya gari

Liam aliendelea kukaa ufukweni mwa bahari, wafanyakazi wake walimvalisha koti nzito kisha wakamuacha pekee yake kwa sababu ndio kitu alitaka.

"Ewe bahari, ni kitu gani nimekukosea.....moyo wangu unaniuma kwa sababu watu wote 280 wamepotea kwa siku moja. Nitawezaje kuitazama jamii....hakika umejua kuniumiza sana, na hata najilaumu kwanini namiliki Kampuni ya Star ships" Liam aliilaumu bahari huku machozi yakimdondoka

Katika hali ya kushangaza, alijikuta akisimama kutokana na kitu alichokiona

Itaendelea ๐Ÿ’ฅ.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SULTANA 06 (Ndani Ya Jumba La Dhahabu)  >>> https://gonga94.com/semajambo/sultana-06-ndani-ya-jumba-la-dhahabu
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest